Kwa jina naitwa Alex Mwezi. Naishi Sweden, mimi mwanachama mpya wa JF. Mimi huwa ninasoma sana magazeti pamoja na blogs za Kitanzania ili kujiweka sawa na hali ya maisha huko nyumbani. Kwa sasa naona siasa imepamba moto kweli kweli kuhusu ufisadi na mafisadi, jambo ambalo naliona kuwa ni zuri.
Lakini kwa kuwa matatizo ya ufisadi huwa yanachukuwa sura tofauti tofauti kila kukicha, yaani watu wakivalia njuga aina fulani ya ufisadi, kabla sulihisho halijapatikana mambo hugeuka, ufisadi mpya unaibuka. Hapo watu hutupilia mbali ule wa awali na kuuvalia njuga ufisadi mpya. Kimsingi nionavyomimi mwelekeo hauna dira .
Lengo la kujitambulisha kwangu ni kwasababu ya uchungu ninaopata mimi na wenzangu hapa Sweden, kuhusu
MAUJI YA KIKATILI YA MAALBINO. Ni swala ambalo naona kama serikali imelihukumu kifo, kisha kunawa mikono, tunabaki tukijiuliza je hukumu ya kifo itasaidia? Sijui.
Mimi na wenzangu tumeungana hapa na kuunda chama, huwa tunakutana mara kwa mara kujadili juu ya swala hili, je tufanyeje ili kuwasaidia ndugu zetu hawa?
Najua wana JF, mlijadili sana swala hili katika siku za nyuma kwa uchungu na umakini, lakini bado sijaona nini suluhisho. Kwa maantiki hiyo basi,
naomba nilirudishe swala hili kwenu wana JF ili tulitafutie ufumbuzi wa kina.
Wito wangu huu hauna maana kuwa sisi watanzani Sweden tunauwezo wa kulitatua, au kuliondoa tatizo hili, hapana ila tunaweza kuungana kwa pamoja ili kulitatua janga hili.
Katika kukutana kwetu tumejadili kuwa, mambo yanayo pelekea mauwaji hayo, (i) Historia ya imani inayowazunguka maalbino, yaani imani ya kuwa wao sio watu wa kawaida. Tangu hapo zamani tumeamini kuwa maalbino hawafi, ukiwaona jitemee mate, geuka nk.
(ii) Umasikini uliokithiri uliochanganyikana na imani hiyo hapo juu.
(iii) Ukosefu wa elimu ambao pia unaambatana na umasikini.
Na mambo yanayo changia kutositisha au kukomesha mauji hayo ni (iv) Kutowajibika kwa viongozi wetu, ambao kwa njia moja au nyingine nao ni waathirika wa imani potofu iliyopo hapo juu. Kuna article niliiona kwenye jamvi hili iliyo mnukuu mwandishi wa habari wa Ikulu (kama sija kosea) akikemea waandishi wa habari wasiandike habari ya maalbino kwenye vyombo vya habari. Kwasababu itafukuza watalii. Jambo ambalo linasikitisha sana na kutisha mno.
(v) Kufumbia macho kwa vyombo vya habari
(vi) Kufumbiwa macho na wasanii wetu, kama wana bongo flavor, waigizaji na kadhlika.
Kwa hali ilivyo sasa, juzi tu katika gazeti la Uwazi la tar 27, sijui kama ni chanzo cha kuaminika kwa kiasi gani lakini bado mauji yanaendelea. Wakati huo huo wananchi wako busy na mafisadi, wanasiasa na viongozi wanajiandaa na chaguzi zao, sasa swala hili tulifanyeje?
Tumeona kupitia mtandao kuwa kuna N.G.O's kadhaa ambazo zinajishulisha na kuwasaidia albino. Kuna jitihada makhususi za kuwatenganisha albino na jamii, kwa kuwajengea kuta na mageti yenye sengenge na vyupa. Sisi tunaona kufanya hivyo ni kutatua tatizo kwasasa, nivizuri lakini pia lina halalisha hisia na imani potofu zilizopo.
Naomba nisipoteze muda wenu mwingi, sisi tumeanzisha chama cha kitanzania lakini wanachama ni watu wote. Lengo ni kukuza, kujifunza mila za kiafrika mashariki. Kwasasa tuna fanya studie circle (darasa mdura) ambalo kila mtu ni mwanafunzi na kila mtu ni mwalimu. Tunatoa na kupokea changamoto ya nini tufanye. Tumedhamiria na tumeamua kufanya jambo juu ya swala hili, tutajichangisha kidogo tulicho nacho, tutaomba misaada kwa watu na mashirika ili tufanye tuchangie kurudisha
haki yao ya kuishi kwa ndugu zetu ambao ni albino.
Kwakuwa hakuna aliye na dawa, majibu, au suhisho la titizo hili lkn tukichangia mawazo tutapata tu suluhisho. Hivyo nawaomba ndugu zanguni karibuni katika darasa mduara hili ili tuchangie mawazo kwa pamoja.
Chama chetu ni kichanga, kinaitwa MWAMKO, Tanzanska förening. Kwasasa hivi mimi ndiyo mwenyekiti.
alexmwezi@gmail.com
Kwa niaba ya wanachama wote nawaomba wana JF kuchangia maoni yenu. Karibuni.
WANALIOGOPA JUA MCHANA, USIKU WANATISHWA NA VIVULI VYA GIZA.