Ha si wajua tena ukishakula chumvi nyingi, kila mtu wamwita mjukuu. Weye ulishasema ni mzee mwenzangu. Kwa hiyo heshima yako nakutumia.
Hii ipo sana TZ, na tutaendelea kuyaona. Kuna viongozi wa Dini waliowahi kusema kuwa JK ni chaguo la Mungu, na hio ilikuwa inamaanisha walikuwa wanaiunga mkono CCM na walio CCM.
cheap cheap cheap cheap... huyu sheikh anataka kuingia kwenye siasa na anatafuta njia rahisi ya kukubalika CCM (hajui bila fedha CCM huwezi kupata nafasi -- labda kama anazo).
Ni wakupuuza, mwandishi alipasa kuandika "Sheikh Mwaipopo apinga operesheni Sangara" lakini kwa kuwa ameshaandika then Baraza la waislamu ni busara likamkana na kuweka bayana kwamba wao na siasa ni kama moto na petrol na watoe 'press release' kwamba yeyote atakayejaribu kulitumia baraza hilo apuuzwe na asihusishwe na uislamu. Hii ndio dawa ya magenge kama haya hasa kipindi hiki cha kuelekea 2010 ambacho warafi wengi wasio na ushawishi watajaribu kutumia njia yoyote kutafuta uhalali kwa wananchi.
Wanapenda sana kudeal na minors, wakati mambo makubwa wanayaona na wanapita hawasemi
Na TZ tutaregret soon, kwa kuruhusu ujinga na upuuzi kama huu kwa watu wajinga wachache. Enzi hizo walikwua wakikusanyika wanapigwa mabomu ya machozi hawafikii hata kuongea, huyu handsome boy kaja na mambo yake ya kuwapa uhuru wa kuongea randomly wanaanza kuongea yasiyowahusu.
Elimu yenyewe wala haiitaji kuwaweka waandishi darasani bali kutoa "official Press Statement" kukemea watu hawa na kuelekeza vyombo vya habari kupuuza 'statement' za namna hii.
Jamani jamani, tuweke uTZ mbele. Hawa watu wengine ni wa kupuuza tu. Kuna wakristo na waislamu wenye udini lakini hautakiwi kuingia katika siasa kabisa. watu kama hawa ni wa kukimbiwa, tusiangalie alisema/aliyefanya kitu ni wa dini gani tuangalie ni kitu gani na manufaa yake.
Hapa wengi ni wazee wenzako, hivyo hilo la "wajukuu zangu' liweke pembeni.
Humu ukumbini; kuna wazee wenzangu, watoto zangu, na wajukuu zangu.
Wewe huko kundi la wajukuu zangu.
Sasa kwa nini utuite wote wajukuu?
Na unajuaje hakuna baba zako humu? Una umri gani wewe? Sijui, siwezi kuaza. Na wewe hujui, hutujui, hutakiwi kuaza kwamba wote humu wajukuu zako.
Turudi kwenye mada ya thread, matumizi sahihi ya lugha. Hizo nukta mbili (semi colon) za nini hapo uliposema "Humu ukumbini; kuna wazee wenzangu...."?
Acha hasira. Kichwa cha habari kiko mbioni kubadilishwa ili kikidhi haja ya mada hii.
Umri wangu ni mkubwa sana.
Sio wote ni wajukuu zangu. Kuna wazee wenzangu na watoto zangu humu.
Nimeweka hiyo koma yenye nukta juu, kutofautisha kati ya humu ukumbini (yapaswa fuatiwa na koma) na mtiririko wa wazee, watoto, na wajukuu. Vinginevyo ningechanganya kama ningeandika "Humu ukumbini"," kuna wazee wenzangu"," watoto zangu"," na wajukuu zangu."
Kwa hiyo unakubali kwamba umekosea kuaza kwamba wote humu wajukuu. Basi usiseme nina hasira. Wewe ndio umekosea!
Mkubwa sana kuliko nani, wote?
Mimi naweza kuwa baba yako? Sijui, hujui. Hivyo huwezi kuaza kwamba unaweza kutuita wote wajukuu humu.
Na labda baba zako! Hujui. Sijui. Huwezi kututia unavyotaka tu. Hususan kwa wewe mwenye kuzingatia matumizi sahihi ya lugha.
Sio kweli. Sio sahihi.
Ukitaka kusema "hapa uwanjani kuna wake na waume" utasema "hapa uwanjani; kuna wake na waume"? Ni makosa. Kama ambavyo huwezi kusema "hapa barazani; kuna viti na mikeka." Huhitaji michanganyo na mikorogo ya semi colons. Unatakiwa usema "hapa barazani kuna viti na mikeka."
Hivyo hivyo basi, ulitakiwa useme "humu ukumbini kuna wazee, watoto na wajukuu." Japo utakuwa umesahau uwezekano wa uwepo wa baba zako.
Hakuna nilichokosea.
Kutokana na umri nilionao, mvi na makunyanzi yalivyojaa usoni kwangu; (naitumia tena hii koma yanye kofia) ninalazimika kuona kuwa pengine mimi ni mzee kuliko wote humu.
Sasa kama unafikiri kuwa una umri wa kuwa baba yangu, basi niambie. Sitasita kukupa heshima yako kama mkubwa wangu.
Maridadi kabisa. Sina upingamizi na ufafanuzi wako...
Natoka kidogo kwenye mada, lakini zote ni lugha- shangaa na wewe..............
Who said English language was easy?
Fill in the blanks with either YES or NO:
1...........I dont have a brain.
2...........Im gay.
3...........Am so stupid.
Tuendelee na kiswahili, lol!
Humu ukumbini; kuna wazee wenzangu, watoto zangu, na wajukuu zangu.
Wewe huko kundi la wajukuu zangu.
Child named Adolf Hitler removed from home in New Jersey- Hanyimwa Keki ya Kuzariwa
Link: https://www.jamiiforums.com/interna...ome-new-jersey-hanyimwa-keki-ya-kuzariwa.html
Tafadhali usimuite Mhe Balozi wa Zain deiwaka. Alihusika kwa kiasi kikubwa katika uanzishwaji wa Photo Point. Amiliki au asimiliki hio siyo issue hapa JF. Nadhani unataka kuleta umbea wa kumtafuta mmiliki halisi wa photo point ili iweje. Maadam ulimsikia Michuzi akisema yeye ni mmiliki, naomba amini hivyo hivyo, waliokuambia yeye ni dei waka ni wanga.
Link: https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/23252-kumbe-michuzi-photopoint-sio-ya-kwake.html
...Alihusika kwa kiasi kikubwa katika uanzishwaji wa Photo Point. Amiliki au asimiliki hio siyo issue hapa
Pasco, yaani ulivyokuwa unaandika haya maneno hukuona kwamba hayajakaa sawa?
Ni Hamiliki ......Hasimiliki
Kha Pasco, yaani ulivyokuwa unaandika haya maneno hukuona kwamba hayajakaa sawa?
Ni Hamiliki ......Hasimiliki
Babu Swahili umechemsha vibaya mno!
Pasco yuko sahihi.
Babu Swahili, nakushauri rejea darasani. Tafuta ile Kamusi ya Kiswahili ya zamani iliyochapwa na Oxford University Press na kurudufiwa na Logmans itakusaidia, usiitegemee kamusi ya TUKI pekee itakuangusha.
Bw. Babu Swahili, nashukuru kwa uungwana wako. Ila sio mimi huyo kwenye nukuu ya pili hapo, sijui imekuwaje hapo.