Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Matatizo sio yangu ni matatizo yenu ya kufuata vibudu :-

The Bible says:
Numbers 23:19 "God is not a man…"

Hosea 11:9 "...For I am God, and not man..."

Jesus is called a man many times in the Bible:

John 8:40 "…a man who has told you the truth…"

Acts 2:22 "Jesus the Nazarene, a man attested to you by God with miracles and wonders and signs which God performed through Him in your midst, just as you yourselves know."

Acts 17:31 "He will judge the world in righteousness through a man whom He has appointed"
1. Tim. 2:5 "…the man Christ Jesus."

Njoo hapa useme kama ni Mtoto wa Mungu. Ndio hapo mkakamatwa na viungo vya alibino kwa kujipachikia uungu mambo yote mmekabidhiwa na shetani.

Pole sana ndg Mwiba, kama uliweka hizi ayat ili ufundishwe Biblia, umepotea njia.

I have better things to do kuliko kuhangaishana na mtu aliyepigwa muhuri wa kupotea na Shetani.
 
Hapana tunawafundisha na kuwaonesha njia kondoo waliopotea ambao wanamfuata jesus wa uongo yule stuntman aliyetundikwa kwenye mti,na pia nampa hongera Mtindiomgongo kwa kuiweka link ambayo wale Wakiristu wenye hamu ya kuona ukweli kuhusu sect wanayoifuata kuwa sio ya kweli na walipotoshwa na kupindishwa kwa maslahi ya jamaa aliekuwa na tamaa ya kujiita Mungu na hivyo kuona njia ambazo alifanikisha baada ya kuahidiwa na shetani na kukabidhiwa nguvu za giza ili ajinyakulie uungu tena kama haitoshi amejinyakulia na kujitengenezea grade tatu za uungu ,kwa kweli mtafaidika sana na kuona muangaza ambao umepewa guarantee kwa yeyote atakaesoma basi ataondoa mzamisho wa kichwa chake kwenye mchanga na kuondokana kabisa na dini ya Ben Pandera,hongera sana Mtindiowaubongo kwa kuwaelekeza wenzako wakajionee ukweli na ndio inavyotakiwa ili muondokane na dini ya shetani. Kwa upande wangu nafunga mjadala maana ukweli umeshajitokeza ni mtu na hiari yake hakuna kulazimishana kajisomee uamue mwenyewe ,narudi kwenye siasa kuizamisha CCM.

Kama nilipokwisha kupata kusema huko ktk siku za awali. Ndg zetu waelekeao njia ya maangamizi huwa wanashindwa kutofautisha baina ya vitu viwili;

1. Madai, na
2. Ukweli

Kuendelea kujibizana na mtu ambaye hajui tofauti baina ya madai / dhana kwa upande mmoja, na ukweli kwa upande mwingine, ni sawa kutwanga maji kwenye kinu.
 
Wakuu napiga hodi maana nimepotea kwa muda, suala la mauaji ya Albino kwa kweli mimi nitasema serikali imelipa mgongo. Tunajengewa mazingira ya kuzoea vifo vya namna hii kama wananchi wa Gaza na kwingineko kufananako huku serikali ya ccm ikiendelea kujitapa kwamba hii ni nchi ya amani na upendo.

Tuchukue mfano kwamba hawa jamaa wameacha albino wameenda kwa viungo vya ndugu wa viongozi ili kupata utajiri au mengineyo wanayotaka wao, kama leo unasikia mdogo wake Masha kakatwa miguu, kesho mtoto wa kaka yake kikwete kakatwa mikono, hujakaa sawa binti yake shangaziye chiligati kanyofolewa mguu mmoja, mara mjomba wake Makamba kanyofolewa "banana" yake... hivyo hivyo... Je, BADO ITAENDELEA? Natamani iwe hivyo nione mwisho wake..!

Wengine watasema hao wana ulinzi, si kweli. Tuko nao mitaani kila siku na kuwapata sio tatizo, ninataka kujua ni mbinu itatumika hapa maana kwa vyovyote lazima watazima hizi style, kwanini wanashindwa kufanya hivyo kwa Albino?????
 
Umesoma post # 75, hapa : http://https://www.jamiiforums.com/international-forum/24411-saudi-arabia-says-only-mosques-allowed-8.html

Yaani askari wanaompigania allah, wanataka kula kisamvu cha kopo.

Astaghfulrrillah!

Aisee 'mwezi mchanga' wako umefikia steji mbaya sana. Yaani wewe kila mstari wa Bible unautolea tafsiri kingonongono na kibashabsha..Nakusikitikia kijana mdogo umeharibikiwa hivi huko nyuma hukuwa hivyo kabisa. Hebu punguza munkari na hamasa usome hizi al 'hadiths labda zitakutuliza kidogo:

Kaaazi kweli kweli... Wapindwa katika buuu-waaa-naa!
 
Huyu mzee anaweza kuwa na uchungu sana na hawa ndugu zetu, ila kwa mawazo yangu nafikiri kilichomliza ni kuona kashindwa kazi anatoa maagizo hakuna linalotekelezeka na watendaji wake, nafikiri amefika mahali anajuta kwanini alikubali kufanya kazi na hawa wasanii ambayo hawatendi wanachoongea ni usanii mtupu!! uliona wapi Rais wa nchi katika issue kubwa kama hii anaongea huku akichekacheka.....
 
Mzee alikuwa na mchungu ya double impact!
 
Nikiingia kwenye ubinadamu naona Babu Pinda alikuwa na hisia nzito juu ya mambo yanayowatokea binadamu aina ya Albino waishio hapa Tanzania hasa sehemu za mikoa ya Magharibi ,kwa kweli hisia au naweza kusema alijikita sana ndani ya mawazo ya mauaji na kuona kiakili namna wanavyouliwa na kukatwakatwa mafungu kiasi ilikuwa kama kitu kinachomtokea live na anaona lakini hawezi kufanya kitu ,si hata wale watizamao michezo ya kihindi kuanzia mwanzo hadi mwisho kuna wengine hutoka machozi kuna wengine huangua kilio cha kwiki ,hivyo hisia za aina ile ambazo zinasema zinakuingia baada ya kujisahau na kuwemo katika janga linalotokea na kuhisia hisia za wazazi ndugu au jamaa wanaofanyiwa Unyama.

Ila katika upande wa upinzani nitamuweka katika fungu la viongozi wenye machozi ya mamba na alikuwa anabubujikwa na machozi hata kabla aibu ya kuezuliwa haijamfika ,maana kama mtendaji Mkuu ameshindwa kutumia nyenzo za ulinzi kuzuia mauaji ya Albino ,mipaka ya Tanzania imejaa matundu ,baadhi ya wauaji wanasemekana hupata tenda nchi jirani ,PM ameshindwa kuviamuru vyombo vya ulinzani na usalama kuidhibiti mipaka ya Tanzania ,tunaona ng,ombe wanaibiwa wanakatisha mipaka na kupekwa Kenya ,Jeshi ambalo tunalisifia kuwa lipo kwa ajili ya kulinda mipaka yetu inakuwaje kuwaje watu wanapenya ,kwa mfano huo tunaweza tukavamiwa na kupewa kisago halafu watu wakatokomea wasiko kujua,kwa nini wanajeshi hawachukui doria za kusitukizia katika Mipaka na kumuhoji kila mruka njia na kuwasachi kama wana silaha ,yote hayo Waziri Mkuu ameshindwa kuyatumia ,kwani uwezo anao na ruhusa anayo ,haiwezekani nyenzo hizo zitumike katika kuwaua wananchi wanaotumia haki yao ya kikatiba katika kupiga kura au kufanya maandamano na kuwawacha wauaji wakipeta kama hakuna polisi na vyombo vinavyohusika kudhibiti hali hiyo ,hivyo Waziri ilikuwa awajibishwe moja kwa moja.
 
Ndugu yangu tusianze kulaumiana.Hii sio kazi ya jeshi kuhakiki wanaoingia nchini bali uhamiaji pia Pinda hana mamlaka ya kuamuru JW bali anaweza kufanya hivyo kupitia kwa RAIS.
Mwisho this is a joke no need to debate on the article
 
Albino aliyekatwa mikono Kagera awasili Hospitalini KCMC

Na Ally Sonda, Moshi


ALBINO Mariamu Stanford ambaye miezi kadhaa iliyopita alikatwa mikono yake yote na watu wasiojulikana mkoani Kagera, ameshawasili katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, tayari kupatiwa viungo bandia.



Mariamu ambaye amefikia katika hosteli ya Umoja mjini hapa, juzi alifanikiwa kuzungumza na wataalamu wa utafiti wa mifugo na kilimo, kutoka vituo mbalimbali vya utafiti na wizarani waliokuwa wakiendesha warsha ya siku kumi katika hosteli hiyo.



Alisema alifika Moshi Machi 3 mwaka huu, akiwa na mtaalamu wa viungo bandia kutoka Idara ya Afya Kagera, mama yake mzazi na mtoto wake, Elisha kwa lengo la kupatiwa mikono bandia katika Hospitali ya KCMC.



“Tayari tumesharipoti KCMC,nipokelewa vizuri Mungu awajalie wote na sasa daktari wangu niliyekuja naye anaendelea kuwasiliana vizuri na wataalamu wa KCMC, ili niweze kupata nilichofuata,”alisema Mariamu.



Watafiti walionekana kuchukizwa sana na kitendo alichofanyiwa Mariamu cha kuongezewa ulemavu mbaya zaidi wa kukatwa mikono,walimpa msaada wa jumla ya Sh 323,500.



Watafiti hao walisema hali hiyo inaashiria kuwa vita dhidi ya watu wanaojihusisha na mauaji ya Albino na vikongwe bado changa na inahitaji kuimarishwa zaidi.


Hata hivyo, walimweleza Mariamu kuwa serikali na jamii ya Watanzania, inampenda na kamwe haitashindwa kumwezesha kumudu maisha yake ya kila siku pamoja na wale wanaomuhudumia.



“Mariamu alikuwa na mikono yake, alikuwa anafanya shughuli zake za kibinadamu,leo hii hana mikono, hawezi tena kula hadi alishwe, mama yake ndiyo anafanya yote hayo,hivyo jamii inapaswa kuelewa taabu ya Mariamu na ya mama yake, naomba wote tusaidiane kumlea Mariamu,” alisema Mbunge wa Vunjo Aloyce Kimaro ambaye alitoa msaada wa Sh 100,000.
 
2009-03-15 13:56:15
Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya

Kwa mara ya kwanza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Zelothe Stephen, ameongea na waandishi wa habari na kusema mchungaji Cosmas Mwasenga anayetuhumiwa kukutwa na viungo vya binadamu pamoja na mwenzake Luseshelo Mwashilindi, walikamatwa na viungo hivyo vinavyosadikiwa kuwa vya albino wakiviuza kwa Sh. milioni 30.

Alisema walikamatwa Februari 13, mwaka huu baada ya polisi kupata taarifa kuwa kuna watu wanauza viungo vya albino na hivyo polisi kuweka mtego uliofanikisha wakakamatwa.

Alisema Februari 12, mwaka huu polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba kuna kikundi cha watu katika mji wa Mlowo wilayani Mbozi wana viungo vya bindamu vinavyodhaniwa kuwa vya albino na kwamba walikuwa wakiwatafuta wateja wa kuvinunua.

Kamanda Stephen alisema watu hao walizagaa kutafuta wateja wa kununua viungo hivyo hadi katika maeneo ya Mwanjelwa na Makungulu jijini Mbeya na ndipo polisi waliweka mtego wa kumtafuta mtu wa kuvinunua ambapo alipotafutwa muuzaji walikubaliana kwa bei ya Sh. milioni 30 na kwamba viungo hivyo vilikuwa vimehifadhiwa nyumbani kwake mjini Mlowo.

Alisema hata hivyo kwa kuwa kiasi hicho cha pesa kilikuwa kikubwa, mnunuzi alimuomba muuzaji ampe muda wa kutafuta pesa zaidi ili kufikia kiwango hicho anachohitaji na ndipo siku iliyofuata Februari 13, polisi walifanya maandalizi na walifika nyumbani kwa Mwashilindi ambaye alitoa vipande viwili vya viungo vya binadamu na papo hapo akatiwa mbaroni.

Alisema polisi walifanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambapo alikutwa na viungo vya binadamu vinavyodhaniwa kuwa vya albino, dawa ya bindamu aina ya penincilin, maji ya kuchanganyia dawa pamoja na koti jeusi ambapo alipohojiwa zaidi alidai alikuwa akishirikiana na mchungaji wa kanisa la Pentekoste Idiwili, Mchungaji Mwasenga.

Wakati huo huo, tukio la kukamatwa kwa mchungaji huyo limeendelea kuzua mapya baada ya kubainika kuwa polisi watano walikwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake usiku wa manane bila kuwa na `search warrant`.

Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Idiwili wilayani Mbozi, Sanston Mkondya, katika taarifa yake aliyoiwasilisha kwa tume ya madhehebu ya dini mkoa wa Mbeya ambayo inachunguza suala hilo, alisema maofisa hao wa polisi baada ya kufika nyumbani kwa mchungaji huyo walianza kufanya upekuzi bila kuwa na `search warrant\' kama taratibu za sheria zinavyoelekeza.

Maofisa wa polisi waliokwenda kuendesha upekuzi huo nyumbani kwa mchungaji ni Staff Sajenti Datstan mwenye namba E.276 D/SGT ambaye ni Mkuu wa kituo cha polisi Mlowo, Saff sajenti Daniel (F 679D/SGT), Inspekta Ndimbo na Inspekta Malindisa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Idiwili, Mkondya, ambayo itapelekwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), imeeleza kwamba maofisa hao wa polisi walifika nyumbani kwa mchungaji huyo majira ya saa 7 usiku wakiwa na mchungaji huyo ambaye alikuwa amewekwa chini ya ulinzi.

Baada ya kufika nyumbani kwa mchungaji huyo, Ofisa Mtendaji ambaye alichukuliwa ili kuwa shahidi wakati wa upekuzi aligonga mlango ambapo mke wa mchungaji huyo, Pili Mwembe, alifungua na Mtendaji kuanza kuwatambulisha maofisa hao wa polisi.

Inadaiwa kabla ya kuingia ndani na kuanza kazi rasmi ya kupekua, Ofisa Mtendaji aliwataka maofisa hao kwanza wampatie `search warrant` ambapo hata hivyo hawakuwa nayo lakini baada ya kujitetea waliruhusiwa kufanya upekuzi kwa makubaliano kuwa wataiandika baadaye.

``Baada ya kazi ya upekuzi kukamilika niliwaambia twendeni ofisini kwangu, ili waandike madhumuni ya kumpekuwa Mchungaji Masenga ambapo walikubali na niliwasha taa ndipo wakaandika hiyo `search certificate,`` imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ambayo Nipashe inayo nakala.

Ofisa Mtendaji huyo hata hivyo katika taarifa hiyo pamoja na maelezo yaliyoandikwa na maofisa wa polisi ameeleza kwamba katika upekuzi huo hawakukuta kitu chochote nyumbani kwa mchungaji huyo.

Alisema baada ya siku 12 Mkuu wa Kituo cha polisi Mlowo, Staff Sajenti Datstan alifika kijijini Idiwili ambapo aliulizwa ni sababu gani zilizosababisha kukamatwa kwa mchungaji Mwasenga na kueleza kuwa Mwashilindi na kundi lake la majambazi walipokamatwa na kupekuliwa walikuta koti jeusi ambalo walidai ni la mchungaji huyo.

Tukio la kukamatwa mchungaji huyo limekuwa gumzo kubwa mkoani hapa ambako kila siku mapya yamekuwa yakiibuka ambapo wiki iliyopita mtu mmoja alikwenda nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Zebadia Mwakatage, akimuomba ampe rushwa ya Sh. 150,000 akidai ametumwa na polisi wanaopeleleza kesi hiyo waweze kumuachia huru mchungaji wake.

* SOURCE:Nipashe
 
Albino African seeks Spain asylum
BBC News Online

_45649853_albino-2.jpg

People with albinism are more vulnerable to skin cancer​
The Spanish government is considering an asylum request from an albino African who claims he might be killed in a witchcraft ritual if sent home.

The 18-year-old from Benin, known only as Moszy, arrived in Tenerife last week with 60 other African immigrants.

Some African nations have reported a growing trade in albino body parts, which some witchdoctors believe can bring wealth and good fortune.

The Spanish Commission for Refugee Aid described Moszy's fears as reasonable.

The director of the commission, Juan Carlos Lorenzo, told reporters: "In Africa albinos are considered to be a bad omen or a factor of good luck.

"It is logical that he fears for his life because among different ethnic groups his body may be used in a sacrifice ritual."

Last year, a BBC reporter in Tanzania posed as a businesswoman who wanted to get rich and went to various witchdoctors.

In some cases she was offered, for a starting price of $2,000, a potion made of albino body parts - including legs, hair, hands, and blood - to make her wealthy.

At least 40 albino people have been killed in Tanzania in recent months and more than 10 in neighbouring Burundi.

These are believed to be the African countries where people with albinism face the most danger.
 
hii inasaidia lakini sio rahisi kwa albino wetu kuweza kusafiri, mara nyingi albino wetu wanakuwa hawana kipato cha kuwawezesha hata kununua ticket ya kukimbilia nchi nyingine na kuomba hifadhi, labda wa kwetu wafanye maandamano kwenda ubalozi mmoja dar na wakatalie hapo, waombe hifadhi kwa nguvu, sababu kusafiri kama huyu haiwezekani.
 
2009-04-19 21:33:48
Na Emmanuel Lengwa

Mtu mmoja amenusurika kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira baada ya kudakwa `laivu` akimkimbiza mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino, kwa nia inayodhaniwa kuwa ni kutaka kumuua na kumnyofoa viungo vyake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Shaibu Ibrahim alisema tukio hilo lilitokea jana mishale ya saa 4:00 usiku katika kijiji cha Isanga C wilayani Bariadi.

Alimtaja mtu huyo aliyenusurika kuuawa kuwa ni Mindwa Mbuga (37) mkazi wa kijiji hicho cha Isanga.

Alisema mtoto Malulu Kusekwa (6), ambaye ni mlemavu wa ngozi na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Isanga C ndiye aliyenusurika kuuawa.

Akasema siku hiyo Malulu alikuwa akitoka nyumbani kwa mama yake ambako ndiko huwa anakula chakula na kwenda kwa babu yake, umbali wa kama mita 150 hivi kwa ajili ya kulala.

Akiwa akiwa njiani, walitokea watu wawili na kuanza kumkimbiza kwa kasi ya ajabu.

Kamanda Ibrahim alisema baada ya kuona hivyo, Malulu alikimbia huku akipiga kelele, hali iliyowafanya wananchi wajitokeze kumsaidia.

Alisema wananchi hao walianza kuwafukuza watuhumiwa ambao ni Mindu na mwenzake Kibishi Ihunduka, wote wakazi wa kijiji hicho cha Isanga C.

Walifanikiwa kumkamata Mindu na kuanza kumshushia kipigo, kabla ya Polisi kuwahi na kumwokoa, kisha kumfikisha kituoni.

Polisi walipompekua mtuhumiwa walimkuta na vitu ambavyo wamedai kuwa ni hatari japo hakuvitaja kwa kuchelea kuharibu upelelezi wa tukio hilo.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa Kibishi aliyefanikiwa kuwatoroka wananchi, ili aweze kuunganishwa na mwenzie kortini.

Aidha akasema Polisi wanaendelea kumhoji Mindwa kujua ukweli.

* SOURCE: Nipashe

Hivi mwendelezo wa zile kesi za waliowadhuru maalibino upoje? mbona kimya?
mbona hamna adhabu ya mfano??
Mahakama vipi banaa? mnatuangusha
 
Watanzania tuache kupoliticise swala la mauaji ya Albino.
Tuwashughulikie wahusika kisheria badala ya michezo ya kisiasa ya kupiga kura za maoni.
Ni aibu kwetu kuona wenzetu waliokutwa na janga hili baada ya sisi kuwa nalo kwa muda mrefu wamefanikiwa kulishughulikia ipasavyo.
Soma link hii BBC NEWS | Africa | Burundi albino murders case opens
 
MAUAJI YA ALBINO NA MILA ZETU
Ndio nimemaliza kuangalia filamu moja inayoitwa Independence Day and After , katika filamu hiii inaonyesha watumwa wa mistri wanavyotumikishwa na viongozi wao wa mistri enzi hizo , hawa viongozi wao walikuwa wameficha albino katika chumba maalumu , mmoja wa viongozi hawa bibi kizee akipata tatizo alikuwa anaenda kwenye kile chumba cha albino na kwenda kuongea nae au kusema shida zake kisha anasaidiwa anaendelea na shuguli zake za utawala .
Watumwa wote walikuwa wanampigia magoti albino huyu , ila wao hawakupata kujua kama ni albino kasoro wale viongozi tu , mwisho wa fulamu hii , Yule albino alitokeza kwa mara ya kwanza ili wale watumwa wengi wao walikuwa ni waafrika wamwabunu baada ya kuasi , akatokea mtu mwingine akarusha mkuki ukamchoma Yule albino kifuani akafa akawaambia watumwa HUYU SIO MUNGU WENU , Fulani hii inaelezea historia ya zamani sana huko mistri na katika jamii zingine zilizokuwa zinatumia albino kwa shuguli zao za kishirikina haswa za kiutawala .
Mimi ni mchaga , kama kawaida niliwahi kuuliza mzee mmoja hivi kuhusu vitu alivyokuwa havipendi kuhusu kabila hili , akaniambia moja ya vitu alivyokuwa hapendi ni kuhusu kuuliwa kwa mtoto mmoja au wote kama ikitokea mama kazaa mapacha , enzi hizo wachaga waliamini mapacha ni mkosi kwahiyo walikuwa wanauwa mtoto mmoja kama ni mapacha sehemu zingine walikuwa wanauwa wote inategemea na sehemu yenyewe .
Enzi hizo makabila mengi yaliyokuwa yanazunguka mlima ule wa Kilimanjaro walikuwa wanauabudu mlima huo kwahiyo chochote wakifanya wanaelekea upande wa mlima , ni sawa na baadhi ya dini wanavyoangalia au kuegemea upande wa sehemu Fulani katika sala zao au katika kufanya baadhi ya vitu vyao sema siku hizi zimeboreshwa zinaitwa dini na sio imani za jadi .
Tukija katika suala hili la maalbino siku hizi watu wamevalia kofia sana , wengi wanaongelea kuuwawa kwa maalbino na kuwa na mikakati kibao ya kupambana na wauaji hawa , wengi hawataki kusema historia inasemaje kuhusu mauaji haya , watafiti wa mambo ya historia mbona hawatuweki wazi kuhusu suala hili la maalbino ? kuna jambo moja napenda kushirikiana na wewe
Zamani wakati wa utoto wangu nilikuwa naambiwa albino hafi huwa anapotea tu , anaenda kusiko julikana na kweli kuna sehemu nilikuwa naishi morogoro , tulikuwa na jirani ambaye ni albino huyo kijana katika ujana wangu nikienda morogoro simwoni wenzake wanasema alipotea ghafla huko vijijini wanajua amepotea kama zile imani zao
Huku mjini habari tunazozipata ni kwamba kuna mauaji ya albino yanaendelea nchini haswa kanda ya ziwa hii ni tofauti moja kubwa kati ya wale wanaokaa vijijini wanaokosa nafasi ya kujua mambo mengi yanayowazunguka na hawa walio mijini wanaopata nafasi ya kujua mambo hayo na kushindwa kuyatumia kwa faida ya wote haswa wale wasio na uwezo huo ambao wako vijijini .
Naomba kufungua mjadala huu kuhusu maalbino na mila zetu , naona tusianze kukamata wauaji wa maalbino bila kujua vyanzo vingine vya mauaji haya , wengine ni mila na desturi zao , wengine ni utajiri kama tunavyoambiwa tuamini , wengine ni kwa ajili ya madaraka kama hiyo filani niliyoangalia , wengine ni katika kutoa nuksi katika familia na jamii wanazokaaa tuchague ipi ?

KUNA NINI KATIKA MAUAJI YA ALBINO NA MILA ZETU
 
Albino aeleza alivyonusurika kunyolewa nywele na mganga
Na Kuruthum Ahmed

ALBINO Joackim Magaza ambaye ni Shahidi katika kesi ya kutaka kutekwa, inayomkabili mganga wa kienyeji Kassium Mayunga wa Shinyanga, ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kuwa, mtuhumiwa alitaka kumvua kofia kwa ajili ya kumnyofoa nywele.

Mayunga anakabiliwa na kesi ya kutaka kumteka mlemavu huyo wa ngozi kwa lengo la kutaka kumwua.

Mlemavu huyo aliiambia mahakama kuwa Desemba 2 mwaka jana saa 10:00 jioni alipokuwa anatoka kupata chakula maeneo ya kituo cha Kimara Mwisho Dar es Salaam, alivuka barabara ili arudi ofisini kwa kaka yake.

Magaza alidai kuwa baada ya kuvuka barabara alikutana na kijana asiyemfahamu ambaye ndio mtuhumiwa alimchangamkia na kumwita rasta vipi? Nikamwambia poa.

Baada ya salaam alidai kuwa mtuhmiwa alimwambia kuna dili anataka ampe,nikiwa naendelea kumsikiliza akataka kunishika kofia ili aivue.

“Nilipoenda mbele kidogo nilimsikia akisema kuwa rasta zako ni nzuri, sikuwa na nia tena ya kuendelea kumsikiliza kwani nilikuwa simfahamu”alidai Magaza

Shahidi wa pili James Magazi alidai kuwa mtuhumiwa alimwambia kuwa alishawahi kwenda pale zaidi ya mara tatu na hakuwahi kumpata ila anashukuru leo kuonana nae kwani kuna dili anataka kumpa.

Shahidi huyo wapili alipomuuliza mtuhumiwa ni dili gani analotaka kumpa ndio akamwambia kuwa yeye anahujihusisha na kutafuta nywele, kidole na kucha za mlemavu wa ngozi au kati ya kimoja wapo kitakacho patikana.

Mtuhumiwa huyo alikuwa na begi jeusi nilimuomba iliniweze kulikagua lakini aligoma alipogoma nilianza kupambana naye hatimaye mtuhumiwa alifanikiwa kunitoroka na nilimfuatilia kwa msaada wa majirani tulifanikiwa kumkamata.

Tulivyomkamata tulianza kumuhoji mara akatokea mdogo wangu ambaye ni albino nikamuuliza kama anamfahamu kijana huyo alinijibu akasema kuwa hamfahamu,alipojieleza watu walitaka kumpiga ndio wakatokea mgambo wakatusaidia na kumfikisha katika kituo cha polisi cha Kimara na baadae kuhamishiwa Mbezi.

Baada ya kusikiliza kesi hiyo, mwendesha mashtaka mkuu Inspekta wa Polisi David Mafwimbo,aliomba kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea na shahidi mmoja aliyebakia.

Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo,Emilius Mchauru aliihairisha kesi hiyo hadi hapo itakapo kuja tena kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa shahidi aliyeongezwa Juni 15.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
Na Paulina David, Mwanza

MLEMAVU wa ngozi (Albino), mkazi wa Ibanda Relini kata ya Mkoalani wilaya ya Nyamagana mkoani hapa Aron Mongo (42), ameuawa na watu wasiojulikana na watu hao kumkata miguu yote miwili na kutoweka nayo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jamal Rwambow, aliwambia wandishi wa habari jana kuwa Aron alifariki dunia Juni 26 mwaka huu majira ya saa 3.45 usiku nyumbani kwake eneo la Ibanda Relini.

Alisema kuwa siku ya tukio watu wasiojulikana ambao idadi yao haikujulikana, kwa mara moja walivamia nyumbani kwa Aron na kupiga jiwe la fatuma na kisha kumvuta ndani ya nyumba na kumshambulia kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alisema kuwa, kabla ya kuuwawa Aron alijitahidi kupambana nao, akiwa na fimbo lakini watu hao walimzidi nguvu na ndipo walipoamua kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo.

“Tulipofika eneo la tukio tulimkuta Aron akiwa amekatwa kuanzia sehemu za mapajani na miguu yake ikiwa haipo na ndipo tuligundua kuwa wauaji wametoweka na miguu yake yote,’ alisema Kamanda

Alisema kuwa tukio hilo la kusikitisha limefanywa na watu ambao wamedhamiria kutenda mauaji ya kinyama, kwani mwili wa marehemu umekutwa ukiwa umeshambuliwa kwa mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili, hali ambayo inaonyesha kuwa alikuwa akijihami na wauaji hao lakini walimzidi nguvu.

Alisema kutokana na tukio hilo jeshi la Polisi mkoani hapa, linatangaza kutoa zawadi ya Sh 1 milioni kwa mtu ambaye atatoa taarifa za kufanikisha kukamatwa kwa wauaji hao.

Awali mtoto marehemu Kulwa Aron (13), aliwaambia wandishi wa habari kuwa kabla ya kutokea kwa mauaji hayo, majira ya saa 2.00 usiku kabla ya kula chakula cha usiku, mbwa za nyumbani kwao zilianza kubweka jambo ambalo liliwashtua.

Alisema kuwa baada ya kula chakula mbwa hao waliendelea kubweka, huku wakizunguka nyumbani kwao na baadaye waliingia ndani kulala.

Kulwa, alisema kuwa muda mfupi wakiwa wamelala ndipo waliposikia vishindo vikipita nyumbani kwao mara walisikia jiwe la fatuma likipigwa mlangoni kwao.

"Baada ya jiwe hilo kupigwa ndipo mlango ulipofunguka na baba yangu, kuchukua fimbo kwa ajili ya kupambana na watu ambao walikuwa wamepiga mlango huo, huku sisi tukipiga kelele," alisema Kulwa.

Kulwa alisema kuwa walipoanza kupiga kelele, watu waliokuwa wamewavamia waliwamulika kwa tochi machoni na kuwazuia kupiga kelele huku watu wengine wakiwa wameenda kwa majirani zao kuwazuia wasitoke ndani.

Aliongeza kuwa baada ya kumuua baba yao, majambazi hayo yaliondoka na kuwafungia mlango kwa nje ambapo mama yake mzazi alisukuma mlango huo kwa nguvu na kufunguka na kisha kutoka nje ambapo walimkuta baba yao tayari ameshafariki dunia na ndipo kupiga kelele ambazo ziliita baadhi ya majirani na kutoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi na mauaji hayo yanafanya matukio ya mauaji ya albino kwa mkoa wa Mwanza kufikia 13 huku jiji la Mwanza likiwa ni tukio la kwanza kutokea.


Wilaya ya Nyamagana inahusisha pia jimbo la uchaguzi la Nyamagana ambalo linaongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha. Jeshi la Polisi liko chini ya Waziri huyo. MM
 
Back
Top Bottom