Matumizi ya madawa/vitanzi vya kupanga uzazi ni hatari

Matumizi ya madawa/vitanzi vya kupanga uzazi ni hatari

zinasababisha kansa hizo njia zetu kikubwa tumieni natural method amabzo ni calender na kuchomoa pindi unataka kupeez
 
siku nyengine tumieni kitanzi/'loop' ni nzuri (haiingiliani na mfumo wa homoni) ila uwekaje wake sasa ndo ishu.
Ndio ni kizuri mwenyewe na kitumia, lakn bleed yale sasa ndo shughuli. Kwanza nyngi pili unaenda siku nyng had 8 halafu mzunguko haueleweki
 
mbona haina shida mkuu,hapo inakubidi usubiri tena kama miaka aliyotumia kizuiz....Yaan hiyo miaka 2 na miez saba ndo uzazi unafunguka.
 
siku nyengine tumieni kitanzi/'loop' ni nzuri (haiingiliani na mfumo wa homoni) ila uwekaje wake sasa ndo ishu.
Kitanzi ni kizuri sana ila kina masharti makubwa. Kwanza kinahitaji usafi wa hatari na hakitaki mpango wa nje kwa mwanamke na mwanamme. Ina maana mke awe mwaminifu na mune vivyo hivyo la sivyo ataumwa sana tumbo mpaka akitoe.
 
Pole, bora yenu nyie mna watoto. Kuna wengine wanakurupuka tu,mtu hana mtoto anaanza tumia njia za uzazi wa mpango sababu hajajiandaa kupata watoto. BAADAE INAKUA MAJUTO TUPU.
Du,sasa hii kali yaani hujapata mtoto unapanga uzazi ,unajuaje kama una huo uzazi?
 
Hii inategemea Na mwili wa mtu ,Mimi niliwahi kuweka Na Mara baada ya kutoa tu sikuchukua muda mrefu kupata ujauzito.ninadhnai Ni vyema ukiwaona wataalamu kabla hujaamua kutumia njia yoyote ya uzazi wa mpango .
Kweli kabisa inategemea na mwili wa mtu hizi dawa ni hormones ambazo zinatengezwa kwa aina ambayo itatofautiana kidogo na utaratibu wa kawaida wa mwili wa Mwanamke na kumfanya asiweze kushika ujauzito,kama ilivyo kawaida ya kila dawa lzm kuwe na side effects au maudhi madogo madogo,km kuona hedhi kidogo au nyingi,kichwa kuuma,kunenepa,mood change na sometimes delay fertility baada ya kuacha kutumia! Kwa ufupi sio kila side effect ya dawa itampata kila mtu anayotumia dawa husika na muda wote mfano dawa ya Chloroquine iliyokuwa inatumika kutibu malaria ilikuwa ina side effect ya mwili kuwasha ila si kila mtumiaji alikuwa anawashwa,wengi tumetumia Flagyl hv tunajua inasababisha mtu kukojoa mkojo kama umechanganyika na damu?ila ni wachache wanaopata tatizo hili lkn ni moja ya side effect,kwa kuhitimisha njia za Uzazi wa mpango ni Salama ila kwa kuwa ni dawa huwa zina side effect kama dawa nyingine na sio kwamba watumiaji wote watapata side effect zinazolingana!
 
Nikwambie tu kuna rafiki yangu daktari bingwa wa wanawake aliwa kuniambia usije mruhusu mkeo atumie hayo mambo ya kupanga uzazi kwani hakuna dawa hata moja ambayo haina madhara zote zina madhara, kuna baadhi ya wanawake wanaenda period mpk mwezi na ikikata anaweza kukaa hata miezi sita bila period! Wengine akibeba kitu kizito tu hata ndoo ya Lita 20 anaanza bleed kifupi hazifai
Ni sawa kabisa hakuna dawa isiyo na side effect lkn sio kila mtumiaji wa dawa lzm apate hizo side effects cha muhimu ni kufahamu kila kitu kuhusu dawa ya uzazi wa mpango husika then wewe mwenyewe ukubali kupata hiyo Huduma (informed choice) sio kulazimishwa mm nimeona akina mama wengi wako kwenye njia za uzazi wa mpango bila matatizo yeyote ni wachache sana!na kama zingekuwa zina madhala kwa watu wengi am sure wala serikali isingeziruhusu ziendelewe kutolewa!narudia tena hakuna dawa isiyo na side effect.
 
Tunatumia condoms kama mechanical contraceptives na ziko za kiume na za kike. Ni salama kuliko vidonge na loop kwani haviingilii mfumo wa kifisiologia wa uzazi. Loop si nzuri ni abortificient. Mimba hutunga kama kawaida ila Inasababisha isikae na itoke. Nyingi zinapo toka huwezi kutambua haraka utadhani hedhi imekuwa ndefu au nzito kupitiliza kumbe ni mimba imetoka. Jihadharini na loop
 
Madaktari wenyewe wanasema njia hizo za uzazi sio nzuri ukitoa condoms, withdrawal n calendars. Though hayo wanasema pembeni sio wakat wakiwa ma makoti yao meupe.

Kitanzi kilimletea matatizo dada angu mpaka akatangulia mbele za haki.
 
Habari Wadau,
Mimi nimeowa na tumebahatika kupata watoto wawili katika ndoa,baada ya hapo tuliamua kutumia njia za kupangza uzazi(Kitiji) kwa sababu kadha wa kadha,ni kweli tulifanikiwa kufanya hivyo kwa muda wa miaka miwili na miezi saba.
Baada ya hapo ukawa ni muda muafaka kupata mtoto tena!Cha ajabu na kusikitisha ni miezi 10 sasa tangu ametoa hicho kijiti na hakuna mafanikio yoyote.

Tumejaribu kuwaowa wataalam katika hospitali mbalimbali bila mafanikio japo bado hatujakata tamaha.Nimeona ni bora niwafahamishe wadau msije rudia makosa kwani wakati ukiwa unawacosult family plan wanakushawishi kwa kusema utakapo hitaji mtoto ukitoa tu unapata kitu ambacho si kweli,kuna watu wengi tu wamenishuhudia shida kama hii.
Kuweni makini
kwenye red rekebisa, binafsi nikutakie pole saana, lakn haimaanishi kuwa eti kwa sababu ya lalamiko lako tu basi tuone haifai labda mpaka pawe na cases nyingi
 
Madaktari wenyewe wanasema njia hizo za uzazi sio nzuri ukitoa condoms, withdrawal n calendars. Though hayo wanasema pembeni sio wakat wakiwa ma makoti yao meupe.

Kitanzi kilimletea matatizo dada angu mpaka akatangulia mbele za haki.
Kweli nawaambia kitanzi sio kizuri. Pole sana kwa kupotelewa na dada yako.
 
Mimi nijuavyo njia za kupanga uzazi ni nyingi. Kuna za kiasili mama anatengana na mume wakati mtoto ni mdogo. Kuna vidonge (pills) vyenye hormones za progesterone zinazomezwa kila siku katika mzunguko wa siku za mwanamke zinazozuia yai kupevuka na mimba kutunga. Pia iko dawa ya sindano inayochukua muda mrefu hadi miezi sita. Nyingine ni hiyo unayoiita kijiti (loop). Hii loop sio contraceptive ila ni abortficient. Mwanamke mwenye loop anapata mimba kila wakati lakini mazingira yaliyo tengenezwa na loop ndani ya kizazi yanafanya ishindwe kukaa na itoke ikiwa bado changa sana. Mimba zikitoka kunakuwa na damu nyingi kupita kawaida ya Mp ya mwanamke. Kizazi kikizoea utaratibu huu wa mimba changa kutoka hali hiyo huendelea hata baada ya kutoa loop na kuleta ugumu wa kupata mimba kwa wanawake wengi wanaotumia njia hii ya uzazi wa mpango.
Nimejifunza jambo hapa.... Asante sana....
 
Ukijaribu kugoogle na kusoma madhara ya uzazi wa mpango sehemu zilizo nyingi wanaandika kwa baadhi ya watu hizo dawa huwa zinamalizika nguvu baada ya kuacha kutumia ndani ya mwaka na kuendelea baada ya hapo mtu anaweza kuendelea na siku zake kama kawaida.
Hivyo kwa kuwa bado dawa iko mwilini nadhani sio vibaya akawa anakunywa maji kwa wingi ili kuipunguza nguvu.

ATHARI 10 ZINAZOWEZA KUSABABISHWA NA MATUMIZI YA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO
  1. Athari kuu 10 zinazoweza kusababishwa na vidonge hivyo ni pamoja na kutokwa na damu ukeni baada ya hedhi ya kawaida. Kwa mujibu wa wataalam wa mpango huo, athari hiyo huweza kuwapata asilimia 50 ya wanawake wote wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango. Hali hii huweza kuwatokea ndani ya miezi mitatu baada ya kuanza matumizi ya dawa hizi. Kwa ujumla, hali hiyo huweza kukoma kwa zaidi ya asilimia 90, pindi mwanamke anapoanza kutumia pakti ya tatu ya dawa hizo katika kipindi hicho cha kutokwa damu ukeni. Mwanamke anapotokewa na hali hiyo kwa mfululizo wa siku tano au zaidi baada ya kumaliza siku zake za kawaida za hedhi, anashauriwa kuwasiliana na mhudumu wa afya wakati akiendelea kutumia dawa hizo.
  2. Athari ya pili, ni kujisikia kichefuchefu. Mara nyingi hali hiihumtokea mwanamke mwanzoni tu baada ya kuanza kumeza vidonge vya uzazi wa mpango, ingawa hali hii inaweza kukoma baada ya siku chache. Inashauriwa pia kwa mwanamke anayepatwa na hali hii ya kichefuchefu kuwasiliana na mhudumu wa afya kama ataona hali hiyo inazidi.
  3. Matiti kujaa au kuwa na maumivu, ni athari nyingine inayoweza kusababisha na matumizi ya vidonge hivyo. Hali hii huweza kumpata baada ya kuanza kutumia vidonge hivyo, na huweza kukoma ndani ya wiki moja tu. Hata hivyo, inashauriwa kwamba ikiwa matiti hayo yatatokwa na uvimbe au maumivu yasiyoisha, ni muhimu kutafuta tiba kwa wahudumu wa afya, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya kinywaji chenye kafeini (caffeine) na chumvi na kuvaa brauzi isiyobana matiti.
  4. Maumivu ya kichwa ni athari nyingine inayoweza kumtokea mwanamke, ingawa pia kuumwa kichwa kunaweza kuwa na dalili za magonjwa mengine. Hata hivyo, kama itatokea maumivu hayo ya kichwa yakaanza tu mara baada ya kumeza vidonge hivyo, hiyo itakuwa ni dalili ya athari mojawapo na ni vyema kutoa taarifa kwa mhudumu wa afya.
  5. Vidonge vya uzazi wa mpango huweza pia kuongezeka uzito wa mtumiaji, ingawa tafiti nyingine zimeshindwa kuthibitisha uhusiano kati ya vidonge hivyo na mabadiliko ya uzito wa mtumiaji. Aidha, baadhi ya wanawake hupatwa na tatizo la maji kuganda kwenye matiti na maeneo ya nyonga baada ya kutumia vidonge hivyo.
  6. Mabadiliko ya hisia huweza pia kumtokea mwanamke anayeanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Inashauri kwamba pindi mwanamke anapoona dalili hii, ni muhimu kumjulisha mhudumu wa afya ili kuweza kujadili ni jinsi gani ataweza kutumia dawa hizo, kwa sababu dalili hii ni mbaya kiafya kwa mtu mwenye historia ya ugonjwa wa Kushuka Moyo (Depression).
  7. Athari nyingine ya dawa hizi ni kutokwa na uchafu ukeni. Baadhi ya wanawake, mara tu baada ya kutumia vidonge hivi hutokwa na uchafu ukeni, ikiwa ni pamoja na kupatwa na uwezekano wa kupungua au kuzidi kwa ute wakati wa tendo la ndoa. Ni muhimu sana mwanamke anapobaini dalili hizi, kuonana na mhudumu wa afya ili kubaini kama hali hiyo imesababishwa na athari ya vidonge au kuna maambukizi ya magonjwa ya zinaa.
  8. Wanawake wengine huweza kujikuta wakikosa siku zao za hedhi baada ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango. Ingawa ugonjwa wa msongo wa mawazo (stress), magonjwa, mchoko wa safari unaweza kusababisha hali hii, lakini inashauriwa kupima kama mtu amaepatwa na ujauzito hata kama anatumia vidonge hivi kama itatokea kukosa hedha katika mazingira tata.
  9. Kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni athari nyingine inayoweza kumkuta mwanamke anayetumia vidonge vya uzazi wa mpango kutokana na vichocheo vilivyomo ndani ya dawa hizo, ingawa pia magonjwa kama ya kisukari, shinikizo kubwa la damu na kadhalika yanaweza pia kuchangia tatizo hilo.
  10. Athari ya 10 na ya mwisho kwa wanawake wanaotumia vidonge hivyo, ni mabadiliko ya taswira ya kitu anachokiona mbele yake, hasa kwa wanawake wanaovaa miwani ya macho. Kwa kuwa macho ni moja ya eneo muhimu la ufahamu kwa mwanadamu, hali hii inapowapata wanawake, inashauri kuonana mara moja na daktari wa macho pindi tu dalili hizi zinapoanza kujitokeza.
Ni tahadhari gani mwanamke anatakiwa kuchukua kabla na baada ya kuanza matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango?

Kwa mwanamke mzazi, hairuhusiwi hata kidogo kuanza kutumia vidonge vya uzazi wa mpango ndani ya wiki tatu tu baada ya kujifungua mtoto au ikiwa atakuwa ananyonyesha mtoto mwenye umri wa chini ya miezi sita.

Aidha, ikiwa mwanamke amefanyiwa upasuaji mkubwa wa aina yoyote katika siku za karibuni, au kama mwanamke husika ni mvutaji wa sigara na ana umri wa zaidi ya miaka 35, haruhusiwi kutumia vidonge hivyo, kama ambavyo pia haruhusiwi kufanya hivyo mwanamke mwenye historia ya ugonjwa wa ini, manjano, moyo, saratani ya matiti, tumbo la uzazi pamoja na shinikizo la damu linalobadilikabadilika kila wakati kwa viwango vya 140/90 mmHg au zaidi, na au kama ana historia ya maumivu makali ya kichwa.
 
Mimi sipo kwenye ndoa.
Nimetanguliza kusema hivyo ili watu waeleze uhalisia ulivyo katika hili ninalotaka kutaja hapa chini.
Kwani ikitumika njia ya asili ya kutazama kalenda i akuaje?
Nadhani ndo njia pekee ambayo haina madhara kiafya
Pili vipi kwa njia ya kuchopoa linapokuja?
Sio ya uhakika Sana , Na wengine hushindwa kuzingatia
 
Ndio ni kizuri mwenyewe na kitumia, lakn bleed yale sasa ndo shughuli. Kwanza nyngi pili unaenda siku nyng had 8 halafu mzunguko haueleweki
Wewe upo kama mimi, nimeweka mwaka jana mwezi wa tano... ila kwa sasa nataka kukitoa
 
Back
Top Bottom