Matumizi sahihi ya Dabo indiketa, gia L,2,3 na O/D katika gari za Automatic

Matumizi sahihi ya Dabo indiketa, gia L,2,3 na O/D katika gari za Automatic

Hakuna kitu kwenye gari kinaitwa 'dabo indiketa', nafikiri ulimaanisha HAZARD LIGHT, but YES, they are for emergency as the name describes. Waendesha magari wasio madereva huwasha kwenye njia panda wakidhani ni kiashiria cha kwenda moja kwa moja.
Wengi sana ambao hawajapita darasani au ambao hawakufanya jitihada kujifunza hudhani ni za kuonesha kuwa unaenda moja kwa moja kwenye njia panda
 
Dabo indiketa inashauriwa itumike wakati una dharula kubwa mf: Ajari au gari Mbovu maana lengo lake ni kuwataarifu madereva wenzako kuwa gari yako inatatizo so wapite kwa uangalifu zaidi lakin utakuta wengi wetu tunatumia visivyo mf; katika kupita njia panda au ukipaki pembezoni mwa barabara. Pia niongezee kuna ambao aki over take gari anawasha indiketa ya kulia (hiyo sawa kabisa ila sasa unapotaka kurudi upande wako wa kushoto hunahaja yak u indiketa tena unless kama kuna gari nyuma yako na iko jirani sana sio Hata uko pekee yako unawasha indiketa tu.

Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, 3 na O/D.
Kwanza ujue kabisa katika hali ya kawaida gari yako inapaswa kuwa katika D kwa maana ya Drive na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali yali ya hewa kama ni nzuri ila 2, 3 hutumika tu pale unapokuwa either unashuka au unapanda mlima/mteremuko mkali sana na mrefu mf sekenke na unataka ushuke au upande kwa speed ile ile ila isizidi 40/60 basi ndo unaruhusiwa kutumia 2, 3. Namba 2, 3 na L inamaana kuwa ina inalock gear box ili gear zisibadilike (-/+) kama ambavyo zinabadika ukiweka D na itambulike kuwa unaweza kubadili toka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe speed zaidi ya 40/60 maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani (disks) zilizomo ndani ya gearbox kufanya gazi nah ii upelekea ile hydrolic iliyomo kupata joto linalotoka katika zile sahani ambalo joto lile husababisha gear box kutokuwa na nguvu ile ile (constant velocity) na ndo maana ukiweka 2, 3 au L gear box inakuwa kwenye lock na sahani hazisuguani maana inakuwa inatumika sahani/disk moja tu kwa hiyo inasaidia ile hydrolick kupoa pia na ndo maana gari huongeza nguvu kwa ghafla. L inatumika pale unapokuwa either umekwama au unavuta gari jingine au tera ila inapaswa itumike kwa muda mfupi sana maana inanguvu sana na pia inaongeza ulajo wa mafuta, so kama ukiishatoka katika mkwamo na unaona bado barabara si nzuri labda utelezi au unavuta mzigo kwa mwendo mrefu basi unaweka 2 au 3 na wakati huohuo unaweza kuweka hata D kama hali ya njia na mzigo vinaruhusu na unaweza kuongeza walau speed 40/60 au zaidi kama utaweka D. kwa maana rahisi zaidi kwamba 2,3,na L inafanya kazi kama gari ya Manual nah ii inakuwa rahisi kwa yeyote ambaye anafahamu kuendesha manual.

Over Drive inatumika pale gari inapokuwa speed zaidi ya 60/80 kutegemeana na aina ya gari na hili hutokea bila wewe kujua maana gari yenyewe ndo inafanya nan do maana unashauriwa iwe on muda wote kusudi gari ichague ni wkati gani iweke on au of maana uukiwa chini ya 60/80 hata kama umeweka on bado inakuwa haifanyi kazi.
Cha mwisho ndugu zangu ni kwamba OD unaweza kuitumia kama break/stop engine hasa unapokuwa zaid ya 80 na wakati huo iko ON yaan katika dashboard taa ya OD izime ikiwaka maana yake iko OFF, basi ili upunguze mwenda kwa haraka unachofanya ni kuweka OFF na wakati huo unakanyaga break taratibu utaona mwenyewe gari lako linavyopunguza mwendo tartibu na wakati mwingine si lazima ukanyage break, we iweke OFF tu halafu toa mguu katika pedal ya mafuta gari lazima li slow down na kama lilikuwa ni tuta na umeliisha lipita basii iweke tena ON ongeza mafuta auu unaweza kuweka 2 au 3 ili gari ianze kwa kasi zaidi na ikiisha changanya basi rudi kwenye D na endelea kama kawaida.

Tahadhari: never ever kata kona wakati uko speed kubwa na gear namba tano (Kwa manual) au rpm iko 3000 Kwa automatic hii husababisha kupitiliza maana gari inakuwa nyepesi sana. Hakikisha ume slow down mpaka gia namba nne na break kidogo na Kwa autimatic either uweke 2 au 3 ila lazima weka OD off na break kidogo

Sijui kama ntakuwa nimeeleweka maana Kiswahili na lugha yetu ila mmh !
n
Asante kwa somo zuri... hasa kwenye matumizi ya 2,3 na L... be blessed!!!

Hongera sana
MHH SIDHANI KAMA HIYO QUOTE HAPO JUU NIMEKUELEWA. NIJUAVYO UKIBONYEZA OD BASI KWENYE DASHBOARD ITAONYESHA OD OFF, HII NI RETROSPECTIVE ALERT KWAMBA DO YOU WANT TO MAKE IT OFF? GARI YANGU MARA NIKIBONYEZA OD MLIO UNABADILIKA KIDOGO NA KITU KINACHOMOKA. BALAAA. EBU JARIBU KURUDIA KUSOMA SWALI LA MKUU. THANKS

Habari Maskin, hapana usitembelee gari ikiwa ktk 2 na OD isiwe off yaana taa ya dashboard izime maana inamadhara makubwa na pia mafuta hutumika sana. Si gari zote zina 3 hasa zenye injini ndogo 4 cylinders. Sina uhakika na madhara ya N as long as umepress button ya Ku release iliyoko ktk gia leaver then ndo uweke N maana kinachofanyika ni kwamba unakuwa umetenganiisha mzunguko wa injin na gear box yaan ni sawa na gari iliyo simama huku hujazima na uwe umeweka N (nutral), binafsi nasema haina madhara ktk disc madhara huwa kwamba, unashuka mteremuko na nutral (N) wether ni manual au Automatic gari huwa nyepesi sana na nirahisi kupata ajari na pia kuna chance kubwa ya vitu vingi Ku fail ila risk yake ni ndogo sana hasa kama unauhakika na ubora wa gari lako maana kuna ambazo ukiweka N inazima na unakuta kila kitu haki operate maana vinakuwa vinatumia upepo au hydrolick pressure sasa paata picha hapo huna breack, cluch wala gear haziingi. Kama unakuwa na mwendo mdogo ni sawa tu Ku N



alfredmkohiatgmaildotcom

Mkuu ukiona gari imekuandikia 'ECONO' maana yake ni economy, huwa inatokea pale ambapo kiwango cha mafuta kinachoingia kwenye injini ni kidogo kulinganisha na kiasi cha hewa kinachoingia kwa hiyo mafuta yanayotumika ni kidogo sana.Kifaa kinachofanya hiyo balance kinaitwa THROTTLE na kuna baadhi ya mafundi hukichezea kwenye baadhi ya magari ili ulaji wa mafuta upungue ila usijaribu kufanya huo mchezo ni hatari unaweza ukaharibu injini. Hali ya ECONOMY hutokea gari inapokuwa kati ya speed 60-90. Ni function ambayo ni common sana kwenye gari za CARINA

Fuatilia nyuzi kuna sehemu nimefafanua ila si kosa japo inaweza kusababisha ajari


alfredmkohiatgmaildotcom

Be blessed kaka

Hakuna kitu kwenye gari kinaitwa 'dabo indiketa', nafikiri ulimaanisha HAZARD LIGHT, but YES, they are for emergency as the name describes. Waendesha magari wasio madereva huwasha kwenye njia panda wakidhani ni kiashiria cha kwenda moja kwa moja.

Poa mkubwa, nimeelewa.

Asante kwa kuniulizia swali hilo. Ila mimi huwa sibonyezi hicho kitufe hivyo huwa hiyo taa haiwaki. Sijui kama huwa niko sahihi au la!

Mwana mtoka uu uzi ulikuwa katika Kiingereza na hata kwangu ilikuwa rahisi sana kuelezea ila kuna mdau ukiangalia ule wa kiingereza aliniomba niandike Kwa kiswahili ili uwe na manufaa Kwa sote na ndo maana hata ukiusoma bado utakuwa maneno mengi yamechakachuliwa hehehe

Kiswahili kigumu jamani, tukubali tu haza katika technologia




alfredmkohiatgmaildotcom

Wakina yakhee kama sisi tusiojua kuendesha kazi tunayo

Ukiisha weka D na ukaanza kuondoka na huna haraka na pia una budget ya mafuta basi hakikisha OD taa yake ktk dashboard imezima na rpm haizidi kwenye 2 (2000rpm) na inapotaka kuzidi au imezidi kidogo maana yake gia box inataka kuongeza gia mf toka 4 kwenda 5 au 3 kwenda 4 na kwa kawaida gia 4 na tano zinaongezeka/ingeji rpm inapofika 3 (3000rpm) ila kwa sababu unataka kusave mafuta na hautaki speed kubwa basi unachofanya ni kulegeza kwa mbali sana pedal ya mafuta kwa sekunde 1.5 au 2 hivi then unaongeza mafuta huku unaangalia rpm yako, matokeo yake gia itaongezeka na rpm itashuka chini ya 2 (2000rpm), hili linawezekana kwa gia kuanzia 3 hadi 5.

Bad news to fuel stations hahahaha...!!!

My next article will be on how to use "Air Conditioning" effectively...kaa mkao wa kula

Mkifata ushauri huu uhai wa gearbox zenu utakuwa mdogo sana.

Ukiona taa ya kijani imewaka na nino "ECONO" liasomeka maana yake ni kuwa hapo gari ya inatumia vizuri mafuta na neno linamaana "ECONOMICAL" wanafupisha tu. which means taa ikizima basi inamaana ulaji wa mafuta unaongezeka pia na hii kutokea hasa ukizidi RPM 3000 (RPM=Revolution Per Minute) inamaana mzungo wa injini ya gari kwa muda wa dakika moja

Sema inafaa kwa barabara ambayo hamna kusimama simama au kona kali..

Umenena vizuri, nadhani watanzania tuzidi kumuomba Mungu atuondolee hii roho ya kukosoa kosoa hata pasipositahiri ili muradi tu ukosoe, ni vizuri kusahihisha na kusaidiana

Ni vizuri muda wote unaendesha gari huku taa ya OD imezima, maana yake ni kuwa gear box itakuwa na uwezo wa ku ingage hadi namba tano au sita, lakini OD ikiwaka maana yake gari itakomea gear namba 4 tu ambapo ualaji wa mafuta utaongezeka lakini pia engine itapiga kelele sana hasa ukiwa speed kubwa na zaidi unaichosha engine

Hutakiwi kuwasha chochote, Hazard huwashwa unapokuwa na dharula tu hasa main road

Ukiweka L maana yake isibadiri gia zaidi ya namba 1, na siku zote namba 1 ndo gia yenye nguvu zaidi na ndo maana tunaitumia unapkuwa umekwama, lengo la kuweka L ni kuwa gear box isijibadirishe gia yenyewe automatically kwa kufuata RPM yake, maana kila gear ina ingia kutegemeana na mzunguko wa injini/RPM. Sasa hili linakuwa tatizo kama umekwama maana unataka gia namba moja itumike kwa nguvu zaidi ili utoke kwenye kwamo let's say wa umbali labda wa mita 100 au zaidi, ambapo ukiwe D basi unaweza kujikuta by the time RPM imefika 3000 uko gia namba 4 ambapo gari inakuwa nyepesi na haina uwezo wa kukutoa kwenye tope au mchanga.

4WD ina maana Four Wheels Drive au mengine huandikwa Full Time Four Wheels hasa kwa gari ndogo, hii inamaana muda wote inakuwa kwenye 4WD haihitaji kubonyeza chochote kwa kuiweka au kuitoa, yaana tairi zote nne zinazunguka kwa mzunguko mmoja na hii inakuwa imetengenezwa moja kwa moja toka kiwandani, uzuri wake zikuwa hazikwami hovyo hovyo na hazina usumbufu wa kuweka au kutoa 4WD, ni nzuri kwa akina mama au watoto hasa wa kike japo ulaji wake wa mafuta ni juu kidogo maana muda wote inakuwa nzito kuliko gari ambayo sio Full Time 4WD ila uzuri mwingine zinanguvu sana


Hapo unakosea. Inatakiwa kile kitaa cha o/d kizimike...
 
Back
Top Bottom