Matunguli au uchawi uliocha ofisini na mtangulizi wako unautoaje kuitakasa ofisi?

Wewe umepangiwa u-DED wapi?
 
Uchawi upo kwa wazungu, nakumbuka nilisha wahi ona wazungu wakizika mbuzi mzima.
Pia kama ushawahi hii series channel e, utagundua kuna wazungu wachawi.
 
Lack of wisdom.
 
Umepona?? Karibu tena jukwaani..matunguli ya boss, unamuita MWANDULAMI...Ukiwaita kina Gwajima hakuna kitu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
nasikia miaka ya zamani hali ilikuwa ya hatari sana kwa wazee waliokuwa wanafanya kazi bandari.

ilikuwa sio rahisi kukalia kitu ambacho sio chako. mabosi walikuwa wanaogopana sana.kila boss alijihami kishirikina.
 

Ikiwa ni mkristo wa kweli unaweza kutumia Silaha za Mungu Kwa imani kama "Damu ya Yesu Kristo inenayo mema, maana imeandikwa hivyo kwenye Biblia Takatifu kwamba "Wakamshinda Kwa Damu ya Mwana Kondoo (Yesu Kristo) na Neno la ushuhuda katika UFUNUO 12:9-11.

Hakuna uchawi wala uganga kwa mtu anayeamini nguvu ya Damu ya Mwana Kondoo au Yesu Kristo yenye uwezo wa kutakasa na kuharibu kazi zote za shetani na wasaidizi katika jina kuu la Yesu Kristo. Amen !

Mwisho sikiliza wimbo huu hapa !
 

Attachments

  • Kuabudu-Damu Ya Yesu Inanena Mema ( 360 X 640 ).mp4
    21.5 MB
Bosi wangu alikuwa akimwaga madawa chumba cha cha pili ofisi yetu ilikuwa haikaliki dawa kama amemwaga kinyesi. Sasa hivi katolewa namwonea huruma anaekuja.
Office gan



Naje anamwaga dawa mkiwepo?
 
Inabidi ufagie ofisi yote upate mchanga kidogo ,huo unatosha katika shughuri za kuondoa uchawi au zindiko lililowekwa ofisini ,pia wanahitajika jogoo wawili wekundu,ubani maka na ubani mashitaka,unga wa salfa kazi yako inakuwa imeisha.Kama kuna vitu vimewekwa vinatolewa live harafu vitachomwa moto.Habari inakuwa imekwisha.
 
Waafrika tuna changamoto sana za kuhusudu ushirikina na uchawi. Ndiyo maana wengi wanashindwa kupiga hatua kimaendeleo.
 
Unaweza pata ajira halafu ikaenda kukuharibia maisha au kukupoteza kabisa . Tafuta mtaalamu wa hayo mambo akusaidie kuweka mambo sawa .
 
Nakumbuka nikiwa JKT miaka ya giza nilikuwa karani wa Mr RSM, aisee yule mzee alikuwa akisafiri kiti chake nakaa mimi tu. Akikaa yule dingi mwenzie aliyemkaimisha madaraka siku hiyo kikosi kizima ni full taflani utasema mzee anakufa muda huohuo.
[emoji23]huko congo kuna kipindi mjeda fulani alipewa ofisi akaenda kumwaga damu ya kuku kama sio kondoo ofisi nzima huku akidai mtangulizi wake hakuwa mtu mzuri so ana clear hali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchawi upo kwa wazungu, nakumbuka nilisha wahi ona wazungu wakizika mbuzi mzima.
Pia kama ushawahi hii series channel e, utagundua kuna wazungu wachawi.
Kuna mwanamke hapa Tanzania alinunua mdori myumbani basi magonjwa yakaanza kumuandama. Kanisani wakamshauri auchome moto ule mdoli na alipofanya hivo alipona. Ilidaiwa kuna mzungu huko ulaya aliweka mashetani kwenye mdoli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wao wenyewe wana matunguli yao.
Huwezi kuwa mwana ccm bila kuwa mchawi
 
Mkuu unakula keki ya Taifa, shikilia hspo hapo wenzako tunataabika hatari, ningekuwa na uwezo ningekuomba connectiom sema hata nkikuomba utasema nakuchunguza
 
Mkuu unakula keki ya Taifa, shikilia hspo hapo wenzako tunataabika hatari, ningekuwa na uwezo ningekuomba connectiom sema hata nkikuomba utasema nakuchunguza
Hapana mkuu.

Mimi nafanya shughuli zangu kama kwa kujishikiza yaani Ad-Hoc.

Natoa ushauri elekezi.

Kwa sasa napata shida kushauri jinsi ya kuwaelewa wazaramo wataka nini.

Pembeni nina vibiashara vyangu vya hapa na pale.

Moja ya kibiashara kangu ninapo pale Tandale kwa Mtogole nakaanga viazi na vipapatio vya kuku, si haba.

Mimi nimepita katika shida mkuu, mtoto wa mkulima ila nikazamia Ulaya miaka hiyooo!, in 90s.

Dah siwezi kumalizia, ila nchi hii ina wenyewe ambao ndo haohao walomkataa Magufuli ambae alitaka sote tufaidi keki ya taifa.

Ila shule nimeenda vya kutosha na niko makini sana na ninachokiandika hapa.
 
Basi shikilia sana ulichonacho na chochote kile kinachokupa kipato sababu mtaani hali inatisha hata kazi za kujitolea nazo zimetoweka kama mvua jangwank
 
Hahaha Beatrice walitaka kukuua na matunguri sasa umerudi maana nusura ufe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…