Matumizi ya Dawa za kuongeza uchungu Kanda ya Ziwa ni janga kwa Wajawazito wengi
Baada ya kusikia hizi stori kwa muda, nikaamua kuingia mitaani kufuatilia kinachoendelea hasa maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa (vijijini hasa pembezoni mwa miji na visiwani).
Mtaani kuna stori kuwa kuna madhara yatokanayo na matumizi ya Dawa za Kienyeji na kuhusu jitihada zinazoendelea kuhusu kuelimisha Jamii juu ya ufahamu wa matumizi ya dawa hizo.
Dawa ninazozingumzia hapa ni zile za kuongeza uchungu ambazo zinatumiwa na Wajawazito kwa lengo la kujifungua haraka.
Dawa hizo zinatumika kwa kuchemsha na kuhifadhiwa kwenye chupa za chai au kwenye chupa za kuhifadhi vinywaji ama kutafunwa.
Nimefanya mazungumzo na Wanawake kadhaa ambapo wanaeleza sababu za kutumia dawa hizo (majina yaliyotumika sio halisi):
Mama Ali wa Sengerema anasema yeye ana mtoto mmoja, anaeleza Wanawake wengi wanashauriana kutumia dawa hizo ili kuogopa mtoto kuzaliwa kabla ya wakati, pia wanaamini inamlinda pindi akijifungua, pia hapotezi muda mwingi wa kukaa hospitalini.
Mmoja wa wajawazito kutoka Kisiwa Juma amesema ana ujauzito wa miezi 5 lakini ana imani zitamsaidia dawa hizo za kienyeji kwani hajui madhara yoyoye, anadai ameshuhudia wakubwa zake wengi tu wanajifungua salama kwa msaada wa watu waliowamzidi umri wa eneo hilo
Mama Jumaa anasema kwa miaka mingi dawa hizo zimetumika na bibi zetu na mama zetu na wanaziamini wanapunguza gharama ya usafiri na kununua vifaa vinavyohitajika wanapoenda hospitali kujifungua, anasisitiza kuwa hata yeye ameona faida ya dawa hizo na hajui kama kuna athari kutokana na yeye kutimiza nzao 7 (watoto wake 7) na mpango wake ni kuendelea.
Monika ambaye ni Bibi wa 65, kutoka Nyankumbu Geita amesema kukaa hospitalini kwa muda mrefu kuna gharama, ni bora wawatumie kinabibi wa vijiji wawape dawa hizo kwasababu wananunua kwa gharama ndogo sana kuanzia Sh. 1000 na kuendelea.
Anaeleza kuwa kuna nyingine zinapatikana katika maeneo wanayoishi kama vile mashambani, porini hata masokoni na baadhi ya dawa hizo ni mnyonyo, Mizizi ya Mgagani, mlongelonge, binzari nyembamba ambapo maelekezo yake ni ni kuchemsha kama chai na unakunywa mpaka utakapofanikiwa.
Wataalamu wanaosimamia Kitengo cha uuguzi wanabainisha:
Tatizo hilo ni kubwa sana kwenye jamii kutokana na baadhi ya Wajawazito kujifungua watoto wenye migongo wazi na viungo kutokamilika lakini kuna wengine utumbo unakuwa nje.
Baadhi ya Watoto inadaiwa wamekuwa wakipoteza Maisha kutokana na changamoto hizo na wengine kulazimika kupata matibabu katika Hospitali kubwa za Rufaa ikiwemo Bugando.
Imeeleza kuwa watumiaji wamekuwa wanaathirika Kisaikolojia kutokana kupitia changamoto hiyo.
Imeshauriwa wajawazito wafike kliniki mapema wakati wanapokuwa na Ujamzito chini ya wiki 12 na sio kutumia hizo dawa.
Kutokana na hayo baadhi ya wananchi wameeleza madhara waliyoyapata baada ya kutumia dawa hizo:
1. John Emiry Mmoja wa wananchi eneo la Usagara ameeleza alishapoteza mama yake mkubwa kutokana na matumizi ya dawa hizo lakini aliacha watoto mapacha
Ameeleza siku ya kujifungua kabla ya kwenda hospitali alikunywa dawa hizo zilizohifadhiwa kwenye chupa ya chai ambapo alipoteza damu nyingi na kupelekea kifo chake.
2. Alphani kutoka Mwanza amesema mke wake tangu apate ujauzito anahudhuria kliniki lakini mpaka sasa anatumia hizo dawa kutokana na kabila lake kuaminika linafahamu dawa nyingi za kienyeji (Wahaya)
Ameeleza kwasasa ana watoto 3 ambapo mmoja wa kwanza alizaliwa na tatizo la mgongo wazi na hafahamu kama kuna madhara yoyote.
3. Asha Mashaka Mkaazi wa Nyamanoro ameeleza wakati wa kujifungua mama yake alimletea mizizi ya kutafuna na kuwahishwa hospitali.
Amesema alijifungua mtoto mfu na kutolewa kikazi kabisa kutokana na mara nyingi alikuwa anatumia dawa hizo kwa watoto wake watatu wengine.
Ushauri wa watalaamu wa afya wanaeleza:
Elimu iendelee kutolewa kwa kina mama wajawazito ili kufahamu madhara wanayoweza kuyapata hasa katika maeneo ya pembezoni mwa miji na visiwani ili wafahamu madhara husika
Aidha elimu juu ya kuachana na mila na desturi ambazo zimepitwa utolewe ili jamii ibadilike kwani zingine zina madhara
Kuwepo na miundombinu ya afya ya kujitosheleza pamoja na vifaa vitakavyowasaidia kinamama wajawazito kuona kuna imani ya kujifungua salama wao na watoto wao ili kupunguza wimbi la vifo vya mama na mtoto
Imeandikwa na: Florencia Peter