Nimetoka kuangalia Video mpya ya Mr bluu "mboga saba" na nasikitika kusema kwamba sijaipenda sio kwamba nyimbo ni mbaya bali ni kwa haka katabia ka wasanii wa Bongo kuwaweka kwenye video Madem weupe(waarabu,wahindi,wazungu na wale wenye muonekano wa light skins). Hii inaonesha ni jinsi gani sisi watu weusi hatujikubali wenyewe na ndo mana sishangai kuona idadi ya wanawake wetu weusi wakijichubua ngozi zao.
Kila Msanii anataka ashoot na dem mweupe. Rejea video za Diamond, Alikiba,Ommy Dimpoz,Blue,Hamonaiza na wengine kibao. Hata hao wazungu wenyewd wanatushangaa kuona jinsi tunavyowanyenyekea. Mfano yule dem alioshuti "Bado" ya Hamonaiza ilitokea ajali kidogo basi dem akagoma, Wacha majamaa wampigie magoti kisa dem mweupe mpaka akakubali na dau wakapandishiwa.
ACHENI USHAMBA WASANII WA BONGO FLEVA