Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

hivi wauwaji hawafikirii vizuri?? albino angekuadeal wangetajirika familia yake
 
Ni zaidi ya miaka kumi sasa imepita tangu haya mauaji ya kinyama yaanze kutekelezwa, kwa nn tusiyakomeshe?

Hv nani hasa wa kupewa lawama ktk hili?

Jibu jepesi kwa watu wenye uelewa mdogo watasema serikali, lakini uhalisia ni jamii yetu ndo mhusika mkuu wa kupewa kapu lote la lawama.

Suluhu.

Hebu tushiriki kuwa wapa elimu hawa watu wasio na hofu ya Mungu, ya kwamba utajiri au uongozi kwa njia za kishirikina na mawazo ya zamani sana, kimsingi hakuna ukweli!

Habari gani nchi za wenzetu mbona wamefankikiwa pasipo kutumia hizi imani potofu?

Twendeni mtaani kwetu tutoe elimu za kijasilia mali watu wapate mbadala wa kufanya maendeleo, hapo ulipo ubaweza ukawa una chembe za albino
 
Kwa uelewa wangu wa wastani kuhusu maumbile ya mwili ni kuwa tofauti na albino na mtu asiye albino ni kuwa katika "kemikali" zinazoshirikiana kutengeneza mtu kamili kuna aina moja ambayo ina kazi ya kuupa mwili rangi "colour pigment". sasa inapotokea kufeli kwa "kemikali" hii ndipo tatizo la mwili kukosa rangi muafaka linapotokea na mtu kuwa albino. Kwa msingi huo sasa ni kuwa utofauti upo kwenye rangi tu na si vinginevyo. habari ya albino au viungo vyake kuwa na uwezo wa kufanya anything supernatural ni mawazo yasiyo na mashiko.

Tuje kwenye mada:
Habari ya nani alaumiwe sidhani kama jamii inabeba lawama kwa kiasi unachoonyesha. Kimsingi ukiona mtu anafanya kitu kwa siri na anafanya chini juu asijulikane au kukamatwa hapo kwa asilimia zote anajua anachofanya si chema...sasa hapo utaingia katika jamii uielekeze nini?

Tatizo linaanzia wapi?
Watanzania tuna msemo wa "usiangalie ulipoangukia, angalia ulipojikwaa". Watu wote wanaohitaji (sio wanaoua) viungo vya albino wanakuwa wameagizwa na waganga wa kienyeji kwa maana kwamba aidha wanaambiwa wavitafute waviweke mahali fulani au wavipeleke kwa mganga akavifanyie kazi ili mambo ya hao wateja yaende kama wanavyotaka.

Mteja akitoka kwa mganga ndo anatafuta wauaji na kuwapa tenda/dili la kimtafutia hivyo viungo. hapo sasa mduara wa mauaji ndo unakamilishwa.

Jamii ijiulize mara mbili kuhusu hawa waganga. Najua hapa nitapingana na wengi: HAWA WAGANGA WOOTE WA KIENYEJI NI WAONGO!!!! Nieleweke hapa kwamba siwasemi waganga wa miti shamba..hao nawakubali..ila kunatofauti kati ya mtu kukupa hirizi ufunge mkononi na yule anayechuma majani fulani na kuyatwanga then akakupa uchemshe na kunywa kwa kuzingatia dosage flani! after all asilimia kubwa ya madawa ya hospitali yanatokana na mimea japo inakuwa refined zaidi.

Ila hawa wa "kapasulie nazi makabulini, kachimbie hii hirizi mlangoni, kalete tako la albino" hawa ndo tatizo kwa jamii.

Nani wa kulaumiwa:

Bila kupepesa macho ni kuwa kuna makundi mawili ambayo yote yanabeba lawama asilimia 100 kila kundi (yeah, mauaji ya albino ni unyama asilimia 200)


Waganga wa ramli na mazindiko:
hawa ndo wanawaagiza watu wakawaue albino so wana lawama zote

serikali
serikali hususani jeshi la polisi na mahakama vinawajibika kuwalinda wananchi wake so ni wajibu wao kuhakikisha hawa waganga WANAFUTIKA kabisa hapa nchini. Na ni rahisi kulitekeleza hilo kwa gharama kidogo mno. Ukitembea hatua 100 bila kuona bango la tangazo la mganga wa kienyeji hapa Dar basi jifinye uone kama hauoti..maana yamejaa mpaka vichochoroni..namba zao za simu zipo. kuwafikia ni rahisi kuliko kumzuia kikwete kuchekacheka!

Ingia mtaa wowote waulize raia watano wapi unaweza kumpata mganga, lazima mmoja wapo atakuelekeza..hata kama ni kukuelekeza kwa mtu atakayekuelekeza kwa mtu anayemfahamu mtu mwenye uwezo wa kukuelekeza kwa mganga...lakini utafika tu

sasa kuna approach mbili:
Uitwe udikteta au la..serikali ipige marufuku shughuli zote za uganga wenye mlengo wa kafara, mazindiko, ramli n.k na itangazwe (na kutekelezwa) adhabu kali kwa atakayejihusisha.

Baada ya hapo ndo watendaji waingie front kuwasaka hao makalumanzira

Approach 2
waganga waendelee kuwepo ila watumwe watu maeneo mengi ya waganga. Hao watu wawe na gadgets za kuweza kunasa anachosema mganga na ikiwezekana moving camera zitegeshwe (ndio, si kuna micro recorder?) ili mganga yeyote atakayeagiza kiungo cha albino akamatwe na kunyongwa within 24 hours, no case, no trial. na lawyers waambiwe wakijitolea kuwatetea basi wahesabiwe accessory to murder!!!!

waganga wakichajua kuna ishu kama hiyo unadhani wataagiza tena viungo? it will be like "mh, huyu mteja nikimuagiza kiungo cha albino then ikaturn out ni mserikali itakuwaje. Sometimes fear is the only solution.

Part ya raia:
tukijiunga wanaharakati then tukifanya mpango wa kuwa "wateja feki" wa waganga, tukakusanya ushahid na kuwapeleka polisi mnaonaje?

Nisameheni kwa gazeti reefu
 
Tuanzeni na hawa wasaka noti na vyeo...wanaotumia uchawi .tukiwaweza kuwakomesha hawa hawa waganga automatically watakosa wateja..hence no criminal offence. ..

Albino ni damu na hekalu Mungu ...tutaulizwa siku ya kiama .kwa nn uliua au ulifanya nn kuzuia kupotea kwa damu ya malaika wangu



........hebu tuwasemmeeni hawa wapuuz na wachawi waache huu uharifu
 
Serikali itangaze kwamba mauaji ya albino ni janga la kitaifa na nchi iingie vitani na wauaji, kama ilivyokuwa kwa operation tokomeza. Na wauaji albino wapewe jina rasmi tena baya kushinda majangili, magaidi... sijui tuwaiteje kila jina ninalolifikiria kichwani naliona zuri kulinganisha na huu ukatili wao.

Zifanyike campaign serious za kupinga mauaji ya albino, kwa kutumia wasanii wenye kuvuta hisia za watu (influential) wa ndani na nje ya nchi kufanya hizi campaign, kampuni za simu, tv, social media zijiunge kwenye hii campaign..... kuvaa hivi vi T shirt peke yake haitoshi.

Pili, haya mauaji yameshakuwa kama vita sasa. Nchi ikiwa vitani raia hukimbilia kwenya kambi rasmi za wakimbizi, ama ndani (kunaweza kuwekwa safe heavens kwa ajili ya albino) ama nje ya nchi (nchi jirani n.k).

Kama mkakati wa muda mfupi, kamati za ulinzi za kila mkoa mahali zitengeneze kambi maalum kwa ajili ya albino na albino wote walioko kwenye mkoa huo, hasa watoto wadogo, wakusanywe huko, wapewe ulinzi mkali (tena na jeshi sio polisi sina imani na polisi, labda jeshi kidogo na wakimbizi hilindwa na jeshi kama sikosei) na huduma zote muhimu. Ikiwezekana hizi kambi ziwe jirani na kambi za jeshi kwa usalama zaidi. Na kama kuna mjamzito katika mkoa huo atakaye jifungua albino akimbilie naye hukohuko asirudi nae nyumbani.

Lengo hapa sio kuwanyanyapaa ila kuwapa ulinzi angalau kwa muda mfupi wakati mikakati ya muda mrefu inatafutwa.

Tanzania tukubali kwamba hili tatizo lipo na ni janga kubwa la kitaifa kama la boko haram au ISIS na tufanye campaign kutokomeza haya mauaji.

Hadi sasa hivi hakuna kitu serious zaidi ya matamko ya mtu mmoja mmoja mara leo Rais kesho sijui nani kuhusu hayo mauaji.

La mwisho la uzushi tu: mimi ningekuwa albino sasa hivi ningejilipua majuu kama asylum seeker nipate maisha bora na usalama, hapa bongo huna uhakika kama ukilala usiku ukiwa na viungo vyako vyote intact utafika navyo asubuhi - ikiwemo na roho yako - au haya mabandidu yatakuwa yameshakupunguzia baadhi au wamekutanguliza mbele za haki bila mwenyewe kupanga.

Waganga wa kienyeji kwenye mikoa yote ambako hilo tatizo ni kubwa wafungiwe kazi zao kwa sasa na serikali ihakikishe hao waganga nao wanafanya campaign ya kupinga mauaji ya albino

Ikiwezekana JF tuanze campaign sasa, hii forum inasomwa na watu wengi hata vijijini
 
Tatizo Polic Wanawaza Kuwadhibiti Chadema, Kuzidi Kununua Mabom Ya Kutoa Machozi Pamoja Na Maji Ya Kuwacha,wamesahau Majukum Yao Ya Msingi Ya Kulinda Rais Na Mali Zake.
 
Hapa nipo kwenye daladala nawaza kwa nn mpka leo tunawakumbatia hawa mashetwani wasio na haya....
Kwa nnn operation tokomeza serikali iliwekeza pesa nyingi na kuita janga la kitaifa
Mathalani operatio kimbunga. ..zote zilitilwa kipaumbele sana japo zilikuwa na kasoro ktk ustaw wa jamii

Kwa hyo sasa bila kupoteza hata sekunde moja campeni ya tokomeza mashetwani ianze maramoja...watu wetu wa nguvu waishi kwa amani kma ilivyo kuwa enzi za mwl...


Tokomeza mauaji ya albino...yes we can
 
Nimeamua kwa moyo wa dhati kabisa kuukana uraia wa Tanzania, sitaki kuwa mtanzania na siitambui Tanzania, ila nafahamu kuwa Jakaya Mrisho Kikwete ni rais wa Tanzania, siwezi kuendelea kuwa mtanzania, naogopa ghadhabu ya Mungu ambayo muda si mrefu itashuka juu ya taifa hili la kishirikina na kuangamiza maelfu ya watu.

Hakika Mungu amechoka na upuuzi wa hili taifa wa kuua ndugu zake kikatili na kubeba viungo kwa imani za kishirikina, kila siku nalia, nimelia hadi nimechoka, ndugu zetu wanaishi kama wanyama mwitu ndani ya taifa lao, ili nikwepe hasira za Mungu juu ya hili taifa ni bora nikaukana utanzania mapema sana, watu wanadhani ni mchezo lakini ipo siku isiyo na jina.

Ambapo Tanzania itakuja kupata pigo kubwa sana, ushenzi wa taifa hili hauvumiliki hata chembe, dunia nzima ni Tanzania pekee inayojua albino kwa imani za kichawi, wakati mataifa yote yanaamini uchawi na hayaui albino, ole wako Tanzania maana siku zako zinahesabika utalia na kusaga meno, kuanzia leo sikutambui Tanzania, kaa na laana yako mimi simo najitoa.
 
Pole ndugu yangu,Pole Watanzania wenye nia njema.Poleni na wenye nia ovu.Hakika hukumu ya Mungu haita waacha wadhalimu waendelee kuishi.Wataaibika mchana kweupee.

Ndugu yangu wiseboy kana uraia wako au usikane kitaeleweka tu
 
mkuu haka ka nchi ketu kana matatizo yake but kuna vinchi vinamatatizo makubwa kuliko haya. ...shauri yako usijekujuta tu.

nami namuunga mkono tunahamia kwenye nchi ya maziwa na asali hatutaenda huko kwenye matatizo!
 
Mungu anatizama tu popote alipo...anatuvu
milia...mvua tunapata na jua pia na kula tunakula ila eti kwa hayo yote tunaua albino
..nilisikia ni last year sijui mwaka juzi tz ndio nchi inayoongoza kwa uchawi duniani na jambo lililotoa marks kubwa ni mauaji ya albino....hakuna duniani ila Tanzania tu ndio albino wanauliwa....khaaaaa jamaaaani kwa mwendo huu mvua za mawe lazima zije tu
 
Tatizo la sisi wabongo tukishakula kande na kuvimbiwa tunaingia jamvin na jaaazba. Dogoo wote tunaguswa na mauaji ya ndugu zetu mazeruzeru lakin kuukana uraia huo ni uahini muulize nyani ngabu faiza foxxy na akina chris lukos wanavyohaha. Achaa wewee mara moja!!
 
Back
Top Bottom