Matumizi ya kiingereza: "Somehow" na "Somewhat"

Sawa sawa... Asante kwa kuwepo kwenye jamii hii ya mtandao wa dunia yetu! Kuwepo kwenye majukwaa ni sehemu muhimu ya uraia.
Nilitaka uniulize hilo ni somo linalohusu nini haswa? Nadhani siku hizi hata sijui kama lipo, uko vizuri sana kichwani mkuu. Miaka miwili tu umejifunza mengi sana.
 
Samahani kwa kushindwa kueleza kwa kiswahili kizuri. Nilivyosema, kiingereza ni lugha yangu ya kwanza. Shuleni nilijifunza kidogo cha kispanya, kiswahili ndicho cha tatu.
Ulijifunza kiswahili huko Marekani? Kumbe lugha yetu imesambaa vilivyo nayo, basi mi sitasumbuka na lugha zingine, hiihii tu itanitosha.
 
Nilitaka uniulize hilo ni somo linalohusu nini haswa? Nadhani siku hizi hata sijui kama lipo, uko vizuri sana kichwani mkuu. Miaka miwili tu umejifunza mengi sana.

Ulijifunza kiswahili huko Marekani? Kumbe lugha yetu imesambaa vilivyo nayo, basi mi sitasumbuka na lugha zingine, hiihii tu itanitosha.
Nashukuru mwalimu. Ilikuwa raha yangu kujifunza yote yaliyowezekana wakati wa ile miaka mifupi miwili. Lugha, utamaduni, jinsi ya maisha. Siku moja nitarudi!

Nilisoma kidogo huku Marekani kabla ya kuenda TZ, lakini nilijifunza mengi kule. Kiswahili ni lugha kubwa! Si milioni nyingi nyingi wanakiongea?
 
East and baadhi ya central Africa
 
Safi kabisa. Naunga mkono hoja yako. Watanzania wengi, siyo tu wale ambao hawajasoma sana, bali hata wale waliosoma sana wanatumia vibaya sana haya maneno! Nishaliona hilo.

Na mimi ni Mbongo pia mkuu ila sichanganyi matumizi ya maneno haya.

Asante...
 
Hata kwetu mjini Missouri wapo wahamiaji kutoka sehemu zile. Nimewatafuta ili niendelee kuongea kiswahili nisikisahau.
kwa kweli hongera sana umefanikiwa kujua kiswahili kwa kiwango cha juu sana.

ni furaha kwetu kuona mtu kutoka marekani amejifunza lugha yetu vizuri namna hii
 
Pia si sahihi kusema "Ni tatizo kwa jinsi fulani". Sema ni "tatizo kwa kiasi fulani" ama "kwa kiwango fulani." Nitaje hilo moja tu niache mengine. Mambo ya lugha kila mtu na ya kwake. Sahihisha wa-Tanzania Kiingereza nao watakusahihisha Kiswahili. Kiingereza si chetu na Kiswahili sio chako. Hatusemi pia "nimejiunganisha", tunasema "nimejiunga," ama "nimeungana na...." Niendeleee? Acha bwana!
 
Hata kwetu mjini Missouri wapo wahamiaji kutoka sehemu zile. Nimewatafuta ili niendelee kuongea kiswahili nisikisahau.
Missouri ni mji ama Jimbo? Ndiyo makosa yenyewe hayo. Ungesema jimboni Missouri basi. Miji ni kama Springfield.
 
Endelea tu. Si kweli kwamba makosa na masahihisho ni fursa ya kujifunza? Wote walimu, wote wanafunzi hapa.

Missouri ni mji ama Jimbo? Ndiyo makosa yenyewe hayo. Ungesema jimboni Missouri basi. Miji ni kama Springfield.

Ni kweli, ni jimbo.
 
Endelea tu. Si kweli kwamba makosa na masahihisho ni fursa ya kujifunza? Wote walimu, wote wanafunzi hapa.

Ni kweli, ni jimbo.

Wewe ni moja ya watu wastaarabu humu. Majibu yako ni ya kiungwana. Umenipa moyo kuendelea.
 
Nilitaka uniulize hilo ni somo linalohusu nini haswa? Nadhani siku hizi hata sijui kama lipo, uko vizuri sana kichwani mkuu. Miaka miwili tu umejifunza mengi sana.

Mkuu usimpoteze mwenzio! Tumia "hasa" badala ya "haswa". Nadhani ulikazia kipwani kwa kusudi jema.
 
Lakini licha ya unyoofu wake ambao unafanya iwe hata rahisi kujifunza [huwa nawaambia watu Kiswahili ni lugha rahisi sana kujifunza], Kiswahili bado kinawapa tabu hata watu ambao ndo lugha yao ya kwanza.

Kinawapa tabu kwenye sarufi, tahajia, msamiati, matamshi, na mengineyo.

Sijui hasa sababu ya hilo ni nini. Ningeweza kusema labda ni athari za makabila mbalimbali tuliyonayo lakini kama hilo ndo lingekuwa tatizo basi wale ambao lugha waijuayo ni moja tu, yaani Kiswahili, wasingekuwa na tatizo kabisa.

Unakuta mtu kazaliwa Dar, kakulia Dar, kasomea Dar, lakini Kiswahili [sanifu] kinampiga chenga!
 
Ndo umuhimu wa muktadha unapokuja!

Wakati mwingine muktadha hubadilisha maana ya neno au hata maneno kulingana na vile yalivyotumika ingawa labda ungechukua maana ya neno moja moja yawezekana ukaona yametumika kimakosa lakini kumbe siyo.

Context is everything!
 
Mkuu usimpoteze mwenzio! Tumia "hasa" badala ya "haswa". Nadhani ulikazia kipwani kwa kusudi jema.
Hata hivyo Mimi ni mzaliwa wa Pwani! Ndo lahaja iliyonilea na kunikuza. Nashukuru kwa Masahihisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…