Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili

Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili

Ha si wajua tena ukishakula chumvi nyingi, kila mtu wamwita mjukuu. Weye ulishasema ni mzee mwenzangu. Kwa hiyo heshima yako nakutumia.

Hapa wengi ni wazee wenzako, hivyo hilo la "wajukuu zangu' liweke pembeni.
 
Hii ipo sana TZ, na tutaendelea kuyaona. Kuna viongozi wa Dini waliowahi kusema kuwa JK ni chaguo la Mungu, na hio ilikuwa inamaanisha walikuwa wanaiunga mkono CCM na walio CCM.

Nafikiri ulikuwa unamaanisha hiyo

cheap cheap cheap cheap... huyu sheikh anataka kuingia kwenye siasa na anatafuta njia rahisi ya kukubalika CCM (hajui bila fedha CCM huwezi kupata nafasi -- labda kama anazo).

Ni wakupuuza, mwandishi alipasa kuandika "Sheikh Mwaipopo apinga operesheni Sangara" lakini kwa kuwa ameshaandika then Baraza la waislamu ni busara likamkana na kuweka bayana kwamba wao na siasa ni kama moto na petrol na watoe 'press release' kwamba yeyote atakayejaribu kulitumia baraza hilo apuuzwe na asihusishwe na uislamu. Hii ndio dawa ya magenge kama haya hasa kipindi hiki cha kuelekea 2010 ambacho warafi wengi wasio na ushawishi watajaribu kutumia njia yoyote kutafuta uhalali kwa wananchi.

Wakupuuzwa....Alipaswa

Wanapenda sana kudeal na minors, wakati mambo makubwa wanayaona na wanapita hawasemi

Sentensi tata...

Sahihi: Wanapenda sana kudeal na minors, wakati mambo makubwa wanayaona na wanayapita bila ya kusema lolote

Na TZ tutaregret soon, kwa kuruhusu ujinga na upuuzi kama huu kwa watu wajinga wachache. Enzi hizo walikwua wakikusanyika wanapigwa mabomu ya machozi hawafikii hata kuongea, huyu handsome boy kaja na mambo yake ya kuwapa uhuru wa kuongea randomly wanaanza kuongea yasiyowahusu.

Walikuwa....... hawafikirii

Elimu yenyewe wala haiitaji kuwaweka waandishi darasani bali kutoa "official Press Statement" kukemea watu hawa na kuelekeza vyombo vya habari kupuuza 'statement' za namna hii.

Sentensi tata..
Unaanza kwa Elimu yenyewe kuashiria kuwa unazungumzia elimu, halafu unaendelea wala haiitaji kuwaweka waandishi darasani ukizungumzia waandishi wa habari. Na mwisho unamalizia kwa kukemea watu hawa na kuelekeza vyombo vya habari kupuuza 'statement' za namna hii

Sahihi:

Serikali wala haihitaji (??) kuendesha elimu hii darasani. Inachopaswa kufanya ni kuendesha "official Press Statement" kukemea waandishi kama hawa, na pia kuelekeza vyombo vya habari kupuuza 'statement' za namna hii

AU

Waandishi wala hawahitaji kuhudhuria darasani kupata elimu hii. Serikali inaweza kuendesha "official Press Statement" kuwaelimisha waandishi hawa, na pia kuelekeza vyombo vya habari kupuuza 'statement' za namna hii.

Jamani jamani, tuweke uTZ mbele. Hawa watu wengine ni wa kupuuza tu. Kuna wakristo na waislamu wenye udini lakini hautakiwi kuingia katika siasa kabisa. watu kama hawa ni wa kukimbiwa, tusiangalie alisema/aliyefanya kitu ni wa dini gani tuangalie ni kitu gani na manufaa yake.

Kupuuziwa

Sahihi: Kuna wakristo na waislamu wenye udini lakini hawaingizi/hawahusishi udini wao kwenye/na siasa kabisa.


Mabandiko haya yanapatikana katika link hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...slam-nchini-kupinga-oparesheni-sangara-2.html
 
Waislam nchini wapinga oparesheni Sangara
Geofrey Nyang'oro na Zaina Malongo

WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa ukabila, ubinafisi na udini.


Katika kifungu hiki cha habari,utagundua kukosekana kwa uhusiano mzuri baina ya maneno ya rangi nyekundu.
Baada ya kusema chama hicho na operesheni hiyo mwandishi anatakiwa kutumia neno havina badala ya haina kwani anatoa reference kwa kitu zaidi ya kimoja.

Ni rahisi sana kufanya makosa kama haya,na hasa katika mazungumzo kwani hayapotezi maana ya kile kinachosemwa.Hata hivyo ili kuimarisha lugha,ni vizuri tuwe makini na vitu kama hivi.
 
Humu ukumbini; kuna wazee wenzangu, watoto zangu, na wajukuu zangu.

Wewe huko kundi la wajukuu zangu.

Sasa kwa nini utuite wote wajukuu?

Na unajuaje hakuna baba zako humu? Una umri gani wewe? Sijui, siwezi kuaza. Na wewe hutujui, hutakiwi kuaza kwamba wote humu wajukuu zako.

Turudi kwenye mada ya thread, matumizi sahihi ya lugha. Hiyo semi colon ya nini hapo uliposema "Humu ukumbini; kuna wazee wenzangu...."?
 
Sasa kwa nini utuite wote wajukuu?

Na unajuaje hakuna baba zako humu? Una umri gani wewe? Sijui, siwezi kuaza. Na wewe hujui, hutujui, hutakiwi kuaza kwamba wote humu wajukuu zako.

Acha hasira. Kichwa cha habari kiko mbioni kubadilishwa ili kikidhi haja ya mada hii.

Umri wangu ni mkubwa sana.

Sio wote ni wajukuu zangu. Kuna wazee wenzangu na watoto zangu humu.

Turudi kwenye mada ya thread, matumizi sahihi ya lugha. Hizo nukta mbili (semi colon) za nini hapo uliposema "Humu ukumbini; kuna wazee wenzangu...."?

Nimeweka hiyo koma yenye nukta juu, kutofautisha kati ya humu ukumbini (yapaswa fuatiwa na koma) na mtiririko wa wazee, watoto, na wajukuu. Vinginevyo ningechanganya kama ningeandika "Humu ukumbini"," kuna wazee wenzangu"," watoto zangu"," na wajukuu zangu."
 
Acha hasira. Kichwa cha habari kiko mbioni kubadilishwa ili kikidhi haja ya mada hii.

Kwa hiyo unakubali kwamba umekosea kuaza kwamba wote humu wajukuu. Basi usiseme nina hasira. Wewe ndio umekosea!

Umri wangu ni mkubwa sana.

Mkubwa sana kuliko nani, wote?

Mimi naweza kuwa baba yako? Sijui, hujui. Hivyo huwezi kuaza kwamba unaweza kutuita wote wajukuu humu.

Sio wote ni wajukuu zangu. Kuna wazee wenzangu na watoto zangu humu.

Na labda baba zako! Hujui. Sijui.

Huwezi kutuita unavyotaka tu. Hususan kwa wewe mwenye kuzingatia matumizi sahihi ya lugha.

Nimeweka hiyo koma yenye nukta juu, kutofautisha kati ya humu ukumbini (yapaswa fuatiwa na koma) na mtiririko wa wazee, watoto, na wajukuu. Vinginevyo ningechanganya kama ningeandika "Humu ukumbini"," kuna wazee wenzangu"," watoto zangu"," na wajukuu zangu."

Sio kweli. Sio sahihi.

Ukitaka kusema "hapa uwanjani kuna wake na waume" utasema "hapa uwanjani; kuna wake na waume"? Ni makosa. Kama ambavyo huwezi kusema "hapa barazani; kuna viti na mikeka." Huhitaji michanganyo na mikorogo ya semi colons. Unatakiwa usema "hapa barazani kuna viti na mikeka."

Hivyo hivyo basi, ulitakiwa useme "humu ukumbini kuna wazee, watoto na wajukuu." Japo utakuwa umesahau uwezekano wa uwepo wa baba zako humu.
 
Kwa hiyo unakubali kwamba umekosea kuaza kwamba wote humu wajukuu. Basi usiseme nina hasira. Wewe ndio umekosea!

Hakuna nilichokosea.

Kutokana na umri nilionao, mvi na makunyanzi yalivyojaa usoni kwangu; (naitumia tena hii koma yanye kofia) ninalazimika kuona kuwa pengine mimi ni mzee kuliko wote humu.

Mkubwa sana kuliko nani, wote?

Mimi naweza kuwa baba yako? Sijui, hujui. Hivyo huwezi kuaza kwamba unaweza kutuita wote wajukuu humu.

Na labda baba zako! Hujui. Sijui. Huwezi kututia unavyotaka tu. Hususan kwa wewe mwenye kuzingatia matumizi sahihi ya lugha.

Nimezaliwa kabla ya vita kuu ya pili ya dunia.

Sasa kama unafikiri kuwa una umri wa kuwa baba yangu, basi niambie. Sitasita kukupa heshima yako kama mkubwa wangu.

Sio kweli. Sio sahihi.

Ukitaka kusema "hapa uwanjani kuna wake na waume" utasema "hapa uwanjani; kuna wake na waume"? Ni makosa. Kama ambavyo huwezi kusema "hapa barazani; kuna viti na mikeka." Huhitaji michanganyo na mikorogo ya semi colons. Unatakiwa usema "hapa barazani kuna viti na mikeka."

Hivyo hivyo basi, ulitakiwa useme "humu ukumbini kuna wazee, watoto na wajukuu." Japo utakuwa umesahau uwezekano wa uwepo wa baba zako.

Maridadi kabisa.

Sina upingamizi na ufafanuzi wako. Huu ndio mfano wa nia na madhumini yangu katika mada hii. Maadam sote tunaweza kurebishana katika uandishi wa kiswahili fasaha, basi hakuna matata. Tuendelee.
 
Hakuna nilichokosea.

Sasa kwa nini umesema mko mbioni kubadili kichwa cha thread kama hakuna ulichokosea?

Kutokana na umri nilionao, mvi na makunyanzi yalivyojaa usoni kwangu; (naitumia tena hii koma yanye kofia) ninalazimika kuona kuwa pengine mimi ni mzee kuliko wote humu.

Uko peke yako mwenye makunyanzi? Unajuaje ?

Sasa kama unafikiri kuwa una umri wa kuwa baba yangu, basi niambie. Sitasita kukupa heshima yako kama mkubwa wangu.

Rais Kikwete akiingia ukumbini akasema "Mabwana hamjambo?," akiamini kuna mabwana watupu, bila kuwa na uhakika kwamba walialikwa mabwana tu, halafu mama mmoja kwenye halaiki akaropoka kwa hasira, "unajuaje hakuna mabibi humu ndani?" Rais akasema "kama wewe unajijua ni bibi nambie nitakusalimu kwa heshima yako"! Hiyo itakuwa sawa? Akiwapa heshima mabibi mmoja mmoja, na mabwana wakitaka heshima yao mmoja mmoja shughuli itaanza kweli? Kwa nini asianze na "mabibi na mabwana" kuondoa uwezekano kwa kughafirisha mabibi humo ndani?

Bubu Ataka Kusema kapinga ujukuu wa kuaza (ku-assume assume) ukamtoa katika wajukuu, Suki kaswalisha ujukuu ukamtoa katika ujukuu. Na mimi pia utanitoa? Utatutoa mmoja mmoja? Vita vya pili vya takriban 1945 ndio ukaaza kwamba ni mkumbwa kuliko wote humu? Si wote ni wajukuu zako humu.

Maridadi kabisa. Sina upingamizi na ufafanuzi wako...

Si kweli kwamba huna pingamizi na matumizi mabaya ya semi-colon.

Ndo maana hapo juu umerudia kutumia ki-semi colon, tena kwa msisitizo wa kunionyesha, kunikumbusha, kwamba umetumia tena semi colon. Hii safari itakuwa ndefu, na itakuwa na misukosuko mingi.
 
Natoka kidogo kwenye mada, lakini zote ni lugha- shangaa na wewe..............

Who said English language was easy?
Fill in the blanks with either YES or NO:
1...........I dont have a brain.
2...........Im gay.
3...........Am so stupid.

Tuendelee na kiswahili, lol!
 
Natoka kidogo kwenye mada, lakini zote ni lugha- shangaa na wewe..............

Who said English language was easy?
Fill in the blanks with either YES or NO:
1...........I dont have a brain.
2...........Im gay.
3...........Am so stupid.

Tuendelee na kiswahili, lol!

Duh! I better abscond 🙂!
 
Tafadhali usimuite Mhe Balozi wa Zain deiwaka. Alihusika kwa kiasi kikubwa katika uanzishwaji wa Photo Point. Amiliki au asimiliki hio siyo issue hapa JF. Nadhani unataka kuleta umbea wa kumtafuta mmiliki halisi wa photo point ili iweje. Maadam ulimsikia Michuzi akisema yeye ni mmiliki, naomba amini hivyo hivyo, waliokuambia yeye ni dei waka ni wanga.

Link: https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/23252-kumbe-michuzi-photopoint-sio-ya-kwake.html

Kha Pasco, yaani ulivyokuwa unaandika haya maneno hukuona kwamba hayajakaa sawa?

Ni Hamiliki ......Hasimiliki
 
Kha Pasco, yaani ulivyokuwa unaandika haya maneno hukuona kwamba hayajakaa sawa?

Ni Hamiliki ......Hasimiliki

Babu Swahili, nakushauri rejea darasani. Tafuta ile Kamusi ya Kiswahili ya zamani iliyochapwa na Oxford University Press na kurudufiwa na Logmans itakusaidia, usiitegemee kamusi ya TUKI pekee itakuangusha.
 
Babu Swahili umechemsha vibaya mno!

Pasco yuko sahihi.

Kweli?

Inaonekana nimeangalia hayo maneno kwa jicho la makengeza...lol

Ahsante kwa kunirekebisha...kwa mara nyingine tena.

Babu Swahili, nakushauri rejea darasani. Tafuta ile Kamusi ya Kiswahili ya zamani iliyochapwa na Oxford University Press na kurudufiwa na Logmans itakusaidia, usiitegemee kamusi ya TUKI pekee itakuangusha.

Nitafuata ushauri wako Bw. Pasco. Je waweza nielekeza wapi nitapata hiyo kamusi ya Oxford?
 
Last edited:
Bw. Babu Swahili, nashukuru kwa uungwana wako. Ila sio mimi huyo kwenye nukuu ya pili hapo, sijui imekuwaje hapo.
 
Back
Top Bottom