Hili swala la TLS Ni zito, na kuna watu wanakuja na hoja dhaifu eti walishambulia sio professional killers au walikua wazembe, mimi nasema la hasha....hawa watu Ni wauaji maalumu na Hawakua wazembe hata kidogo, kwanini?
Kwasababu ukiangalia vizuri matobo ya zile risasi yalilenga sehemu zote muhimu....KICHWANI, MIGUUNI, KIFUANI, UBAVUNI NA TUMBONI ...Risasi nyingine zilipigwa mlango wa nyuma means yake Ni kwamba hata angelaza seat bado angekutana nazo!!! Oh my God this was not just an attack,, it was a serious killing incident.
Sasa swali la kujiuliza aliponaje?????? Hapa sijui wengine mna majibu gani ila mimi nasema Mungu yupo (God Exists) kama unabisha jiulize zile risasi za chini, juu, pembeni katikakati ziliishia wapi na sio mwilini mwa Lisu?????
Kama Mungu amemuokoa Lisu katika hili Basi wauaji kuweni makini Jicho lake linawatazama... japo maneno kama haya wengi huyapuuza wakidhani yanatolewa na wafia dini watu wasiofikiri sana.
Kwa hili lazima serikali ihusishwe na msijifiche kwenye mgongo wa kusema hatuwezi kumdhuru Lisu waziwazi wakati kila mtu anajua migogoro iliyopo!!! La hasha....kina Mwangosi waliuawa hadharani na kikao mtu alikua anajua migogoro iliyokuwepo,,kina Alphonce Mawazo, kina Ulimboka waking'olewa meno bila ganzi wakaponea chupuchupu na kila mmoja alikua anajua migogoro yao na Serikali ovu ya CCM.
Ben Saanane alihoji vyeti akapotea hadharani na kila mtu anajua,,Roma alitekwa kila mtu anajua,,, Sasa la Lisu linadhindikana??????
Serikali na viongozi wa Afrika wakishaapishwa nadhani wanakatwa mishipa yote ya aibu...wakiamua kufanya Jambo lolote hulifanya bila aibu na bila uoga wala kujali nani atawaza au kusema nini...Kwa kusema hayo siituhumu serikali moja Kwa moja ila nasema haiwezi kujisafisha kutokana na mlolongo wa matukio ya huko nyuma.
Kikubwa hapa sio Siasa na propaganda za kina Sirro na mkuu kufunifunika mambo, Ni kuja na majibu kamili ya maswali yafuatayo.
1. Nani alivamia Clouds FM na kwanini na hatua gani zilichukuliwa,
2. Nani amemteka Ben Saanane, amempeleka wapi na hatma yake Ni Nini,
3. Nani alimteka Roma na kwanini na hatua zilizochukuliwa dhidi yake,
4. Nani alimtolea nape Bastola na hatua zilizochukuliwa dhidi yake,
5. Kina nani wamemmiminia Lisu risasi kama mvua ya mawe na nani kawatuma na kwanini.
Serikali ikiyajibu haya maswali, narudia tena bila siasa wala propaganda za kina Sirro na Mwenyekiti wa chama...Basi hapo itaweza kutuambia kwamba kweli haihusiki na haya matukio.
Toa maoni yako