Matumizi ya Bendera ya Taifa kwenye makazi binafsi

Matumizi ya Bendera ya Taifa kwenye makazi binafsi

Ulongupanjala

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
8,273
Reaction score
13,567
Happy Saba saba day!

Niende kwenye mada,Watanzania tuna bendera yetu ya taifa,na nimeona watanzania wengi wakiweka bendera za taifa kwenye magari yao,makanisa yao,ofisi zao nk na wengine kupewa bendera wanapoenda nje ya nchi hasa wasanii.

Nauliza je ninaweza kuweka mlingoti wenye bendera ya taifa nyumbani kwangu?
Naomba wenye uelewa waje kunipa mwongozo.

Asanteni.
 
Hiyo haina tatizo weka tu Tena ile kubwa jion unaishusha na asubuhi unaipandisha tena ila usisahau kutuletea mlejesho kwa yale yatakayokupata
Aiem ze fest tudei where u josefu evarist
Happy Saba saba day!
Niende kwenye mada,Watanzania tuna bendera yetu ya taifa,na nimeona watanzania wengi wakiweka bendera za taifa kwenye magari yao,makanisa yao,ofisi zao nk na wengine kupewa bendera wanapoenda nje ya nchi hasa wasanii.

Nauliza je ninaweza kuweka mlingoti wenye bendera ya taifa nyumbani kwangu?
Naomba wenye uelewa waje kunipa mwongozo.

Asanteni.
 
yeah why not,weka tena kama ulivyoambiwa ile kubwa,be a proudy Tanzanian,jivunie maana bendera yetu ya taifa ni moja ya vitambulisho vyetu,ikibidi hata cushions zako ziwe na rangi ya bendera yetu,ila heshimu pls usipigie deki,usikanyagie etc etc
 
Happy Saba saba day!
Niende kwenye mada,Watanzania tuna bendera yetu ya taifa,na nimeona watanzania wengi wakiweka bendera za taifa kwenye magari yao,makanisa yao,ofisi zao nk na wengine kupewa bendera wanapoenda nje ya nchi hasa wasanii.

Nauliza je ninaweza kuweka mlingoti wenye bendera ya taifa nyumbani kwangu?
Naomba wenye uelewa waje kunipa mwongozo.

Asanteni.
JK wakati anaingia madarakani alisema hata mtu akishona nguo yenye rangi ya bendera ya Taifa la Tz haina shida hata ukipamba kwako alifanya hivyo ili tuwe wazalendo
 
Bendera ni nembo ya taifa inapaswa kupepea kwenye ofisi maalum zinazotambulika na serikali..kuna taratibu pia za kufuata..
 
Una uhuru wa kufanya utakalo ndani ya sheria.

Binafsi naishi kwenye nchi ya watu wanaoisujudia bendera yao sijapata kuona (Marekani).
Lakini sijaingiwa na wazimu wa kupeperusha bendera ya Tanzania wala Marekani.

Kuna Bibie mmoja Muingereza alikuja kutembea Marekani akawa anasema "Wamarekani nawashangaa sana jinsi wanavyopewa chakulakingi hotelini, na kinywaji hawalipii kwa glasi ila ukimaliza unajaziwa tena, halafu na bendera, kila sehemu bendera bendera bendera tuu"

Nikaona kumbe tusioelewa kuwehuka na bendera ni wengi.

Lakini wao angalau wamefundishwa "American exceptionalism" na wanaona nchi yao kama mbingu fulani ya uhuru, na ukishakunywa maji hayo utaona bendera yako nikama dhahabu.

Kwetu sasa naona kuna watu wananyweshwa maji hayo na kuanza kukubali exceptionalism ambayo hata haipo.

Binafsi sifagilii bendera, ukielewa historia za bendera na zilivyoua watu katika vita za uzalendo wa kijinga, huwezi kufagilia habari za bendera.

Pia, I am toomuch of a freethinker to tie myself to a schedule around a flag.

Kujipa kazi kila siku saa kumi na mbili asubuhi na jioni uwe nyumbani kupandisha na kushusha bendera ya nini?
 
Ni Kosa Kupeperusha Bendera Ya Taifa Nyumbani Kwako Isipokuwa Inatakiwa Majengo Yote Ya Umma Ndiyo Huruhusiwa Kupeperusha Bendera Saa 12 Asubuhi Na Kuishusha Saa 12 Jioni

Ukipeperusha Nyumbani Kwako Ni Kosa Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Usalama Wa Taifa.
 
Kwenye nchi za wenzetu hili la kuweka bendera ya Taifa tena kubwa tu ni jambo la kawaida sana na hakuna atakayekusumbua lakini hapa nchini nina wasiwasi unaweza kuishia lupango. Uliza kwanza kama unaruhusiwa kufanya hivyo.
 
Ni Kosa Kupeperusha Bendera Ya Taifa Nyumbani Kwako Isipokuwa Inatakiwa Majengo Yote Ya Umma Ndiyo Huruhusiwa Kupeperusha Bendera Saa 12 Asubuhi Na Kuishusha Saa 12 Jioni

Ukipeperusha Nyumbani Kwako Ni Kosa Kwa Mujibu Wa Sheria Ya Usalama Wa Taifa.
Weka vifungu mkuu.
 
Unaweka!ila hapo nyumbani kwako kuna shughuli gani inayo litambulisha taifa?
 
Back
Top Bottom