Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Nimeamua Kwa Moyo Wa Dhati Kabisa Kuukana Uraia Wa Tanzania,sitaki Kuwa Mtanzania Na Siitambui Tanzania,ila Nafahamu Kuwa Jakaya Mrisho Kikwete Ni Rais Wa Tanzania, siwezi Kuendelea Kuwa Mtanzania, naogapa Ghadhabu Ya Mungu ambayo muda si mrefu itashuka juu ya taifa hili la kishirikina na Kuangamiza Maelfu Ya Watu,

hakika Mungu amechoka na upuuzi wa hili taifa wa kuua ndugu zake kikatili na kubeba viungo kwa imani za kishirikina,kila siku nalia, nimelia hadi Nimechoka, ndugu Zetu Wanaishi Kama Wanyama Mwitu Ndani Ya Taifa Lao, ili Nikwepe Hasira Za Mungu Juu Ya Hili Taifa Ni Bora Nikaukana Utanzania Mapema Sana, watu Wanadhani Ni Mchezo Lakini ipo siku isiyo na jina

ambapo Tanzania itakuja kupata pigo kubwa sana, ushenzi wa taifa hili hauvumiliki hata chembe, dunia nzima ni Tanzania Pekee inayoua albino kwa imani za kichawi, wakati mataifa yote yanaamini uchawi na hayaui albino, ole Wako Tanzania Maana Siku Zako Zinahesabika Utalia na kusaga meno,kuanzia Leo Sikutambui Tanzania,kaa Na Laana Yako Mimi Simo Najitoa.

Wiseboy ulichosema ni sawa lakini kukana Uraia sio suluhisho la matatizo,wala hutakuwa umewasaidia ndugu zetu Albino,badala yake ungekuja kutueleza mbinu mbadala ya kuwanusuru hawa wapendwa wetu,Elewa kwamba''kukimbia tatizo si njia sahihi ya kutatua tatizo''.je ukiukana uraia wako ndo Abino watasalimika?.
 
Wiseboy ulichosema ni sawa lakini kukana Uraia sio suluhisho la matatizo,wala hutakuwa umewasaidia ndugu zetu Albino,badala yake ungekuja kutueleza mbinu mbadala ya kuwanusuru hawa wapendwa wetu,Elewa kwamba''kukimbia tatizo si njia sahihi ya kutatua tatizo''.je ukiukana uraia wako ndo Abino watasalimika?.
Well said...Ushauri wako mzuri!!
 
Only critical thinkers ndio watakaokuelewa,majority watakuja hapa kukukashifu na matusi juu

kwa hiyo Critical thinker wanafikiri juu ya kukimbia tatizo badala ya kuleta ushauri wa nini kifanyike ili kuwanusuru Albino?,duh! km anayekimbia tatizo badala ya kulisuruhisha ni Critical thinker basi nikutakie asubuhi njema.
 
Nchi hii kila siku utasikia viingozi wetu wanatuhakikishia kuwa jambo "hili" halitatokea tena!

Mbona yanazidi kutokea tu?Au wahusika wakuu ni ninyi wenyewe?Na sana sana kila tunapoelekea kwenye uchaguzi mambo haya huwa pacha!

tatizo viongozi wetu hawajadhamiria kutatua tatizo hili,mbona mengine wanashughulikia vizuri na yanaisha,iweje mauaji ya Albino yashindikane?,Je wauaji wana nguvu zaidi kuzidi serikali?,Basi ikiwa wauaji wamewazidi nguvu serikali,si waseme ili wasaidiwe! serikali itangaze hali ya hatari na kuomba msaada kutoka nje,vinginevyo tutalia mpaka tutapike nyongo.
 
Adhabu imeanzia kahama
Wataipata kanda yote ya ziwa mpk wawaache ndg yetu albino waishi kwa amani
 
Tatizo halikimbiwi mkuu, wala huwezi kuikimbia dhambi wala kumkwepa shetani, yupo dunia nzima, kwa pamoja tutatue tatizo
 
Wiki hii hapa Malawi vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa katika mjadala mkubwa kuhusiana na usalama wa maalbino na baada ya albino mmoja kutendewa unyama.

Chakusikitisha ni kuwa katika Afrika nzima, nchi yetu imekuwa kinara na watu wake wamekuwa mfano mbaya kwa usalama wa maalbino. Ukishajitambulisha au wakakujua wewe ni mswahili basi ni shida 'huaminiki' na utachunguzwa mpaka basi.

Shime viongozi wa Tanzania ondoeni aibu hiyo mbona mnataka kuiondolea heshima nchi yetu iliyosifika kama kisiwa cha amani na utulivu, nchi iliyopigiwa mfano wa watu kuwa wamoja na wenye upendo, nchi ambayo wakimbizi toka nchi jirani walipakimbilia na kujiona kama wako nyumbani lakini na sisi leo tunataka kutengeneza wakimbizi wa kuogopa au kunusuru maisha yao?

Tanzania ya mafisadi imekuwa si salama
 
Nimeamua kwa moyo wa dhati kabisa kuukana uraia wa Tanzania, sitaki kuwa mtanzania na siitambui Tanzania, ila nafahamu kuwa Jakaya Mrisho Kikwete ni rais wa Tanzania, siwezi kuendelea kuwa mtanzania, naogopa ghadhabu ya Mungu ambayo muda si mrefu itashuka juu ya taifa hili la kishirikina na kuangamiza maelfu ya watu.

Hakika Mungu amechoka na upuuzi wa hili taifa wa kuua ndugu zake kikatili na kubeba viungo kwa imani za kishirikina, kila siku nalia, nimelia hadi nimechoka, ndugu zetu wanaishi kama wanyama mwitu ndani ya taifa lao, ili nikwepe hasira za Mungu juu ya hili taifa ni bora nikaukana utanzania mapema sana, watu wanadhani ni mchezo lakini ipo siku isiyo na jina.

Ambapo Tanzania itakuja kupata pigo kubwa sana, ushenzi wa taifa hili hauvumiliki hata chembe, dunia nzima ni Tanzania pekee inayojua albino kwa imani za kichawi, wakati mataifa yote yanaamini uchawi na hayaui albino, ole wako Tanzania maana siku zako zinahesabika utalia na kusaga meno, kuanzia leo sikutambui Tanzania, kaa na laana yako mimi simo najitoa.

Utakuwa umezidisha dozi si bure. Tangu lini umekuwa msemaji wa mungu? Yaani watu wanauawa wewe unalialia alafu unakimbia badala ya kupambana? Nani amekwambia uraia unakanwa jf? Mwisho karibu somali
 
Hbr za asubuhi watanzania wenzangu na wale wasio watanzania,

Ni kwamba jana usiku km saa tatu hivi, nilikuwa nafuatilia kipindi fulani kwenye TBC,Mheshimiwa RAIS,alikuwa akizungumza na ndugu zetu ambao ni Walemavu wa ngozi(ALBINO),miongoni mwao walikuwepo na viongozi wa chama cha Maalbino Tanzania,TAS,Aidha walikuwepo Albino ambao ni wanaharakati na walikuwepo pia wale ambao wameshawahi kufanyiwa ukatili kwa kukatwa baadhi ya viungo vyao mfano ni dada mmoja anayeitwa Mariamu,huyu alinifanya nitoe machozi nilipomwona kwenye Runinga na kusikia maelezo yake kwamba alikatwa mikono yake yote miwili mwaka 2007,na mtu ambaye ni jirani yake,ambaye alikamatwa lkn baadaye aliachiwa huru,kilichonifanya nitoe Machozi pamoja na uanaume wangu ni pale aliposema kuwa eti Polisi walibatilisha maelezo yake aliyotoa dhidi ya watuhumiwa,kwamba maelezo yake si ya kweli na wakati yeye mwenyewe aliwaona wauaji hao wakati wakimfanyia unyama huo.

Swali langu kwa POLISI;Hivi ni ushahidi upi mnautaka zaidi ya huo uliotolewa na mtendewa? Lakini nyie waoneeni tu,ipo siku isiyo na jina mtakuja juta!maana MUNGU yupo,kweli inasikitisha nani atawatetea hawa?.Haya Swali kwa serikali;Hivi ni kweli kabisa mmeshindwa kuwapigania Albino?

Mbona yalipofanyika mauaji ya RPC-Mwanza,Mliwakamata wauaji kwa muda mfupi sana,mnashindwaje kwa wauaji wa Albino?,Daaah! ngoja niishie hapa nisije nikaanza kulia tena maana machozi yangu yapo karibu sana.
 
Karibia na uchaguzi ndio haya mauajibya albino yanakithiri.. Wanaowaua albino ni wanasiasa na madiwani na biongozi wanaotaka madaraka, sasa hao hao ndio walioshika dola wewe unategemea nini?
 
Sidhani kama imeshindwa .............,hili saga ni aibu ya Taifa.
 
Mi kale katoto ka rukwa kalinisababisha kulia maana kalikua kanatia huruma sn. Yaan hii serikali kwakweli basi tu haijali kbs kwavile wao ndio wahusika wakubwa.
Ndg zetu albino kwakweli wapo ktk wakati mgumu sn,tuungane sote kwa pmj kuwalinda na kuwatetea.
 
Hutakuwa wa kwanza hata nabii yunus (yona )alitoka nduki na bado watu wake wakaokolewa na pia taratibu za kuukana uraia zipo hapa jf inakuwa ni porojo.
 
Adhabu imeanzia kahama
Wataipata kanda yote ya ziwa mpk wawaache ndg yetu albino waishi kwa amani

Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa wale waliopatwa na maafa kule Kahama ni wadhambi siyo??? kwa hiyo kwa uelewa wako kwakuwa Kanda ya ziwa matukio ya mauaji ya Albino ni mengi,basi kila mkazi wa huko anahusika sivyo??,jiangalie sana ndugu ipo siku na wewe yatakukuta halafu watu tutakuuliza hivi kumbe na wewe una dhambi????
 
IPO Siku Tz itatakiwa kulipa kwa Mungu kwani kumwaga damu ya MTU ni laana ya milele,iangalieni Uganda na mashaidi waliochomwa moto hadi kesho ile nchi itakwenda kwa mtutu na damu
 
Hii serikali itakuwa inahusika kwa njia moja au nyingine, maana wamepewa watu wakunyonga na mahakama ili iwe mfano kwa wengine wanaojihusisha na huu ufedhuri wamekaa kimya as if hakuna kinachoendelea
 
Mikoa hii unakutana na albino machinga hadi usiku wala hana wasiwasi, wengine bar wanakunywa wala hawana hofu yoyote, nashangaa sana mikoa ya kanda ya ziwa kuwaona dili kama ni kwa ajili ya madini pia huku kuna migodi mingi tu ya tanzanite, green ganet tormalin nk, kama ni uvuvi hata huku kuna ziwa bBabati, nyumba ya mungu, jipe,nk kama ni kwa ajili ya uongozi hata huku wanagombea pia. Na hakuna watu wanapenda pesa kama wa huku ingekuwa wana dili wachaga, wameru na waarusha wangewaua mchana kweupe. Kanda ya kaskazini itabaki kuwa na maendeleo miaka yote.
 
Back
Top Bottom