SoC04 Matumizi ya Bio gesi kama nishati safi ya kupikia yenye gharama nafuu na pia kama njia ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi

SoC04 Matumizi ya Bio gesi kama nishati safi ya kupikia yenye gharama nafuu na pia kama njia ya kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

HARUNI IDDI

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
8
Reaction score
3
Bio gesi ni nishati ambayo hutengezwa kwa kutumia kinyesi cha wanyama kama vile ngombe, mbuzi na kondoo, na wanyama wengine ambao ni wakufugwa,pia huzalishwa baada ya kuoza kwa mbolea ya wanyama au taka za kikaboni.
Screenshot_20240601-233233_1.jpg

Picha Baraza la usimamizi wa mazingira
(NEMC).​

Nishati hii inaweza kutumika kama njia Moja wapo ya kuhakikisha jamii ya kitanzania ina pata nishati safi ya kupikia ambayo ni rafiki kwa mazingira na ni ya gharama nafuu the zaidi kwani upatikanaji wake siyo mgumu kwani Tanzania ni miongoni mwanchi zenye idadi kubwa ya mifugo ikizidiwa na Ethiopia hivyo upatikanaji wa malighafi upo kwa wingi zaidi katika mikoa kama morogoro, mwanza, manyara, arusha, na Kilimanjaro na pia kwenye mikoa kama rukwa, iringa n.k.

Serekali ya awamu ya sita imejipambanua katika Matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza Matumizi ya Kuni, mikaa, na rasilimali nyinginezo kama makaa ya mawe ambazo huaribu uoto wa asili na kuleta madhara hasi kwenye mazingira kama kupelekea ukame,mafuriko, na mmomonyoko wa udongo.

Matumizi ya biogesi kama njia Moja wapo ya kulifikisha taifa katika mpango wa Matumizi ya nishati safi ya kupikia katika miaka ijayo kutokana na sababu zifuatazo;

Upatikanaji wa malighafi za biogesi; kutokana na kuwepo kwa malighafi ambazo ni nyepesi kupatikana katika mazingira ambayo ni kinyesi cha wanyama kama ngombe, mbuzi serakali kupitia wadau na taasisi zinanzohusika zinapaswa kuweka mkazo kwenye Matumizi ya biogesi kwani ni rafiki wa mazingira.

Nishati hii haina gharama kubwa: gharama za kutengeneza mtambo wa biogesi ni nafuu zaidi pia, gharama za kununua malighafi za kuendeasha mtambo wa biogesi ni bei nafuu zaidi kulinganisha na Matumizi ya gesi asilia, mafuta ya taa, Matumizi ya umeme.

Nishati hii ni rafiki kwa mazingira; kutokana na kuto chafua mazingira kama Matumizi Kuni au mkaa hivyo husaidia katika kuepusha madhara yanayo letwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Kwa namna nyingine biogesi kama nishati safi ya kupikia pia inaweza kutumika kama njia Moja wapo ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwani itasaidia wananchi wa Tanzania hasa wale wanaishi katika mazingira ya vijijini na jamii za kifugaji kama vile jamii za kisukuma, kimasai, baribai, na jamii nyingine za kifugaji kwani upatikanaji wa malighafi ni rahisi zaidi.

Matumizi ya biogesi kama nishati safi ya kupikia pia inaweza kutumika kama njia ya kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi kwani itapunguza ukataji wa miti hovyo kama sehemu ya kupata nishati ya kupikia kwa kutumia Kuni na mkaa.

Screenshot_20240601-233801_1.jpg

Picha kwa msaada wa mtandao​

Kutaweza kupunguza mmomonyoko wa udongo, uchafu wa anga kutokana Moshi wa kuni na mkaa ambao hupelekea kuharibu utandaa wa ozone na kupelekea kuongezeka kwa joto Katika uso wadunia,


Screenshot_20240601-233829_1.jpg

Picha kwa msaada wa mtandao​
Maporomoko ya matope kwenye milima kama ilivyo tokea katika wilaya ya hanangi, na mkoani mbeya ambapo kulikuwa na maporomoko ya matope kutoka kwenye milima kutokana na shughuli za kibinadamu kama uchomaji mkaa.

Nishati hii pia hulinda ekolojia na kusaidia kupunguza ukame na upotevu wa uoto wa asili kwani watanzania hasa wale ambao wanaishi vijijini kuachana na kukata miti hovyo kama sehemu ya kupata nishati ya kupikia, kwa maeneo ya mjini wananchi wanaweza kutumia nishati mbadala kama gesi asilia, joto la ardhini, umeme, joto la Jua n.k.

Screenshot_20240601-233330_1.jpg

Picha Baraza la usimamizi wa mazingira
(NEMC)​
Katika miaka mitano ijayo nakuendelea Tanzania tuitakayo jamii inapaswa kutumia nishati safi ya kupikia ambayo ni rafiki kwa mazingira ambayo ni biogesi kwani Ina faida mbalimbali hivyo serekali ipasa kuweka mkazo kwa nishati hii kama mkakati moja wapo kufikia malengo ya nchi kupata nishati safi ya kupikia.
 

Attachments

  • Screenshot_20240601-233829_1.jpg
    Screenshot_20240601-233829_1.jpg
    160.6 KB · Views: 4
Upvote 1
Back
Top Bottom