Mauaji na wauaji wa marehemu Notorious B.I.G

Mauaji na wauaji wa marehemu Notorious B.I.G

Suge Knight alikuwa member wa crispy Gang akiwa na cheo kikubwa tu...hapo imekuaje watu wa Gang ya Suge knight wakajumuika pamoja kwenye party ambayo baadhi ya member wa Bad boy records ambayo ilikuwa na uhasama na Death row ya suge knight ambae ni member wa crispy tena cha kushangaza zaidi hadi Blood Gang walikuwepo kwenye party ambao ni mahasimu wa crispy..I think hii interaction hapa ndio inayoleta mkanganyiko juu ya mauaji yalotokea siku hiyo.

Kuna Crips na Bloods. Ndani humo kuna sets mbali mbali kulingana na mtu anapotokea. Kutokana na upinzani, wanachama wa Bloods hawatumii herufi 'C', wala Crips hawatumii herufi 'B', especially not in naming their sets. Suge alikuwa member au associate wa Bloods (you can't miss the red suits), siyo hiyo uliyoitaja.

For your info pia, Bloods and Crips can hang out, kwa sababu sometimes hawa watu wamekuwa pamoja. Vile vile kunaweza kuwa na tofauti kati ya sets tofauti ndani ya gang moja.

Ukihitaji elimu zaidi kuhusu gangs and their politics, usisite mzazi.
 
Notorious BIG au kwa jina lake la ubatizo Christopher Wallace, anasafiri kwenda Los Angeles Marekani, ilikua Februari 1997, anaenda ku promote albamu yake ya "Life after Death", na video ya nyimbo yake ya "Hypnotize".

Tarehe 5 Machi, alialikwa kwenye mahojiano ya Radio, hapo ilikua mji wa San Francisco, na hapo anakiri wazi kwamba anahofia maisha yake, hivyo imembidi aongeze ulinzi. Anasema zaidi ni uhasama unaondelea kati ya makundi ya hip hop ya mashariki na magharini yaani "East coast and west coast", pia mauaji ya Tupac Shakur miezi sita kabla, na ukizingatia yeye ni msanii wa hip hop mkubwa.

Albamu yake ya Life after death ilipangwa kutolewa tarehe 25 Machi 1997.

Tarehe 7 Machi, anatoa tuzo za Soul Train Music Awards kwa Toni Braxton, hapa ilikua Los Angeles Marekani, wakati wa utoaji wa tuzo alizomewa na baadhi ya mashabiki. Kesho yake jioni anaenda kwenye after party ambayo alialikwa, wageni wengine walikua Faith Evans, marehemu Aaliyah, Sean Combs au P.Diddy, na memba wengine wa kikundi kijiitacho Bloods na Crips.

Tarehe 9 Mach, muda wa saa 6:30 usiku, B.I.G anaondoka na usafiri wake kurudi hotelini kwake, na hii ni sababu jeshi la zimamoto la Los Angeles liliamua kusimamisha party mapema sababu ya wingi wa watu kuzidi kipimo,

B.I.G yupo kiti cha mbele karibu na dereva, ambapo hakua peke yake bali alikua na wenzie, "D-Roc", "Lil Cease", na dreva wake "G- Money". P.Diddy yeye alikua kwenye gari nyingine na alikua na mabodigadi watatu, gari zingine mbili zilikua zimembeba Mkurugenzi wa Usalama wa Bad Boy Records.

Muda wa saa 6:45 usiku, mitaa tayari ilikua imejaa watu wengi, waliokua wanaondoka kwenye party, gari aliyopanda Notorious B.I.G, inasimama kwenye taa za barabarani wakati huo ilikua imewaka taa nyekundu, mita 46 tu kutoka mahali alipokua kwenye sherehe, gari nyeusi aina ya Chevrolet Impala SS, taratibu ikaja kusimama karibu na gari aliyokuwamo Notorious BIG, dereva aliyekua anaendesha anashusha kioo chake taratibu anatoa bastola aina ya Geko 9mm na kupiga risasi nne za nguvu, zote zinampata Notorious BIG, risasi moja kati ya nne ndio ilikua ya kuua , ikipiga moyo na pafu la kushoto, baada ya kufanya mauaji hayo, gari iliyokua na muuaji aliyefyatua risasi inaondoka kwa kasi eneo hilo, watu aliokua ameongozana nao Notorious BIG, wanamkimbiza hospitali ili kujaribu kuokoa maisha yake, madaktari wanajaribu kuokoa maisha lakini wanachelewa na kutangaza kifo cha Notorious BIG muda wa saa 7:15 usiku.

Tumfahamu Russell Poole

Kwa kiasi kikubwa alifanya uchunguzi wa nani au akina nani walimuua Notorious BIG, uchunguzi wake mkubwa pia uliweka hadharani maovu mengi yaliyokua yanaendelea katika jeshi la polisi la Los Angeles Marekani, ambapo iligundulika baadhi ya ma afisa wa polisi kuhusika na mauaji ya Notorious BIG, na zaidi walikua wanafanya kazi pia na mmiliki wa lebo ya Death Row, Suge Knight, japo Detective Poole alikwamishwa na kukutana na vikwazo vingi katika kuutafuta ukweli lakini kwa kiasi kikubwa alifichua mengi ambayo hadi hivi leo ndio yanakuja hadharani, alifariki mwaka 2015 kwa mshtuko wa moyo. Anasema waliohusika na kifo cha B.I.G walikua

Mwana afisa usalama Rafael Perez, David Mack au D-Mack, na mshukiwa ambaye anatajwa alionekana eneo alipokua anaondoka BIG na alikuja kusimama mbele ya mmoja wa mabodigadi wa Notorious BIG kwa sekunde chache kabla ya kuondoka, majina yake ni Amir Mohammed ambaye anasemekana ndie aliyemmiminia risasi BIG, kwa pamoja hawa ndio wanahusishwa kwa kias kikubwa kwenye mauaji ya Notorious BIG, Afisa usalama D Mack au David Mack alifanya uporaji katika mojawapo ya benki Marekani na mpenzi wake ambaye alikua mfanyakazi wa hio benki alikiri kushirikiana na boyfriend wake huo kutekeleza uhalifu huo ambao baadae D Mack alipatikana na hatia na kufungwa ambapo jumla ya dola 720,000$ ziliibwa na hadi anaingia gerezani hakuwahi kusema hizo hela aliziweka wapi, na inasemekana ilikua ni kwa ajili ya malipo ya Amir Mohammed ambaye hakulipwa pesa yote baada ya kutekeleza mauaji hayo ya BIG, sababu ya kutolipwa kiasi chote alichoahidiwa ni kua alitakiwa pia afanye mauaji au assassination ya rapa P.Diddy siku hio hio mana walikua wote na BIG.

Lakini hadi hivi sasa hakuna ushahidi wowote uliopatikana ili kuwatia nguvuni na kuwachukulia hatua washukiwa hao, lakini kabla ya umauti kumfika Mwana Afisa Usalama Russell Poole alifanikiwa kuikuta gari iliyotumika kwenye mauaji ya Notorious BIG nyumbani kwa afisa D Mack lakini hilo "limezibwa" kama sio kuzimwa.

Credit iende katika movie ya "city of lies" ambayo ilitakiwa itoke mwaka 2018, ila kutokana na vikwazo vya hapa na pale ilicheleweshwa isitoke ila hatimaye imetoka mwaka huu na inaeleza kwa kiasi kikubwa ukweli wa kilichotokea kwa mafahari hawa wawili wa hip hop, Notorious BIG na Tupac Shakur. View attachment 1132532View attachment 1132533View attachment 1132534

!
!
Sasa Mwananafisa Usalama Ni Nani Hapo? Maana Naona Umekoroga Kweli Kweli Hapo.
 
Kuna Crips na Bloods. Ndani humo kuna sets mbali mbali kulingana na mtu anapotokea. Kutokana na upinzani, wanachama wa Bloods hawatumii herufi 'C', wala Crips hawatumii herufi 'B', especially not in naming their sets. Suge alikuwa member au associate wa Bloods (you can't miss the red suits), siyo hiyo uliyoitaja.

For your info pia, Bloods and Crips can hang out, kwa sababu sometimes hawa watu wamekuwa pamoja. Vile vile kunaweza kuwa na tofauti kati ya sets tofauti ndani ya gang moja.

Ukihitaji elimu zaidi kuhusu gangs and their politics, usisite mzazi.
Mkuu naelewa sana haya mambo i used to be a gangsta..nakuunga mkono SUGE ni member wa bloods lakini napingana na wewe hapo unaponiambia kwamba ni kawaida kuchangamana kati ya Bloods na Crispy hii kitu haiwez kutokea kamwe kwan kuna uhasama mkubwa kati ya magroup haya na lengo la kuundwa kwa blood ilikua ni kuweaken the superiority of Crispy gang in USA and Canada.Crispy ana Allies wake ambao amashirikiana nao na pia Blood hivyohivyo lakini kuna rivalry kubwa kati ya Bloods na Crispy hili bifu lipo enzi na enzi angalia hata wimbo wa Michael Jackson Beat it video yake utaelewa naongea nini..
 
Mzee Crispy ndio nn hiki mkuu?
 
Moja, hawaitwi 'Crispy', ni Crips. Crips na Bloods uhasama huo ulikuwa zamani sana. DeathRow ilikuwa associated na Bloods wengi, kuanzia security details mpaka artists, ila bado walikuwa associates wa Crips kama Snoop, Tha Dogg Pound, n.k. Hayo mengine unayozungumzia hayapo.
 
Tusibishane yawezekana hakuna unalolijua kuhusu hizi Gangs ingia google halafu search about American Gangs rivalies halafu ubaki na knowledge utakayoipata
 
Sababu zipo nyingi ila kwa uelewa wangu hizi zinaweza kuwa sababu.
1. Hip hop chimbuko lake ni marekani

2. Wanatumia advanced materials kurekodia miziki yao pia wanaproducers wenye elimu kitu kinachofanya miziki yao kuwa bora

3. Wasanii wa hip hop marekani wanasikilizwa dunia nzima(internationaly) kitu kinachofanya kuwa na wigo mpana wa soko.

4. Wapo makini kwenye masuala ya hati miliki wanalipwa kwa mikataba isiyo wakandamiza

5. Wapenzi wengi wa hip hop ni mahustler wauza poda na wanapesa chafu so ikija kwenye masuala ya kununua albamu au kuingia kwenye shoo wanatoa sana sapoti kwa wasanii wanaowapenda.

6. Kupewa airtime ya kutosha kwenye media zao.

7. Msanii husika kujiongeza kwenye masuala mengine kama brand za nguo na mengine mengi.
mkuu unamjua jamaa mmoja anajiita BIG MEECH(sina hakika kama nimepatia jina lake)....?? ambaye inasemekana kuwa ile nyimbo ya akina Fat Joe inayoenda kwa jina la "I MAKE IT RAIN" idea yake waliitoa kwenye lifestyle ya huyo jamaa..

umeongelea wauza madawa ambao ndio mashabiki wakubwa wa hip hop kuwa na pesa chafu, sasa inasemekana huyo jamaa alikuwa ananunua hata copy laki moja kwa kila album ya hip hop inayotaka na akaipenda.

Jamaa alikuwa na hela chafu hata Flyod Maywheather ana Subiri...
 
Ndani ya black mafia family..
Big meech utaskia wafuasi wanajibu hallelujaaah
 
Mkuu naelewa sana haya mambo i used to be a gangsta..nakuunga mkono SUGE ni member wa bloods lakini napingana na wewe hapo unaponiambia kwamba ni kawaida kuchangamana kati ya Bloods na Crispy hii kitu haiwez kutokea kamwe kwan kuna uhasama mkubwa kati ya magroup haya na lengo la kuundwa kwa blood ilikua ni kuweaken the superiority of Crispy gang in USA and Canada.Crispy ana Allies wake ambao amashirikiana nao na pia Blood hivyohivyo lakini kuna rivalry kubwa kati ya Bloods na Crispy hili bifu lipo enzi na enzi angalia hata wimbo wa Michael Jackson Beat it video yake utaelewa naongea nini..
" Mkuu naelewa sana haya mambo i used to be a gangsta.."
US au wapi mkuu
 
Cash Money Records - Birdman na lol wayne mwanzoni walikuwa hawafichi hisia zao kwenye gangs (Blood) siku hizi wameachana na hayo mambo

Wannabes tu. Crips and Bloods asili na ngome yao ni California, Birdman na Wayne hawatokei California. Sio kila anataja gangs ni gang-banger, kuna wazushi na wazugaji wengi tu.
 
Back
Top Bottom