Matumizi ya asali, tango na limao

Matumizi ya asali, tango na limao

Inasemekana ni asali ya nyuki wadogo je ww umetumia asali gan? Kama nyuki wadogo R.I.P
 
Si kweli tena kuna faida nyingi kiafya kunywa mchanganyiko wa asali majiya moto na maji ya limao wakati wa asubuhi unapoamka kabla ya kula ama kunywa chochote.

Miongoni mwa faida zake ni kama ifuatavyo;

-husaidia kupunguza uzito wa mwili bila ya madhara yoyote mwilini.

-Usaidia kuimarisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na kuongeza ufanisi wake.

-Kuimarisha mfumo wa upumuaji

-kuondoa harufu mbaya mdomoni.


-kusafisha kibofu cha mkojo.

-ulisaidia ini kuzalisha nyongo(bile) kwa wingi inayosaidia katika usagaji wa chakula.

-usaidia kusawazisha kiwango cha uasidi na ualikalaini katika damu na kufanya damu kuwa na kiasi kikubwa kidogo cha base kuliko acid jambo ambalo lina faida kwa mwili kwani huzifanya seli za damu kufanya kazi vizuri.


hivyo nakushauri usiache kunywa huo mchanganyiko kwa faida ya afya yako.
 
Mzee nakuona ona nyuma ya "kemera" nowadays, unataka ingia kwenye "tasnia"yetu? Kwanza nitwangie simu, kitambo sana baba swalehe! Teh
Baba Swalehe acha mbwembwe. Hiyo ni tasnia yangu long tu ila huwa naisusa. Maslahi yake makavu. Hebu nipatie namba yako nkupigie.
 
Inasemekana ni asali ya nyuki wadogo je ww umetumia asali gan? Kama nyuki wadogo R.I.P
Acha kumtisha ndugu hakuna kitu kama hicho.

unajuaje hii ni asali ya nyuki wadogo na hii ni ya nyuki wakubwa?.
 
Hufi bhana kuna Kinyaji cha Hot Lemon, honey n ginger watu si wangedanja!!!
 
Me nilisikia tango na asali ndo ukichanganya unaweza kufa. Hiyo limao na asali nimetumia wanasema dawa ya mafua
 
Ule asali usile asali uchanganye usichanganye utakufa tu maana hakuna namna. Ila hatujui Siku SAA mahala ila ni swala LA mda tu.
 
Hizi stori nimekuwa nikizisikia tangu primary. Zina ukweli wowote au stori za vijiweni. Nisaidieni wazee manake leo nimejisahau. Niliweka asali kwenye mkate nikagonga na chao iliyochanganywa na limao. Si unajua nina mafua.
Wewe sasa ndio unatakiwa utupatie jibu, maana umeshakula asali na limao. Sasa unauliza nini tena? Subiria kidogo, kama hautakufa utakuwa umeshapata jibu la swali lako, na kama ukifa, vivyo hivyo.
 
Dawwa yangu kubwa ya flu ni limao na asali, kila wakati acheni uzushi nyiye
 
Hizi stori nimekuwa nikizisikia tangu primary. Zina ukweli wowote au stori za vijiweni. Nisaidieni wazee manake leo nimejisahau. Niliweka asali kwenye mkate nikagonga na chao iliyochanganywa na limao. Si unajua nina mafua. ASALI NA TANGO siyo limao mkuu
 
Ndugu yangu, kwanza nakupa pole kwa kujazwa woga.

Lakini pia leo ujue kuwa hakuna juice tamu duniani kama ya mchanganyiko wa limau na asali.

Hata mie nilikuwa naamini hvyo ila wakati nimedhamiria kuacha pombe ndo kilikuwa kinywaji changu. Ni juisi tamu sana.

Robo lita ya limau+vijiko 5 vya asali+ sukari vijiko 3. Utaenjoy sana.
 
Back
Top Bottom