Matunda ya Diaspora: Namna Wanawake Diaspora 2 walivyoweza kumuweka Kagame na Rwanda kwenye kona. Tanzania tuna la kujifunza

Tatizo moja wapo kubwa la tanzania ambalo ndio chanzo hasa cha kila uozo uliopo nchi hii ni kwamba watu hawafanyi maamuzi kwa kuangalia ustawi na future ya taifa hili hasa linapokuja suala la teuzi.

Linapokuja suala la teuzi kinachizingatiwa hasa ni kulipana fadhila za kisiasa na ushikaji/undugu kwamba huyu alinisaidia kipindi fulani au huyu ni ndugu yangu au huyu mtoto wa rafiki yangu basi acha nimpe ulaji hili na yeye aneemeke aishi vizuri.

Na kwa bahati mbaya hayo yanafanyika hadi kwenye nafasi nyeti ambazo ni muhimu sana kwa ustawi na usalama wa taifa, matokeo yake tumekuwa na viazi wengi ambao waledi hawana wanachojua wao ni kubadilisha magari ya kutembelea tu na kuponda starehe eti ndio wanalinda usalama wa taifa letu, binafsi mimi nilishaona kutokana na huu upumbavu lolote baya litukute tu huko mbeleni hili iwe fundisho.
 
Che Guevara alikwenda Congo kusaidia mapinduzi ya kizalendo! Akakuta wanajeshi wanakula pombe na Waawake daily!

Congo ni chi ya Bata tu, Sio kazi kazi! Watatawaliwa milele!
Sebene ndombolo na kukata mauno ndo kazi wanaweza kutawaliwa kunawahusu
 
Hapo kwenye Wagner!
 
Chawa wa Tanganyika.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Namkubali sana huyu dada Therese Kayikwamba,siku ya kwanza kumsikiliza nilitamani niwe na binti kama yeye mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza na kujiamini huku akitabasamu
 
Ukimwangalia yule Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo alafu ukimlinganisha na huyu wa kwetu unajisemea tu Mungu ihurumie Tanzania. Fanya jambo.
Yaani nilimlinganisha huyo dada Therese na kile kingereza cha debate cha Makamba alichokuwa anasifiwa kule X nikasema Mungu tusamehe Tanzania
 
Yaani nilimlinganisha huyo dada Therese na kile kingereza cha debate cha Makamba alichokuwa anasifiwa kule X nikasema Mungu tusamehe Tanzania
Yuko fluent vizuri sana kwenye Kiingereza na Kifaransa. Kule UN Security Council anashushaga madini hadi Balozi wa Rwanda anatafutaga pa kutokea🤣🤣
 
Katika dunia ya sasa bado una mawazo kuwa vita ya msituni ngumu?
 
Tuna Rais mwanamama ni mfano wa Dunia wewe unaleta stori za hao vibaraka wa diaspora 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…