Matundu 19 ya Risasi Katika Gari ya Tundu Lissu.. Hao wahalifu hawana mafunzo ya kitaalamu ya silaha!

Matundu 19 ya Risasi Katika Gari ya Tundu Lissu.. Hao wahalifu hawana mafunzo ya kitaalamu ya silaha!

halafu wakamkosa Lissu makusudi tu, na hawakuwa na lengo la kumuua?
Kama una lengo la kumuua mtu aliye kwenye gari ambaye hana silaha, unaendesha gari lako mpaka karibu naye na kumpiga risasi 20 kupitia dirishani kutoka karibu katika namna ambayo huwezi kumkosa.

Risasi nyingi kupigwa mlangoni zinaashiria kilichotakiwa hasa ni kumjeruhi miguuni na kumpa ulemavu/ tishio.

Watu wanaotaka kuua wanalenga kichwa na kifua, hawalengi ilipo miguu.

Watu wanaotaka kuua mtu ambaye hana ulinzi kama huyo wanapiga risasi point blank, hawapigi risasi za rasharasha kutoka mbali.
 
Ukifuatilia tukio zima lilivyo na mazingira yalivyo na aina ya upigaji ulivyo,


Inakupasa kwenda mbaaali zaidi ya haya tunayoyafikiria.


Hapa ukifuatilia chanzo cha kutaka kuuchukua uhai wa Lissu unaweza baki bumbu wazi. Usiku kucha nilikuwa nawaza na sikupata usingizi kabisaa.

Nimewaza mpaka nikafika mbaaali mnooo.

Toka jana mi nilikuwa na hasira sana na serikali, lakini nikaluweka swala hili kwa undani zaidi, kuna sababu lukuki hapa. Nadhani vyombo vya dolla vikifanya uchunguzi vizuri vitajikita katuka maeneo kadhaa na kona kadhaa hizi fitina zutajulikana

Sema tuliowengi tumekwisha hukumu na hata ukweli ukitika ukiwa kinyume na matarajio yetu hatutokubali katika hili.

KUNA KITU NYUMA YA PAZIA ZAIDI YA TUNAVYOWAZA NA KUONGEA KWA JAZVA. ASANTE MUNGU KWA KUMNUSURU HUYU MTEULE WAKO.


Apone tuu na naamini kuna mengi anayajua juu hili atatwambia ukweli
Tatizo ni kwamba, hata kama serikali haihusiki, kauli za kijinga za viongozi wa serikali, hususan rais Magufuli, zinawafanya watu wengi waone kama serikali inahusika.

Hilo tu ni tatizo.

Hata kama serikali haihusiki.
 
Hili swala la TLS Ni zito, na kuna watu wanakuja na hoja dhaifu eti walishambulia sio professional killers au walikua wazembe, mimi nasema la hasha....hawa watu Ni wauaji maalumu na Hawakua wazembe hata kidogo, kwanini?

Kwasababu ukiangalia vizuri matobo ya zile risasi yalilenga sehemu zote muhimu....KICHWANI, MIGUUNI, KIFUANI, UBAVUNI NA TUMBONI ...Risasi nyingine zilipigwa mlango wa nyuma means yake Ni kwamba hata angelaza seat bado angekutana nazo!!! Oh my God this was not just an attack,, it was a serious killing incident.

Sasa swali la kujiuliza aliponaje?????? Hapa sijui wengine mna majibu gani ila mimi nasema Mungu yupo (God Exists) kama unabisha jiulize zile risasi za chini, juu, pembeni katikakati ziliishia wapi na sio mwilini mwa Lisu?????

Kama Mungu amemuokoa Lisu katika hili Basi wauaji kuweni makini Jicho lake linawatazama... japo maneno kama haya wengi huyapuuza wakidhani yanatolewa na wafia dini watu wasiofikiri sana.

Kwa hili lazima serikali ihusishwe na msijifiche kwenye mgongo wa kusema hatuwezi kumdhuru Lisu waziwazi wakati kila mtu anajua migogoro iliyopo!!! La hasha....kina Mwangosi waliuawa hadharani na kikao mtu alikua anajua migogoro iliyokuwepo,,kina Alphonce Mawazo, kina Ulimboka waking'olewa meno bila ganzi wakaponea chupuchupu na kila mmoja alikua anajua migogoro yao na Serikali ovu ya CCM.

Ben Saanane alihoji vyeti akapotea hadharani na kila mtu anajua,,Roma alitekwa kila mtu anajua,,, Sasa la Lisu linadhindikana??????

Serikali na viongozi wa Afrika wakishaapishwa nadhani wanakatwa mishipa yote ya aibu...wakiamua kufanya Jambo lolote hulifanya bila aibu na bila uoga wala kujali nani atawaza au kusema nini...Kwa kusema hayo siituhumu serikali moja Kwa moja ila nasema haiwezi kujisafisha kutokana na mlolongo wa matukio ya huko nyuma.

Kikubwa hapa sio Siasa na propaganda za kina Sirro na mkuu kufunifunika mambo, Ni kuja na majibu kamili ya maswali yafuatayo.

1. Nani alivamia Clouds FM na kwanini na hatua gani zilichukuliwa,

2. Nani amemteka Ben Saanane, amempeleka wapi na hatma yake Ni Nini,

3. Nani alimteka Roma na kwanini na hatua zilizochukuliwa dhidi yake,

4. Nani alimtolea nape Bastola na hatua zilizochukuliwa dhidi yake,

5. Kina nani wamemmiminia Lisu risasi kama mvua ya mawe na nani kawatuma na kwanini.

Serikali ikiyajibu haya maswali, narudia tena bila siasa wala propaganda za kina Sirro na Mwenyekiti wa chama...Basi hapo itaweza kutuambia kwamba kweli haihusiki na haya matukio.

Toa maoni yako
Watu wasiojulikana ndio wimbo wao

Wamelipua IMMA advocates hamna chochote kilichofanyika

Tena aliyemtolea bastola Nape alionekana hadharani Hamna kilichofanyika

Yani kupitia hili la Lissu wanaenda kuaibika vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejaribu kuhesabu kitaamu risasi zilizopigwa ktk gari ya Tundu Lissu yanafika 20 kwenye kioo,kitasa na chini kidogo mpaka ktk tairi ya mbele kushoto.

Kwa jinsi zilivyopigwa inaonekana hao wahalifu sio watu waliojifunza matumizi ya silaha maana zimepigwa rondom bila mpangilio.

Wengi waliojifunza matumizi ya silaha huwa wanapiga kwa target na mpangilio maalumu.

Nakumbuka niliwahi kuanzia Uzi humu kama wito wa kukusanya silaha haramu toka kwa wanainchi kama Lyatonga Mrema alivyofanya.

Hao si wahalifu ni magaidi .Au ugaidi ni kitu gani??
 
Watu wasiojulikana ndio wimbo wao

Wamelipua IMMA advocates hamna chochote kilichofanyika

Tena aliyemtolea bastola Nape alionekana hadharani Hamna kilichofanyika

Yani kupitia hili la Lissu wanaenda kuaibika vibaya

Sent using Jamii Forums mobile app

Hao si watu wasiojulikana hao ni magaidi. Wasiwatese wale masheikh bure Kwa kutoa maoni Yao kuhusu muungano
 
Wewe bure kabisa ,haya maneno ungeongelea mbele ya haraiki ya watu ungegeuzwa jina!

So Watu kama nyie ndo wauaji ehhh Afu unataka kuongoza Nchi bila Demokrasia ya mawazo. Ana akili sana huyo jamaa kuliko wewe mtihani katunga mwingine. Majibu unayo wewe na unataka usahihishe mwenyewe.
 
Zetas kule Mexico wengi ni ex special forces, wakishambulia kwa dhamira ya kuua wanahakikisha nyumba au gari inabaki na matobo ya risasi za kutosha... Na mara nyingine wanatumia hadi RPGs kabisa...so hoja ya kiasi cha risasi na professionalism ya wapigaji ni muflisi kabisa....
 
Hujui hata risas ni nini ndio maana unadhani utaona tundu moja
 
So Watu kama nyie ndo wauaji ehhh Afu unataka kuongoza Nchi bila Demokrasia ya mawazo. Ana akili sana huyo jamaa kuliko wewe mtihani katunga mwingine. Majibu unayo wewe na unataka usahihishe mwenyewe.
sijamaanisha hivyo no,nimejaribu kuonyosha kuwa kwa maneno yake yasiyo na utu anastahili kutendewa bila kujali utu wake.
 
kama bashite na baba yake ndio walikuwa maoperation manager ungetegemea zoezi lifanyike kwa ustadi ni kwa sababu mission leader wana vvichwa vya samaki unataka kumuuwa mtu ambaye mumejiapiza mbele za kamera kwamba lazima alazwe lazima anyamazishwe lazima apotezwe si ndio maana Mungu akawafunga warusha risasi mikono wakawa hawajuwi walenge wapi laana indani ya vizazi vya baba bashite
 
Wawe wajuzi wasilaja wasiwe pia yote tunamwachia MUNGU kwasababu yeye aliwaona nayeye ndiye atakaye wahukumu wao na aliye watuma, kwetu ni MAOMBI tu kumwombea apone haraka ili aendelee na mapambano AMINA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikua plan b baada ya plan A kushndwa kutokushuka kwenye gali ..planB nikupga sehem aliyo kaa .......fikilia ilo acha siasa
 
Baada ya kuchemka kumteka wakaamua wampoteze

da MUNGU WA DAUDI na MUNGU WA YOHANA wanaodai ni mbatizaji
 
Back
Top Bottom