Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Jamani hivi hawa albino wana makosa gani hadi wanauliwa kinyama kama vile siyo binadamu? Nilisoma gazeti moja la kijapani online kuwa nyama ya watu wenye ngozi nyeupe inaliwa na watanzania hivyo maalbino wanauwasa sana kwa ajili ya nyama yao; nilishangaa sana.
 
I'm just sitting here and it just hit me... familia zote zenye Albino zipewe leseni na bastola za kujihami nazo. Wapewe mafunzo ya kuzitumia. Hii ni kwa vile serikali imeshindwa kuwalinda na haki yao ya kujilinda na kulinda maisha yao itumiwe.

Wale maalbino watu wazima wapewe bunduki zao wao wenyewe na wale wenye wana familia basi wapewe silaha hizo ili kulinda familia zao.

Mungu akuone na kukupa jazzah yako mkuu. Inaonyesha kiasi gani unachukuia mtu mwingine kutoa uhai wa mwenziwe bila huruma. Sisi waislamu tunaamini kuwa hata mnyama mpaka alete madhara ndio auliwe kwani kila kiumbe kina haki ya kuwa hai sembuse binadamu.
Kuhusu Familia zenye maalbino kupewa bastola mie sina pingamizi lakini ujue pia familia hizi nyingi ni masikini wasije wakawa tempted kuzikodisha hizo bastola ili ziwaingizie chochote kitu. Ninaloogopa zaidi ni kujipanga kwa hao wanaosaka hivyo viumgo vya Binadamu wenzao pindi wakijua kuwa wanaowawinda wana silaha wao wakatafuta silaha kubwa zaidi kama SMG zilizokatwa vitako na AK 47. Wazo zuri lakini sijui ni jinsi gani linaweza likawa wazo linye kutekelezeka na kuzuia madhara kwa asilimia kubwa.
 
Inaweza kuanzisha kitu kingine kabisa,tunaweza labda kuwa na majambazi maalbino.

Serikali ikiliwekea hili tatizo mkazo,hawa watu wataishi kwa amani tu.

Lakini i support what u said on the notion that,drastic steps have to be taken immediately
 
Nimeshangaa kidogo leo kusikia kuwa eti Serikali haina takwimu za albino katika nchi yetu. Yaani hawajui kuna albino wangapi, hawajui ni wangapi wameuwawa toka mauaji haya yenye mtazamo wa kishirikina yatokee???. Na haijui hawa albino wako wapi!! Usingizi huu ni mzito kwelikweli.

Kwa mtazamo wangu kuwapa silaha za kujilinda ni moja ya suluhisho. Lakini tukumbuke kuwa nyingi ya familia hizi zipo vijijini na wengi wa watu hawa (albino) ni watoto ambao huishi chini ya uangalizi wa wazazi au watu wao wa karibu. Tukumbuke pia kwamba kwa imani zetu za hovyo, huko nyuma familia kupata mtoto albino ilionekana kama ni nuksi kubwa na mara nyingi watoto hao walikuwa wanauwawa na ndungu hata wazazi ili kuondokana na nuksi hiyo. Sina hakika ni kwa kiasi gani dhana hii potofu imeondoka miongoni mwetu hususan wale wa vijijini. Kama imani hii bado ipo, si ajabu ulinzi wa ndugu zetu hawa ukawa mgumu kupindukia, kwani adui mkubwa huenda ikawa ni jamii inayomzunguka, ndugu na jamaa zake. Hili ukiongezea na imani za kishirikina, nachelea kusema kwamba ndugu zetu hawa wamo kwenye viumbe vilimo hatarini kutoweka.

Kwakuwa mengi ya mauaji haya hutokea vijijini, na hadi leo hakuna sababu zinazokidhi haja juu ya nini hasa sababu ya mauaji haya, natamani albino wote watengewe maeneo maalumu yenye ulinzi wa kutosha sehemu za mijini. Kwani sijapata kusikia mauaji haya yakifanyika mijini. Na baada ya kupata hifadhi hiyo, sisi wanajamii wengine tujitolee kwa hali na mali kuwa na mfuko wa kuwasaidia na kuwahudumia ndugu zetu hawa kwa kuwapatia maisha bora ya elimu na afya. Nasisitiza mfuko huu usisimamiwe na mafisadi ili kuleta imani kwa wachangiaji. Hili litawezekana tu iwapo kutakuwa na takwimu sahihi na uelewa wa makazi halisi ya ndugu zetu hawa kwa sasa.

Umasikini wa watanzania waliopo vijijini, tukiwapatia silaha za kujilinda wenyewe, tusije tengeneza taifa la wanyang'anyi kwani silaha hizo zaweza kutumia kinyume na matarajio yetu na kuleta maafa makubwa kwa wananchi wetu.
 
Ni uongo mtupu kusema eti adhabu ya kifo haitoondosha mauaji haramu ya hawa binadamu wenzetu wasio na hatia isipokuwa tu kwasababu ya rangi yao ya ngozi. Uongo mtupu!!!. Itaondosha!!! na itaondosha uharamu huu, na itaufuta kabisa. Subirini ipite wahukumiwe na muuone.
Hizi falsafa zenu za haki za binadamu mnatoa wapi nyinyi, maana haziendani na reason hata kidogo. Mwenye kuua roho ya binadamu pasipo haki basi nae auawe. Umasikini, eti umasikini, what the hell is that?. Nafikiri itakuwa busara mkizirudisha hizi falsafa huko mnakozitoa. Wengine wameshakuambieni hapa kwamba, hii sheria hapa kwetu ipo, ipo, ipoooooooooo, haijabadilishwa kama mnavyoota. Na kama nyinyi mnasema haitaoondosha subirini, na tuone. Its "Reason" that strongly suggest that it will stamp out this cruelty. It will really dig deep into these murderers' hearts and shake their very being. Let it be done publicly. I mean it, na vinginevyo, hakuna haki. Natoa hoja
 
I'm just sitting here and it just hit me... familia zote zenye Albino zipewe leseni na bastola za kujihami nazo. Wapewe mafunzo ya kuzitumia. Hii ni kwa vile serikali imeshindwa kuwalinda na haki yao ya kujilinda na kulinda maisha yao itumiwe.

Wale maalbino watu wazima wapewe bunduki zao wao wenyewe na wale wenye wana familia basi wapewe silaha hizo ili kulinda familia zao.

I dont think if it can work out.
 
Pundit ana kibastola....labda tumwulize yeye alikinunua wapi kwa bei rahisi....
 
Miye hapa naangalia haja ya mtu kulinda maisha yake. Endapo serikali haiwezi kunilinda au kunihakikishia usalama wa uhai wangu ninayo haki ya kutumia uwezo na nguvu yeyote kulinda maisha yangu na ya familia yangu. Of course tukiwapa hizo silaha matumizi yake yatakuwa monitored....

Nafikiri tuna watu wenye akili ya kutosha kufikiri jinsi gani tunaweza kuhakikisha hii programu inafanya kazi. Nawahakikishia wakitangaza tu kuwa maalbino watapewa bunduki kwa siri na watakuwa na haki ya kutembea nayo kwa kuificha (concealed weapon) majambazi na hao wanaowatuma watafiikiria mara mbili hasa jambazi moja likitundikwa risasi jichoni likajaribu kumkamata mzee wa watu. Na ikisikika watu wanne tu wameuawa na Maalbino katika jaribio la kuwaua ili wapate viungo basi ball game ita change kwani huyo Mganda akisema uende kutafuta kiungo cha Albino ahakikishe anakupa "Chekeche"!!
 
hehehehehe...nimependa hiyo ya "li"....umezungumza kwa machungu na hasira za kuchukizwa na kinachoendelea dhidi ya ma albino....
 
hehehehehe...nimependa hiyo ya "li"....umezungumza kwa machungu na hasira za kuchukizwa na kinachoendelea dhidi ya mazeruzeru....

that is a derogatory term; wenyewe hawapendi kuitwa hivyo kwani ndiyo asili ya unyanyapaa dhidi yao. Labda wenyewe kwa wenyewe wanaitana hivyo... siku hizi ukiita hivyo in public utajikuta kwenye matatizo.
 
[media]http://www.youtube.com/watch?v=FZuu_oHGosI[/media]
 
Makubwa haya hebu waende Tanzania wawafanye wezi wa EPA kurudisha kila kitu na kuonekana hadharani.....
 
Polisi mkoani rukwa inamshikilia mkazi mmoja kwa kosa la kupanga dili la kuumuuza mkewe albino kwa sh mil 3.6,habari zinasema john alifanya dili hiyo na wafanyabiashara wawili wa kutoka kongo,mtuhumiwa alikamatwa wiki hii baadaya kugundulika dili lake na hao wakongo,..hata hivyo mtego huo haukuzaa matunda maana hata wanunuzi hawakutokea baada ya kutorka,habaro zinasema wakongo hao walifika katika kijiji hicho na kujifanya wachuuzi wa samaki,na kuanza kuonekana mara kwa mara!!!nyumbani kwa mtuhumiwa,habari zinasema mtuhumiwa alikiri kushiriki katika jaribio hilo la kumuuza mkewe albino janeth mlele,maskini!!!jeshi la polisi linasema mara baada ya hilo walimchukua janth na kumpeleka nyumbani kwa wazazi wake!!!!

Rais kikwete tutafika kweli,ona huruma hawa binadamu kama sisi!!!
 
Sasa kama hatuwambii watu ukweli tutegemee nini?

Siku zote tunawambia WaTz kuwa mtaji wao ni nguvu zao na si akili zao, kwa kuzitumia vizuri katika kuyafanya mazingira yao yawapatie mahitaji yao muhimu na ziada! Pia watu wanazidi kulishwa sumu kwamba Bongo unaweza kulala masikini ukaamka tajiri! Kwa kupata bingo, bahati na sibu ya aina yoyote au kupigiwa simu toka mchezo wa NDOTO wa Zain!

Tutegemee nini kama ndoto hazitimii na sisi tunazidi kuzeeka! Kwanini tusirudi kwenye ukweli kuwa hakuna mafanikio (kwa watu waadilifu lakini, ukiacha mafisadi) bila ya kufanya kazi; tena kwa kutumia akili zaidi kuliko nguvu!!
 
...Huyo jamaa alimuoa huyo dada kwa mapenzi kweli au ndio alikuwa natafuta njai rahisi ya kumsogeza ili ampige bei?

Nadhani anatakiwa kupewa kifungo na adhabu kali kabisa hana maana.
 
Watu wa namna hii sio tu kuwafunga/Kuua pia wanatakiwa miili yao au sehemu ya miili yao iwekwe na makumbusho au maabala ili vizazi na vizazi viweze kujifunza kama brain zao ziko sawa sawa kweli au ni kamasi.

Mtu unayemtegemea awe mlinzi namba wani kweli ndio anasuka dili, binafsi nina muhukumu kifo na kichwa chake kikawekwe makumbusho na ubongo upelekwe maabala. Sidhani kama jamii yetu inahitaji watu wa namna hii. i am sorry kwa kuwa na emotion, inaudhi!
 
Hicho kitendo alichotaka kufanya mwanaharamu huyo cha kumuuza mkewe kinafanana na Utumwa....jinsi wakoloni walivyokuwa wakiwapiga bei mababu na mabibi zetu......
Inasikitisha....!!!
Hivi kweli hali ngumu ya uchumi inaweza kumfanya mtu auze mkewe.....?
 
Police in southern Tanzania say they have arrested a man accused of attempting to sell his albino wife.

The man was allegedly planning to sell his wife to two Congolese businessmen for around $3,000.

Albinos have been living in fear in Tanzania after a series of killings due to a belief their body parts can make magic potions more effective.

Soma zaidi hapa

Sasa yaliobaki ni maombi tu.
 
Ebwana wadau hivi ni kwanini hili sakata la mauaji ya albino linazidi kupamba moto na naomba wadau wanaojua kama kuna kesi ambazo zimeshakwenda mahakamani hadi sasa na kutolewa hukumu, zinafikia ngapi hadi hivi sasa? Tusaidiane kupiga vita suala hili kwa kuibua mbinu mbalimbali za kupambana na suala hili
 
kwa kiswahili, albino ni zeruzeru. hivi kwa nini karibu kila maandishi kuhusu suala la watu hawa linatumika neno albino, ambalo ni la kigeni? au ni taratibu ile ile ya kumwita mkamata panya sio 'rat catcher' ila ni 'rodent officer'?

macinkus
 
Back
Top Bottom