Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Ili mradi tu nisitumie somehow au somewhat? Haya maneno yanamatumizi moja tu?
Endelea kutumia somehow na somewhat, ni maneno ya kawaida tu. Lakini strange na unusual ni maneno mengine kwa ajili ya zile scenario zisizo za kawaida, kama siku ya baridi wakati wa msimu wa joto.
 
Ninapenda sana kile kilichomo kwenye quote yako! Ulikikuta wapi?
Nadhani ulitaka kumaanisha nembo yangu, haswa picha ktk avatar. Huyu ni Rais wetu wa kwanza wa Jamhuri ya Tz, sawa na G. Washington kwa USA. Vipi, miaka miwili ya kukaa Tz uliitumia tu kujifunza kiswahili fasaha na si kuijua historia ya hii nchi mkuu?
 
Ni picha nzuri, asante kwa kunielimisha. Nilikuwa mwalimu wa sayansi kwa ile miaka miwili. Na wewe je? Unafanya kazi gani?
 
Naomba kujifunza kwako ndugu Mimi ni mdau Wa lugha hii, nielekeze yafuatayo; hivi unajua kuna dialectical patterns ambazo zinaathiri maana na mantiki.?
Pili naomba maana ya hizo interrogatives
How
What
Tatu, Mimi nlivyofundishwa hapa bongo ni kuwa some ni determiner ambayo ina determine quantity. Sasa swali je unazo reference ambazo zinaeleza kitu tofauti, ili tupanue maarifa?
Kama ni kweli kosa ,swali who is the meaning owner ?
Speaker or listener.
Mwisho, naomba email address yako pm, ili unipe maarifa
 
I got you sir, the problem is the meaning extracted from the two phrases. Na sio tatizo la nchi kama alivyojaribu kushawishi, halafu huyo kama ni linguist anajua kuwa regularities zipo pote duniani. Atuelimishe huku akionesha references
 
Wew kaka upo serious kweli jibu ulichoulizwa ,show credible sources tujadili kisayansi.
 
Wew kaka upo serious kweli jibu ulichoulizwa ,show credible sources tujadili kisayansi.

Tayari nimetoa source moja:

 
Nahisi brother ,wew sio linguist ila hiyo lugha unajua kuiongea tu. Mi nilidhan utachangamsha ubongo wangu kwa kunirudisha kwenye mabenchi ya maktaba za lugha ,enzi zile tunayatafuta majoho. Ila asante
Nenda kwa google. Ingiza "define: somewhat" na "define: somehow". Hivyo utasoma malinki mengi mengi tu ya makamusi kote kote mtandaoni. Yote yanakubaliana kuhusu maana ya hayo maneno mawili. Unafikiri kila kitu kilichopo kwenye intaneti ni uwongo, kisipokuwa kwenye kitabu cha maktaba?
 
Kwa wao wanaoamini kwamba maana ya "somehow" ni "kiasi fulani" badala ya "jinsi fulani", nakuombea hii: nielezee kwa nini unaamini hivyo wakati "how" maana yake kwa kiswahili ni "vipi"? Uhusiano kati ya "somehow" na "jinsi" si unaonekana?
 
Sawa buana mmarekani, sijawahi kuidharau internet , nafkir hukunielewa
 
Nilisahau kuomba msamaha kwa uwezo wangu mdogo wa kiswahili... Sielewi maneno yafuatayo:

mpogoro
malinyi
ulanga
ras

Tafadhali nielezee, nijifunze mimi mwenyewe!

Ndiyo, ni mmarekani, na kiingereza ni lugha yangu ya kwanza.
ww hujui kiingereza wacha porojo afande maku
 
Na wewe ni mmarekani mkuu? Mmarekani katufundisha kidhungu kwa kiswahili fasaha.
Nafikiri kwa kushindwa kutufundisha kizungu kwa kiswahili fasaha, yaweza kumaanisha kuwa amegoogle kupata tofauti ya maneno hayo na asingeweza kupata maana halisi ya maneno hayo na tofauti zake kwa lugha tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…