Matumizi ya Fedha za Bunge huchunguzwa na Nani?

Matumizi ya Fedha za Bunge huchunguzwa na Nani?

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2016
Posts
6,974
Reaction score
8,750
Ikiwa CAG huchunguza matumizi Kwa taasisi za Serikali Kuu na Serikali za mitaa (halmashauri) kisha huleta ripoti bungeni. Je huchunguza matumizi katika Bunge letu tukufu? Hawa waheshimiwa wanafaidi keki ya Taifa ipasavyo Kwa njia zifuatazo (ukiacha mishahara minono).

1. Posho Nono za kamati za kisekta (zikiwemo safari za nje na ndani ya nchi).

2. Gharama za kukodisha hoteli za hadhi ya juu Kwa vikao vya kamati.

3. Matibabu nje ya nchi kwa waheshimiwa na wategemezi wao.
 
Ikiwa CAG huchunguza matumizi Kwa taasisi za Serikali Kuu na Serikali za mitaa (halmashauri) kisha huleta ripoti bungeni. Je huchunguza matumizi katika Bunge letu tukufu? Hawa waheshimiwa wanafaidi keki ya Taifa ipasavyo Kwa njia zifuatazo (ukiacha mishahara minono).

1. Posho Nono za kamati za kisekta (zikiwemo safari za nje na ndani ya nchi).

2. Gharama za kukodisha hoteli za hadhi ya juu Kwa vikao vya kamati.

3. Matibabu nje ya nchibkea waheshimiwa na wategemezi wao.
Ni swali fikirishi!.
Hizi taarifa kuwa wamejiongezea posho ya perdiem kufikia kiwango cha Tsh 800,000/= siku wakiwa kwenye vikao vyao Dodoma niza kweli?.

Wahusika au anaejua uhalisia watuambie ukweli!.

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Waheshimiwa wanafaidi mema ya nchi mpaka Raha.
1. Posho Kama zote.
2. Deals kama zote (tenders).
3....
 
Kiswahili kina baadhi ya mapungufu. Katika kiingereza tunaambiwa Kuna three organs of the Government which are executive, judiciary and Parliament, sasa sijui ni kukosa neno sahihi la kiswahili la executive na kupelekea kusema bunge na mahakama sio government (serikali) .

Ndio maana bajeti inaposomwa inasomwa ya serikali nzima, ya mahakama na bunge pia ikiwemo. Na pia ukaguzi wa bunge na mahakama ufanyika kupitia wizara husika nafikiri ni wizara ya katiba na Sheria kwa upande wa mahakama na wizara ya bunge, sera na uratibu kwa upande wa bunge. Ni hayo tu kwa uchache ninavyoona
 
Mbona hujauliza mahakama na bunge bajeti zao zinatokana na nini ikiwa hawazalishi mapato?
 
Mbona hujauliza mahakama na bunge bajeti zao zinatokana na nini ikiwa hawazalishi mapato?
Hoja ni kuwa pamoja na kutumbua pesa za umma Kwa kufanya matumizi yasiyo na tija husikii popote wakitajwa Kama zilivyo Halmashauri au mashirika ya umma
 
Back
Top Bottom