Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Ni mtoto wa darasa la pili, just imagine wandugu, it pains very much to me🙁
 
WATU wasiojulikana wamemuua mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) na kumnyofoa mguu.

Albino huyo ameuawa Jumanne saa 2.30 usiku katika kijiji cha Nyawilimilwa kata ya Kagu wilayani Geita mkoani Mwanza.

Mtoto huyo, Gasper Elikana (10) alikuwa mwanafunzi wa darasa la pili, katika shule ya msingi Nyawilimilwa kijijini hapo. Albino huyo alivamiwa nyumbani kwao, akauawa na kunyofolewa Mguu.

Habari zilizopatikana kijijini hapo na kuthibitishwa na jeshi la polisi wilayani Geita zimebainisha kwamba, wauaji wamemjeruhi baba mzazi wa mtoto huyo, Elikana Kaswahili (42) kwa kumkata mapanga kichwani wakati akijaribu kumuokoa mwanawe.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Elias Kalinga, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, na amesema, hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Amesema, Polisi wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote waliohusika kwenye tukio hilo ili washitakiwe. Inadaiwa kuwa mtoto huyo alivamiwa wakati anatoka jikoni kwenda chumbani kulala.

Kwa mujibu wa taarifa hizo,watu watatu wenye mapanga walimvamia wakamuangusha chini.

"Baada ya kumuangusha chini walimkata shingo na alipoanguka walimkata na kumnyofoa mguu wake na kutoweka nao kusikojulikana, na kumuacha mtoto huyo akikata pumzi yake ya mwisho ya uhai…..’’ kilisema chanzo chetu cha habari kutoka katika eneo la tukio.

Inadaiwa kuwa,baba mzazi wa mtoto huyo, Elikana Kaswahili (42),alivyoona mwanae anakatwa mguu alitoka jikoni kwenda kumuokoa, wauaji walimdhibiti na kumshambulia kwa mapanga, kajeruhiwa sana.

‘Baada ya baba kuona mwanaye anashambuliwa na kukatwa mguu wake aliwavamia watuhumiwa hao na kuanza kuwashambulia kwa magumi kwa lengo la kumuokoa mwanaye,lakini walifanikiwa kumdhibiti kwa mapanga, wamemuumiza vibaya sehemu ya kichwani na shingoni…..’’ kimesema chanzo cha habari hizi.

Majeruhi huyo amelazwa katika wodi namba nane katika Hospitali ya Wilaya ya Geita,hali yake ni mbaya. Alipoteza fahamu, hadi leo mchana alikuwa hajazinduka.

Mauaji ya albino huyo ni ya kwanza Geita katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, kulikuwa na walemavu wa ngozi 92 wilayani humo, hivyo wamebaki 91.


Chanzo: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=3954
 
Eh Mungu wangu tusaidie. May he rest in peace and I wish the father quick quick recovery!
 
Chanzo cha Habari,ni Gazeti la Majira la tarehe 21-10-2009

MWANAFUNZI wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Nyawilimilwa, wilayani Geita, Mwanza mwenye ulemavu wa ngozi, Gasper Elikana (10) ameuawa kwa kukatwa shingo na mguu wake kunyofolewa.

Mbali na kumuua albino huyo saa 2:30 usiku juzi, wauaji hao walimjeruhi vibaya kwa mapanga, baba yake mzazi, Elikana Ngelela (44).

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limetangaza zawadi ya sh 1,000,000 kwa yeyote atayetoa taarifa za kukamatwa kwa wahusika, kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Bw. Elias Kalinga alipozungumza na Majira jana jioni baada ya kufika eneo la tukio.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw. Abbas Kandoro alisema kuwa alipokea taarifa za tukio hilo kwa masikitiko makubwa na kwamba kitendo hicho lazima kikemewa na kila Mtanzania anayejali maisha ya binadamu
wenzake.

Bw. Kandoro alisema utajiri haupatikani kwa kukata viungo vya albino bali ni watu kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo.

Alisema kuwa serikali inatoa wito kwa jamii kutoa ulinzi kwa walemavu wa ngozi mkoani Mwanza na si kuiachia serikali pekee katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo hivyo vya kinyama.

Bw. Kandoro alisema ameagiza timu maalumu kutoka mkoani Mwanza, ikiongozwa na Bw. Kalinga kwenda wilayani Geita kufanya uchunguzi kuungana na Kikosi Kazi kinachoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Geita, Bw. Philemon Shelutete.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dkt.Cassian Kabuche alisema kuwa majeruhi ambaye amelazwa wodi namba nane hospitali hapo hali yake si ya kuridhisha kutokana na majeraha aliyopata kichwani.

"Alifikishwa hapa jana (juzi) usiku akiwa hajitambui kiasi kwamba iwapo hali ingeliendelea hivyo hadi leo (jana), tungempeleka katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, lakini kutokana na juhudi zilizozifanya hali yake angalau inatia moyo kidogo," Alisema Dkt.Kabuche.

Habari zilizopatikana kijijini hapo, zinasema wauaji hao wakiwa na mapanga, walifika nyumbani kwa Bw. Ngelela na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kisha kumuua mwanaye.

Mkazi wa kijiji hicho, Bw. Makami Nkilijiwa, alisema majirani walisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa mama wa mtoto huyo, na
walipofika walikuta wauaji wamekwishatoweka na mguu wa kulia wa mtoto huyo, huku mwili wake ukiwa umekatwa shindo huku baba yake akiwa ajitambui.

Baada ya kuona hali hiyo, wakazi wa kijiji hicho walimchukua majeruhi na mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Wilaya ya Geita ambako maiti imehifadhiwa na majeruhi akiendelea na matibabu.

Waziri Masha,kazi kubwa tuliyokupa ni kutulinda sisi watz na mali zetu,na tambua kuwa unalipwa mshahara na posho nzuri kwa kazi hiyo,lkn kila mwezi albino wanaendelea kuuawa kinyama TZ;

Kama Rais Mstaafu Mwinyi alijiuzuru kwa sababu tu vijana wake walipiga vikongwe kule Shinyanga mwaka 1972,iweje hadi leo Waziri Masha usiachie ngazi kwa kushindwa kuwalinda albino wanaouawa kinyama?
 
Aisee hii ni hatari,hawa watu hawasikii la muadhini wala mnadi sala,ee mola tunaomba ulinzi wako juu ya hawa ndugu zetu albino!!
 
😡ngriiiiiiii Najaribu kupata picha wakati wa tukio - mtoto mdogo anaona baba anagaragazwa na anajua punde tu nae atachinjwa. what a pain? wasiwasi, hofu nk. nyie wasukuma mna nini?????

Tafuteni kazi mbadala za kuwaletea kipato, no easy money, ng'ombe nyie😡
 
Kwa jina naitwa Alex Mwezi. Naishi Sweden, mimi mwanachama mpya wa JF. Mimi huwa ninasoma sana magazeti pamoja na blogs za Kitanzania ili kujiweka sawa na hali ya maisha huko nyumbani. Kwa sasa naona siasa imepamba moto kweli kweli kuhusu ufisadi na mafisadi, jambo ambalo naliona kuwa ni zuri. Lakini kwa kuwa matatizo ya ufisadi huwa yanachukuwa sura tofauti tofauti kila kukicha, yaani watu wakivalia njuga aina fulani ya ufisadi, kabla sulihisho halijapatikana mambo hugeuka, ufisadi mpya unaibuka. Hapo watu hutupilia mbali ule wa awali na kuuvalia njuga ufisadi mpya. Kimsingi nionavyomimi mwelekeo hauna dira .
Lengo la kujitambulisha kwangu ni kwasababu ya uchungu ninaopata mimi na wenzangu hapa Sweden, kuhusu MAUJI YA KIKATILI YA MAALBINO. Ni swala ambalo naona kama serikali imelihukumu kifo, kisha kunawa mikono, tunabaki tukijiuliza je hukumu ya kifo itasaidia? Sijui.
Mimi na wenzangu tumeungana hapa na kuunda chama, huwa tunakutana mara kwa mara kujadili juu ya swala hili, je tufanyeje ili kuwasaidia ndugu zetu hawa?
Najua wana JF, mlijadili sana swala hili katika siku za nyuma kwa uchungu na umakini, lakini bado sijaona nini suluhisho. Kwa maantiki hiyo basi, naomba nilirudishe swala hili kwenu wana JF ili tulitafutie ufumbuzi wa kina.
Wito wangu huu hauna maana kuwa sisi watanzani Sweden tunauwezo wa kulitatua, au kuliondoa tatizo hili, hapana ila tunaweza kuungana kwa pamoja ili kulitatua janga hili.
Katika kukutana kwetu tumejadili kuwa, mambo yanayo pelekea mauwaji hayo, (i) Historia ya imani inayowazunguka maalbino, yaani imani ya kuwa wao sio watu wa kawaida. Tangu hapo zamani tumeamini kuwa maalbino hawafi, ukiwaona jitemee mate, geuka nk.
(ii) Umasikini uliokithiri uliochanganyikana na imani hiyo hapo juu. (iii) Ukosefu wa elimu ambao pia unaambatana na umasikini. Na mambo yanayo changia kutositisha au kukomesha mauji hayo ni (iv) Kutowajibika kwa viongozi wetu, ambao kwa njia moja au nyingine nao ni waathirika wa imani potofu iliyopo hapo juu. Kuna article niliiona kwenye jamvi hili iliyo mnukuu mwandishi wa habari wa Ikulu (kama sija kosea) akikemea waandishi wa habari wasiandike habari ya maalbino kwenye vyombo vya habari. Kwasababu itafukuza watalii. Jambo ambalo linasikitisha sana na kutisha mno.
(v) Kufumbia macho kwa vyombo vya habari (vi) Kufumbiwa macho na wasanii wetu, kama wana bongo flavor, waigizaji na kadhlika.
Kwa hali ilivyo sasa, juzi tu katika gazeti la Uwazi la tar 27, sijui kama ni chanzo cha kuaminika kwa kiasi gani lakini bado mauji yanaendelea. Wakati huo huo wananchi wako busy na mafisadi, wanasiasa na viongozi wanajiandaa na chaguzi zao, sasa swala hili tulifanyeje?
Tumeona kupitia mtandao kuwa kuna N.G.O's kadhaa ambazo zinajishulisha na kuwasaidia albino. Kuna jitihada makhususi za kuwatenganisha albino na jamii, kwa kuwajengea kuta na mageti yenye sengenge na vyupa. Sisi tunaona kufanya hivyo ni kutatua tatizo kwasasa, nivizuri lakini pia lina halalisha hisia na imani potofu zilizopo.
Naomba nisipoteze muda wenu mwingi, sisi tumeanzisha chama cha kitanzania lakini wanachama ni watu wote. Lengo ni kukuza, kujifunza mila za kiafrika mashariki. Kwasasa tuna fanya studie circle (darasa mdura) ambalo kila mtu ni mwanafunzi na kila mtu ni mwalimu. Tunatoa na kupokea changamoto ya nini tufanye.
Kwakuwa hakuna aliye na dawa, majibu, au suhisho la titizo hili lkn tukichangia mawazo tutapata tu suluhisho. Hivyo nawaomba ndugu zanguni karibuni katika darasa mduara hili ili tuchangie mawazo kwa pamoja.
Chama chetu ni kichanga, kinaitwa MWAMKO, Tanzanska förening. Kwasasa hivi mimi ndiyo mwenyekiti. alexmwezi@gmail.com Kwa niaba ya wanachama wote nawaomba wana JF kuchangia maoni yenu. Karibuni.
 
Kwa jina naitwa Alex Mwezi. Naishi Sweden, mimi mwanachama mpya wa JF. Mimi huwa ninasoma sana magazeti pamoja na blogs za Kitanzania ili kujiweka sawa na hali ya maisha huko nyumbani. Kwa sasa naona siasa imepamba moto kweli kweli kuhusu ufisadi na mafisadi, jambo ambalo naliona kuwa ni zuri.
Lakini kwa kuwa matatizo ya ufisadi huwa yanachukuwa sura tofauti tofauti kila kukicha, yaani watu wakivalia njuga aina fulani ya ufisadi, kabla sulihisho halijapatikana mambo hugeuka, ufisadi mpya unaibuka. Hapo watu hutupilia mbali ule wa awali na kuuvalia njuga ufisadi mpya. Kimsingi nionavyomimi mwelekeo hauna dira .

Lengo la kujitambulisha kwangu ni kwasababu ya uchungu ninaopata mimi na wenzangu hapa Sweden, kuhusu MAUJI YA KIKATILI YA MAALBINO. Ni swala ambalo naona kama serikali imelihukumu kifo, kisha kunawa mikono, tunabaki tukijiuliza je hukumu ya kifo itasaidia? Sijui.
Mimi na wenzangu tumeungana hapa na kuunda chama, huwa tunakutana mara kwa mara kujadili juu ya swala hili, je tufanyeje ili kuwasaidia ndugu zetu hawa?

Najua wana JF, mlijadili sana swala hili katika siku za nyuma kwa uchungu na umakini, lakini bado sijaona nini suluhisho. Kwa maantiki hiyo basi, naomba nilirudishe swala hili kwenu wana JF ili tulitafutie ufumbuzi wa kina.

Wito wangu huu hauna maana kuwa sisi watanzani Sweden tunauwezo wa kulitatua, au kuliondoa tatizo hili, hapana ila tunaweza kuungana kwa pamoja ili kulitatua janga hili.
Katika kukutana kwetu tumejadili kuwa, mambo yanayo pelekea mauwaji hayo, (i) Historia ya imani inayowazunguka maalbino, yaani imani ya kuwa wao sio watu wa kawaida. Tangu hapo zamani tumeamini kuwa maalbino hawafi, ukiwaona jitemee mate, geuka nk.
(ii) Umasikini uliokithiri uliochanganyikana na imani hiyo hapo juu.
(iii) Ukosefu wa elimu ambao pia unaambatana na umasikini.

Na mambo yanayo changia kutositisha au kukomesha mauji hayo ni (iv) Kutowajibika kwa viongozi wetu, ambao kwa njia moja au nyingine nao ni waathirika wa imani potofu iliyopo hapo juu. Kuna article niliiona kwenye jamvi hili iliyo mnukuu mwandishi wa habari wa Ikulu (kama sija kosea) akikemea waandishi wa habari wasiandike habari ya maalbino kwenye vyombo vya habari. Kwasababu itafukuza watalii. Jambo ambalo linasikitisha sana na kutisha mno.

(v) Kufumbia macho kwa vyombo vya habari
(vi) Kufumbiwa macho na wasanii wetu, kama wana bongo flavor, waigizaji na kadhlika.
Kwa hali ilivyo sasa, juzi tu katika gazeti la Uwazi la tar 27, sijui kama ni chanzo cha kuaminika kwa kiasi gani lakini bado mauji yanaendelea. Wakati huo huo wananchi wako busy na mafisadi, wanasiasa na viongozi wanajiandaa na chaguzi zao, sasa swala hili tulifanyeje?

Tumeona kupitia mtandao kuwa kuna N.G.O's kadhaa ambazo zinajishulisha na kuwasaidia albino. Kuna jitihada makhususi za kuwatenganisha albino na jamii, kwa kuwajengea kuta na mageti yenye sengenge na vyupa. Sisi tunaona kufanya hivyo ni kutatua tatizo kwasasa, nivizuri lakini pia lina halalisha hisia na imani potofu zilizopo.

Naomba nisipoteze muda wenu mwingi, sisi tumeanzisha chama cha kitanzania lakini wanachama ni watu wote. Lengo ni kukuza, kujifunza mila za kiafrika mashariki. Kwasasa tuna fanya studie circle (darasa mdura) ambalo kila mtu ni mwanafunzi na kila mtu ni mwalimu. Tunatoa na kupokea changamoto ya nini tufanye. Tumedhamiria na tumeamua kufanya jambo juu ya swala hili, tutajichangisha kidogo tulicho nacho, tutaomba misaada kwa watu na mashirika ili tufanye tuchangie kurudisha haki yao ya kuishi kwa ndugu zetu ambao ni albino.

Kwakuwa hakuna aliye na dawa, majibu, au suhisho la titizo hili lkn tukichangia mawazo tutapata tu suluhisho. Hivyo nawaomba ndugu zanguni karibuni katika darasa mduara hili ili tuchangie mawazo kwa pamoja.

Chama chetu ni kichanga, kinaitwa MWAMKO, Tanzanska förening. Kwasasa hivi mimi ndiyo mwenyekiti. alexmwezi@gmail.com
Kwa niaba ya wanachama wote nawaomba wana JF kuchangia maoni yenu. Karibuni.

WANALIOGOPA JUA MCHANA, USIKU WANATISHWA NA VIVULI VYA GIZA.
 
Katakata ya Albino, yaibukia tena Morogoro


Bw Said Abdallah [41], ambaye ni albino, akiwa amelala kitandani katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, huku akiwa amefungwa bandeji kwenye mkono wake wa kushoto baada ya kukatwa kiganja chake na watu wanaodaiwa kuwa Wamasai na kisha kuondoka na kiganja hicho.

Katakata ya Albino, yaibukia tena Morogoro
. Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
- Baada ya serikali kulivalia njuga suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi [ma albino] na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi yake, vitendo hivyo vimeibuka tena mkoani hapa ambapo Bw
Said Abdallah[41] mkazi wa kijiji cha Melela Wilaya ya Mvomero Mkoani hapa
amelazwa katika hospital ya mkoa baada ya kudaiwa kukatwa mkono wake wa kushoto
na wamasai kisha kutimka nao!



Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi April 10 Majira ya saa 9 Alasili katika kijiji cha Melela ambacho kiko umbali wa kilometa 30 hivi kutoka morogoro mjini, ambapo imeelezwa kwamba wamsai hao walimvamia albino huyo ndani ya shamba lake na kuanza kumchapa bakora na baadae kumfyeka mkono wake wa kushoto kwa kutumia masime waliokuwa nayo.


Akizungumza na mtandao huu kwa taabu ndani ya wodi nomba 1 ya hospitali ya mkoa wa morogoro, Bw Said alisema kwamba siku ya tukio majira ya saa 9 alikuwa akilima katika shamba lake hilo lililopo maeno ya Kongolelo katika kijiji hichoambacho wakazi wake wengi ni wamasai.


Akisimulia zaidi mkasa huo Albino huyo alikuwa na haya ya kusema:



"Jana majira ya 9 nilikuwa nalima katika shamba langu ghafla niliona wamasai wawili wakiingiza Ngo'mbe kwenye shamba langu nilipowauliza kulikoni badala ya kunijibu waliniomba ugoro nikawaeleza kwamba sina.


"Kitendo hicho cha kuwanyima ugoro kiliwauzi na kuamua kunichalaza bakoro kichwani kutokana na wingi wa bakola hizo walizokuwa wakinipiga kichwani nilianguka chini nakupoteza fahamu, nilipopata fahamu nilijikuta nimeshakatwa
mkono wangu.



"Nilitafuta hicho kipande cha mkono wangu pale eneo la tukio sijakiona mpaka naondolewa eneo lile, nahisi wamasai wale waliondoka nao na kwamba lengo lao lilikuwa ni kuchukua kiungo changu kwani sina ugomvi nao
wowote", alisema Albino huyo ambaye bado hajaoa.



Muuguzi wa zamu wa wodi, Bi Rose Sengo, akizungumza na wanahabari kuhusiana na hali ya Albino huyo jana asubuhi
 

Attachments

  • Image000.jpg
    Image000.jpg
    19.8 KB · Views: 69
  • Image002.jpg
    Image002.jpg
    14.1 KB · Views: 47
Oo maskini kaka wa watu yaani serikali inabidi iwasaidie sasa amepewa kilema cha maisha yaani hao wamasai wakikamatwa lazima wapewe adhabu kubwa!!!
 
Inasikitisha sana kuwa katika wiki chache zilizopita vitendo vya kuua au kudhuru albino vimeanza tena kushika kasi. Inaonekana wauaji wamebaini kuwa serikali haiko makini katika kuwashughulikia kwani zile kesi zilizofunguliwa kwa majigambo sasa hivi hazisikiki tena. Ni moja tu ambayo tulisikia hukumu yake. Zingine zote hata kutajwa mahakamani hatusikii. Binafsi naanza kuhisi kwamba kunaweza kuwa na ukweli kuwa biashara ya viungo vya albino inahusisha watu wazito - viongozi na wafanyabiashara wakubwa. Kuna mahali nimesoma, sikumbuki vizuri kama ni hapa JF, mdau mmoja akipendkeza maalbino kuomba ukimbizi Marekani na kwingineko. Kwa hali hii nashawishika kumuunga mkono. Nawashauri viongozi wa vyama vya maalbino na wasamaria wema wengine tuanzishe huu mkakati wa kuwaombea ukimbizi hawa ndugu zetu. Hili litawahakikishia usalama wao lakini pia litawatia aibu watawala wetu mbele ya kadamnasi ya kimataifa. Mnasemaje?
 
no mnajua tusiwalaumu viongozi wetu sana kuusu ili swala la maalibilino
,ili swala ljnaitaji mimi na wewe kuusu kuwalinda awa ndugu zetu
ni ngumu sana kwa sbb serikali aiishi na awa watu mjumbani mwao'sisi
ndo tunaishi nao ni majirani zetu,na ni ndugu zetu pia'kwa iyo jukumu la kuwalinda
ni letu wote
 
Wana JF kama kunajambo linalonikera na kunifanya nikose raha kabisa ni haya matukio ya kuwakata viungo ndugu zetu maalbino.

Hivi watanzania tumekuwa wanyama kiasi gani ? Tulianza na mauaji ya vikongwe tukidai kuwa ni wachawi kutokana na macho yao kuwa mekundu kwa moshi wa kuni, tukaingia mauaji ya uchunaji ngozi na sasa viungo vya maalbino. Ukiangalia mauaji yote hayo yanauhusiano na imani za kishirikina.

Nauliza hivi kweli jamii pamoja na vyombo vya dola vimeshindwa kabisa kuzuia mauaji na unyama wanaofanyiwa maalbino?
 
Sijui kweli tatizo ni nini Albino ni jamii inayotuzunguka lakini bado wanaendelea kupata mateso na kuishi kwa hofu na mashaka utadhani sio Binadamu wenzetu.

Adhabu kali zitolewe kwa wote waliohusika na wanaoendelea kuwaua na kukata viungo vya Albino, Kifungo cha maisha kwa mtuhumiwa nadhani itakuwa fundisho
 
Mimi sijawahi kusikia mtu katiwa hatiani kwa kumuua au kumkata vioungo albino! Ingekuw vizuri kama vyombo vya habari vingekuwa vina report kesi hizi kama vinavyoshabikia kesi za Mafisadi. Huenda hii ingewatisha kidogo hawa wauaji kwa kujua kuw wakiua nao wananyongwa.
 
Kweli inahuzunisha sana...
Lakini tusiibebeshe serikali mzigo mkubwa sana. Kwani unataka kuniambia kwamba wananchi hawawafahamu kabisa hawa watu wanaotenda vitendo vya kinyama namna hii.
Suluhisho ni kuwa na uhusiano mzuri baina ya wananchi na serikali...
 
Jana 27/11/2012,BBC wameonyesha,kuhusu maalbino tanzania,inasikitisha sana,that dunia ya leo haya mambo yapo-watanzania this really shows how backwards we are-sijui tumemkosea nini mungu tu deserve such barbarism-tears flowed as i was brought back crushing to earth by events in the land of my birth-GOD HELP US
 
bunge.jpg

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.

Serikali yakiri ni jambo la aibu, Wabunge waitaka ichukue hatua za dhati kuzuia mauaji kwa wenye ulemavu.

Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema kuwa suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa ni aibu kubwa kwa nchi hivyo jamii nzima iangalie jinsi gani watu hao wanalindwa.

Pinda alisema hayo juzi Dodoma alipokuwa akifungua semina iliyoandaliwa na UNDP kwa wabunge kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Alisema mfumo wa watu wenye ulemavu wa ngozi katika elimu ni tofauti na watu wanavyofikiri kwa kuwa kama wakifundishwa kama wengine hawawezi kufika popote.

"Wana tatizo la kuona ukiancha tatizo la ngozi, hivyo ni muhimu wakaangaliwa vizuri," alisema Pinda.

Kwa upande wake Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema ni muhimu wabunge wakaelewa tatizo la watu hao ili waweze kuwaangalia katika majimbo yao na hata kuwafikiria katika bajeti wanazozipitisha.

"Ni muhimu utaratibu wetu wa bajeti tukawafikiria hawa kwa kuwa mimi binafsi kuna mambo wamenieleza ambayo mnapaswa kuyajua," alisema Makinda.

Alisema ni muhimu wakafikiria kutunga sheria za kuwalinda watu wenye ulemavu huo ili waweze kulindwa na sheria hiyo.

Akijadili suala hilo, Mbunge wa Kisarawe (CCM), Selemani Jafo alisema ni muhimu Bunge likapitisha sheria ya kuondoa kodi kwenye vifaa na dawa za kuwakinga walemavu wote.

"Pia Hospitali ya Ocean Road isaidiwe ili iweze kuwasaidia hawa walemavu," alisema Jafo.
Mbunge wa Busega (CCM), Dk Titus Kamani alishauri halmashauri zote nchini kuweka mazingira maalumu kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu huo na kuwapa dawa.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy alisema kuwa Serikali ndiyo inachangia watu wenye ulemavu wa ngozi kuuawa kwa kuwa inawalinda waganga wa jadi.

Mbunge wa Mpanda Mjini(Chadema), Said Arfi aliitaka Serikali iwawekee utaratibu maalumu wa kuwafikisha hospitalini na kuwapatia matibabu watu hao.


Chanzo: mwananchi.co.tz

 
Back
Top Bottom