Mnafanyaje KU-Verify account zenu Upwork? Vitambulisho gani mnatumia.
Kweli mbongo ni mbongo
Mbongo kumwelekeza mbongo mwenzie hususani linapokuja swala la umate mate na chapaa anakua mzito saaaana ni wachache saaana wenye mioyo ya kukunjua roho na kuachia pumzi yao iseme ila wengi wao wanapenda kukunja roho wanachohitaji ujipambanie wewe kivyako usipende mseleleko, ukumbane na changamoto na ujifunze mwenyewe usijifunze kupitia wao ili hata km yakikukuta makuu usipate mtu wa kumlaumu kwamba huyu ndie alienisababishia haya yote
Ingia Google andika upwork zitakuja link zaidi ya million za wazungu waliokunjua roho wanaelezea mchongo unavyokua
Ingia YouTube andika upwork utakutana na video zaidi ya million za wazungu wenye roho safi wameelezea step by step
Ukikwama rudi tena Google rudia tena YouTube
Ukikwama rudi Google rudia tena ingia YouTube soma jifunze kwa watu tofauti sio mtu mmoja jifunze kwa hatua kila unapokwama jifunze tena chukua makala km kuna vitabu chukua soma, pdf chukua soma
Kuna wabongo km wawili nilikua nawafuatilia YouTube nilifuatiliaga video zao nikafungua hadi account upwork ila kuna step baadhi nilikwama nikakosa wa kumuuliza nikaachana nayo mpaka leo
Sababu kuna vitu hua hawakuambii wabongo wanapenda sana kuficha 'source code' inabidi ufukue mwenyewe ujue nini na nini ni sahihi na nini na nini sio sahihi
Yaan hapo mpaka umejua ni nini ushapata hasara angalau ushaingia gharama ya muda na pesa pia, wakati mzoefu wa muda mrefu angekwambia tu hapa fanya hivi pale fanya vile kile weka pale hiki usiweke kule kile ondoa pale na pale usiguse kile usikifanye vile na kile mpe yule hiki fanya hivi boom dollars hizi hapa