Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Albino body exhumed, parts cut off in Ukerewe

2008-04-11 10:20:18
By Regional Reporters


Mwanza
In a grisly incident linked to witchcraft beliefs, especially with regard to ongoing albino killings in the country, unidentified people have exhumed the body of an albino in Ukerewe District, Mwanza Region, and made away with some of its parts.

In a second incident of its kind in a month in the district, some people believed to be driven by witchcraft beliefs unearthed a grave in which an albino had been buried and made away with the body`s left hand and right leg.

Reports from Ukerewe District said that the event occurred last week at Nakamwa Village in which the body of an albino, Benedicto Riziki (10), who died on March 9, this year, and buried the following day, was exhumed.

``This is the second case to happen here in Ukerewe,` a police source, who preferred anonymity, said.

He explained that last February unidentified persons exhumed an albino's body from a freshly dug grave and disappeared with the whole body in an incident linked to witchcraft beliefs.

Since last year there had been continuous countrywide albino assassinations on superstitious beliefs. At least nine albinos had already been killed in Mwanza Region alone.
 
This is too much pamoja na kukemewa kote bado watu wanakwenda kufukua maiti na kuiba viungo, kweli tunaitaji elimu Tanzania, unadhalilisha maiti sababu ya properity, je akikutokea mwenyewe unafanyaje.
 
Lets look at the bright side, Wameacha kuua siku hizi inaonekana. Huu ni mwanzo, mwisho wa yote haya yataisha.
 
Albino auawa kinyama na kunyofolewa viungo

2008-04-24 11:11:56
Na Ahmed Makongo, Musoma


Mwanamke albino, Bi. Nyamiti Nyamakanya (33), mkazi wa kijiji cha Bwai, Wilaya ya Musoma Vijijini, ameuawa kinyama kwa kukatwa mapanga na kisha kunyofolewa miguu na mikono yote na sehemu ya ngozi yake ya kisogoni kuchunwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Bw. David Saibullu, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Bwai baada ya watu hao kumvamia mama huyo akiwa amelala nyumbani kwake.

Kamanda Saibullu alisema baada ya watu hao kuingia nyumbani humo, walimkamata na kumshambulia kwa mapanga hadi kufa na kisha kunyofoa baadhi ya viungo vyake na kutoweka.

``Wauwaji hao waliingia kwa urahisi katika nyumba hiyo kwa sababu mlango wake haukuwa imara, si unajua nyumba za vijijini nyingi zilivyo,`` alisema.

Alisema polisi wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kuwasaka wauaji hao ambapo mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, mauaji ya albino huyo yanadaiwa kutokana na imani za kishirikina, ambapo wauaji wana imani kuwa, viungo vya albino vitawapatia utajiri.

``Huu ni ujinga mtupu, yaani unaua mwenzako kwa imani za kijinga kiasi hicho! Ninawaomba wananchi wote tushirikiane ili tukomeshe ujinga huu,`` alisema Kamanda.

Mauaji ya albino huyo yametokea wakati taifa likiwa katika mapambano makali dhidi ya watu wanaoendesha mauaji ya aina hiyo.

My Take:

Bado nimetoa changamoto ya shilingi laki mbili kuanzisha mfuko wa kutoa "donge nono" kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazosababisha kukamatwa, kufikishwa mahakamani na kutiwa hatiani kwa wahusika. Mwema bado hajajibu!!
 
hii ni changamoto nzuri sana Mwanakijiji, na donge hilo nono linafaa kutangazwa kwa kupitia vipindi vya redio na tv.
iwapo kuna mtu ana contacts na redio kama bbc swahili, sauti ya Ujerumani, Marekani, Japan, China, Iran, tuutume ujumbe huu ili upate kusikika kule hsa unakohitajika. ambako ni vijijini
 
hii ni changamoto nzuri sana Mwanakijiji, na donge hilo nono linafaa kutangazwa kwa kupitia vipindi vya redio na tv.
iwapo kuna mtu ana contacts na redio kama bbc swahili, sauti ya Ujerumani, Marekani, Japan, China, Iran, tuutume ujumbe huu ili upate kusikika kule hsa unakohitajika. ambako ni vijijini

I'm working on it right now... great idea!! shukrani.
 
Dunia Inakwenda Mrama..........jamani Inatisha,kusikitisha Na Kutojua La Kusema.....
 
mungu wangu!
nimeshindwa hata na cha kusema kwa kweli.
mungu awape subira wazee wa mtoto huyo mdogo aliyefanyiwa ukatili wa aina hii.
mungu ajaalie hii iwe sababu ya wanaofanya vitendo vya ukatili kama huu na mwengine wa kuuwa wenzao kufichuliwa na kuchukuliwa hatua.
la haula.
 
samahani kwanza nikuulize, hii umeiona wewe kwa macho yako au?
nauliza hivi kwa sababu nimeona hii hii kwa michuzi na yeye hajasema kama kaitoa kwa mdau
 
Mimi sielewi nini kilitokea kati ya kushuka na ungo hadi hii itokee. Kuna kitu hakijakaa sawa.

Halafu kuna kitu sielewi, naona blog zetu zina uhuru sana wakuweka graphic pics, sana sana mambo ya ajali za gari etc, na hii ya leo. Mtu uki-hit tu page, unakutana na picha. Bora hizo picha ziwe zinawekwa kama link, mtu akitaka anabonyeza mwenyewe.
 
Wazazi kazanieni elimu ya dini sambamba na elimu ya dunia. Naamini binaadamu yeyote anayemuogopa mungu hawezi fanya kitendo kama hiki.
 
This is unbelievable, sasa watz kwa uchawi tunaidizi hata NIgeria! Mi najiuliza kila wakati wachawi wanafaidika na NINI wanapofanya unyama kama huu???? ndio maana huwa sisikitiki hata chembe wanavyojichukulia sheria mikononi na kuwaua. Huyu kijana na achomwe moto hadharani!hawezi akaua mtoto wa mtu na kumla nyama halafu kuzungumza kama vile ameua paka na sio binadamu!!! kama alitaka nyama si ale mbwa!I am out of speech am just too upset with what happening in Tanzania. Well, tuzidi kumwomba Mungu atulinde na azilinde familia zetu huko nyumbani.
 
Hii nimeipata gazeti la Mwananchi:


Mtoto akamatwa na kichwa cha mtu, akitafuna mbele ya askari
Festo Polea na Kuruthum Ahmed

MTOTO Ramadhani Mussa (12) anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo.

Mtoto huyo alikutwa na kichwa hicho jana alfajiri baada ya kutiliwa mashaka na Fulgence Semfukwe ambaye ni mlinzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili wakati akijaribu kuingia chuoni hapo akiwa na mfuko mkononi.

Baada ya askari hao kumuuliza mtoto huyo hakujibu kitu na badala yake akatoa kichwa cha mtoto kilichokuwa katika mfuko huo na kuanza kuking'ata na kutafuna nyama yake jambo ambalo liliwastua askari hao kumweka chini ya ulinzi huku wakiwasiliana na askari polisi kwa msaada zaidi.

Polisi walipomhoji mtoto huyo alisema anaishi Jeti Lumo na anaishi na bibi yake aliyemtaja kwa jina moja la Andenga na kuongeza kuwa mama yake mzazi anaitwa Khadija na ni mkazi wa Tabata kwa Bibi.

Mtoto huyo alijieleza zaidi kuwa yeye na bibi yake huwa wanaishi kwenye makaburi yaliyopo Jeti Lumo na kazi yao huwa ni kula nyama za watu.

Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Charles Mkumbo akizungumzia tukio hilo alisema linahusishwa na tukio lililotokea juzi saa 3.00 usiku ambapo mwili wa mtoto uliokotwa ukiwa umechinjwa kichwa eneo la Segerea.

Alisema katika tukio hilo, wakazi wa Kimara Baruti, Upendo Dastan (27) na mumewe Yohana Mussa Majani (26) aliyekuwa na mtoto wao Salome Yohana (3), juzi walikwenda kumtembelea bibi yao Furaha Majani anayeishi Segerea kwa Bibi kwa lengo la kulala huko.

Mkuu huyo wa upelelezi alisema walipofika kwa bibi yao mtoto wao alianza kucheza na ilipofika saa 3.00 usiku mtoto huyo akapotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kamanda Mkombo aliongeza kuwa ilipofika juzi alfajiri, Lukas Kibaya (32) ambaye ni anafanya kazi ya kufyatua matofali katika eneo hilo alipokwenda kujisaidia chooni mita 800 kutoka kwa nyumba waliyofikia alikuta shimo la choo hicho limefunikwa na tofali huku likiwa limegandamizwa na nguo.

Alipolifunua akakuta kiwiliwili cha mtoto mdogo bila kichwa ndipo alipotoa taarifa polisi Sitakishari ambao walifika kuuchukua mwili huo hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Mkumbo aliongeza kuwa baada ya kutukia tukio polisi iliwapeleka wazazi wa mtoto aliyepotea polisi kutambua kichwa cha mtoto kilichokamatwa na kuthibitisha kuwa ni cha mtoto wao.

�Tuliwasiliana na wazazi na wakathibitisha kuwa ndiye mtoto," alisema na kuongeza kuwa Ramadhani aliyekamatwa na kichwa hicho anashikiliwa na polisi SitakiShari kwa uchunguzi zaidi na kichwa hicho kimehifadhiwa katika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza na Mwananchi jana mama wa mtoto huyo, Upendo Dustani alisema mtoto wao Salome alishinda nyumbani kutwa nzima ilipofika saa 3:45 usiku baada ya kumlisha chakula cha usiku ndipo alipotoroka na kukutwa alfajiri akiwa amekufa.

Mama wa mtoto huyo alisema walikuja kwa ajili ya kumsalimia shangazi yake anayeishi Tabata Segerea ambaye hawakuonana kwa muda mrefu.

"Kifo cha mwanangu kimetokea katika mazingira ya kutatanisha na nina imani Mungu atatulipia kwa waliofanya kitendo hicho cha unyama", alisema mama huyo kwa uchungu.

Naye Mjumbe wa Shina wa eneo hilo, Salum Pembe alisema amepata taarifa hiyo alfajiri kutoka kwa majirani na kumueleza kuwa Salome alikutwa akiwa amekufa kwenye shimo la choo akiwa maiti yake ameviringishwa matambara na akiwa amekatwa kichwa.

 
Back
Top Bottom