Matumizi ya connect za Upwork

#Mrejesho.

Aisee Nilimaliza Kazi zote Salama. Nimekabithi Kwa Boss Kwenye UPWORK . Mimi nilifanya Kutoa Pesa Kupitia Kwa bank Direct Nilikatwa $30 withdrawal fees. Hela Ilifika ndani Ya Siku Tatu.

Mteja, aliacha review Kali Sana na Ndefu Ivi ya 5 Stars. Ila Mwingine Kimya lakini aliacha Ile contract Open.

Mzungu Kutoka Uswizi (Client) alinipigia kuniuliza Tanzania ilipo. Aka Gugo akaona Vitu vilivyopo akanipigia Tena Simu Na Akasema Atakuja Kutembelea akasema ni Pazuri. Tuzidi Kuombena.

Kwa Sasa, natafuta Kazi za $150, $350 kwenda Juu Pekee. Sijapata kazi Mpya tenaa mpka Sasa.. Naendelea na Mapambano.

Vijana wenzangu Kupata Pesa Kupitia Mtandao inawezekana jifunzeni na Mchangamkie Fursa.

Good luck 👋
 
Ili kuweza kutuma pesa kutoka payoneer lazima uwe umepokea kuanzia dola 5000 na kutuma ni bure Payoneer to Payoneer. Pia ukishawithdraw mara kadhaa inachukua masaa 24 pekee kutoka Payoneer kuja kwenye bank yako hivyo haina umuhimu sana wa kutumia skrill kisha utume kwenye safaricom kuna makato then uje utoe tena safaricom uzishike mkononi ni mchakato mrefu.
 
Kutuma peaa from mastercard to safaricom makato yaliyopo ya FX ila skrill hawana charges.
Payoneer mimi naweza mtumia mtu mwingine wa payoneer to payoneer sema kwa kuwithdraw pesa ndogo ndogo kwenye payoneer to skrill to safaricom ni saf kabisa
 
Mliopo Upwork ama freelancing platforms zingine please usikate tamaa ni mchakato muhimu ni kuendelea kujifunza. Upwork huwa wanatoaga webinars zao mara kwa mara almost kila mwezi mara 2 so jiunge utajifunza kitu.

1. Namna ya kuandika winning proposals

2.Negotiation skills

3. kuweka vizuri profile yako search freelancers wengine wanaofanya kazi kama zako ona wameandikaje, jifunze kwao.

4. Ukipata muda tengeneza portifolio projects

5. Kama shughuli zako huwa unakaa ofisini na unatumia Internet hakikisha umelogin kwenye Upwork account yako, hii itasaidia algorithm kukutambua na kupata kipaombele kwenye kupata invitations.

6. Omba kazi kwa umakini ukiona proposals ni nyingi mfano 20-50 na kuna ambao wanetumiwa invitations proposals achana nayo.

7. Mvumilivu ndio msingi ukishafanya kazi nyingi kuanzia 50+ itafika mahali clients wa zamani wanakutafutia kazi mpya ama kukuunganisha na wateja wapya hivyo kufanya wewe usiombe tena kazi.
Kufikia hiyo hatua sio mchezo muhimu ni kuendelea kujifunza by the way bahati pia zinahusika[emoji1241][emoji1241].

8. Upwork kuna option ya kujiunga na freelancers wengine unamtumia request kumuomba . Ukipata marafiki mnashare changamoto na kupeana moyo hivyo kuendelea kuomba.

9. Tricks ni nyingi muhimu kuendelea kuwa active na kujiunga na platforms zingine hata Facebook na LinkedIn kuna madili ya Kazi usistick sehemu moja be flexible and
 
Safi

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Soka La Juu Sana. Pamoja Sana.
 
👏👏👏👏👏👏👏👏👏
 
kuna kazi nimepata hapo ni ngumu kuliko nilivotegemea
client anataka link za video za kibena zaidi ya masaa 500( Yaani total length ya video zote ziwe masaa 500) hapo hawahitaji nyimbo za asili wala ngoma!!
 
kuna kazi nimepata hapo ni ngumu kuliko nilivotegemea
client anataka link za video za kibena zaidi ya masaa 500( Yaani total length ya video zote ziwe masaa 500) hapo hawahitaji nyimbo za asili wala ngoma!!
Aisee ni Noma
 
Naomba elimu. UPWORK ni nini hasa. Inafanyaje kazi?
 
Nilijiunga kwenye hizo platforms zote na kufungua account payoneer lakini baada ya muda nikasahau kabisa uwepo wake.
 
Ndugu Yangu Tembelea Kuna Nyuzi Wadau Walileta Humu Zipo Zina Elimu ya Ufanyaji Kazi.
Kwa jibu hili wala sitothubutuhata kuiwazia hiyo bizness yenyewe.

Nakomaa na genge langu la nyanya. Lazima mtakuja tu kununua fungu la dagaa mtake msitake
 
Kwa jibu hili wala sitothubutuhata kuiwazia hiyo bizness yenyewe.

Nakomaa na genge langu la nyanya. Lazima mtakuja tu kununua fungu la dagaa mtake msitake
Hyo Ni kitu Cha Ziada Tu Cha Kutengeneza Pesa Sio Cha Kutegemea.
 
Mnafanyaje KU-Verify account zenu Upwork? Vitambulisho gani mnatumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…