akohi
JF-Expert Member
- Jul 13, 2012
- 787
- 526
- Thread starter
- #81
Mkuu na kigari changu Auto kimeandikwa kina 4WD lkn sioni sehemu yoyote ya Ku activate. Always huwa nafikiri hiyo L ndo sehemu ya ku activate hiyo four wheel. Na hii nilipata nguvu baada ya kuiweka hiyo L na kuona garo haibadirishi via, iko constant kwenye gia Moja. Je nipo sahihi juu ya hilo?
Ukiweka L maana yake isibadiri gia zaidi ya namba 1, na siku zote namba 1 ndo gia yenye nguvu zaidi na ndo maana tunaitumia unapkuwa umekwama, lengo la kuweka L ni kuwa gear box isijibadirishe gia yenyewe automatically kwa kufuata RPM yake, maana kila gear ina ingia kutegemeana na mzunguko wa injini/RPM. Sasa hili linakuwa tatizo kama umekwama maana unataka gia namba moja itumike kwa nguvu zaidi ili utoke kwenye kwamo let's say wa umbali labda wa mita 100 au zaidi, ambapo ukiwe D basi unaweza kujikuta by the time RPM imefika 3000 uko gia namba 4 ambapo gari inakuwa nyepesi na haina uwezo wa kukutoa kwenye tope au mchanga.
4WD ina maana Four Wheels Drive au mengine huandikwa Full Time Four Wheels hasa kwa gari ndogo, hii inamaana muda wote inakuwa kwenye 4WD haihitaji kubonyeza chochote kwa kuiweka au kuitoa, yaana tairi zote nne zinazunguka kwa mzunguko mmoja na hii inakuwa imetengenezwa moja kwa moja toka kiwandani, uzuri wake zikuwa hazikwami hovyo hovyo na hazina usumbufu wa kuweka au kutoa 4WD, ni nzuri kwa akina mama au watoto hasa wa kike japo ulaji wake wa mafuta ni juu kidogo maana muda wote inakuwa nzito kuliko gari ambayo sio Full Time 4WD ila uzuri mwingine zinanguvu sana