Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Ili mradi tu nisitumie somehow au somewhat? Haya maneno yanamatumizi moja tu?
Endelea kutumia somehow na somewhat, ni maneno ya kawaida tu. Lakini strange na unusual ni maneno mengine kwa ajili ya zile scenario zisizo za kawaida, kama siku ya baridi wakati wa msimu wa joto.
 
Ninapenda sana kile kilichomo kwenye quote yako! Ulikikuta wapi?
Nadhani ulitaka kumaanisha nembo yangu, haswa picha ktk avatar. Huyu ni Rais wetu wa kwanza wa Jamhuri ya Tz, sawa na G. Washington kwa USA. Vipi, miaka miwili ya kukaa Tz uliitumia tu kujifunza kiswahili fasaha na si kuijua historia ya hii nchi mkuu?
 
Nadhani ulitaka kumaanisha nembo yangu, haswa picha ktk avatar. Huyu ni Rais wetu wa kwanza wa Jamhuri ya Tz, sawa na G. Washington kwa USA. Vipi, miaka miwili ya kukaa Tz uliitumia tu kujifunza kiswahili fasaha na si kuijua historia ya hii nchi mkuu?
Ni picha nzuri, asante kwa kunielimisha. Nilikuwa mwalimu wa sayansi kwa ile miaka miwili. Na wewe je? Unafanya kazi gani?
 
Naomba kujifunza kwako ndugu Mimi ni mdau Wa lugha hii, nielekeze yafuatayo; hivi unajua kuna dialectical patterns ambazo zinaathiri maana na mantiki.?
Pili naomba maana ya hizo interrogatives
How
What
Tatu, Mimi nlivyofundishwa hapa bongo ni kuwa some ni determiner ambayo ina determine quantity. Sasa swali je unazo reference ambazo zinaeleza kitu tofauti, ili tupanue maarifa?
Kama ni kweli kosa ,swali who is the meaning owner ?
Speaker or listener.
Mwisho, naomba email address yako pm, ili unipe maarifa
 
Namna gani ikiwa mtu akisema "Somehow it is cold today", akimaanisha kwa namna fulani leo kuna baridi. Akimaanisha baridi wakati wa msimu wa joto ama mahala ambapo kwa kawaida hapapashwi kuwa baridi. Kwa lugha nyingine hamaanishi kiwango cha baridi bali aki refer namna ilivyotokea kukawa na baridi.

Au akasema "Somehow it is a problem", kwa kumaanisha kwamba suala analoliongelea katika hali ya kawaida siyo tatizo lakini kuna namna fulani linaweza kuleta tabu kwa upande mwingine. Au a kwalugha nyingine akawa hana maana ya ukubwa ama kiwango cha tatizo bali ni kwamba kwa namna fulani hilo suala ni tatizo.

?
I got you sir, the problem is the meaning extracted from the two phrases. Na sio tatizo la nchi kama alivyojaribu kushawishi, halafu huyo kama ni linguist anajua kuwa regularities zipo pote duniani. Atuelimishe huku akionesha references
 
Ndiyo kuna matofauti kati ya kiingereza cha marekani na kile cha uingereza, hasa kwenye mwandiko (colour vs color) na mtamsho (aLUminum vs aluMINium). Lakini nafikiri mwingereza angekubali nami kuhusu hilo jambo la "somewhat" na "somewhere". Hilo ni jambo la definition na matumizi ya neno, siyo la mtamsho au mwandiko.
Wew kaka upo serious kweli jibu ulichoulizwa ,show credible sources tujadili kisayansi.
 
Wew kaka upo serious kweli jibu ulichoulizwa ,show credible sources tujadili kisayansi.

Tayari nimetoa source moja:

Tusome article hii: https://www.quora.com/What-is-difference-between-somewhat-and-somehow

Somehow is used to refer to a way that has not been specified.
Somehow linatumika kurejea jinsi ambayo haijatajwa

Although somewhat has the same first four letters as somehow, it is not used to refer to unknown information. Instead it means 'a little or to a small degree.
Yapokuwa somewhat lina herufi nne za kwanza zile zile na somehow, halitumiki kurejea taarifa ambazo hazijulikani. Badala ya hiyo, lina maana 'kidogo au kiasi kidogo'
 
Nahisi brother ,wew sio linguist ila hiyo lugha unajua kuiongea tu. Mi nilidhan utachangamsha ubongo wangu kwa kunirudisha kwenye mabenchi ya maktaba za lugha ,enzi zile tunayatafuta majoho. Ila asante
Nenda kwa google. Ingiza "define: somewhat" na "define: somehow". Hivyo utasoma malinki mengi mengi tu ya makamusi kote kote mtandaoni. Yote yanakubaliana kuhusu maana ya hayo maneno mawili. Unafikiri kila kitu kilichopo kwenye intaneti ni uwongo, kisipokuwa kwenye kitabu cha maktaba?
 
Kwa wao wanaoamini kwamba maana ya "somehow" ni "kiasi fulani" badala ya "jinsi fulani", nakuombea hii: nielezee kwa nini unaamini hivyo wakati "how" maana yake kwa kiswahili ni "vipi"? Uhusiano kati ya "somehow" na "jinsi" si unaonekana?
 
Nenda kwa google. Ingiza "define: somewhat" na "define: somehow". Hivyo utasoma malinki mengi mengi tu ya makamusi kote kote mtandaoni. Yote yanakubaliana kuhusu maana ya hayo maneno mawili. Unafikiri kila kitu kilichopo kwenye intaneti ni uwongo, kisipokuwa kwenye kitabu cha maktaba?
Sawa buana mmarekani, sijawahi kuidharau internet , nafkir hukunielewa
 
Nilisahau kuomba msamaha kwa uwezo wangu mdogo wa kiswahili... Sielewi maneno yafuatayo:

mpogoro
malinyi
ulanga
ras

Tafadhali nielezee, nijifunze mimi mwenyewe!

Ndiyo, ni mmarekani, na kiingereza ni lugha yangu ya kwanza.
ww hujui kiingereza wacha porojo afande maku
 
Na wewe ni mmarekani mkuu? Mmarekani katufundisha kidhungu kwa kiswahili fasaha.
Nafikiri kwa kushindwa kutufundisha kizungu kwa kiswahili fasaha, yaweza kumaanisha kuwa amegoogle kupata tofauti ya maneno hayo na asingeweza kupata maana halisi ya maneno hayo na tofauti zake kwa lugha tofauti.
 
Back
Top Bottom