SoC02 Matumizi mabaya ya Rasilimali Asili ni Chanzo cha Mabadiliko ya Tabianchi

SoC02 Matumizi mabaya ya Rasilimali Asili ni Chanzo cha Mabadiliko ya Tabianchi

Stories of Change - 2022 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Mazingira Duniani [“UN Environment Progromme –UNEP”] (Juni, 2022), athari za ongezeko la nyuzijoto 1.1 ziko hapa leo na zinaongezeka kwa kasi, hivyo kusababisha matukio mabaya ya hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na mawimbi ya joto, ukame, mafuriko, dhoruba za msimu wa baridi, vimbunga na mioto ya mwituni. Taarifa inaendelea kusema, joto la wastani ulimwenguni mwaka wa 2019 lilikuwa nyuzijoto 1.1, juu kuliko kipindi cha kabla ya viwanda, kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (“World Meteorological Organization – WMO”).

Kwa mujibu wa WMO, mwaka 2019 ilihitimisha muongo wa joto la kipekee ulimwenguni, kupungua kwa barafu na usawa wa bahari kutokana na gesi za ukaa zinazozalishwa na shughuli za binadamu. Wastani wa joto kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2019) na kipindi cha miaka kumi (2010-2019) ndio wa juu zaidi kuwahi kurekodiwa (WMO, 2019).

Asilimia 30 ya idadi ya watu ulimwenguni wanakabiliwa na mawimbi mabaya ya joto yanayotokea zaidi ya siku 20 kwa mwaka (UNEP, Juni 2022).

Uharibifu mazingira I.jpg

Ukataji magogo katika moja ya misitu Tanzania. Chanzo: Gazeti la Mwananchi, (Novemba 15, 2016)

Uharibifu mazingira.jpg


Uchomaji moto ndani baadhi ya misitu Tanzania. Chanzo: Dodoma FM Radio (Mei 24, 2021)

Makundi ya ardhi
Kwa mujibu wa Sheria za Ardhi Na. 4 na Na. 5 za mwaka 1999, na sheria nyingine zenye mguso katika ardhi, Ardhi imegawanyika katika makundi matatu ambayo ni:-

1. Ardhi ya kawaida/jumla: ni ardhi yote ya umma ambayo siyo ardhi ya hifadhi wala ardhi ya kijiji. Hata hivyo, kwa mujibu wa sheria ya ardhi Na.4, 1999 inajumuisha ardhi ya kijiji ambayo haikaliwi wala kutumiwa na wanavijiji. Kamishna wa ardhi ndiye msimamizi wa kundi hili la ardhi.

2. Ardhi ya Hifadhi: ni ardhi iliyotengwa kwa shughuli maalumu, kama vile hifadhi za misitu, barabara, vyanzo vya maji nk. Kundi hili liko chini ya usimamizi wa mamlaka mbalimbali za aina ya ardhi husika.

3. Ardhi ya Kijiji: hii ni ardhi iliyo ndani ya kijiji kilichosajiliwa na kubainishwa mipaka. Kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa (mamlaka za wilaya) ya mwaka 1982, inakuwa chini ya usimamizi wa halmashari ya kijiji. Pia ardhi ya kijiji ni ardhi iliyotengwa chini ya sheria ya uundwaji wa vijiji, 1965.

Migogoro inayotokana na Matumizi ya Rasilimali Asili
Migogoro mingi kuhusiana na matumizi ya rasilimali asili, mara nyingi hutatuliwa kupitia mifumo iliyopo ndani ya jamii, kama polisi, na maafisa maliasili, kwa kushirikiana na viongozi wa jamii katika eneo husika.

Pamoja na uwepo wa mifumo hii, bado maeneo mengi nchini kuna uharibifu mkubwa wa mazingira: uchomaji wa misitu, uchomaji wa mkaa, matumizi ya kuni katika viwanda vikubwa na vidogo, upanuzi wa kilimo, nk. Wakulima wengi hufanya kilimo cha kuhamahama kutokana na kutokuwa na elimu ya kurutubisha ardhi.

Ndio maana Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Stephan Ngailo, katika taarifa yake kwa mkuu wa mkoa wa Lindi (mnamo tarehe 11 Aprili, 2022), alisema ni muhimu wakulima wakahamasishwa juu ya matumizi sahihi ya mbolea, kusudi waepukane na kilimo cha kuhamahama.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mussa Mkilanya wa Buha FM Radio (17 Aprili, 2021), katika kikao maalum cha mpango kazi cha kutafuta ufumbuzi wa namna ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji; mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, alisema mkoa huo umepata changamoto za vifo vya mara kwa mara, watu kupata ulemavu na kuzorota kwa shughuli mbalimbali za maendeleo hali inayosababishwa na mapigano kati ya wakulima na wafugaji.

Mbali na kuwa chanzo cha migogoro inayopelekea maafa kwenye vijiji mbalimbali hapa Tanzania, wafugaji, wengi wao wakiwa ni wa makabila ya Masai na Wasukuma, huchangia katika uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa, kwani hufyeka miti na mifugo husababisha mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa vyanzo vya maji; pia huchoma moto mapori, kufukuza wanyama wakali. Hivi ndio husababisha migogoro mingi kati yao na wakulima, kiasi cha kusababisha vifo, ulemavu na madhara mengine.

Pamoja na ukweli kwamba kuna sheria na mifumo mizuri ya kulinda mazingira, uharibifu wa mazingira na migogoro baina ya wakulima na wafugaji bado vipo maeneo mbalimbali ya Tanzania; hii inachangiwa na mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali kuonekana kuwa na maslahi katika upande mmoja (hasa wa Wafugaji);

Ndio maana mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alinukuliwa katika kikao maalumu mkoani Pwani na Buha FM (17 Aprili, 2021) akisema, amebaini kuwa wapo baadhi ya viongozi wa serikali ambao wanachochea migogoro kati ya wakulima na wafugaji kwa sababu wana maslahi yao.

Wafugaji wa Tanzania..Aug 2022 Nipashe.jpg

Wafugaji wilayani Misungwi, Mwanza - Tanzania. Chanzo: Gazeti la Nipashe (Julai 21, 2017)

Nini cha Kufanya?
Serikali kuweka ruzuku katika nishati mbadala kama gesi, umeme wa jua, nk. ili wakazi wengi, hasa wa mijini wapunguze matumizi ya mkaa.

Kipekee, serikali isambaze kwa wakazi wengi gesi asilia ambayo ipo kwa wingi mkoani Mtwara. Hii itatumika badala ya kuni na mkaa, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa litapunguza hewa ya ukaa.

Serikali itoe ruzuku katika vifaa vya kubadilisha mfumo wa magari ya mafuta ya petrol/dizeli kwenda mfumo wa kutumia gesi. Mbali na kupunguza hewa ya ukaa kwa kiasi kikubwa, mpango huu utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za mafuta, na serikali itapata nafuu kubwa ya matumizi ya fedha za kigeni kuagiza mafuta nje ya nchi.

Serikali itenge maeneo maalum ya wafugaji na wakulima, ili kupunguza kama sii kumaliza kabisa migogoro kati yao; ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwawezesha wafugaji kufuga kisasa, na hivyo kuepukana na ufugaji wa kuhamahama.

Serikali kwa kushirikiana na nchi nyingine, iendelee kushawishi mataifa makubwa kutekeleza ahadi zao walizotoa katika makongamano mbalimbali kufadhili mikakati wa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.

Hitimisho
Kila mtu katika nafasi yake ana mchango katika harakati za kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.

Rejea

Mussa Mkilanya, Buha FM Radio (17 Aprili, 2021), Migogoro ya Ardhi, Wakulima na Wafugaji itazamwe upya.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania (2022), Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 - Matokeo Muhimu.

Shirila la Misaada la Marekani – USAID (Aprili, 2022,) “Natural Resource Management and Biodiversity Conservation”

Taarifa ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mbolea Tanzania (12 Aprili, 2022), Elimu ya matumizi ya mbolea kupunguza kilimo cha kuhamahama Lindi.

 
Upvote 9
Bro jaribu kufikiria uniqueness and differently mambo ya darasa la nne ayo
Asante sana Mkuu kwa maoni yako! Katika jukwaa hili hakuna kigezo cha kiwango cha elimu kilichowekwa kwa mshiriki yeyote; yamkini hujui kiwango changu cha elimu - pengine hata hilo la nne sina, ila najua kusoma na kuandika! Mawazo yoyote yenye nia njema, yanahitajika kwa umma bila kujali kwamba ni ya darasa la nne au ni ya chuo kikuu! Nathamini makala zote zinazotolewa katika jukwaa hili, bila kujali ni za kiwango gani cha elimu.

Natamani kusoma makala yako/zako, nitathamini, na kama nitakuwa na maoni, nitayatoa kwa mrengo chanya kwa faida yako na ya umma kwa ujumla!
 
Asante sana Mkuu kwa maoni yako! Katika jukwaa hili hakuna kigezo cha kiwango cha elimu kilichowekwa kwa mshiriki yeyote; yamkini hujui kiwango changu cha elimu - pengine hata hilo la nne sina, ila najua kusoma na kuandika! Mawazo yoyote yenye nia njema, yanahitajika kwa umma bila kujali kwamba ni ya darasa la nne au ni ya chuo kikuu! Nathamini makala zote zinazotolewa katika jukwaa hili, bila kujali ni za kiwango gani cha elimu.

Natamani kusoma makala yako/zako, nitathamini, na kama nitakuwa na maoni, nitayatoa kwa mrengo chanya kwa faida yako na ya umma kwa ujumla!
PERCEPTIONS then do as competition and tried to create and not to copy and paste
 
Matumizi ya nishati mbadala kama gesi asilia tulionayo, yatachangia pakubwa kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Hakuna haja ya kusubiri wafadhili kuja kufanya miujiza hapa wakati sisi tuna cha kuanzia!
 
Nishati mbadala inaweza kupatikana kila kaya. Vi'nyesi vya binadamu na wanyama vinaweza kutumika kuzalisha gesi ("bio gas") na ikatumika badala ya mkaa na kuni.
 
Napendekeza viwanda vinavyotumia miti kama nishati viwe katika kipaumbele cha kupata gesi asilia, ili kunusuru misitu yetu!
 
Misitu inafwekwa vijijini, kuchoma mkaa kwa ajili ya wakazi wa mijini. Gesi asilia ikisambazwa kwa wakazi wengi wa mijini, uchomaji mkaa .utapungua kwa zaidi ya asilimia 90!
 
Back
Top Bottom