jemsic
Member
- Jul 1, 2020
- 21
- 51
Picha: RF studio
DIBAJI
Uwajibikaji ni moja ya nguzo muhimu sana ya ustawi wa taifa lolote duniani. Hata maitaifa makubwa na yenye ustawi kimaendeleo kama Marekani yamezingatia uwajibikaji ili kufikia hapo walipo sasa. Teknologia ni moja ya nyezo umuhimu katika karne ya ishirini na moja ambayo ikitumika kwa uzuri itaeleta matokeo chanya katika kukuza uwajibikaji Tanzania. Teknolojia ni nyenzo yenye uwezo wa kuleta mapinduzi makubwa katika nyanja ya uwajibikaji. Kwa kufanya habari ipatikane na kwa uwazi zaidi kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano nchini inaweza kusaidia kuiwajibisha serikali na taasisi nyingine kwa kuangalia na kutoa habari sahihi zenye dhumuni la kukuza uwajibikaji baina wafanya kazi, watendaji pamoja na viongozi katika sekta zote. Inaweza pia kusaidia kuwawezesha wananchi kushiriki kwa ufanisi zaidi katika mchakato wa kisiasa wa uchaguzi ili kupata viongozi walio bora.
UTANGULIZI
Uwajibikaji ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa nchi yoyote ile duniani na hasa pale inapoambatana na uwazi ndani yake. Hata baba wa taifa hayati Mwl. Julius Nyerere alisisitiza sana kuhusu umuhimu wa uwajibikaji ili Tanzania idumu kupanda kiuchumi ili kufikia kilele cha maendeleo. Panapokuwa na uwajibikaji, utawala wa sheria, ushirikiano na mwitikio mzuri huwa ni matokeo mema yanayozaliwa hasa katika nyakati hizi za sayansi na teknologia. Sayansi na teknolojia vinachukua nafasi kubwa katika kukuza uwajibikaji kwa kuwezesha upatikanaji wa habari madhubuti na kuwafanya wananchi kushiriki kwa ufanisi zaidi katika mchakato na shughuli mbalimbali za taifa. Hii ni kwa sababu tecknolojia huwapa wananchi habari kemkemu za kila kinachoendelea na kila hatua ya nchi inapokwenda hivyo basi kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kipi kifanyike katika wakati husika.
UMUHIMU WA TEKNOLOJIA KWENYE KUKUZA UWAJIBIKAJI
Teknolojia tangu kuibuka kwake imekuwa na umuhimu mkubwa katika sekta na tasnia mbalimbali nchini na kwa sasa umuhimu unaonekana katika kukuza uwajibikaji nchini Tanzania. Umuhimu wa kwanza ni kwamba teknolojia inaweza kusaidia kupunguza rushwa katika vyombo tofautitofauti vya umma. Kwa njia ya kurahisisha ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya serikali na kufichua ufisadi, teknolojia inaweza kusaidia kupunguza ufisadi na kuboresha uwajibikaji kwa mtu mmojammoja kama raia na vingozi wa taifa zima kwa ujumla.
Pili, teknolojia inaweza kusaidia kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya umma na hata sekta binafsi kwa kuwarahisishia wananchi kupata huduma wanazostahili na kwa wakati uliopangwa. Teknolojia inaweza kufanya sehemu kuboresha utoaji wa huduma na kufanya serikali kuitikia zaidi mahitaji ya wananchi na kuyawajibikia kwa weredi na ustadi wa kutosha.
Tatu, teknolojia inaweza kusaidia kujenga uaminifu mkubwa kati ya wananchi na serikali yao kwa kufanya serikali iwe wazi zaidi juu ya kila hatua ya juhudi za kuwajibika kwao katika kuwatumikia wananchi wake. Kupitia matumizi ya teknolojia wananchi wataiamini sana serikali yao na umuhimu wa kuaminiwa ni kwamba watu watawajikaji kwa nguvu na moyo zaidi katika kutulitumikia taifa lao kwa uzalendo.
UKUZAJI WA UWAJIBIKAJI KUPITIA TEKNOLOJIA
Kuna njia nyingi ambazo teknolojia inaweza kutumika kukuza uwajibikaji na hasa kwenye nchi zetu zinazondelea ambapo migogoro ya kidemokrasia inasababishwa na ukosefu wa uwajibikaji umekuwa mwingi. Njia hizi ni pamoja na:
- Kuongeza na kudumisha uwazi: Teknolojia inaweza kutumika kurahisha upanikanaji wa habari za utendaji kazi wa shughuli za serikali. Kwa kutumia vizuri tenolojia ya habari na Mawasiliano, taarifa na habari za mipango na maendeleo yote yanafanyika yataweka wazi na kuweza kufikiwa zaidi na umma kwa ajili ya utoaji wa maoni, changamoto na mawazo mbalimbali yenye tija ili kufikia lengo la maendeleo endelevu. Hii inaweza kufanywa kupitia hifadhi za takwimu za mtandaoni, tovuti za serikali, na mitandao ya kijamii ambazo watanzania huweza kuingia na upata taarifa zote muhimu za utendaji kazi wa serikali.
- Kuwawezesha raia kupiga kura mtandaoni: Teknolojia ilipofikia kwa sasa inaweza kutumika kuwawezesha wananchi kushiriki kwa ufanisi zaidi katika mchakato wa kisiasa hasa wa kuchagu viongozi wanaona wa sifa stahiki za uwajibikaji ili kulitumikia taifa. Hili linaweza kufanywa kupitia upigaji kura mtandaoni, maombi ya nafasi za kugombea mtandaoni, Kwa kutumia teknolojia kwa upigaji wa kura kuchangua viongozi kwa kutukia mitandao itaongeza ufanisi wa uchaguzi huru na wa haki kama kipengele muhimu cha kuwapata viongozi wenye kuliwajibikia taifa lao.
- Kuifatilia serikali kwa ukaribu: Teknolojia inaweza kutumika kuifatilia serikali kwa ukaribu ili kujua kila hatua. Hili linaweza kufanywa kupitia ufuatiliaji wa mtandaoni, kutambua na kufichua madhaifu mbalimbali kwa uanaharakati wa mitandao ya kijamii ili kuifanya serikali kuwa yenye ubora wa kulivusha taifa kutoka hatua moja hadi nyingine.
CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBUKA TAKNOLOJIA
Nchi ya Tanzania bado ipo nyuma kwa upande wa teknolojia na baadhi ya changamoto zinzoikumba teknolojia na hivyo kudumaza uwajibikaji ni pamoja na:
Nchi ya Tanzania bado ipo nyuma kwa upande wa teknolojia na baadhi ya changamoto zinzoikumba teknolojia na hivyo kudumaza uwajibikaji ni pamoja na:
- Uwekezaji mdogo sana katika tasnia ya teknolojia hasa ya habari na Mawasiliano
- Ukosefu wa sera za takwimu huria
NAMNA YA KUKUZA TEKNLOJIA ILI KUKUZA UWAJIBIKAJI
Kuna mbinu mambo kadhaa ambazo zinaweza kutumika kuongeza uwezo wa teknolojia ili kukuza uwajibikaji na hizi ni:
Kuna mbinu mambo kadhaa ambazo zinaweza kutumika kuongeza uwezo wa teknolojia ili kukuza uwajibikaji na hizi ni:
- Uwekezaji katika miundombinu ya kidijitali kama vile mtandao wa kasi kubwa (5G kwa sasa) na kanzidata za mtandaoni ili kurahisishia wananchi kupata taarifa kuhusu shughuli za serikali. Swala la kukuza uwekezaji katika miundo mbinu ya kidijitali inaweza kufanywa kusaidiana na nxhi zenye maendeleo makubwa ya kiteknolojia mfan China na Korea ya Kusini.
- Serikali zinapaswa kupitisha sera za kuruhusu upatikanaji wa takwimu huria ambazo zitafanya takwimu za shughuli mbalimbali za maendeleo ya nchi zinafonywa na serikali kufikiwa na umma zaidi. Hii itasaidia watu kutoa maoni mema na yenye kujenga yatakayo kuza uwajibikaji wa watendaji na viongozi.
HITIMISHO
Mwisho, teknolojia ina uwezo wa kuleta mapinduzi makubwa kwenye uwajibikji zaidi kwa nchi zinzoendelea kama Tanzania kwa kuwekeza na kuifanya matumizi mazuri. Kwa kurahisisha upatikanaji wa habari na kuleta uwazi zaidi, teknolojia inaweza kusaidia kudumisha uwajibikaji uliotukuka serikalini na hata katika taasisi nyingine. Pia, inaweza kusaidia katika kuwawezesha wananchi kushiriki kwa ufanisi zaidi katika mchakato wa kisiasa hasa katika uchguzi mkuu n ahata kutoa mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali. Kwa kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, kupitisha sera za takwimu huria, kukuza ushiriki wa wananchi kutoa hoja na pendekezo kwenye tovuti za uwajibikaji na kujenga utamaduni wa uwazi uletea uwajibikaji, serikali zinaweza kuongeza uwezo wa utendaji wa kazi na maendeleo makubwa yatafikiwa.
Mwisho, teknolojia ina uwezo wa kuleta mapinduzi makubwa kwenye uwajibikji zaidi kwa nchi zinzoendelea kama Tanzania kwa kuwekeza na kuifanya matumizi mazuri. Kwa kurahisisha upatikanaji wa habari na kuleta uwazi zaidi, teknolojia inaweza kusaidia kudumisha uwajibikaji uliotukuka serikalini na hata katika taasisi nyingine. Pia, inaweza kusaidia katika kuwawezesha wananchi kushiriki kwa ufanisi zaidi katika mchakato wa kisiasa hasa katika uchguzi mkuu n ahata kutoa mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali. Kwa kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, kupitisha sera za takwimu huria, kukuza ushiriki wa wananchi kutoa hoja na pendekezo kwenye tovuti za uwajibikaji na kujenga utamaduni wa uwazi uletea uwajibikaji, serikali zinaweza kuongeza uwezo wa utendaji wa kazi na maendeleo makubwa yatafikiwa.
Upvote
17