Serikali itangaze kwamba mauaji ya albino ni janga la kitaifa na nchi iingie vitani na wauaji, kama ilivyokuwa kwa operation tokomeza. Na wauaji albino wapewe jina rasmi tena baya kushinda majangili, magaidi... sijui tuwaiteje kila jina ninalolifikiria kichwani naliona zuri kulinganisha na huu ukatili wao.
Zifanyike campaign serious za kupinga mauaji ya albino, kwa kutumia wasanii wenye kuvuta hisia za watu (influential) wa ndani na nje ya nchi kufanya hizi campaign, kampuni za simu, tv, social media zijiunge kwenye hii campaign..... kuvaa hivi vi T shirt peke yake haitoshi.
Pili, haya mauaji yameshakuwa kama vita sasa. Nchi ikiwa vitani raia hukimbilia kwenya kambi rasmi za wakimbizi, ama ndani (kunaweza kuwekwa safe heavens kwa ajili ya albino) ama nje ya nchi (nchi jirani n.k).
Kama mkakati wa muda mfupi, kamati za ulinzi za kila mkoa mahali zitengeneze kambi maalum kwa ajili ya albino na albino wote walioko kwenye mkoa huo, hasa watoto wadogo, wakusanywe huko, wapewe ulinzi mkali (tena na jeshi sio polisi sina imani na polisi, labda jeshi kidogo na wakimbizi hilindwa na jeshi kama sikosei) na huduma zote muhimu. Ikiwezekana hizi kambi ziwe jirani na kambi za jeshi kwa usalama zaidi. Na kama kuna mjamzito katika mkoa huo atakaye jifungua albino akimbilie naye hukohuko asirudi nae nyumbani.
Lengo hapa sio kuwanyanyapaa ila kuwapa ulinzi angalau kwa muda mfupi wakati mikakati ya muda mrefu inatafutwa.
Tanzania tukubali kwamba hili tatizo lipo na ni janga kubwa la kitaifa kama la boko haram au ISIS na tufanye campaign kutokomeza haya mauaji.
Hadi sasa hivi hakuna kitu serious zaidi ya matamko ya mtu mmoja mmoja mara leo Rais kesho sijui nani kuhusu hayo mauaji.
La mwisho la uzushi tu: mimi ningekuwa albino sasa hivi ningejilipua majuu kama asylum seeker nipate maisha bora na usalama, hapa bongo huna uhakika kama ukilala usiku ukiwa na viungo vyako vyote intact utafika navyo asubuhi - ikiwemo na roho yako - au haya mabandidu yatakuwa yameshakupunguzia baadhi au wamekutanguliza mbele za haki bila mwenyewe kupanga.
Waganga wa kienyeji kwenye mikoa yote ambako hilo tatizo ni kubwa wafungiwe kazi zao kwa sasa na serikali ihakikishe hao waganga nao wanafanya campaign ya kupinga mauaji ya albino
Ikiwezekana JF tuanze campaign sasa, hii forum inasomwa na watu wengi hata vijijini