Matumizi ya CCTV camera Tanzania na uvunjifu wa haki ya faragha

Utakuja kupinga hata Camera za mtaani ni maendeleo hayo na kuwa na ulinzi kwa mfumo wa kisasa nimedokezwa pia ndege nyingi zimefungwa Camera kwenye vyoo ila abiria hawezi kuiona hiyo inatoka na mambo ya Ugaidi kuenea kwa kasi...
sipingi tunataka sheria ambayo itataja maeneo ambayo hizo camera zinatakiwa kufungwa siyo kila mtu anafunga anavyo jisikia.
 
 
sawa zimefungwa kwenye coridor unajua baada ya hizo kurekodiwa hakuna mtu anayejua hizo taarifa zinapelekwa wapi na zinahifadhiwa kwa mda gani Tunataka sheria ambayo itatupa muongozo.
watenda maovu mna shida. Kwani hizo taarifa zikihifadhiwa kuna shida gani.
 
lazima tujue zinahifadhiwa kwa njia ipi na mtu akiziitaji utaratibu gani aweze kufuaata ambao umewekwa kisheria.
 
Ukifika nyumba za wageni shusha mapazia zima taa ili pawe gizaa kabisa afu washa camera ya simu bila flash light anza kuzunguka chumba kama una shoot video kama kuna kamera imewekwa itaonekana kwa mbali kama mwale mwekundu kwenye kioo cha simu yako๐Ÿ˜
 
Kama sio sheria lakini kanuni ipo nayo ni kuweka tangazo la kuonyesha kuwa eneo hilo lipo chini ya uangalizi wa CCTV camera.Bank wanaogopa wezi lakini bado wameweka matangazo hayo ambapo kwa akili ya kawaida unaweza waza "kwa nini wamstue mwizi?"
 
m'bongo mpe picha tu maelezo atatoa yeye,๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
CCTV zinasaidia Sana Kwenye ishu za ulinzi na usalama.
Ambapo Mara nyingi zinawekwa sehemu za wazi Kama magetini, mapokezi, counter, na Kwenye korido,Kwenye fensi za nyumba.
Ila tatizo siku hizi kuna watu wanaweka hidden camera maeneo ya hadi vyumbani
 
sawa zimefungwa kwenye coridor unajua baada ya hizo kurekodiwa hakuna mtu anayejua hizo taarifa zinapelekwa wapi na zinahifadhiwa kwa mda gani Tunataka sheria ambayo itatupa muongozo.
Labda ndiyo ile ya PM
 
tunataka kuwepo na sheria ambayo itatoa taratibu na adhabu kwa mtu atakaye funga camera na kuzitumia kinyuma na matakwa ya sheria.
Kama kawaida. Watanzania ni wepesi wa kupinga bila kutafakari. Wengi hawaoni implication ya watu kujifungia kamera holela tu. Wanatoa majibu mepesi. Hii ni kwa sababu hawataki kutafakari. Nchi zilizoendelea zina kamera kibao lakini kuna sheria na kanuni zinasimamia ufungaji na kuhifadhi na kuangalia kilichorikodiwa. Wengi wanadhani umetaka serikali ipige marufuku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ