Heshima mbele wakuu. Jamani hivi:
Tatizo wataalamu wetu nao wanachukulia kila kitu anachosema rais kuwa ni halali. sheria yetu ya barabara hairuhusu kuweka matuta kwenye highway. kwa hiyo hata rais akisema, bado ni ukiukwaji wa sheria tu. nadhani hapa walipaswa kufikiria ushauri wa rais na kufanya kitu ambacho ni convinient kutekeleza aguizo la rais na kuwarahisishia watumiaji wa barabara maisha
Mkuu MN, unajua kwa nini matuta yamekwekwa, sababu wahusika walikuwa hawana alternative solution ya kumwambia Mhe Raisi against matuta.. Hili sio kosa la Raisi ni kosa lao kwa kutokuwa na alternative!! Basi kama hakuna alternative then wangemwambia kitaaluma na sio kuweka kilicho sicho (kama kweli matuta ni mabaya kisais hicho against loss of lives). MM kusema Raisi ana kosa narudia tena na kumuonea Mkuu kwa kosa la wataaluma ambao tunao in plenty!!
kwa maoni yangu ni vitu viwili tu wanachoweza kufanya ni kujenga subway au flayover kama la pale manzese,kila polipo na kituo cha basi.
kisha sehemu zilizobakia za barabara wajenge uzio kuzuia watu kukatisha barabara ovyo.
Mkuu KK, huo ushauri wako ni mzuri kwelikweli lakini ukiangalia Dar - Mlandizi - Chalinze Road (especially Dar - Mlandizi) kuna kijiji karibu throughout the road. Pia ukiangalia kwa ukaribu utaona kuwa kila kwenye vituo (vituo vyote/vingi vimejengwa pacha, to and from adjacently) kuna alama ya kwenda 50kmph na maeneo ya shule as low as 30kmph, lakini madereva pretends nothing exists, solution, weka tuta pinduka au punguza mwendo..... Pia ushauri wako kwa pesa zipi Mkuu, hii ni Bongo tunaongelea na sio ahera!!
unaonaje kuhusu watu watakaoendelea kuumia na kufa kwenye ajali za magari yanayogongana kutokana na msongamano wa matuta.....au yale yanayopinduka usiku wa manane kwa kukosa alama za kuonekana..
why guys dont we come with immediate compromise to suit both pedestrians and motor drivers....[pasengers]
Mkuu PM, magari kugongana kutokana na msongamano wa matuta, Mkuu umesahau sheria za barabarani au ni jazba?? Kuna ile inayosema "Keep a safe following distance" Hilo la magari kupinduka kwa kukosa alama zinazoonekana sio kosa la matuta, ni kosa la maintenance agency (na wizi wa alama za barabarani na kugongwa na madereva husika) kushindwa kumaintain standard signs - sio kosa la matuta kuwepo bali ni alama!!
On your second part ya compromise solution to suit both hapo tunaweza ongea lungha ya aina moja. Ndicho tulichosema kwenye ile thread ulianzisha ya Mh Raisi kuingilia majukumu ya watalaam. Kwenye post yangu ya kwanza in this thread nilikuwekea kwa ukumbusho. Tuliongelea mengi yakiwemo safety audit (kwakuanzia na kutafuta blind/danger spots along our roads etc, kisha tutafte best solution considering all users requirement, costs etc)
MANZESEE KUNA DARAJA NA WATU WANAGONGWA, KAWAWA ROAD 'SOKO LA MACHINGA' WANAWEKA DARAJA NA WATU WATAGONGWA VILE VILE.
kwa solution ya kitanzania, kilicho fanyika ni best option, ukitaka kuwahi toka mapema.
Mkuu watu, asante kwa hilo..... Solution za nchi/sehemu nyingine may not necessarilly be the best to our scenario and mind sets!!!
Mungu Ibariki JF, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu tubariki waTanzania!!!