Matumizi ya pombe safarini ni hatari kwa uhai wako mwenyewe

Matumizi ya pombe safarini ni hatari kwa uhai wako mwenyewe

Kipindi napiga dili za moro dar.Kuna siku nikachelewa kupanda abood nikapanda islam ilikua mida y asaa kumi na mbili na nusu jioni tumeoboka km dar tunafika mbezi kuna lijimama likapanda bonge la mtu kumbe limetoka kwenye sherehe na bado liko tungi na lina bapa ndogo linafyonza.mpaka nafika moro nimelinanawa sana tukachukua kitax pale tukaenda zetu msufini nikachukua guest pifa sana miti...
dodo jangwani dah
 
umesema kitu ya maana sana,
ulimbukeni wa pombe unawafedhehesha na kuwadhalilisha sana kwenye public...
Watu tunalewa safarini lakini hauwezi kutambua kama tupo high.unaweza vipi kusafiri safari ya km 1200 ? Ukiona umesafiri safari ya hivyo bila kunywa kileo lazima upate dhambi ya makwazo
 
Sasa wanakutibu aje na uko na pombe? Ufariki?
Nadhani kama ilivyo ukiwa ktk dose/ matumizi ya dawa hairuhusiwi pombe, ndivyo itakavyo fanyika ukiwa na pombe
Nina nani alisema mlevi haruhusiwi kutibiwa akiwa amelewa? Au ndio zile stories ukinywa maziwa uko katika dozi,dozi inaharibika.?
 
Yes,
dawa ya mwanzo kabisa ya mgonjwa aliebainika kanywa pombe huwa ni dripu tu,
Sasa kwa mfano akipigwa sindano ya quinine na amekunywa pombe si atakufa chap, tunamzika na kumsahau?

ndio maana nasema ukipata ajali ukiwa umelewa unaweza ukashindwa kujiokoa na unaweza ukashindwa kujieleza matokeo yake wakakuchoma sindano au wakakupa dawa itakayokuangamiza kwasabb haisikilizani na pombe....
Unaongelea quinine wakati haipo katka standard guidelines treatment
Quinine uwe umelewa au haujalewa ,,,medical personnel akifanya mistake imekula kwako
 
Kuna siku nilikua niko tungi ndani ya basi natoka Arusha naenda dar nikamwambia dereva asimame nikojoe akagoma!
Nilichofanya nikachukua chupa kubwa ya maji ya Kilimanjaro nikaikojolea nikatupa dirishani!
Kwisha
 
I conquar with you.
Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu, lazima tutuinze na kuithamini zawadi hii muhimu kwetu sote. Tufurahie uhai na mema mengi ya Mungu alieyoyajaza katika ulimwengu huu.

Imeibuka kasumba kwa wanywaji pombe hasa vijana, mathalani, anasafiri kutoka mkoa moja kuelekea mkoa mwingine, kutumia vilevi hususani pombe.

Unakuta abiria huyo ama ana mzinga mkubwa wa Konyagi, K-vant au hivi vipombe flani vyenye flavor tofauti tofauti lakini kilevi ni kilekile, ambazo konyagi nao pia wameiga.

Baadhi yao wanakua wamejaza kwenye chupa za maji kukwepa kuonekana wanakunywa pombe, lakini wengine bila soni wanafakamia na michupa vilevile. Mnafika mwisho wa safari kijana kalewa chakari.

Sasa, shaka langu hapa ni kwamba ikitokea ajali, mtu huyu si, ni rahisi sana kupoteza maisha, kwasabb kupata ajali katika hali ya ulevi, hali ambayo inaweza kupelekea ashindwe kujiokoa mwenyewe panapostahili kujiokoa. Na mtu akishalewa akili yake inakua slow kumake decision, lakini pia anaweza akapitiwa usingizi fofofo ambao hata akiamshwa anaweza asiweze kuamka kabisa.

Lakini pia kwasababu pombe huchochea msukumo na mgandamizo wa damu kuwa wa kasi zaidi mwilini, mtumiaji pombe huyu akiumia anaweza kupoteza damu nyingi zaidi na hatimae akapoteza maisha pia.

Rai yangu kwa vijana na wanywa pombe safarini.

Kuweni wastahimilivu na wenye subra hadi mwisho wa safari ndipo kuzitafuta na kuzinywa vilivyo hizo pombe.

Pili, makondakta wa mabasi ambao pia miongoni mwa hutumia pombe wakiwa kazini, kuacha mara moja tabia hii isiyo yakiungwana, na kuwakemea abiria wanao tumia pombe ndani ya mabasi.

Mwisho ni kwa dereva bodaboda wote, ndugu zangu acheni izo mtaisha na kuwa walemavu wote. Kunywa pombe zako baada ya kazi, itakusaidia kuepuka ajali na ulemavu.

Ni kero na usumbufu kwa abiria wasiotumia aina hiyo ya kinywaji.

Asante.
 
Shida yenu mnasafiri bila tahadhari ,siwezi safiri bila kuruhusiwa na kibuyu ,kikiashiria damu sisafiri na ikiashiria weupe nasafiri


Safari inaazia nyumbani kwako ,sio muda wa departure
 
Kama starehe yako ni uji focus na uji.

Pombe ilikuepo na itadumu milele 🍸🖤
 
Mkuu wewe unapiga gambe au hautumii, maana wasiotumia huwa ni wanafiki sana kila siku kutusema na kutuombea mabaya
 
Back
Top Bottom