Matumizi ya "Drone" na zana nyingine za kiupelelezi pamoja na ndege zenye teknolojia za hali ya juu sana, zinafanya mfumo kupigana vita ubadilike

Matumizi ya "Drone" na zana nyingine za kiupelelezi pamoja na ndege zenye teknolojia za hali ya juu sana, zinafanya mfumo kupigana vita ubadilike

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Vita ya Ukraine na Urusi na sasa mashambulizi ya Israel huko Gaza na Lebanon, imethibitishwa pasipo shaka kuwa aina za kizamani za zana za kivita, hazina msaada mkubwa kwa sasa.

Matumizi ya "Drone" na zana nyingine za kiupelelezi pamoja na ndege zenye teknolojia za hali ya juu sana, zinafanya mfumo na mitindo ya kupigana vita ibadilike.

Nimeona maelezo haya, yamenitia hofu Sana. Kama ni kweli jee majeshi yetu Afrika yana aina hii ya teknolojia?

Afrika Kila kitu tuko nyuma.Ona hata maonesho ya jeshi letu Kila siku zana ni zilezile Toka miaka ya 1960 lakini wao wanajisifu pamoja na kupiga ngumi matofali na kubeba mabokisi mgongoni Kwa kutudanganya wamebeba kilo miamoja
 
Vita ya Ukraine na Urusi na sasa mashambulizi ya Israel huko Gaza na Lebanon, imethibitishwa pasipo shaka kuwa aina za kizamani za zana za kivita, hazina msaada mkubwa kwa sasa.

Matumizi ya "Drone" na zana nyingine za kiupelelezi pamoja na ndege zenye teknolojia za hali ya juu sana, zinafanya mfumo na mitindo ya kupigana vita ibadilike.

Nimeona maelezo haya, yamenitia hofu Sana. Kama ni kweli jee majeshi yetu Afrika yana aina hii ya teknolojia?

View attachment 3132766
Nenda kaangalie movie inaitwa "eyes in the sky"
 
Yeah, ziko secret weapon nyingi wenzetu wanazo, ndio maana Kwasasa hivi vita za mataifa makubwa mshindi ni yule atakayewahi kupiga pigo takatifu, ukisema waende direct kwenye mapambano na kuoneshana umwamba basi hakuna mshindi bali uharibifu mkubwa Kwa wote, ndio maana siku hizi hutumia proxies.
 
Bro hii eyes in the sky,ndio namna wenzetu wanavyofanya wako zao ofisini lakini mnachunguzwa na wanamtaka mlengwa yule wanamtaka bila kumdhuru mtu mwingine asiye na hatia,kuna mtoto muuza mikate alikuwa karibu na nyumba wanamoishi magaidi,yaani?!
Ile kitu ukitulia kuiangalia unahisi matukio yale yanatokea mtaani kwenu tu hapo.
 
Kwa dunia ya ulimwengu Kwanza imezihirisha kabisa kwamba nchi inaweza miliki military logistics za kizamani za kutosha pamoja na wanaume wenye mbavu kama wote lakini mtoto mrembo mikono yake laini kama mtoto mchanga aliye pata mafunzo ya kutosha ya namna ya kutumia Morden technology akawa anatoa dozi Kwa wanaume huku akiwa kwenye kiyoyozi anatafuna popcorn .
 
Mambo yamebadirika Sana duniani, bila kusomesha watu na kuwapa maarifa makubwa tutakuwa slave tu hapa duniani.

Kama kila kukicha tunawapa promo wahuni akina Doto Magari, Msukuma nk eti wanatukana wasomi na kuhubiri Elimu haina dili na tunacheka baada ya kuwakemea na kuhakikisha tunaseti mfumo wetu wa elimu utoe wahitimu bora wenye uwezo wa kufikiria na kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
 
Ukraine akiwa Hana serious navy kupitia sea drones na technolojia ya drones za angani ameweza kuihenyesha Russia yenye serious navy yenye kumiliki submarines, frigates, mine sweapers, Coverttes, destroyer, aircraft and helicopter carrier nk.
 
Back
Top Bottom