Matumizi ya Bendera ya Taifa kwenye makazi binafsi

Matumizi ya Bendera ya Taifa kwenye makazi binafsi

Imenikumbusha miaka ya nyuma (1994) nilikuwa maeneo ya Kinondoni karibu na Mahakama (ilipo Tumaini Univ kwa sasa). Ilikuwa mida ya saa 12 jioni...muda rasmi wa kushusha bendera ya Taifa.

Ikapigwa filimbi tukasimama (tuliokuwa karibu na eneo la bendera). Kuna jamaa mmoja sijui ni kutokujua taratibu au makusudi/haraka yeye aliendelea kutembea.

Kilichotokea hapo sitakisahau na mpaka leo hii kilinifanya niithamini na kuiheshimu Bendera ya Taifa.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Allegiance to the flag....uzalendo huo ila tafuta taarifa sahihi za kuipeperusha hapo kwako.
 
Kwenye nchi za wenzetu hili la kuweka bendera ya Taifa tena kubwa tu ni jambo la kawaida sana na hakuna atakayekusumbua lakini hapa nchini nina wasiwasi unaweza kuishia lupango. Uliza kwanza kama unaruhusiwa kufanya hivyo.
[HASHTAG]#FreeHalimaMdee[/HASHTAG]
 
Natumaini wazima wa hali.

Jambo lenyewe ndo hilo nalotaka kulifanya sio kwamba nimekosa kazi ya kufanya hapana, ni maamuzi yangu binafsi.

Nataka niweke iwe inapepea nje? Jinsi gani? Nakupenda Nchi ya Yangu Tanzania, Msaada nifate vigezo gani?
 
Natumaini wazima wa hali.

Jambo lenyewe ndo hilo nalotaka kulifanya sio kwamba nimekosa kazi ya kufanya hapana, ni maamuzi yangu binafsi.

Nataka niweke iwe inapepea nje? Jinsi gani? Nakupenda Nchi ya Yangu Tanzania, Msaada nifate vigezo gani?
Hiyo sio mali binafsi kwahiyo huwezi kuimiliki
 
Kama nyumba yako ni jengo la serikali utatumia ule mlingoti mrefu wa bendera ila kama ni makazi ya kawaida utaweka kama wanaoziweka bendera za vyama wakati wa kampeni
 
Kuipenda Tz ni pamoja na kuwafukuza fisiemu madarakani, anza na hilo kabla ya kiweka bendera kwako
 
Paka nyumba yako rangi za bendera ya taifa hakuna atakae kusumbua
 
Back
Top Bottom