Matumizi ya kuni na Mkaa, husababisha vifo vya ghafla

Matumizi ya kuni na Mkaa, husababisha vifo vya ghafla

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
KUNI NA MKAA HUSABABISHA VIFO VYA GHAFLA

Na Mwandishi wetu
Musoma, Mara.

Waziri wa Nishati, Mh. January Makamba akiwa kwenye siku ya kwanza ya ziara inayolenga kuhamasiha matumizi ya nishati safi nchini mkoani Mara, alipata wasaa wa kuzungumza na Daktari wa Magonjwa ya Ndani, Dkt. Mary Mahenge ambaye alimweleza athari za matumizi ya nishati ya mkaa na kuni ambazo hutoa moshi wenye hewa ya carbon monoxide ambayo ina chembe ndogondogo ambazo zikiingia kwenye damu zinapunguza oxygen ambayo inafanya mwili ufanye Kazi. Carbon monoxide ikiwa nyingi inaweza kusababisha vifo vya ghafla.

Mara baada ya kupokea taarifa hio ya Kitabibu Waziri Makamba amesema “Serikali imeamua kuweka msukumo katika suala la upatikanaji wa nishati safi ya kupikia hasa vijijini ili kuondoa adha ya matumizi ya kuni na mkaa kwa wananchi wa vijijini na wa kipato cha chini. Kwa wananchi wa vijijini ubora wa maisha yao unatokana pia na nishati wanayopikia kwani moshi unaotoka kwenye kuni si sumu inayoua taratibu”.

Waziri Makamba bado yuko kwenye ziara yake ya siku 21 itakayofika kwenye Mikoa 14 na Wilaya 38 kukagua miradi mbalimbali na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

IMG-20220712-WA0003.jpg
IMG-20220712-WA0005.jpg
IMG-20220712-WA0002.jpg
IMG-20220712-WA0006.jpg
IMG-20220712-WA0007.jpg
IMG-20220712-WA0000.jpg
IMG-20220712-WA0001.jpg
IMG-20220712-WA0004.jpg
 
Huyu Makamba anazunguka kutafuta Promo ya Gesi sababu huko ndiko iliko 20% ya walamba asali Gang.

Wameliacha Bwawa la Nyerere (Stiegles Gorge) kwa makusudi ya kutaka mradi wao wa gesi ukamilike kwanza ili wapate chao kwanza.

Mradi wa Bwawa la umeme hauna maslahi makubwa kwao sababu Mikataba mingi ilikwishaingiwa na serikali ya JPM hapo awali.

Na Makamba anachofanya ni kuibua miradi mipya yenye maslahii kwake na kundi lake.
Ili wapate mikataba yenye 10% au 20% na hakuna la zaidi.

Anachofanya Makamba na team yake ni Danganya Tanzania [emoji1241] [emoji1241].
 
True
 
gesi kujaza bei juu sana wapunguze bei kwenye..Tofaut na hapo mkulima tutaendelea kutumia kuni na mkaa
 
Huyu Makamba anazunguka kutafuta Promo ya Gesi sababu huko ndiko iliko 20% ya walamba asali Gang.

Wameliacha Bwawa la Nyerere (Stiegles Gorge) kwa makusudi ya kutaka mradi wao wa gesi ukamilike kwanza ili wapate chao kwanza.

Mradi wa Bwawa la umeme hauna maslahi makubwa kwao sababu Mikataba mingi ilikwishaingiwa na serikali ya JPM hapo awali.

Na Makamba anachofanya ni kuibua miradi mipya yenye maslahii kwake na kundi lake.
Ili wapate mikataba yenye 10% au 20% na hakuna la zaidi.

Anachofanya Makamba na team yake ni Danganya Tanzania [emoji1241] [emoji1241].
mwache apige pesa kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.hiyo gesi hata hapa mjini inatushinda pia sisi wengine tumekulia katika maisha hayo lkn hatukuona madhara yake.wazazi wetu waliishi ktk mazingira hayo halafu ndo kwanza waliishi kwa muda mrefu kuliko tunavyoishi siku hizi hawa wasomi wa kisasa ni wa ajabu sana.hiyo ndo shida ya copy and paste.nchi huliwa na wajanja wilaya 21 si haba na miko 14 perdiem za kutosha.suluhisho ya hayo mambo ni katiba tu.waliotangulia walituingiza chaka baya sana.
 
Biashara ya mkaa na kuni ni mojawapo ya biashara za hovyo sana kwenye karne ya 21
 
Back
Top Bottom