Matumizi ya Kiswahili katika usaili wa kazi

Matumizi ya Kiswahili katika usaili wa kazi

Kama umesoma na umeelewa KOZI yako hauwezi kupata shida.
 
Jamani Mnaonaje matumizi ya Kiswahili katika usaili wa kazi….toa maoni yako
Ni sawa na kubadirisha gia angani..!!! Siwezi fundishwa kwa kiingereza then uje unisaili kwa kiswahili..!!! Hii inatakiwa ianzie darasani. Mfano leo hii ukiulizwa jinsi MFULUMBATO unavyofanya kazi, bila desa hapo ulipo utaweza..!? Lakini huo huo MFULUMBATO ukitajiwa kwa kiingereza, mbona utaseleleka..!
NB. Kutumia lugha yako inatakiw uwe na nguvu kiuchumi
 
Wewe unaongea nini... mtu aliyesoma software engineering aelezee mifumo kishwahili anaweza sasa mbona unabishia uhalisia

Mtu wa biotechnology! usichukulie vitu simple
We mbugila umekariri, kuna vitu utataja kwa lugha ya kiingereza na vingine utaeleza namna vinafanya kazi kwa kishwahili.

Ina maana akikuuliza FACEBOOK imafanye kazi utashindwa kujibu?
 
Utakuwa umekariri, Yaan ww huwezi elezea kitu kwa lugha ya kiswahili?? Mbona hapa umeendika kiswahili??
Kuna haja gani ya kusomea kwa kiswahili halafu interview ifanywe kwa kiingereza? Hawa wanasiasa uchwara wanaposhindwa jambo wanataka kupindisha sheria. Watu walisoma elimu ya kuungaunga hawajui kiingereza wanalazimisha kila kitu kiwe kwa kiswahili wakati shule zinasomesha kwa kiingereza.
 
We mbugila umekariri, kuna vitu utataja kwa lugha ya kiingereza na vingine utaeleza namna vinafanya kazi kwa kishwahili.

Ina maana akikuuliza FACEBOOK imafanye kazi utashindwa kujibu?
Sasa hapo utakuwa umetumia kiswahili..!?
 
Back
Top Bottom