Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
KUNI NA MKAA HUSABABISHA VIFO VYA GHAFLA
Na Mwandishi wetu
Musoma, Mara.
Waziri wa Nishati, Mh. January Makamba akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara inayolenga kuhamasiha matumizi ya nishati safi nchini mkoani Mara, alipata wasaa wa kuzungumza na Daktari wa Magonjwa ya Ndani, Dkt. Mary Mahenge ambaye alimweleza athari za matumizi ya nishati ya mkaa na kuni ambazo hutoa moshi wenye hewa ya carbon monoxide ambayo ina chembe ndogondogo ambazo zikiingia kwenye damu zinapunguza oxygen ambayo inafanya mwili ufanye Kazi. Carbon monoxide ikiwa nyingi inaweza kusababisha vifo vya ghafla.
Mara baada ya kupokea taarifa hio ya Kitabibu Waziri Makamba amesema “Serikali imeamua kuweka msukumo katika suala la upatikanaji wa nishati safi ya kupikia hasa vijijini ili kuondoa adha ya matumizi ya kuni na mkaa kwa wananchi wa vijijini na wa kipato cha chini. Kwa wananchi wa vijijini ubora wa maisha yao unatokana pia na nishati wanayopikia kwani moshi unaotoka kwenye kuni si sumu inayoua taratibu”.
Waziri Makamba bado yuko kwenye ziara yake ya siku 21 itakayofika kwenye Mikoa 14 na Wilaya 38 kukagua miradi mbalimbali na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.