1. Pia nilimuuliza kama alikuwa akijua mahali ninakoweza badili fedha kwa kiwango kizuri. Ninajua kwa uzoefu wangu wa kusafiri India, Kenya, Uganda, Ghana na Misri, kuwa wafanyabiashara wakubadiri fedha kwa njia zisizo halali uwa na wana viwangu vizuri vya kubadirisha fedha kuliko wale wenye vibari. Alisema anafahamu duka la kubadiri fedha lililopo karibu na hapo ambalo huwapeleka wateja wake na akadai kwamba atanipeleka kesho yake muda wa chakula cha mchana, atakapokuwa ameachana na wateja wake wengine. Hakuwa na hakika ni muda gani atanipeleka ila alidai atanitaarifu. Tongo aliniuliza kama nilihitaji aandae safari za kutuzungusha kama safari ya mvinyo na safari ya kwenda kutazama ndege maji. Nilimjibu kuwa nitazungumza na mke wangu nione angependa nini. Nilimpatia namba yangu ya simu na nikaondoka. Tongo alionekana kuwa mtu mwenye maarifa mengi, kujua mambo mengi, na wa msaada mkubwa pia alionekana ni mtu mwenye heshima na kujali. Alikuwa kava kinadhifu, tax yake ilikuwa bado nzuri, alizungumza kingereza kizuri na alikuwa na business card iliyokuwa imetengenezwa kitaalamu ikiwa na habari zake zote muhiumu kuhusu nhuduma anazotoa.
2. Nilirudi ndani ya hoteli na kwenda kuangalia viwango vya kubadirishia pesa pale hotelini kwa mpokea pesa. Viwango havikuwa vya kuridhisha hivyo nilimuuliza Yule dada aliyekuwa mapokezi ni wapi ninapoweza kubadirisha fedha za kigeni, akanielekeza kwnye jengo la maduka la V&A.
3. Nilielekea chumbani kwetu ambapo nilimkuta Anni akipakua nguo toka kwenye mabegi na akijiandaa kwenda kuoga. Alitaka akishaoga aanze kutengeneza nywele zake na aliniambia zoezi hilo litachukua muda wa masaa kadhaa. Wakati nilipobadirisha pesa kwenye duka la Amrican Express, walihitaji pasi yangu ya kusafiria hivyo nilihisi hata V&A wanaweza kuhitaji pasi yangu ya kusafiria ilinibidi niichukue niondoke naye , niliweza kubadirisha pesa kiasi cha Pound za Uingereza 800 na nikapewa R8,242.25 katika duka la Western union ambapo hicho kiwangi kilikuwa chini kwa R10.30 ukilinganisha na nilivyobadirisha kwenye duka la Ameircan Express. Kabla ya kurudi hotelini nilipita kwenye duka na kununua ua rose kwa ajili ya Anni, alikuwa akipenda sana maua rose.
4. Jioni tulienda kwenye bar ya hoteli kwa ajili ya vinywaji, kabla ya kutembea kuelekea kwenye Mghahawa wa Sevruga kwa ajili ya chakula cha usiku.
5. Tulipofika tuliagiza sushi. Siku ya Jumatatu tukiwa London, Anni alikuwa kanunua Bikini kwa pound 90, na hili liliibuka katika mazungumzo yetu. Anni hakuwa napenda kuniomba ela alikuwa anapenda kufanya kazi apate elea yake mwenyewe. Alidai kuwa ikitokea akaishiwa ela uwa ana kadi ya benki ya baba yake atatumia ela ya baba yake, mimi nilimtania kwamba itabidi baba yake aifungie kutoa ela kwa maana kwa sasa ni mke wake na ni mwanafamilia ya Dewan hivo inabidi pesa achukue kwa Dewan. Alijibu kuwa baba yake hawezi kuifunga, mimi nikamwambia anaweza iwapo nikimuomba. Nilimtania kuwa ninaenda kumtumia ujumbe mfupi nikimuomba aifunge. Huu wote ulikuwa utani. Baada ya kusema hili niligundua kuwa sikuwa na simu yangu. Sikuweza kuwa na hakika kama niliiacha hotelini au nimeipoteza, hivyo niliamua kurudi hotelini kutafuta simu yangu kwakua nilitaka kuwa na hakika kama sijaipoteza. Niliikuta ikiwa juu ya meza chumbani kwetu.
6. Nilikuta kuna simu ilipigwa na kuna ujumbe mfupi wa maneno, kutoka ka Tongo. Niliingia msalani na nikampigia Tongo nikiwa huko. Aliuliza kama tumefurahia hoteli na akauliza ni nini tulikuwa tukifanya jioni hiyo. Pia akauliza kama nilizungumza na mke wangu kuhusu ni matembezi gani ambayo angependa tufanye. Nilimjibu kuwa bado tunajadiriana. Aliniambia kuwa basi nikiwa tayari nimtaarifu pia akauliza kama bado nina mpango wa kwenda kubadirisha pesa kesho yake. Nilijibu kuwa ndiyo bado nina mpango huo, na tukakubariana kwamba atanifuata kesho yake mchana. Nilimuuliza kama kafanikiwa kufanya mpango wa safari ya helkopta niliyomwambia. Alinijibu kuwa mpango ulikuwa unaenda vizuri na alikuwa amekweisha zungumza na rubani wa ndege ambaye ataweza kufanya mpango wa sisi kufanya safari ya helkopta kwa kiwango cha pesa niliyomwambia yani R15,000. Alidai kuwa alihitaji alipwe nje ya ofisi tena kwa pesa taslimu na itabidi tuendane na ratiba atakayotupatia. Nilimjibu kuwa ni sawa kwa kuwa tuko huru hatujabanwa na lolote hivyo tunaweza kuendana na ratiba yake. Nilimkubusha kuwa nahitaji iwe safari ya kipekee yani yangu mimi rubani na Anni tu. Tongo alikubari kuwa itakuwa hivyo na akadai kwamba itabidi tukutane na huyo rubani siku ya Jumamosi kufanya mipango na kufanya malipo. Nilirudi Sevruga.
7. Nilimtaarifu Anni kuwa Tongo alinipigia na kesho nitaenda naye kubadiri fedha. Alidai kwamba ingekuwa msimu wa joto angependa kuogelea kwenye bwawa la hoteli. Baada ya kula chakula mazungumzo yetu yalirudi tena kwenye kadi ya bank na nilimtumia ujumbe mfupi baba yake nikimwambia kuwa Anni anataka uifunge kadi yako. Alijibu kuwa hilo halikuwa tatizo na akaomba nimtumie namba za kadi. Sote tulicheka sana kwa jibu lake kwakuwa Anni hakufikiria kama anaweza toa jibu lile. Baada ya chakula tulitembea kuelekea kwenye sehemu maji yanaporuka (waterfront) mpaka kwenye baa. Tulipata vinywaji pale halafu tukatembea kurudi hotelini.
Siku ya Jumapili – Cape town
8. Baada ya kupata kifungua kinywa, tulielekea kwenye bwawa la kuogelea la hoteli. Nilipokea ujumbe mfupi toka kwa Tongo kuwa alikuwa akinisubiria nje ya hoteli. Nilikuwa nimekwisha sahau kuwa tulipanga kwenda kubadiri fedha. Anni alichagua kubaki kwenye bwawa kuogelea, nilimtumia Tongo ujumbe mfupi kuwa anisubiri nakuja sasa hivi. Nilienda chumbani kwetu nikabadiri nguo na kuchukua Pound 5,000 zikiwa katika noti za pond 50 pia nilibeba pasi yangu ya kusafiria na nikaelekea kwenye mlango wa mbele wa hoteli ambapo Tongo alikuwa kanisubiri.
9. Tongo alinitaarifu kuwa tunaenda kubadirisha fedha mjini na kuwa alikuwa kapata namba ya anayebadirisha fedha toka kwa mteja wake siku za nyuma na akadai wanabadiri fedha ka viwango vizuri sana. Alikuwa akijinadi kuwa yeye ni mtu ambaye anakuwa na kazi nyingi (busy). Aliegesha gari pembeni ya barabara na tulitembea tukavuka barabara mpka kwenye duka lilikuwa na bango limeandikwa Golden Touch.
10. Kweneye duka alikuwepo mwanamama kwenye uzio wa kioo, nilimuuliza viwango vyao vya kubadirishia fedha akajibu ni 10.5 nikamwambia anipe kiwango kizuri zaidi kwa maana nataka badirisha Pound 5,000 kwakuwa kiwango alichonitajia hakikuwa kizuri sana kuliko kiwango cha Western Union, lakini aligoma hivyo nikaamua kubadirisha Pound 1,000 tu kutoka kwenye pesa niliyokuwa nimebeba kiasi cha pound 5,000. Nilipokea R10,500. Muda wote huu Tongo pia alikuwa mle dukani akizungumza na mfanyakazi mmoja ambaye nilihisi kuwa wanafahamiana.
11. Wakati tukirudi kwenye gari nilimuuliza Tongo kuhusu mipango ya safari ya helkopta. Nilitaka anipe uhakika kama kweli jamaa yake ataweza kuandaa hiyo safari au nifanye mpango wa kutafuta sehemu nyingine. Alinihakikishia kuwa ni kweli atanda safari hiyo na kamba anatafuta muda ili atukutanishe na huyo rubani kwa mazungumzo na malipo. Nilimuuliza Tongo ni lini naweza kukutana na huyo rubani na kama inawezekana nikutane naye muda huo. Tongo alinijibu kuwa kwa muda huo rubani alikuwa kazini ila akadai ya kamba atapanga ili tukutane join kuzungumzia mipango ya hiyo safari na kufanya malipo. Nilimwambia kuwa hiyo safari ilikuwa ni surprise kwa ajili ya Anni na inabidi asitoe hiyo siri. Nilimuuliza Tongo mahali tunapoweka kwenda kula kwakuwa Sevruga japo walikuwa na huduma nzuri ila ilikuwa kuna watu wengi sana. Aliniambia kuna mghahawa katika eneo la Stellenbosch –somerset West ambao alidai ni mzuri kwa wapenao ila akasema jina la huo mghahawa kalisahau. Aliongeza kuwa wateja wake wengine aliwahi kuwapeleka na walipapenda sana. Nilimuuliza kama jioni anaweza kutuzungusha mjini kwakuwa tulikuwa hatujazunguka mji wa Cape Town, na nikamwambia baada ya hapo atatupeleka kwenye huo mghahawa aliosema ili tule chakula cha usiku. Tulikubariana atufuate saa 1 na nusu jioni.
12. Tulipokaribia hotelini nilimuuliza ni kiasi gani ananidai kama mallipo ya usafiri wa kunipeleka kubadirisha pesa na ni kiasi gani atanitoza kwa ajili ya kutuzungusha join, kutupeleka mghahawani na kuturudisha. Nilimuuliza kama vyote anaweza nifanyia R1000 na alikubari akasema basi nitamlipa usiku atakapoturudisha.
13. Nilirudi chumbani nikahifadhi pesa na kubadiri nguo nikavaa nguo kwa ajili ya kuogelea. Nilienda kwenye bwawa la kuogelea ambapo Anni alikuwa bado anaogelea. Nilimtaarifu kuwa nilipanga na Tongo aje kutuchukua kutuzungusha mjini na baadae atatupeleka kula chakula cha jioni. Alijibu kuwa hiyo itakuwa safi.
14. Anni alitaka nikanyoe nywele zangu na kuwekewa dawa nyeusi kuficha mvi zangu. Nilienmda katika Salon, na huko niliulizia kuhusu mghahawa ulioko Stellabosch-somerset West. Nilitafuta mighahawa mbalimbali kupitia simu yangu na nilizungumza na mhudumu wa mapokezi kama anajua mghahawa mzuri, na niliamua kumwambi dada wa mapokezi anifanyie booking kwenye mghahawa wa ujulikanao kama 96 Winney Road na kuwa tutakuwa pale saa 3 na nusu usiku kwa ajili ya chakula hivyo tuandaliwe meza kwa ajili ya watu walioko kwenye fungate.
15. Nilirudi salon baadae maana maa ya kwanza niliambiwa nirudi baada ya saa moja, hivyo nilinyolewa na kuwekewa rangi ya nywele, na baada ya zoezi hili nilirudi kwenye bwawa tukaagiza chakula kwakuwa tulikuwa hatujala chakula cha mchana toka tulipopata kifungua kinywa. Baada ya kula chakula sote tulisnzia pembeni ya bwawa. Niliposhtuka toka usingizini Anni alikuwa tayari amekwisharudi chumbani kwetu na alikuwa kanitumia ujumbe mfupi.
16. Tulijiandaa kwa ajili ya safari hiyo ya jioni. Sikuwa nimeongea na Tongo toka tulipoachana na nilitaka kujua mipango ya Helkopta ianendaje. Aalikuwa kaniambia kuwa ataandaa nikutane na rubani join hiyo na nilitakiwa kulipa pesa taslimu. Nilichukua R10,000 niliyokuwa nimebadiri kwa ajili ya kufanyia malipo ya awali. Kwakuwa ela haikuweza kuingia kwenye mfuko wa suruali la suti yangu nilimwomba Anni anihifadhie ile pesa kwenye pochi yake. Pia kwenye mfuko wa suruali langu nilikuwa na R4000 kwa ajili ya kumlipa Tongo malipo yake ya R1000 na kwa ajili ya malipo ya mambo mengine tutakayofanya.
17. Wakati mimi na Anni tukiwa India kwa ajili ya maandalizi ya harusi yetu tulikuwa tukitembea na pesa nyingi kwa kuwa wasambazaji wa vifaaa vya harusi tuliokuwa tukiwatumia wengi walikuwa wamiliki wa makampuni madogo ambao walikuwa wanakubari malipo kwa njia ya pesa taslimu tu. Hivyo Anni ndiye alikuwa akibeba pesa kwenye pochi yake muda wote kwakua tulikuwa tukitembea na maburungutu makubwa ambayo yasingeweza kuingia kwenye mifuko ya suruali zangu.
18. Tulielekea kwenye baa ya hoteli mnamo mida ya sa 12 na nusu na kukaagiza vinywaji. Tulipiga picha na kuongea mamabo mablimbai. Tongo alinitumia ujumbe mfupi kabala ya saa1 na nusu kuwa angechelewa kidogo. Pia alinibip nikampigia, aliniambia kuwa hatoweza kuwahi atachelewa sana hivyo tulielekea kwenye sehemu ya mapumziko ya hotei tukakaa huko tukimsubiri. Baadae alinitumia ujumbe mfupi akinitaarifu kuwa amekwishafika yuko nje ya hoteli. Tulienda kwenye gari lake na kumwambia jina kla mghahawa ambao tulifanya booking na tulimtaarifu kuwa inatubidi tuwe pale saa 3 na nusu. Hivyo tulianza kwa Tongo kutuzungusha mjini. Nakumbuka niliona sehemu ya kufugia samaki kwenye kioo kikubwa, karakana ya magari ya BMW na uwanja wa michezo wa Cape Town. Pia tulielekea kwenye barabara ilielekea milimani ambapo ukiwa huko unaweza kuona mji kwa chini ambapo usiku unaona ukwiaka na kuvutia. Katika safari yetu mimi na Anni tulikuwa tukizungumza na kucheka kwa lugha ya Gujirati. Tulizungumza mambo mengi ikiwemo tafrija ya motto wa Preyern na kuhusu hii safari yetu ya fungate.
19. Baadae tulianza safari ya kuelekea mghahawani na tukiwa safarini Tongo alisema kuna jambo moja ambalo anataka kutonyesha, na ni mghahawa maarufu hapo kwakuwa Jamie Oliver aliwahi kula hapo. Tuliacha njia kuu na kuingia kwenye kitongoji ambacho kilikuwa kimejaa watu waliofungulia mziki kwa sauti ya juu sana. Watu wengi niliwaona kitongoji kile walikuwa ameshikilia chupa za pombe na walionekana kuwa walikuwa wakiburudika, Tongo aligeuza gari tukarudi kwenye barabara kuu.
20. Kwenye safari kuelekea mghahawani mimi na Anni tuliamua kwamba hatuhitaji chakula kizito kwakuwa tulikuwa tumekwishakula hivyo tutakula chakula cha kawaida . hivyo tuliamua kwamba tutakula sushi kama tuliyokula Sevruga. Tulimuuliza Tongo tutapata wapi sushi nzuri, akatujibu kuna mghahawa ila uko mbali kidogo tunaweza kupata sushi nzuri pale.
21. Kwa makubariano Tongo alitupeleka kwenye huo mghahawa ambao ulikuwa kando kando ya bahari, akapaki gari na kutuongoza kuingia kwenye jingo ambalo ngani tukajikuta tuko kwenye mghahawa wenye jina la Surfside.
22. Nilimwambia Tongo kuwa nitamtumia ujumbe mfupi tutakapomaliza hivyo yeye hakuingia mghahawani.
23. Tulikuwa tumekaa pembeni ya dirisha kubwa la kioo tukitazama bahari. Mghahawa ulikuwa na sakafu ya mbao na pembeni ya mlango wakuingilia kulikuwa na sehehmu ya kuchezea mziki na mziki laini ulikuwa ukipigwa.
24. Nilienda msalani, na nikiwa huko nilibipia na Tongo. Nilimpgigia simu , lakini mtandao ulikuwa chini na ghafla mziki waliongeza sauti hivyo ikanilazimu kutoka nje ya mghahawa niweze kuzungumza naye. Nilimuuliza alitka kitu gani akasema alitaka kujua tutakaa muda gani. Nilikuwa sina hakika kwakuwa ndipo kwanza tulikuwa tumeagiza chakula, nilimuuliza kama ameongea na rubani akajibu kua bado anamtafuta pia akauliza kama nilibeba pesa ya kulipia. Nilimjibu asiwe na wasiwasi kuhsu pesa na nikamwambia anitaarifu kama itawezekana kwenda kukutana na rubani. Nilimwambia kuwa mghahawa haukuwa wa hadhi yetu na nilimuuliza nini tunaweza kufanya baadae na akajibu kuwa kuna sehemu nyingi anaweza kutupeleka atatuelezea tukimaliza.
25. Nilirudi mezani kwetu, na chakula kililetwa. Nakumbuka wakati tunakula nilipokea ujumbe mfupi toka kwa Tongo akidai kuwa amekwisha tatua tatizo na mimi nilimjibu. Nilichukulia ujumbe huo kuwa kamaanisha kuwa amekwihsa zungumza na rubani wa helkopta. Nilipomaliza kula nilimtumia ujumbe mfupi Tongo kumtaarifu kuwa tulikuwa tunatoka mghahawani.
26. Wakati tunatoka kwenye mghahawa, tuligundua kuwa Tongo alikuwa kasogeza gari karibia na mlango wa kuingia na kutoka mgahawani. Tulipoingia kwenye gari mimi na Anni hatukuwa tumepanga tutafanya nini baada ya chakula cha usiku hivyo tulimuuliza Tongo atupe mawazo yake naye alitoa mapendekezo ya vile vitu ambavyo alihisi vinaweza kutvutia na Anni alikubariana naye.
27. Kutokana tukio baya lilitokea na kusababisha kumpoteza mke wangu, nimekaa hospitali miaka mitatu nikiwa nimepata matatizo ya kiakili na msongo wa mawazo kwasababu ya kumbukumbu ya tukio hilo baya, japo nimeathirika kumbukumbu na inakuwa vigumu kupangilia matukio kwa usahihi lakini nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuweka ukweli wa kile kilichotokea.
28. Mimi na ANni tulikuwa tukitazama picha tulizopiga kupitia kamera yetu wakati majadiriano yakiwa yanaendelea kuhusu nini tufanye usiku huo.
29. Katikati ya safari nilipokea ujumbe mfupi kutoka ka Tongo, japo siwezi kukumbuka maneno halisi aliyoandika ila ujumbe huo ulikuwa unahusu pesa. Alikuwa akiuliza kama nimebeba pesa, na mimi moja kwa moja nikahisi anaongelea pesa kwa ajili ya malipo ya safari ya hrlkopta na nikawaza kuwa kaamua kunitumia ujumbe mfupi ili Anni asijue maana inabidi iwe surprise kwake. Hivyo na mimi nilimjibu kwa ujumbe mfupi kuwa pesa ninayo.
30. Tulitoka barabara kuu na kwa mbele niliona alama ya barabarani yenye rangi ya kijana ikiwa inaanzia na herufi ‘G”.
31. Kitu nachokumbuka ni ghafla kusikia sauti za watu wakigongagonga gari kulia na kushoto. Kulikuwa na kelele nyingi katika lugha ambayo mimi sikuielewa. Mara ghafla kuna mtu akawa amekaa pembeni yangu akiniamuru kuinama chini huku akiwa kashikilia bunduki mkononi japo sikumbuki ni mkono gani. Alikuwa akipunga bunduki hewani. Alikuwa akipiga kelele “tazama chini, inama chini!”. Sote tuliogopa sana na mara moja tulitekeleza amri zake. Nilikua nimemlalia Anni na mtu mwingine alikuwa ndiye anaendesha gari sikujua Tango alikuwa wapi kwa wakati huo.
32. Nilijaribu kuwabembeleza watuachie, nakumbuka saa yangu ilichukuliwa kutoka mkono wangu wa kushoto. Kuna kipindi Yule aliyekuwa kashikiria bunduki alipiga kelele “simu na Pesa”. Nilimpatia pesa yote iliyokuwa kwenye mifuko yangu na simu yangu nilikuwa nimeificha kwenye mfuko wa suruali. Anni alininong’oneza kwa kiGujirati kuwa alikuwa kaficha pete zake katikati ya siti za nyuma. Yule mtu mara ghafla alielekeza bunduki kwa Anni, alizungumza Kingereza ila kutokana na jinsi alivyokuwa akitamka maneno ilikuwa vigumu kuelewa nini anaongea.
33. Mara akaniambia “simu”. Akaanza kunikagua na kupata simu yangu kwenye mfuko wa suruali. Alikasirika sana. Aligandamiza bunduki kwenye sikio langu la kushoto na kuniambia maneno ambayo yalimaanisha kuwa nisirudie tena kumdanganya la sivyo atanipiga risasi. Nilisikia sauti ya kuonyezwa kwa bunduki na nilizidi ogopa sana. Sikuwahi kuwa karibu ama kushikiria bunduki kabla ya hapo. Muda huu wote gari ilikuwa inakimbia kwenye barabara ya vumbi yenye mashimo. Baada ya kutuchulia mali zetu aliendelea kusema “tazama chini”. Hivyo sikuwezi kuona vizzuri ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Mara ghafla gari lilisimama. Nilitazama juu na kumuona Tongo nje ya gari kwa kupitia kioo cha abiria upande wa mbele. Niliona uso wake kwa sekunde na mara ghafla gari likaondoka kwa kasi. Mtu ambaye alikuwa kaka pembeni yangu muda huu alikuwa kaka mbele kwenye siti ya abiria.
34. Nakumbuka niliamriwa kukaa. Nilipokaa niligundua tuko kwenye barabara kuu. Gari lilipunguza mwendo, na tulipishana na gari la polisi. Niligundua kuwa dereva wa gari letu alikuwa amevaa gloves za njano. Tulipopishana na gari la polisi niliambiwa tena nilale chini na Yule aliyekuwa kashikiria bunduki.
35. Tulitokamkwenye barabara kuu tuaingia kwenye barabara nyembamba. Anni alikuwa akipiga makelele. Wote waliniamuru nimwambie Anni aache kupiga kelele akae kimywa. Dereva lituambia kuwa hawatotudhuru wao wanataka tu gari na wangetuachia tuondoke ila kila mtu kwa njia yake. Niliwaomba watuachie tuondoke wotenilimwomba Anni anipatie pete zake. Alinipatia pete lakini sikuona vizuri ni pete gani aliyonipatia kati ya pete ya uchumba au ndoa. Niliwaonyesha pete na kuwambia chukueni hii pete tuachieni twende. Yule aliyekuwa na bunduki aliichukua na kuitazama.
36. Walianza kuzungumza baina yao lugha nisiyoielewa na mara ghafla wakaanza piga kelele wakiniamuru nishuke kwenye gari. Niliwaomba sana watuachie sote twende. Waligoma na dereva akasema kuwa Anni watamucha kituo cha polisi. Nilizidi sisitiza kuwa mimi na Anni inabid tukae wote. Walikasirika sana na kuniamuru nishuke kwenye gari. Nilijaribu kufungua mlango haukufunguka mara ghafla nikaona kioo kinafunguka ghafla na mara nikajikuta nimedondoshwa chini na gari ikaondoka kwa kasi. Nilipiga kelele kumambia Anni abaki kimya asiseme chochote na nilimwambia kwa lugha ya Gujirati.
37. Nilikimbia kwenye nyumba iliyokuwa karibu na kubisha hodi lakini hakuna aliyeitika. Niligonga kwenye nyumba nyingine na kupiga kelele nikiomba msaada, lakini hakuna aliyejitokeza. Kwa mbele upande wa kushoto wa barabara niliona gari ikiwa inaingia kwenye maegesho. Nilikimbia mpaka kwenye gari na kumuomba dereva awapigie askari polisi, naye alifanya hivyo. Baada ya muda askari wawili waliwasili na niliwaeleza jambo lililotokea. Mwanzo hawakunielewa, labda kwakuaw nilikuwa nimechanganyikiwa na matamshi yangu ya lugha pia. Niliulizwa namba za usajili za hilo gari na pia niliulizwa kama nina namba ya dereva tax. Niliwambia ninaweza kupata hiyo namba kutoka kwenye server ya blackberry kwa kumpigia mtu anitumie toka London na pia wataweza kuifuatilia simu. Nilitaka kupiga simu UK lakini ilishindikana kwakuwa simu ya askari ilikuwa haiwezi kupiga simu za kimataifa.
38. Basi niliingia kwenye gari la polisi na tukaanza kuzunguka sehemu mbalimbali tukitafuta ile tax. Walikuwa wakizungumza katika lugha ambaye sikuielewa na mara chache sana walikuwa wakizungumza kingereza. Askari police alielewa vibaya rangi ya gari tofauti na nilivyomueleza hivyo nilikasirika sana. Walinipeleka kituoni ambapo nilianza kujaza dodoso na kuanza kuniuliza nitoe maelezo ya kitu gani kimetokea. Niliwahadithia upya na polisi mmoja alikuwa akiandika kenye daftari maelezo yangu. Ilikuwa vigumu kwangu kuelewa walikuwa wanazungumza kitu gani kutokana na sababu kwamba walikuwa wakizungumza lugha nisyoelew.
39. Nilirudishwa kwenye hoteli ya Cape Grace kwa gari la polisi ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari polisi mweupe. Aliniambia wataweza kupata picha ya gari kutoka kwenye kamera za ulinzi za hapo hotelini. Pia niliweza kupiga simu za kimataifa kutokea hapo. Pale hotelini askari alizungumza na mkuu wa ulinzi wa hoteli. Nilizungumza na Preyer na preyer alifanya mkutano wa simu kwa kumuunga baba pia ambaye aliweza kunitumia namba ya Tango kutoka kwenye server za blackberry, pia aliwapigia Vodafone kuona kama wanaweza kujaribu fuatilia simu.
40. Polisi wengine waliwasili huku wengine wakiwa wamevaa kiraia na kila askari alikuwa anaiuliza maswali na nilikua nikiwajibu. Ilikuwa inakuwa vigumu kunielewa na wao nilikuwa npaa ugumu kuwaelewa. Colonel Els aliagiza kila mtu kutoka kwenye chumba isipokuwa askari mmoja tu wa kuandika maelezo yale niliyoyasema. Askari aliandika maelezo na kuniambia niweke sahihi yangu. Sikujishughulisha kusoma alichokiandika ila nilitia sahihi kila sehemu aliyoniambia. Kuna wakati nilipelekwa kwenye maktaba ambapo kuna askari alikuwa kaka na kompyuta na waliniambia niwasaidie kutambua wavamizi. Nilimwona Tongo yuko pale alionekana akiwa anajaribu kutoa msaada kwa askari.
41. Nilizungumza na familia yangu mara kadhaa kupitia simu. Kuna wakati polisi walikuwa wakijadiriana juu ya kutuma helkopta kusaidia katika kutafuta hilo gari. Nakumbuka baada ya kuambiwa kuwa atatuma helkopta waliondoka na kuniacha na Tongo. Alikuwa akinihakikishia kuwa askari watampata mke wangu na alionekana akiwa ametishika na kile kilichotokea.
42. Kuna wakati asubuhi nilizungumza kwa simu na Preyern ambaye aliniambia nikae chumbani kwangu nisitoke. Nilirudi chumbani kwangu na daktari alikuja na kukaa name.
43. Kuna mtu alikuja na kusema kuwa kuna simu yangu kwenye chumba cha mawasiliano. Ilikuwa Preyern na aliniambia wamempata Anni akiwa kapigwa risasi. Hapo hapo niliona kama dunia inaniangukia. Kitu ninachokumbuka nilijikuta niko na daktari na ninapewa vidonge chumbani kwangu.
Jumapili – Cape Town
44. Jumapili niliomba nipelekwe kwenye nyumba ya ibada yaw a Hindu ambako nilizungumza na kiongozi wa dini.
45. Baadae nilirudishwa hotelini, na baada ya hapo nilipata simu na jumbe fupi za maneno toka kwa marafiki na wanafamilia wakijaribu kunipa pole na kunitia moyo. Nilikuwa nina taarifa kuwa baba yangu na baba yake ANni walikuwa safarini kuja Cape Town.
46. Jinoni Kapteni Hendrikse, Colenel Theron na Kapteni Lutchman walikuja hotelini.
Walikuwa wameleta makaratasi na pete ya uchumba ya Anni. Nilishangaa kuiona hiyo pete kwakuwa nilikuwa ninakumbuka niliapatia wale watekaji tukiwa kwenye gari. Niliwaelezea jinsi gani Anni alikuwa kaficha pete zake na niliwambia wajaribu kutazama kama ile pete nyingine kama ipo kwenye gari. Kapteni Hendrikse alikubari kufanya hivyo. Ilikubariwa kwamba Kapteni Luchman atanifuata pale hotelini asubuhi ya siku inayofuata ili nipelekwe kutambua mwili wa mke wangu.
47. Jioni ya siku hiyo baba yangu na baba yake Anni wote waliwasili pale hotelini.
Jumatatu – Cape Town
48. Nlichukuliwa na Kapteni Luchman na nikapelekwa kuona mwili wa Anni na kuuambua. Lilikuwa ni tukio ngumu sana kwangu na nilipata mshtuko baada ya kuona mwili wa marehemu mke wangu.
49. Kapteni Luchman alinirudisha hotelini na siku hiyo nilishinda na familia yangu na baadhi ya marafiki waliofika pale hotelini kutuunga mkono.
50. Kapteni Hendrikse alikuja pale hotelini join na akasema kuwa alitaka kuzungumza na mimi. Aliniambia twende wote kwenye ofisi yake iliyoko Belleville.
51. Tukiwa ofisini kwake aliniambia kuwa amesoma maelezo yangu ambayo niliyatoa siku ya Jumamosi na anahisi hayakuwa maelezo yanayojitosheleza. Na akadai kuwa kichwa cha habari cha yale maelezo hakikuwa na mawasiliano yangu. Aliniuliza maswali ya moja kwa moja kuondoa alichodai yalikuwa makosa kwenye maelezo hayo. Alinipatia pete yandoa ya Anni na vito vingine, na akaniambia niweke sahihi ya kuthibitisha kuwa nimepewa vitu vya marehemu. Alinirudisha hotelini.
Juma nne – Cape Town
52. Asubuhi ya siku ya Jumanne Kapteni Luchman aliwasili pale hoteini kama ilivyokuwa imepangwa kuwa atatupeleka kwenye nyumba ya kuandaa mazishi kuona mwili wa Anni, wakati tumekaa ubarazani pale hotelini, Kapteni luchman alipokea simu. Kwa mazungumzo aliyokuwa akizungumza kwenye simu ilionekana kama anazungumza na Tango. Nilikuwa sijazungumza na Tango toka siku ya Jumapili nilipomuona hapa hotelini. Nilimuuliza Luchman kama ninaweza kuzungumza na Tango. Nilicukua simu na nikamuuliza Tango anaendeleaje. Sauti yake ilionekana haikuwa sawa na alisema kwakweli hayuko sawa. Alidai kwamba vyombo vya habari vinamsumbua sana alidai kuwa hakuwa na pesa na kwasasa hakuwa na gari hivyo hana jinsi ya kupata kipato cha kujikimu. Aliongeza kuwa hajui ataishije. Nilimuonea huruma na nikaamua kuwa nitampa ile R1000 ambayo ningemlipa kwa huduma aliyotupatia siku ya Jumamosi.
53. Nilimwambia Tango kuwa ninaondoka usiku wa siku hiyo kurudi Uk, na nina kitu nataka nimpatie hivyo basi aje anione kabla sijaondoka. Aliniambia kuwa hana uhakika kama ataweza kuja kwakuwa hakuwa na gari ila ataona kama atweza kupata lifti kutoka kwa rafiki yake. Nilimpa namba ya simu ambayo hoteli ilikuwa imenipa nitumie kwa muda na nikamwambia anatakiwa anipigie atakapokuwa tayari kuja pale hotelini.
54. Baba yangu na baba yake Anni waliondoka na Kapteni Luchman kwenda kwenye nyumba ya kuandaa mazishi kuona mwili wa Anni. Nilichagua kutokwenda kwakuwa ilikuwa imeniathiri sana nilioona mwili wake jana yake.
55. Nilielekea madukani kununua vitu vya kuwapa kama shukurani wale wote waliokuwa wakitupatia msaada kwa kipindi chote. Wafanyakazi wa hoteli walinitaarifu kwamba nje kuna waandishi wa habari na itakuwa vizuri nikitoka na gari la hoteli ili kujificha na waliniandalia gari hilo.
56. Nilienda kwenye duka na kununua box la kadi kumi za kutengenezwa kwa mkono zenye asili ya mandhari ya kiafrika. Mhudumu aliweka hilo box kwenye mfuko mweupe wa palsitiki.
57. Nilikuwa bado madukani nilipopigiwa simu na Tongo. Aliniambia kuwa alikuwa kapata lifti na mimi nilimwambia niko madukani na nilikuwa nakaribia kurudi hotelini. Nilirudi hotelini, na kwenda chumbani kwangu nikachukua kadi moja na kuandika maneno ya kumshukuru, kasha nikaweka hiyo kadi na R1000 ndani y bahasha. Niliweka hiyo bahasha katika mfuko wa plastiki mweupe niliopewa kule dukani na kutoka chumbani nikiwa niubebelea.
58. Sina kumbu kumbu kama mimi ndiye nilimpgia Tongo ama ni yeye alinipigia. Nilimuomba aingie hotelini sikutaka kutoka nje kwakuwa nilikuwa ninajua kuna waandishi wa habari. Nilipomuona Tongo anaingia hotelini nilitoka kwenye korido na kutembea kuelekea kwenye chumba cha mawasiliano cha hoteli ambapo matukio yote yalifanyika usiku wa Jumamosi. Tongo alinifuata nyuma. Nilimshukuru kwa msaada wake na nilimpatia mfuko mweupe nikamwambia kulikuwa na kitu kwa ajili yake. Aliniambia nasikitika kwa yale yaliyotokea. Nilimuuliza kama anajua ni lini atapata gri lake na aliniambia hajui. Tulipeana mikono na mimi nilitoka kwenye chumba cha mawasiliano nikimwacha humo.
59. Jioni nilichukuliwa na baba yangu pamoja na baba Mkwe mpaka kwenye uwanja wa ndege wa Cape Town ambapo tuliondoka na ndege kuelekea Amsterdam ambapo tulichukua ndege mpaka Bristol.
Hitimisho
60. Napinga kuwa nina hatia juu ya makosa ninayotuhumiwa nayo.
Hukumu
Shrien Dewan hakukutwa na hatia ya kupanga mauaji ya mke mkewe, Anni Dewan katika fungate ya ndoa yao mwaka 2010.
Jaji aliysikiliza kesi hiyo ajulikanaye kama Jeannette Traverso, alikubariana na upande wa utetezi uliotaka kesi ifutwe, huku ukilaumu waendesha mashitaka kwa kufungua kesi ambayo imeegemea tu kwenye ushahidi wa wa watuhumiwa kama mashahidi wakuu huku mmoja wao akiwa aliwahi kufungwa kwa kosa la kuongopea mahakama.
Jaji Traverso akisoma hukumu alisema kuwa ushahidi uliotolewa ulikuwa umejaa makosa mengi, uongo na mpangilio mbovu wa matukio jambo ambalo limenisababisha nisiuzingatie. Hivyo kwa kufuta hiyo kesi Shrien hakutakiwa hata kusimama kujitetea mahakamani.
Familia ya Anni Dewan walidai kwamba haki haikutendeka kwa kumuachia huru Shrien. Mdogo wake wa kiume Anni Dewan alidai kuwa kwa kufutwa kesi hiyo hawatoweza kusikia upande wa Shrien akitoa mlolongo wa matukio kwa upande wake mahakamani.
Mwisho.
Inapatikana kwa pdf na kwenye video kwa lugha ya Kiswahili.
Jiandaeni kusoma Mauaji ya vizazi vitatu vya familia moja ili kurithi kampuni.