UTANGULIZI:
Tanzania ni miongozi mwa nchi za bara la Afrika zinazopatikana kusini mwa jangwa la Sahara, pia ni miongoni mwa nchi zinazoendelea kiuchumi duniani. Tanzania ni nchi iliyobarikiwa rasilimali nyingi ambazo ni pamoja na ardhi yenye rutuba, bahari ya Hindi, maziwa makubwa na madogo, mito, mabwawa, mlima Kilimanjaro, misitu, mbuga za wanyama pori, mapori ya akiba, migodi yenye madini ya dhahabu, almasi, tanzanite, rubi, chokaa, chuma, chumvi na makaa ya mawe.
Karibu nusu ya watanzania wanaishi chini ya dola 1 kwa siku. Ongezeko kubwa la idadi ya watu na uzalishaji mdogo katika sekta zinazotumia nguvukazi kubwa kama kilimo, ambacho huajiri karibu asilimia 75 (75%) ya idadi ya watu, linatishia kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi.
Pamoja na hilo rasilimali za Tanzania ni muhimu kwa nchi na husaidia ustawi wa maisha ya watanzania walio wengi, hivyo matumizi yasiyo endelevu ya rasilimali hizi yanatishia kurudisha nyuma uchumi wa nchi. Kinachotakiwa kufanyika sasa ni kuhimiza, kuwezesha, na kuzidisha juhudi na maarifa katika uzalishaji kutokana na rasilimali tulizonazo.
Maendeleo endelevu na ukuaji uchumi wa nchi ni masuala ambayo yanategemea sana matumizi endelevu ya ardhi.
Matumizi ya ardhi ni pamoja na makazi,viwanda,Kilimo, ufugaji, hifadhi za misitu na wanyamapori, hifadhi za barabara na vyanzo vya maji.
Matumizi sahihi ya ardhi ni hazina kwa Taifa na huchochea maendeleo ya sekta mbalimbali, maendeleo ya wananchi na kupelekea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kumekuwa kukitokea migogoro ya mara kwa mara inayohusiana na uendelezaji wa ardhi aidha baina ya Serikali na wananchi ama Wananchi kwa wananchi hasa katika uendelezaji wa makazi, shughuli na biashara.
Wananchi wamekuwa wakiingia katika migogoro na Serikali kwa kubomolewa makazi ama biashara zao ambazo wamewekeza kwa muda mrefu hali inayosababisha kurudisha nyuma jitihada za kujikomboa na wimbi la umaskini ili angalau kuufikia uchumi wa nchi zilizoendelea.
Hii ni kutokana na kutokuwepo ama kutokutekelezwa kwa mipango thabiti kuhusu uendelezaji wa ardhi iliyopo ili iinufaishe nchi pamoja na wananchi wake.
Nikirejea sheria ya ardhi na. 4 ya mwaka 1999 sura ya 113 kifungu cha 19 kinaeleza wazi kwamba kila mtanzania ana haki ya kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria.
Hivyo katika kuboresha maendeleo ya jamii na uchumi ni vyema kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima katika umiliki wa ardhi.
Mpango wa matumizi bora ya ardhi
Maana yake ni mpango wowote uliyotayarishwa na mamlaka husika katika kupanga na kusimamia matumizi sahihi ya ardhi ambayo pia hujumuisha mpango wa sekta wa usimamizi wa rasilimali.
Kwanini matumizi bora ya ardhi?
Mpango wa matumizi bora ya ardhi una manufaa/faida zifuatazo katika jamii:-
(i) Kuepusha migogoro ya ardhi baina ya Serikali na wananchi ama wananchi kwa wananchi. Maeneo yaliyopimwa na kupangiwa matumizi huepusha migogoro katika matumizi,
Mfano;
1) Wafugaji hawataweza kuingia eneo lililotengwa kwaajili ya kilimo na maeneo mengine ya hifadhi za misitu, wanyamapori na vyanzo vya maji kwani watakuwa wametengewa maeneo yao kwaajili ya malisho.
2) Wananchi kujenga makazi ama kuanzisha biashara katika maeneo ya yaliyotengwa kwaajili ya Taasisi za Serikali na hifadhi za barabara, hivyo kuleta usumbufu na migogoro pale Serikali inapoamua kuendeleza maeneo hayo ama barabara hizo kwa kupanua ukubwa wa barabara kutokana na kuongezeka kwa mahitaji.
(ii) Kuongeza usalama na usawa katika kumiliki na kutumia rasilimali zilizopo, kutokana na kutokuwepo kwa mwingiliano wa shughuli tofauti na ile iliyopangwa kufanyika katika eneo lililotengwa.
(iii) Kulinda mazingira ya makazi ya binadamu na mfumo wa ikolojia dhidi ya uharibifu wa mazingira ili kufikia maendeleo endelevu.
(iv) Kuwezesha upatikanaji wa maeneo kwaajili ya makazi yaliyopimwa yenye huduma zote muhimu kwa jamii nzima (v) Kuepusha uvamizi wa maeneo yasiyopimwa na kupangiwa matumizi.
Mpango wa matumizi bora ya ardhi husaidia kutekeleza miradi kwa ufanisi kwani maeneo yaliyotengwa ama yatakayotengwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi yatakidhi vigezo vya mradi husika pasipo kuathiri utekelezaji wa mradi kutokana na uchaguzi sahihi wa eneo la utekelezaji wa mradi. Pia itaepusha ama kupunguza kabisa athari mbaya za mazingira kutokana na shughuli za utekelezaji wa mradi husika, mfano kujenga makazi ama Taasisi za Serikali/ binafsi maeneo oevu hali itakayopelekea kukumbwa na mafuriko kila msimu wa mvua za masika unapowadia na kuharibu miundo mbinu iliyokwisha kujengwa kwa gharama kubwa.
Kwa upande mwingine kuna athari nyingi zinazoweza kutokea kutokana na kukosekana kwa mpango wa matumizi ya ardhi, badala yake ardhi kutumika pasipo kufuata utaratibu maalum uliowekwa. Zifuatazo ni baadhi ya athari zitokanazo na kukosekana kwa mipango bora ya matumizi ya ardhi:-
i/ Kuwepo/kuongezeka kwa idadi ya migogoro ya ardhi miongoni mwa watumiaji wa ardhi,
ii/ Umiliki wa ardhi na matumizi ya ardhi kutokuwa ya uhakika kutokana na kutokuwa na hati miliki ya kipande cha ardhi.
iii/ Kuongezeka kwa soko lisilo rasmi la ardhi (Vishoka).
iv/ Mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake kama vile upepo mkali (Kimbunga), mafuriko, na ukame, ukame uliokithiri unaweza kusababisha uwezekano wa kutokea kwa jangwa.
v/ Uharibifu wa ardhi ikiwa ni pamoja na mmomonyoko wa udongo kutokana na kuhama hama kwa wakulima na wafugaji.
vi/ Uharibifu wa rasilimali misitu na mapori kwaajili ya makazi, kilimo na malisho ya mifugo.
Kwanini kurasimisha ardhi?
i/ Kutambulika kisheria kuwa ni mmiliki halali wa eneo husika.
ii/ Kuongeza usalama katika eneo la mmiliki ili kuepusha mtu mwingine kujimilikisha eneo hilo ama kuliendeleza pasipo ridhaa ya mmiliki.
iii/ Kuondoa migogoro ya mipaka na kutokuleta usumbufu endapo mhusika atahitaji kuuza eneo lake kwa maana atakuwa na nyaraka ambazo ni rasmi kisheria.
iv/ Kujiinua kiuchumi kupitia hati miliki ya mmiliki wa eneo kwani itatumika kama dhamana katika ukopaji wa fedha benki kulingana na thamani ya eneo la mmiliki.
v/ Kuongezeka thamani kwa eneo lako kwani litakuwa linatambulika kisheria tofauti na awali.
Vielelezo 1 & 2 kuonesha athari za kutokuwa na matumizi bora ya ardhi.
Kielelezo 1
Kielelezo 2
Mapendekezo
1) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutambua na kuainisha maeneo yasiyokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili mchakato wa upimaji, utengaji na umilikishaji wa maeneo hayo uweze kufanyika kwa maendeleo ya Nchi.
2) Jamii ielimishwe na kuhimizwa umuhimu wa kurasimisha maeneo yao wanayoyamiliki na kupata umiliki halali wa kipande cha ardhi.
3) Ili kufanikiwa katika hili na kufikia angalau 80% ya lengo kusudiwa, Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi iliyo chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujaribu kupitia upya viwango vya gharama zilizowekwa kwaajili ya urasimishaji ili kama kuna uwezekano wa kupunguza viwango vya gharama za urasimishaji ifanye hivyo ili kila mwananchi aweze kurasimishiwa eneo lake na kuwa mmiliki halali kisheria. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeepusha migogoro mingi ya ardhi inayosikika karibu katika kila kona ya Tanzania na itakuwa ni hatua kubwa sana ya maendeleo ya Nchi.
Wananchi wenye uchumi wa hali ya chini walirahisishiwa /wamerahisishiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata unafuu katika kumudu baadhi ya huduma za jamii baada ya kupunguza / kuondoa kabisa gharama za kulipia huduma za jamii kama ifuatavyo:-
(i) Huduma ya nishati ya umeme.
Wananchi walio wengi hasa vijijini walishindwa kumudu gharama za kuwekewa umeme kutokana na hali ya uchumi wao wa kuendelea kubangaiza kupata angalau milo mitatu kwa siku, jambo ambalo bado liliendelea kuwa tete kwao.
Baada ya Serikali kushusha gharama za kupata huduma ya umeme majumbani, wananchi wenye uchumi wa hali ya chini wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kupata huduma ya umeme kwani kwasasa wanaweza kumudu gharama hizo.
(ii) Elimu
Pia Serikali kwa kutambua haki ya kila mtoto kupata elimu ikaenda mbele zaidi kwa kuondoa gharama za kulipia masomo (ada) kwa shule za msingi na Serikali (kutwa), hali iliyopelekea kila mtoto kupata haki ya kupata elimu.
(iii) Afya
Huduma ya matibabu kutolewa bure kwa wazee wasiojiweza kutokana na sera ya taifa ya mwaka 2007 inayofungua milango kwa wazee wasiojiweza kupatiwa matibabu bure.
Pia kuanzishwa kwa bima ya afya ya jamii (CHF iliyoboreshwa) kwa lengo la kusaidia wananchi wenye uchumi wa hali ya chini mijini na vijijini kupata matibabu kwa gharama nafuu zaidi.
Huduma hii ya bima ya afya ya jamii (CHF iliyoboreshwa) imeainisha gharama kama ifuatavyo:-
1/ Kwa Mkoa wa Dar es salaam huduma hii inagharimu kiasi cha Tsh. 40,000 kwa mtu mmoja na kiasi cha Tsh.150,000
kwa familia ya watu wasiozidi sita (6).
2/ Kwa mikoa mingine yote iliyobaki huduma hii inagharimu kiasi cha fedha Tsh. 30,000 kwa familia ya watu wasiozidi sita (6).
Hii inaweza kuwa ni dalili nzuri na kuashiria kuwa “yajayo yanafurahisha” kwani kuna uwezekano mkubwa pia Serikali kujikita kutoa huduma ya matibabu bure kwa wananchi wote kama ilivyo kwa baadhi ya nchi nyingine 11 (Rwanda, Afrika ya kusini, Mauritius, Algeria, Misri, Tunisia, Botswana, Shelisheli, Burkina faso, Ghana, na Morocco) za barani Afrika ambazo hutoa huduma ya matibabu bure kabisa kwa wananchi wake ingawa wenye uwezo mkubwa kifedha wana hiari ya kulipia huduma ya matibabu.
HITIMISHO:
Tanzania sio nchi ya kufikirika, ina muundo rasmi wa utawala na mamlaka kamili, ina miongozo inayotambulika kisheria. Serikali na miongozo yake isimamie rasilimali zetu ili zitumike kwa usahihi na usawa kwa maendeleo endelevu. Maendeleo hayana budi kuwa na uhusiano na maisha ya wananchi.
Wasalaam.
Dianka.

Upvote
1