Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili

Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili

Hebu oneni sahihi ya mwanachama wa JF.......hilo neno sijui la kisukuma au kinyantuzu.....nafikiri limekosewa kiufasaha angeandika "potofu"
Fikra ni nyenzo endelezi au potoshi. Changamoto tuliyonayo ni kuchanganua na kutenganisha kati ya fikra endelevu na fikra potoshi, kwani mwisho wa fikra ni matendo pale fikra hazibakii kuwa fikra. SDD6-07Rev.1-09.
 
Thanks Yo Yo! Now we're talking and that's what's up, will rectify.... lol
 
Nadhani hapa ulimaanisha ''hupo'' na si ''huko'' kama ulivyo ainisha.

Kaka Dar Es Salaam , kama unataka kuweka mtiririko mzuri wa kiswahili ulipaswa kuweka neno "UPO" na wala sio "HUPO" kama ulivyoandika hapo juu.
 
Kaka Dar Es Salaam , kama unataka kuweka mtiririko mzuri wa kiswahili ulipaswa kuweka neno "UPO" na wala sio "HUPO" kama ulivyoandika hapo juu.

Jee angeweka neno "Uko" lina tofauti na "Upo"?. Wajua maana ya huu msemo "Upo upo hapo".
 
UPO akimaaniksha u miaongoni mwao, ama Hupo ni kanushi ya upo hivyo hupo(haupo) nisawa na kusema si miongoni mwao.
 
Babu Swahili, eti ni: "zoea" au "zowea", kama lilivyotumika HAPA, naomba msaada tafadhali.
 
Hebu oneni sahihi ya mwanachama wa JF.......hilo neno sijui la kisukuma au kinyantuzu.....nafikiri limekosewa kiufasaha angeandika "potofu"

Mkuu Yo Yo, naomba kukupinga kwamba neno potoshi ni sahihi na ni la Kiswahili.
POTOSHI ni neno la kiswahili lenye maana ya "yenye kupotosha" ama neno POTOFU pia ni la kiswahili lenye maana ya "iliyopotoka" hivyo yote ni maneno ya kiswahili na ni maneno sahihi kabisa ila tatizo ni pahala maneno hayo yatumike na ni wakati gani yatumike.
 
wakuu haya maneno yanatumikaje
yoyote na yeyote

je neno lipi ni sahihi kati ya "dharura na dharula"
 
Hebu oneni sahihi ya mwanachama wa JF.......hilo neno sijui la kisukuma au kinyantuzu.....nafikiri limekosewa kiufasaha angeandika "potofu"

Mimi mbona sioni tatizo hapo:

Potoshi = "enye kupotosha"
Potofu = "iliyo potoka"

Kwa jinsi mtumiaji alivyolitumia neno 'potoshi' naona kama inaswihi.
 
wakuu haya maneno yanatumikaje
yoyote na yeyote

je neno lipi ni sahihi kati ya "dharura na dharula"

Haya maneno (yoyote na yeyote)ni kweli husumbua kidogo katika maongezi ila ni maneno yanayo tumika kwa vitu tofauti ni vigumu kidogo kufafanua bila kutoa mfano.
Yoyote hutumika kwa vitu na yeyote hutumika kwa wanaadamu.
Mfano: 1.)chagua habari yoyote uipendayo na uiandike habari hiyo kwa kifupi.
Mfano: 2.) Mchague Mwana JF yeyote kati yao awe rafiki yako.
ni makosa kutumia neno yoyote kwenye mfano 2.) na vile vile yeyote kwa mfano 1.) hapo juu.
pia watu wengi hutumia maneno kama ambayo na ambaye kimakosa sana. yo hutumika kwa vitu. na ye huchukuwa nafasi ya mwanadam ama mara nyinge mnyama. mfano Nyumba ambayo nimemjengea Farasi ambaye alinisaidia nisiuawe na Majambazi ni tuzo kwake. nafikiri kwa mifano hiyo nitakuwa nimesaidia kidogo.

Ama kuhusu "dharura" na "dharula"
Dharura ndio neno sahihi na Dharula si neno la kiswahili.
 
Matumizi ya maneno....." aidha ........au " ni makosa. Linatumika sana.
neno "aidha" lina maana ya "vile vile, kadhalika nk..." Siyo Kiingereza either ...... or

Tutumie ..."ama........au"
 
Ni sentensi ipi ya kiswahili inahusisha maneno haya kwa usahihi katika matumizi?
Si...
Sio...
Siyo...
Ndio...
Ndo....
Ndiyo..
 
Je, kuna tofauti yeyote iloyopo katika matumizi sahii ya vilinganishi hivi katika sentensi

Kuzidi...
Kushinda...
Kuliko...
Kupita...
Zaidi ya...
Sawa na...
Kama...

Usahihi hapa ni upi?
Kamba hii ndefu ('kuzidi' 'kuliko' 'kushinda' 'sawa na' 'zaidi ya' ) ile.
 
Back
Top Bottom