Mwakilishi
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 483
- 34
Mie nahofu siku waganga wa wanasiasa waambie wanasiasa mkitaka mshinde uchaguzi leta kuingo cha albino!sijui itakueje hapo!
Mie nahofu siku waganga wa wanasiasa waambie wanasiasa mkitaka mshinde uchaguzi leta kuingo cha albino!sijui itakueje hapo!
Anyofoa nywele za albino, atokomea
2008-04-03 09:07:14
Na Elisante John, PST, Singida
Chokoraa mwenye umri wa miaka 12 anayeishi katika mazingira magumu, amehukumiwa kifungo cha miezi 36 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnyoa nywele albino kinyume na matakwa yake na kutoweka nazo. Chokoraa huyo atatumikia kifungo hicho katika jela ya watoto watukutu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Bi. Agatha Chigullu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Utemini mjini hapa. Ilidaiwa kuwa, mshtakiwa huyo alikwangua nywele za albino huyo baada ya kupewa ujira wa Sh. 500 na mchimba madini ya Tanzanite huko Mererani, wilayani Simanjiro.
Akitoa adhabu hiyo, Hakimu Bi. Chigullu alisema, amemtia hatiani mshtakiwa baada ya kumkanya mara kadhaa katika mahakama hiyo kutokana na tabia yake mbaya, lakini alishindwa kujirekebisha.
Alisema vitendo anavyowafanyia watu mbalimbali wakiwemo raia kutoka nje ya nchi kwa kuwaibia mali, havitavumiliwa na jamii, hivyo atalazimika kufunzwa adabu kwa miezi 36 katika shule maalum ya watoto watukutu ya Irambo iliyoko mkoani Mbeya.
Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Bw. Philipo Mzirai alidai kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Februari 14, mwaka huu saa 4:00 asubuhi katika mtaa wa Kindai, Wilaya na Mkoa wa Singida.
Alidai kuwa, mshtakiwa alimfuata Bw. Joseph Rashid (24) maarufu kwa jina la `Mchina` mkazi wa Utemini ambaye ni albino akiwa amejipumzisha na kumweleza kichwani kuna mdudu, hivyo anaomba amuondoe.
Alidai kuwa, alipokubali, mshtakiwa huyo alimkwangua nywele kwa wembe na kutoweka nazo.
Aliongeza kuwa, tukio hilo lilitokea nje ya duka la reja reja lililoko mtaa wa Kindai, Singida mjini mlalamikaji na mshtakiwa walipokutana pamoja na watu wengine huku wakiendelea na mazungumzo yao ya kawaida.
Ilidaiwa kuwa, baada ya muda mfupi kupita, chokoraa huyo alirudi eneo hilo na kumkuta albino ambapo alimwonyesha Sh. 500 huku akidai kuwa, alizipata kutokana na nywele zake.
``Kama siyo nywele zako, ningepata wapi hizi Sh. 500,`` mshtakiwa alikaririwa akimdhihaki albino.
Kabla ya adhabu kutolewa, Mzirai aliiomba Mahakama impe mshtakiwa adhabu kali kutokana na uhalifu alioufanya katika umri mdogo, pia kuwalinda watu wa jamii ya albino ambao baadhi ya watu wanataka kutumia viungo vyao kujitajirisha.
Akijitetea, mshtakiwa alionekana akibubujikwa machozi na kuiomba Mahakama imsamehe kwa madai kwamba, hatarudia kufanya kosa lolote.
Hata hivyo, Hakimu Chigullu alimweleza kuwa, Mahakama imemsamehe kiasi cha kutosha, lakini ameshindwa kubadili tabia, hivyo atalazimika kwenda kutumikia adhabu hiyo.
SOURCE: Nipashe
Ni kwa sababu hiyo basi, binafsi nakerwa na kushindwa kwa jeshi letu na watu wa Usalama wa Taifa (kama nilivyozungumza wiki iliyopita) kuja na operesheni kabambe ya kuwatafuta, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wale wanaoua ndugu zetu maalbino.
Kinachoniudhi zaidi ni jinsi gani serikali ya Rais Kikwete inalichukulia jambo hili kana kwamba ni "mojawapo tu ya uhalifu" kiasi cha kuunda kamati kama walivyofanya kuhusu EPA!
Kama kweli wanataka kukamata hawa wahalifu kwanini wasitoe ‘donge nono' kwa sababu tunajua pesa husaliti mtu. Watoe donge nono ambalo si chini ya sh milioni 20 kwa mtu au watu ambao watatoa taarifa zitakazosababisha kupatikana kwa watu wanaohusika na mauaji ya albino na kusababisha kutiwa kwao mbaroni na hatiani?
Hivi serikali inaweza kufanya hivyo ukizingatia kuwa kwa siku wanalipa sh milioni 150 kwa kampuni yenye mkataba hewa ya Richmond?
mi nimesikitikaa sana kuhusu hili swala na article ya mwanakijiji imezidi kuniumiza.hivi nchi hii imefikia wapi?hata haki ya msingi kwa kila binadamu ya kuishi inaweza kunyanganya hivi hivi na hamna hata mtu anashtakiwa kwa kuuwa hawa ndugu zetu.Hivi priority zetu zipo wapi jamani,blue chip companies baada ya kusupport causes kama hizi wao wanaona bora kusponsor Miss Tanzania.Hii idea naisapport lakini sithani kama tunatakiwa tuishie hapa.Wo walioshiriki wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na wote waliohusika kwenye huu uzembe wa hali ya juu tukianzia na IGP wawajibike.Sitaki kukubali na kuamini kuwa wahusika hawajulikani,na haki ya kuishi ni ya msingi na inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote.Mimi pia ntachangia kwenye hili.
Albino body exhumed, parts cut off in Ukerewe
11 Apr 2008
By Regional Reporters
Mwanza
In a grisly incident linked to witchcraft beliefs, especially with regard to ongoing albino killings in the country, unidentified people have exhumed the body of an albino in Ukerewe District, Mwanza Region, and made away with some of its parts.
In a second incident of its kind in a month in the district, some people believed to be driven by witchcraft beliefs unearthed a grave in which an albino had been buried and made away with the body`s left hand and right leg.
Reports from Ukerewe District said that the event occurred last week at Nakamwa Village in which the body of an albino, Benedicto Riziki (10), who died on March 9, this year, and buried the following day, was exhumed.
``This is the second case to happen here in Ukerewe,` a police source, who preferred anonymity, said.
He explained that last February unidentified persons exhumed an albino's body from a freshly dug grave and disappeared with the whole body in an incident linked to witchcraft beliefs.
Since last year there had been continuous countrywide albino assassinations on superstitious beliefs. At least nine albinos had already been killed in Mwanza Region alone.