Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Huu ni unyama na ushenzi wa hali ya juu! Hivi kweli leo hii karne ya 21 bado tunang'ang'ania imani za kipumbavu namna hii, jamani!
Dr. Watson akituita mambumbumbu, tunaanza kulialia!
 
Mie nahofu siku waganga wa wanasiasa waambie wanasiasa mkitaka mshinde uchaguzi leta kuingo cha albino!sijui itakueje hapo!
 
Mie nahofu siku waganga wa wanasiasa waambie wanasiasa mkitaka mshinde uchaguzi leta kuingo cha albino!sijui itakueje hapo!


doh! tena usiwape mawazo maana hakuna tamaa mbaya kama ya ukubwa, maana inatangulia tamaa ya fedha..
 
Naona ile mipasho (Mitusi) yote imetoweka. Siku zote huwa na jiuliza jukwaa la siasa mbona safi sana. Sasa najua kuwa ma Mods wanawabeba. Anayesema section ya dini chafu na ifungwe anyooshe mkono.

None? Yeah I thought so. We are both as bad as each other. No exceptions.
 
Mie nahofu siku waganga wa wanasiasa waambie wanasiasa mkitaka mshinde uchaguzi leta kuingo cha albino!sijui itakueje hapo!

Siku hizi wenyewe wanawaita HOT CAKE ,naweza kusema ni spishi ambayo inahitaji kulindwa la si hivyo itaangamia kama walivyotoweka madainasourouvirusiuz ,ila hapo Mwanakijiji wazungu tayari wamekuwa mazeruzeru asilia hivyo hawahitajii kipuri cha albino ,ila hawa wenye asili ya mchonga ndio kazi kweeli.
 
Jamii yetu ikiendelea na imani hizi sijui tunaelekea wapi!

Anyofoa nywele za albino, atokomea
2008-04-03 09:07:14
Na Elisante John, PST, Singida

Chokoraa mwenye umri wa miaka 12 anayeishi katika mazingira magumu, amehukumiwa kifungo cha miezi 36 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnyoa nywele albino kinyume na matakwa yake na kutoweka nazo. Chokoraa huyo atatumikia kifungo hicho katika jela ya watoto watukutu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Bi. Agatha Chigullu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Utemini mjini hapa. Ilidaiwa kuwa, mshtakiwa huyo alikwangua nywele za albino huyo baada ya kupewa ujira wa Sh. 500 na mchimba madini ya Tanzanite huko Mererani, wilayani Simanjiro.

Akitoa adhabu hiyo, Hakimu Bi. Chigullu alisema, amemtia hatiani mshtakiwa baada ya kumkanya mara kadhaa katika mahakama hiyo kutokana na tabia yake mbaya, lakini alishindwa kujirekebisha.

Alisema vitendo anavyowafanyia watu mbalimbali wakiwemo raia kutoka nje ya nchi kwa kuwaibia mali, havitavumiliwa na jamii, hivyo atalazimika kufunzwa adabu kwa miezi 36 katika shule maalum ya watoto watukutu ya Irambo iliyoko mkoani Mbeya.

Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Bw. Philipo Mzirai alidai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 14, mwaka huu saa 4:00 asubuhi katika mtaa wa Kindai, Wilaya na Mkoa wa Singida.

Alidai kuwa, mshtakiwa alimfuata Bw. Joseph Rashid (24) maarufu kwa jina la `Mchina` mkazi wa Utemini ambaye ni albino akiwa amejipumzisha na kumweleza kichwani kuna mdudu, hivyo anaomba amuondoe.

Alidai kuwa, alipokubali, mshtakiwa huyo alimkwangua nywele kwa wembe na kutoweka nazo.

Aliongeza kuwa, tukio hilo lilitokea nje ya duka la reja reja lililoko mtaa wa Kindai, Singida mjini mlalamikaji na mshtakiwa walipokutana pamoja na watu wengine huku wakiendelea na mazungumzo yao ya kawaida.

Ilidaiwa kuwa, baada ya muda mfupi kupita, chokoraa huyo alirudi eneo hilo na kumkuta albino ambapo alimwonyesha Sh. 500 huku akidai kuwa, alizipata kutokana na nywele zake.

``Kama siyo nywele zako, ningepata wapi hizi Sh. 500,`` mshtakiwa alikaririwa akimdhihaki albino.

Kabla ya adhabu kutolewa, Mzirai aliiomba Mahakama impe mshtakiwa adhabu kali kutokana na uhalifu alioufanya katika umri mdogo, pia kuwalinda watu wa jamii ya albino ambao baadhi ya watu wanataka kutumia viungo vyao kujitajirisha.

Akijitetea, mshtakiwa alionekana akibubujikwa machozi na kuiomba Mahakama imsamehe kwa madai kwamba, hatarudia kufanya kosa lolote.

Hata hivyo, Hakimu Chigullu alimweleza kuwa, Mahakama imemsamehe kiasi cha kutosha, lakini ameshindwa kubadili tabia, hivyo atalazimika kwenda kutumikia adhabu hiyo.

SOURCE: Nipashe
 
Ndugu zangu bado tunajenga hoja kutoka hapa hadi kwenye hotuba ya Rais.. na bado nadhani suluhisho analolipendekeza halitasaidia sana kupata wauaji wa ndugu zetu maalbino.

NAIROBI, April 3 (Reuters) - Tanzania's President Jakaya Kikwete has condemned witchdoctors who kill albinos and harvest their body parts in the hope it will bring prosperity.

He said 19 albinos had been murdered since March 2007, and another two were missing presumed dead in the east African country.

"Sometimes, word spreads around that body parts of people with certain physical attributes like bald people or albinos contribute greatly to attaining quick prosperity," Kikwete said in a monthly state of the nation speech late on Wednesday.

"These killings are shameful and distressing to our society," he added.

Albinos are often accused in Tanzania of being witches themselves.

There are an estimated 270,000 people who suffer from the condition which stops them producing pigment in their skin, hair and eyes in the country of 39 million.

Kikwete blamed charlatan witchdoctors, many masquerading as traditional healers, for extracting body parts such as genitals, tongues and breasts.

"Many of the witchcraft killings happen because of a false belief that by using other peoples' body parts they can succeed in business or in activities like mining or fishing," Kikwete said.

Most killings took place in the Victoria region and were committed by gangs for hire, he said
 
Niliona kama Lecturer wangu ananikosea pale alipoongelea suala la Mauaji ya Albino na imani za uchawi na darasa zima kucheka, nilijisikia vibaya lakini sikuwa na budi ya kukaa kimya na Lecture ilipokwisha ilinilazimu kujibu maswali ya wanafunzi wenzangu wadadisi....

Leo naiona tena ndani ya BBC


Tanzania fear over albino killing
Albino woman
Albinos are also at high risk of getting skin cancer

Tanzania's Albino Society has accused the government of turning a blind eye to the killing of albinos, after four deaths in the past three months.

An albino spokesman said there was a belief that the condition was the result of a curse put on the family.

Some witch-doctors also say they can use albino body parts in a potion to make people rich.

A teacher in the northern town of Arusha has been arrested for killing his own child, who was albino.

As well as the four killings, the body of an albino has also been exhumed. It was found with its limbs cut off.

The BBC's Vicky Ntetma in Dar es Salaam says there is now fear in the albino community there.

Christopher Dadenekeye from the TAS said the witch-doctors must also be arrested.

Some people in Tanzania think albinos are a kind of ghost-like creature.

"We need to clear out all these beliefs," Mr Dadenekeye said.

There are more than 8,000 registered albinos in Tanzania.

Old women with red eyes have been killed in parts of Tanzania in the past, after being accused of witchcraft but our correspondent says this is the first time that albinos have been targeted in ritual killings.

TAS also wants more help for albinos and says the condition should be treated as a disability.

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7148673.stm

Ninachojiuliza ni kweli serikali imeshindwa kupata ufumbuzi wa hili jamani?
Kimsingi naona pia si kuitupia serikali mzigo pia mashirika ya haki za kibinaddamu yanatakiwa kusaidia kuelimisha jamii kuhusu suala hili au wadau mnaonaje?
 
Nimefuatialia kwa karibu habari za mauaji ya ndugu za Maalbino ambayo yamekuwa yakiendelea na hivi jana kuna habari kuwa mwili wa Albino umefukuliwa toka makaburini na kunyofolewa viungo vyake. Habari hizi siyo tu ni za kusikitisha lakini kwa hakika zinatia aibu na kuhuzunisha.

tanz632.jpg

Ni kwa sababu hiyo nimeandika makala ya "Mauaji ya Albino, Aibu ya Taifa letu" na unaweza kuisoma HAPA. Katika makala hiyo nimesema mengi (na jambo fulani very personal, I rarely write something about me) na mojawapo ya niliyoyasema ni kuwa:

Ni kwa sababu hiyo basi, binafsi nakerwa na kushindwa kwa jeshi letu na watu wa Usalama wa Taifa (kama nilivyozungumza wiki iliyopita) kuja na operesheni kabambe ya kuwatafuta, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wale wanaoua ndugu zetu maalbino.

Kinachoniudhi zaidi ni jinsi gani serikali ya Rais Kikwete inalichukulia jambo hili kana kwamba ni "mojawapo tu ya uhalifu" kiasi cha kuunda kamati kama walivyofanya kuhusu EPA!

Na pia nikasema hivi:

Kama kweli wanataka kukamata hawa wahalifu kwanini wasitoe ‘donge nono' kwa sababu tunajua pesa husaliti mtu. Watoe donge nono ambalo si chini ya sh milioni 20 kwa mtu au watu ambao watatoa taarifa zitakazosababisha kupatikana kwa watu wanaohusika na mauaji ya albino na kusababisha kutiwa kwao mbaroni na hatiani?

Hivi serikali inaweza kufanya hivyo ukizingatia kuwa kwa siku wanalipa sh milioni 150 kwa kampuni yenye mkataba hewa ya Richmond?

Ni kwa sababu hiyo basi; nimetoa changamoto ya kuanzisha Mfuko wa kuzawadia wale wote watakaotoa taarifa:

a. Ambazo zitasaidia kukamatwa kwa watu waliohusika na mauaji ya Albino mahali popote Tanzania na zitalipwa endapo watu hao watatiwa hatiani.

b. Kusaidia kupatikana kwa watoto wawili maalbino ambao wametoweka hadi sasa wakiwa hai au iliko miili yao.

c. Kusaidia kukamatwa kwa waganga wa jadi mafisadi ambao ndio wamekuwa wakitoa maelezo kwa watu kwenda kuua maalbino ili wapate utajiri wa haraka haraka.

Mfuko huo usimamiwe na Jeshi la Polisi, Chama cha Maalbino cha Tanzania na taasisi nyingine ya kiraia.

d. Pia fedha hizo zitakazochangwa zitumike pia kusaidia matibabu ya maalbino wote ambao wameumizwa au kuathirika na vitendo hivi vya kinyama na udhalilishaji.


Niko tayari kutoa kiasi kingine chochote kile katika kushirikiana na Jeshi la Polisi na vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa fedhedha hii inakwisha na vitendo hivi vya kinyama vinakoma na kurudisha utu, hadhi na heshima ya kila Mtanzania bila kujali rangi, kabila, hali ya maisha, au ulemavu wowote ule. Kuendelea kulaani mauaji haya hakutoshi, ni wakati wa vitendo!

Kiasi hiki kiko tayari mikononi mwa mtu jijini Dar na kitakabidhiwa wakati wowote ambapo Jeshi la Polisi litakubali kuanzisha mfuko huo wa Donge Nono. Kitatolewa kwa jina la KLHN na JF (Jumuiya za Watanzania kwenye Mtandao)

Nakaribisha mtu yoyote kutoa ahadi ili wajue kuwa tuko serious. Fedha hizo zinazoahidiwa zitatumwa moja kwa moja kwenye huo mfuko. Kwa wale wanaotaka different arrangements (kuficha ID zao wasiliana na mimi chemba).

Ndugu yenu,
Mwenzenu,
Rafiki yenu,
Kwa wengine ni Adui yenu

M. M. M
 
Ndugu watanzania,

Niko Tayari kujiunga na Mwanakijiji,
Niko Tayari kuchangia mtu atakayetoa taarifa hizi,
Niko Tayari kuchangia mjadala wa kuundwa sheria kuhusu hili,
Niko tayari kulinda maalbino wote nchini,
Niko tayari kuilinda haki ya wananchi,


Tuungane pamoja kwa hili kwa wale tulio makini,
Asante Mzee Mwanakiji kuonesha unajali,
Nashukuru kwa JF kwa kuwa viongozi,

hili ni wazo zuri na nadhani wao kama polisi wana pesa za ziada ambazo huwa wanwapa wale wanaoleta habari za uhalifu,kinachotakiwa na Mwema kutangaza Azimio la Mwanakijiji
 
mi nimesikitikaa sana kuhusu hili swala na article ya mwanakijiji imezidi kuniumiza.hivi nchi hii imefikia wapi?hata haki ya msingi kwa kila binadamu ya kuishi inaweza kunyanganya hivi hivi na hamna hata mtu anashtakiwa kwa kuuwa hawa ndugu zetu.Hivi priority zetu zipo wapi jamani,blue chip companies baada ya kusupport causes kama hizi wao wanaona bora kusponsor Miss Tanzania.Hii idea naisapport lakini sithani kama tunatakiwa tuishie hapa.Wo walioshiriki wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na wote waliohusika kwenye huu uzembe wa hali ya juu tukianzia na IGP wawajibike.Sitaki kukubali na kuamini kuwa wahusika hawajulikani,na haki ya kuishi ni ya msingi na inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote.Mimi pia ntachangia kwenye hili.
 
Asante mbangaizaji.. there comes a time when a nation has to stand up for the weakest among us.. Asante sana.

Kwa Albino, ufisadi hauonekani EPA, unaonekana kwenye kunyofolewa viungo vyake kwa ajili ya kumpatia mtu pesa!
 
mi nimesikitikaa sana kuhusu hili swala na article ya mwanakijiji imezidi kuniumiza.hivi nchi hii imefikia wapi?hata haki ya msingi kwa kila binadamu ya kuishi inaweza kunyanganya hivi hivi na hamna hata mtu anashtakiwa kwa kuuwa hawa ndugu zetu.Hivi priority zetu zipo wapi jamani,blue chip companies baada ya kusupport causes kama hizi wao wanaona bora kusponsor Miss Tanzania.Hii idea naisapport lakini sithani kama tunatakiwa tuishie hapa.Wo walioshiriki wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na wote waliohusika kwenye huu uzembe wa hali ya juu tukianzia na IGP wawajibike.Sitaki kukubali na kuamini kuwa wahusika hawajulikani,na haki ya kuishi ni ya msingi na inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote.Mimi pia ntachangia kwenye hili.


nakubaliana na wewe idea ni nzuri lakini tunahitaji tuwe na mikakati zaidi labda nadhani kwa wale walio Dar wafanye mpango kuandaliwe kipindi katika ITV/TVT kiwahusishe wazazi na watoto Maalbino halafu hii ishu ya kuanzisha huo mfuko itaje hapo...nadhani hii inaweza kusaidia
 
Ngoja nijaribu kuwasiliana na Dar na nitawaambia kama IGP amepokea hii changamoto na yuko tayari kuifanyia kazi.
 
Kumbe saa nyingine if we decide to do something GREAT, really i believe it can be done !

Naunga mkono !
 
Mwana Kijiji Hongera Sana Wote Tuko Nyuma Nahisi Hata Kada Mp... Atakuwa Pamoja Nawe Katika Hili,,imefikia Swala La Kutia Aibu Jinsi Nchii Hii Inavyolichukulia Hili Swala Si La Mchezo Kama Uamini Ulizeni Ndugu Zetu W Tanzania Wanajua Hali Halisi Wtu Wanakufa Jamani Si Mchezo Na Afadhali Wakutwe Na Viungo Vyote Ni Swala La Aibu Kukutwa Mtu Na Viganja Vya Mkono Wa Albino,,,mi Nampongeza Jk Kwa Kuteua Huyu Dada Labda Nae Atakuwa Serious Na Hili...ninachoomba Ni Kwamba Hawa Wahuni Waganga Wa Kiejnyeji Inavyoonekana Ni Watu Wanaojulikana Na Kwa Wakati Mwingine Hata Hawa Vigogo Wetu Msione Wanaendesha Magari Ya Hali Ya Juu Nendeni Muulize Kama Wanalala Kwa Amani,,,so Nahisi Upitishwe Semina Ya Kuwaonya Hawa Wakubwa Kwanza Waache Huu Mchezo Mchafu Then Waende Kwa Wananchi Wa Kawaida
Hatutaona Wenzetu Wakipotea Kirahisi Watanzania Tuwe Pwmoja Katika Hili

Ahsanten
 
Kada, ni rahisi watu "kulaani mauaji ya Albino" kuliko kuchukua msimamo... Hivyo sitarajii wengi kuunga mkono lakini wachache watakaofanya hivyo nina uhakika tutakuwa na impact..
 
.......inasikitisha, kutisha na kukasirisha, how long should this go for? Imani potofu !!

Albino body exhumed, parts cut off in Ukerewe

11 Apr 2008
By Regional Reporters


Mwanza


In a grisly incident linked to witchcraft beliefs, especially with regard to ongoing albino killings in the country, unidentified people have exhumed the body of an albino in Ukerewe District, Mwanza Region, and made away with some of its parts.

In a second incident of its kind in a month in the district, some people believed to be driven by witchcraft beliefs unearthed a grave in which an albino had been buried and made away with the body`s left hand and right leg.

Reports from Ukerewe District said that the event occurred last week at Nakamwa Village in which the body of an albino, Benedicto Riziki (10), who died on March 9, this year, and buried the following day, was exhumed.

``This is the second case to happen here in Ukerewe,` a police source, who preferred anonymity, said.

He explained that last February unidentified persons exhumed an albino's body from a freshly dug grave and disappeared with the whole body in an incident linked to witchcraft beliefs.

Since last year there had been continuous countrywide albino assassinations on superstitious beliefs. At least nine albinos had already been killed in Mwanza Region alone.

Source: ippmedia.com

SteveD.
 
Back
Top Bottom