Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

kwa kiswahili, albino ni zeruzeru. hivi kwa nini karibu kila maandishi kuhusu suala la watu hawa linatumika neno albino, ambalo ni la kigeni? au ni taratibu ile ile ya kumwita mkamata panya sio 'rat catcher' ila ni 'rodent officer'?

macinkus

Mzee, umepindisha hoja, sasa sijui ni makusudi au wewe hayakuhusu? Kwa nyie wakongwe haitakiwi muwe hivyo, tatizo la mazeruzeru ni ukweli usopingika lina linasikitisha sana yaani wamegeuzwa mawe ya kunole mapanga, mashoka na visu!
 
Mbaroni kwa kumwita albino 'dili'

MKAZI wa kijiji cha Uzunguni wilayani Maswa mkoani Shinyanga, Bw. Mashaka John (45), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kutishia kumuua albino kwa kumwita 'dili' anayefaa kuuawa ili kufanyiwa biashara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shaibu Ibrahim, alisema tukio hilo lilitokea wilayani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kamanda Shaibu alimtaja mtu anayetishiwa kuuawa kuwa ni Bibi Penina Ezekiel (23) mkazi wa Unyanyembe wilayani hapo.

Alisema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi pamoja na kuhojiwa kama anahusika na mauaji hayo na akigundulika sheria kali zichukuliwe dhidi yake.

Wakati huo huo, Kamanda Shaibu alisema Polisi mkoani hapa inafanya uchunguzi wa matukio matatu ya vifo vilivyotokea Bariadi, Maswa na Bukombe, na kusababisha vifo vya watu wanne.

Alisema tukio la kwanza lilitokea katika kijiji cha Kalabela kata ya Mwandabena, Bariadi ambapo Kulwa Maduhu (11), mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Kilabela alikufa baada ya kuangukiwa na paa la shule wakati akijikinga mvua.

Tukio la pili lilitokea katika wilaya ya Maswa ambapo mkulima, Bw. Nenji Mboje (45), aliuawa kwa kupigwa fimbo.

Aidha, alisema kuwa polisi wanawashikilia Bw. Nshoma Magembe (40), Bw. Sayi Bucheyeki (42) na Bibi Mwalu Bushasha, wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.

Pia alisema tukio la tatu linalofanyiwa uchunguzi ni lililotokea Bukombe kijiji cha Ilangwe ambapo Bw. Shilumikila Nkelezu (90) na mkewe Bibi Shikumbi (80) walikutwa wameuawa nyumbani kwao kwa kukatwa mapanga na watu wasiofahamika.
 
Wenzetu malbino kweli wanataabu .. wanateseka mpaka dunia wanaiona chungu .. je are we/the government doing enough to protect them? cant even answer this my self ... kwenye kipima joto nitajibu "S" sijui
 
Jamani watanzania mungu atawapiga makofi,muwe na hofu ya mungu!!!!1
 
Too bad jamani, Halafu waziri mwenye dhamana anautangazia ulimwengu kwamba mambo yenyewe ni madogo yanakuzwa tu na media?
 
Na Richard Fundi,Kigoma

MAUAJI ya albino yanaendelea kutikisa, na safari hii kwa kutumia silaha kali, licha ya serikali kuanza operesheni maalum ya kupambana na uovu huo baada ya mlemavu wa ngozi anayefahamika kama Ezekiel John, 47, kuuawa kwa risasi na watu wasiojulikana ambao walitoweka na mkono wake wa kulia.

Mlemavu huyo wa ngozi aliuawa wakati akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Abdihaki Rashid alisema katika taarifa yake jana kuwa watu hao walivamia nyumbani kwa marehemu na kumpiga risasi mgongoni, na baadaye kumkata mkono ambao walitoweka nao.

밫ukio hilo lilitokea juzi, katika Kijiji cha Muyama wilayani Kasulu na askari waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali katika eneo la tukio hawajarudi, hivyo watakaporejea tutatoa taarifa za kina zaidi,?inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Mauaji ya albino yametapakaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yakihusishwa na imani za kishirikina na tayari watu wengi wenye ulemavu wa ngozi wameshauawa kikatili na watu wasiojulikana ambao hukata viungo vya albino na kutoweka navyo.

Serikali imepeleka askari wa kikosi maalum cha kupambana na ukatili huo, lakini taarifa za kuuawa kwa albino zinaendelea kumiminika, huku polisi wanne wakiripotiwa kuwekwa ndani kwa tuhuma za kuwaachia wauaji wa albino baada ya kuhongwa fedha.

Mwanzoni mwa wiki hii watu waliokuwa wamejifunika sura zao walimvamia mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye ulemavu huo, Mateso Dunia, 13 na kumuua kikatili.

Mtoto huyo wa darasa la tatu alikuwa mkazi wa Kijiji cha Gunihuna kilicho katika Kata ya Iponya wilayani Bukombe. Hilo lilikuwa tukio la pili wilayani humo kwa mtoto albino kuuawa tangu mauaji hayo ya kikatili yanayohNa Richard Fundi,Kigoma

MAUAJI ya albino yanaendelea kutikisa, na safari hii kwa kutumia silaha kali, licha ya serikali kuanza operesheni maalum ya kupambana na uovu huo baada ya mlemavu wa ngozi anayefahamika kama Ezekiel John, 47, kuuawa kwa risasi na watu wasiojulikana ambao walitoweka na mkono wake wa kulia.

Mlemavu huyo wa ngozi aliuawa wakati akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Abdihaki Rashid alisema katika taarifa yake jana kuwa watu hao walivamia nyumbani kwa marehemu na kumpiga risasi mgongoni, na baadaye kumkata mkono ambao walitoweka nao.

밫ukio hilo lilitokea juzi, katika Kijiji cha Muyama wilayani Kasulu na askari waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali katika eneo la tukio hawajarudi, hivyo watakaporejea tutatoa taarifa za kina zaidi,?inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Mauaji ya albino yametapakaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yakihusishwa na imani za kishirikina na tayari watu wengi wenye ulemavu wa ngozi wameshauawa kikatili na watu wasiojulikana ambao hukata viungo vya albino na kutoweka navyo.

Serikali imepeleka askari wa kikosi maalum cha kupambana na ukatili huo, lakini taarifa za kuuawa kwa albino zinaendelea kumiminika, huku polisi wanne wakiripotiwa kuwekwa ndani kwa tuhuma za kuwaachia wauaji wa albino baada ya kuhongwa fedha.

Mwanzoni mwa wiki hii watu waliokuwa wamejifunika sura zao walimvamia mwanafunzi wa darasa la tatu mwenye ulemavu huo, Mateso Dunia, 13 na kumuua kikatili.

Mtoto huyo wa darasa la tatu alikuwa mkazi wa Kijiji cha Gunihuna kilicho katika Kata ya Iponya wilayani Bukombe. Hilo lilikuwa tukio la pili wilayani humo kwa mtoto albino kuuawa tangu mauaji hayo ya kikatili yanayohusishwa na imani za uchawi yaanze Kanda ya Ziwa.

Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya jeshi hilo kuwakamata polisi wanne ambao wanatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa wauaji wa albino na kuwaachia huru.

Mwanafunzi huyo albino aliuawa juzi majira ya saa 6:00 wakati akiwa anarudi nyumbani na wenzake. Walikuwa wakitoka kuangalia video.

Hata hivyo baadaye miguu miwili ya albino ilikamatwa kwa mganga wa jadi ambaye alikimbia kabla polisi hawajamfikia.

Katika hatua nyingine taarifa hiyo ilisema kwamba, katika Kijiji cha Munyange, Polisi wakiwa katika doria ya kawaida, waliwakurupusha watu waliodhaniwa kuwa ni majambazi na kukimbia.
Taarifa hiyo ilifafanua kwamba watu hao wakiwa katika harakati za kukimbia, walidondosha mabomu mawili ya kutupa kwa mkono.

usishwa na imani za uchawi yaanze Kanda ya Ziwa.

Hizi nguvu wanazotumia hawa jamaa zinanitisha,watabakki hawa watu!
 
Wakulu,

Hivi humu barazani(JF) hamna mganga wa kienyeji kweli?
Nasema hivi kwasababu lazima tufahamu kiini cha hili tatizo,ili tuweze kulitatua katika njia stahiri.
Haingii akilini hata kidogo (akili yangu),hawa Maalbino si watu tu...,kama watu wengine?
Inakuaje inakuwa wao ndio Deal?
Mganga atuambie nini hasa hao maalbino walichonacho cha ziada kuliko binadamu wengine.maana hata hao walio huko police hawasemi ukweli kwani wamekamata baadhi ya waganga lkn hawajasema nini hasa kinachowafanya hawa ndugu zetu kusakamwa hivo na kukoa amani.
Na tafadhali ndugu zetu mlio karibu na duru za kipolicee vujisheni hizo data ilitujue wanafanya nini na hivyo viungo vya binadamu.
Zamani, hao mazeruzeru tuliambiwa walikua hawafi bali wanapotea wakifika umri furani,kumbe wallikuwa wana uliwa,jamani ukatiri gani huu?
Au hayo maghorofa hapo kariakoo ni mazeruzeru hao?
 
Swala hili linatia uchungu na linaiaibisha nchi sana. Siku tatu zilizopita nilisoma hadithi ya mtoto aliyekuwa akirudi nyumbani kwae na rafiki zake, halafu njiani akakutana na hao majambazi. Mtoto yule alifahamau kuwa hiyo ndiyo kiama yake na kuanza kulia kuwaomba wasimdhuru lakini wale mabwana bila huruma walimuua kikatiri na kumkata mikono yote miwili. Rafiki zake ambao hawakuwa target ya wale majambazi walifanikiwa kukimbia huku wakijua mwenzao anauwawa; nina imani kuwa tukio hilo litaathiri sana ukuaji wa akili zao kama raia wa baadaye.
 
Imetolewa mara ya mwisho: 09.12.2008 0156 EAT
•
'Muuaji' asimulia walivyomchinja albino

]

Na Bahati Mwiko, Shinyanga

JESHI la Polisi wilayani Bariadi mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na wanannchi wa kijiji cha Mkingwabie, wamefanikiwa kukamata kichwa na miguu miwili iliyonyofolewa kwenye mwili wa albino, Bw. Lyaku Nkanyabilu (50), aliyeuawa kikatili mjini hapo na kuzikwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Viungo hivyo vilipatikana jana nyumbani kwa Bw. Mbonje Mawe (41), mkazi wa kijiji hicho na Majira ilishuhudia polisi wakishirikiana na wananchi kufukua kichwa cha marehemu Nkanyabilu nyumbani kwa mtuhumiwa wa mauaji.

Baada ya kufukuliwa kichwa hicho, Bw. Mawe aliongoza kundi la polisi na wananchi hao kwenda sehemu iliyokuwa imefukiwa miguu ya albino huyo ambapo ilifukuliwa ikiwa imefungwa na gunia.

Bw. Mawe alikiri kushiriki mauaji hayo na kuwataja wenzake sita anaodai kushirikiana nao, akiwemo Mwenyekiti wa kijiji hicho, pamoja na wenyeviti wawili wa vitongoji. Alisema walikuwa na nia ya kuuza viungo hivyo kwa wateja ambao walikuwa wakiwasiliana.

Akisimulia tukio zima lilivyokuwa, Bw. Mawe alidai siku ya tukio akiwa na wenzake sita, walipanga kumuua Bw. Nkanyabilu kwa kushirikiana na shemeji yake, Bw. Sayi Gamani.

Alidai Bw. Gamani alimdanganya Bw. Nkanyabilu kuwa anampeleka hospitali kumtibu maradhi yaliyokuwa yakimsumbua kabla ya kushirikiana kumkamata na kwenda kumuua.

"Ilipofika saa saba usiku, tulimkamata Bw. Lyaku (Nkanyabilu) na kumpeleka mtoni, tulipofika huko tulimlazimisha kuingiza kichwa kwenye maji hadi alipokufa, tukamchinja, tukamkata miguu na baada ya hapo, tukaiingiza viungo hivyo kwenye gunia moja na mwili wake kwenye gunia lingine na kutumbukiza mwili wake kwenye maji," alidai.

Alidai baada ya hapo, walibeba kichwa na miguu na walishauriana waviweke nyumbani kwake (kwa Bw. Mawe) wasubiri wateja hao ambao walikuwa wakiwasiliana nao kutoka Mwanza mjini, Lamadi na Kahama

Mkuu wa Polisi wilayani Bariadi, Mrakibu wa Polisi, Bw. Paul Kasabago, akiwa eneo la tukio alisema kupatikana kwa viungo hivyo kumetokana na ushirikiano mkubwa wa wanakijiji hicho ambao aliwashukuru kwa kuonesha ushirikiano wa dhati na ulizi shirikishi.

Aliwataja wanaoshukiwa na Polisi kuhusika katika tukio hilo kuwa ni Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Chenyenye Kishiwa (64), Bw. Sayi Gamanya (47), Bw. Gumbu Nzige (48), Bw. Mboji Mawe (48), Bw. Sayi Mafize (32) na Bw. Salum Mshamamba (52). Wote ni wakazi wa Mkingwabie.

Naye Anneth Kagenda anaripoti kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Walemavu la Haki za Kisheria na Maendeleo, Bw. Gidion Mandesi, jana jijini Dar es Salaam alisema Serikali imeshindwa kudhibiti mauaji ya albino yanayoendelea.

"Serikali inataka kutuambia imani za kishirikina zimeanza wakati huu, mbona hata zamani zilikuwapo na (albino) walikuwepo mpaka wamezeeka hawa kuuawa kama ilivyo sasa," alisema Bw. Mandesi.

Bw. Mandesi alishauri serikali itumie raslimali zake kuwakusanya maalbino na waganga wa jadi, ili wajadili jinsi ya kukomesha mauaji hayo.

Naye Gladness Mboma, anaripoti kuwa Kitengo cha Makosa Dhidi ya Wanadamu kimewanasa zaidi ya watu 57 wakiwemo waganga wa jadi, wafanyabiashara wa madini na wavuvi na kuwafungulia mashtaka ya kuhusika na mauaji ya albino katika maeneo mbalimbali nchini.

Mdhibiti Mkuu wa Kitengo hicho, Bibi. Sidney Mkumbi, alisema hayo juzi wakati alipokuwa akiojiwa katika kipindi cha kipima joto kilichorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Bi. Mkumbi alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika mikoa sita baada ya polisi kufanya msako mkali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo na kwamba wengi wa watuhumiwa hao wanatoka katika mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Mara, Kigoma, Kagera na Mbeya.

"Watu wengi wanadhani sisi hatufanyi kazi dhidi ya matukio haya ya kikatili, juhudi zipo na mafanikio yake ni kukamatwa kwa watu zaidi ya 57 wakiwemo wafanyabiashara 13 miongoni mwao watano walikutwa na viungo vya binadamu ambavyo havijathibitishwa kama ni vya albino au la," alisema.
 
Jamani .........mhhhhhhhhhhhhh hapana mungu shusha garika yako
kuanzia serikali mpaka kwa wahusika kwa kushindwa kuthibiti
haya mauaji......eeee mola twakuomba
 
... 😱 khee? hebu temea chini, puuuuu!

Be careful what you wish for!

...kumbuka, nawe ni mhusika, do something to stop it!
 
Pesa ni issue kweli kweli. Yaani mpaka uamue kuua mtu kwa namna hiyo, lazima pesa pia ina elements za ushirikina
 
Ni kweli jambo ili linasikitisha sana. Jana nilimsikia Dr Tibaijuka akitoa sikitiko lake kulingana na hali hii ya kuondoa uhai wa ndugu zetu hawa kwenye BBC swahili service. Nadhani ni vyema vyombo husika vikatoa elimu kwa jamii ili tuondokane na ili tatizo.
 
Hili ni janga la Taifa ambalo ukatili wake kwa binadamu haujawahi kutokea katika nchi yetu. Vyombo vya dola peke yake haviwezi kuthibiti mauaji ya ndugu zetu hawa.Unyama huu utakoma pale tu wananchi wote na hasa serikali za vijiji vitakapofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na jeshi la polisi, kuwafichua wote wanaohusika hasa hasa wale wanaonunua viungo hivyo vya binadamu. Mahakama pia zisaidie kwa kutoa adhabu kali kwa wale wote watakaopatikana na makosa yanayohusiana na mauaji ya albino.
 
Unajua kuna vitu vingine huwezi kuamini kama vinafanywa na binadamu. Its very unthinkable. Binadamu kumuua binadamu mwenzako kwaajili ya viungo vyake. Ukichunguza kwa haraka haraka utagundua ni umaskini unaopelekea haya yote. Maana wanatumia viungo hivi kwaajili ya kujiongezea utajiri ni watu ambao tayari wanauwezo. Sasa, wao hawashiriki moja kwam moja katika vitendo vya mauaji, bali wanatuma watu wasio na uwezo kufanya hiyo kazi. Kwahiyo unakuta vijana kwa wazee wenye maisha magumu wanajiingiza kwenye shughuli kama hiyo ili kujikwamua na lindi la umaskini. Na kwa ujumla hii yote inasababishwa na sera mbovu za CCM. Chama kimekosa mwelekeo na kimeshindwa kutimiza ahadi zake za maisha bora kwa kila mwananchi. Hivyo basi, ningependa kuhitimisha kwa kusema kwamba, tunaposhutumu mauaji ya albino, tuinyooshee CCM kidole moja kwa moja kwa kuleta umaskini unaopelekea watu kufanya vitendo visivyofikirika.
 
Waziri wa Mambo ya ndani masha yuko wapi? hatujawahi hata siku moja aongelee hii issue au afanye chochote cha maana kusafisha hili tatizo ...endeleza majungu tuu Vs Mengi maana ndio unachoweza!
 
Serikali ya CCM imeshindwa kabisa kuthibiti mauaji ya hawa raia wenzetu, huu ni unyama wa hali ya juu kabisa kumfanyia binaadamu mwenzako asiye na hatia. Yaani inatia hasira na inatia huruma. Mungu Azilaze Roho za Marehemu Wote katika majanga kama haya Pema Peponi.
 
Hivi serikali kweli inashindwa kutoa ulinzi wa karibu kwa hawa Albino maana hata number yao sio kubwa sana....ningewapatia ulinzi binafsi hata wa mgambo sehemu wanazoishi kwa zamu maana wako wachache sana,hii hali inatisha sana na Masha kakaa tuu hafanyi chochote
 
Back
Top Bottom