Matunduizi's Journal: mambo mbalimbali ninayojifunza kila siku kutoka katika vyanzo mtambuka

Matunduizi's Journal: mambo mbalimbali ninayojifunza kila siku kutoka katika vyanzo mtambuka

Ni ujinga Kuburudika kwa Kuangalia mpira badala ya Kucheza mpira.
Mwenzako anaingiza kipato, anaimarisha mwili wakati wewe unapooteza afya kwa kukaa ovyoovyo huku ukipoteza napesa na nguvu za kiume kwa kukaa kizembekizembe hadi usiku wa manane unaangalia wanaume wanapiga pesa na kuimarisha miili yao.
 
Kwa wakristo ndoa sio mkataba ni agano la milele.
 
Mtoto anaweza kupatikana kwa njia haramu, ila hakuna mtoto haramu.
 
Utafiti unaonyesha KWA KADILI PESA NYINGI ZINAVYOTUMIKA KATIKA NDOA NDIVYO NDOA HIVYO ITAKAVYODUMU NDANI YA MUDA MFUPI.

" The more expensive your wedding is, the shorted your wedding is likely to last"
 
Nchi ya Swiden haijui Historia yake kuanzaia karne ya 12 kurudi nyuma. Na hawana hata kabrasha moja linalohusu matukio ya huko. Hivyo hawajui hata Ufalme wa nchi hiyo ulianzaje anzaje.

Vilaza ni wengi.
 
Miaka ya 90, kampuni ya Magari SUBARU, iligundua wateja wake wengi ni Wanawake WASAGAJI, Ikaanza kufanya matangazo ya biashara moja kwa moja kwa kundi hilo la wanadamu.
img04.jpg
 
Faida ya NA NGUVU YA MZIKI MZURI WA KIMAADILI WA INJILI MAISHANI MWAKO

1:Unanguvu ya Kushusha Kiburi.
2:Kuusafisha Moyo na mawazo potofu
3:Huamsha Huruma
4:Hufariji
5:Hulegeza Nguvu ya Majaribu
6:Hubadili maisha
7:Huipa nafsi Nguvu na ujasiri
 
Usipukutisha nguvu zako zoote kwenye mambo yasiyo na maana usijejikuta na nguvu kidogo sana kufanya mambo makubwa ya msingi.
 
Siku zote Mbele za Mungu, Tunafanya maamuzi sahihi au Maamuzi ya Kiovu.
Hakuna maamuzi maovu kidogo (Lesser evil)
 
There is always a right choice available any time an evil choice is given to us
 
Ethical holiness always exacts a price
 
See Yourself as Capable of doing nothing less than Brilliant
 
Wazazi waliopotoka hudhani jukumu la malezi huisha Pale Vijana wao wanapopata kazi, au wanapokwenda masomoni hasa elimu ya juu.
Dhana hii ni potovu. Mzazi Unajukumu la malezi kwa watoto wako hadi wanakwenda kaburini. Hata wakiwa watu wazima wewe kama mzazi bado unanafasi ya kushauri na kutoa mwelekeo ukiona mwanao anakwenda katika njia isiyosahihi.
Usiseme Shauri yake ni mtu mzima huyo anajitambua.
 
Neno moja zuri Linalofaa, linaweza kuwa na maana kubwa sana kuliko neno Bovu ambalo kama lisingetamkwa madhara Yanayokupata hadi sasa Yasingekuwepo.
 
" You don't have to be a Manager in Your organization to have a wonderful influence on your organization Culture"
 
Wekeza katika kuwafanyia wenzako mazuri bila kujali wala kutegemea malipo.
Malipo ni Kwa Mungu kwa kila mwanadamu anayeona Mbali.
 
Back
Top Bottom