Matumizi ya Kiswahili katika vituo vyetu vya Redio

Matumizi ya Kiswahili katika vituo vyetu vya Redio

4guz

New Member
Joined
Nov 13, 2013
Posts
2
Reaction score
0
Unapoisikiliza BBC au Redio ya Ujerumani, unapata maneno sahihi ya lugha ya Kiswahili bila ya kuwepo mchanganyiko wa lugha. Watangazaji wetu wa Redio hapa Tanzania ni tofauti sana.
Je!tatizo ni nini hasa,watangazaji wetu ni wavivu wa kujua lugha au ni makusudi?
John
 
Nadhani - Nazani
Athari - Asari
Makabidhiano - Makaziano
Magharibi - Mangalibi
Lugha za Kibonde hizo
 
Nilienda "NIKAMKUTA" hayupo,
Hii ni TAALIFA YA HABALI kutoka...
fikiria kauli hizi anaitoa mtu tena anasikika sehem mbalimbali,kweli kuna umuhimu watangazaji&waandishi wa habari waki-Tanzania kunolewa kila mara kuhusu kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
 
ni wapumbavu fulani wanaojifanya wanajua lugha za kigeni kuliko lugha za mama zao.
Nalog off
 
Hayo ni madhara ya kufikri kila muongeaji mzuri anaweza pia mwandishi wa habair mzuri, makosa haya hayapo kwenye radio na luninga tu ni mengi zaidi kwenye magazeti! tatizo ni ukanjanja!
 
1)Hawana nia ya kujifunza
2)Kwa vile hakuna kitengo kinachofuatilia mwenendo mzima wa utangazaji wa lugha ya Kiswahili kwenye taasisi zetu za habari
3)Kwa bahati nzuri, utakuta watangazaji wengi wa mashirika ya habari uliyo yataja hapo juu ni Watanzania, sasa kwanini hawa waliopo Tanzania washindwe kama sio makusudi na dharau
 
Tatizo kubwa ni mtindo unaotumika katika kuajiri hawa watangazaji
1) Rushwa imechukua nafasi ya juu katika ajira zetu, wanaachwa wenye uwezo wanachukuliwa wasio nao
2) Inapaswa Kiswahili kinacho tumika kwenye vyombo vya habari kiwe fasaha, kwani wale wasio jua Kiswahili hujifunza kwa kusikiliza watangazaji wa vyombo vyahabari
3) Kunawatangazaji wachahe ambao kweli navutiwa na utangazaji wao, wa lugha iliyo fasaha na ya uwazi zaidi, kama dada Regina Mwalekwa na Kaka Ephrahim Kibonde, hawa ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wapya wanaoingia kwenye fani hii
 
Tuna shida sana na hii kitu..na kuna wapinzani wengi sana wanaokipinga Kiswahili Yani ukiongea kiingereza unaonekana bonge la msomi
 
Leo nilimwona mtangazaji wa ITV kwenye kipindi cha AFYA YA JAMII akishika uyoga na kusema ' Haya ni uyoga,' badala ya kusema 'Huu ni uyoga.' Nilicheka sana. Watangazaji wengi wa BONGO ni wataalamu wa KISWA-KINGE badala ya KISWAHILI FASAHA.
 
Tatizo kubwa ni kwa wa TZ wote kwani tunakichulia km lugha ya mazoea hivyo hatuna passion kubwa na hii.
Angalia waingereza hata km ni msanii anafanya komedi kiingereza chake utakipenda
 
tatizo si lugha peke yake, jaribuni kuuangalia kwa undani huu utitiri wa vituo vya redio vya masafa ya fm. vimekuja na kuharibu kabisa heshima ya vyombo vya habari. watangazaji wengi walioko huko ni vijana wahuni wasioelewa kitu chochote, wanajifanya matozi kumbe ni wajinga tu, wanaigana kila kitu. binafsi sioni tofauti ya hizi redio kwakuwa kila redio unayoweka unakuta kipindi kimoja kina watangazaji watatu, wawili wakiume na mmoja wakike, kinachojadiliwa humo ni mambo yao binafsi pia mambo ya ngonongono tu. nachukia sana huu utamaduni mpya wa vipindi vya redio ambao kwao wanadhani ndio ujanja
 
Leo nilimwona mtangazaji wa ITV kwenye kipindi cha AFYA YA JAMII akishika uyoga na kusema ' Haya ni uyoga,' badala ya kusema 'Huu ni uyoga.' Nilicheka sana. Watangazaji wengi wa BONGO ni wataalamu wa KISWA-KINGE badala ya KISWAHILI FASAHA.


Hali ni mbaya sana katika vyombo vya habari vya utangazaji, mfano maneno kama 'siku ya kesho', 'ki-ukweli''mwisho wa siku''lisaa limoja',ni maneno ambayo yana kera sana ukisikia yanapotumiwa na watangazaji,
 
Unapoisikiliza BBC au Redio ya Ujerumani, unapata maneno sahihi ya lugha ya Kiswahili bila ya kuwepo mchanganyiko wa lugha. Watangazaji wetu wa Redio hapa Tanzania ni tofauti sana.
Je!tatizo ni nini hasa,watangazaji wetu ni wavivu wa kujua lugha au ni makusudi?
John
kwenye katiba mpya kiswahili kina nafasi kubwa na redio zetu zinatakiwa kuwa kioo. kuna redio inaitwa TIME FM ya dar kila alfajiri ya saa 11 imewapa kipindi wahubiri wana kiswahili kibovu. bbc hawawafikii ujerumani. maneno wanayo lakini baadhi ya watangazaji wa bbc kiswahili kibovu. ujerumani iko juu
 
Back
Top Bottom