Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Ukizingatia kuwa mauaji ya albino yanahusishwa na imani za ushirikina na kwamba wengi katika nafasi zao za uongozi na biashara katika nchi hii wanategemea sana nguvu za giza kupitia 'KAMATI za UFUNDI' ambazo kiungo cha albino kwao ni 'ingredient' muhimu sana, ni dhahiri kwamba vita ya kukomesha mauaji ya albino bado ni ngumu sana. Tuendelee tu kumwomba MUNGU atokomeze janga hili.
 
Tumeambiwa kabisa na mwenyezi mungu kuwa jisaidie na me ntawasaidia,ujinga wawachache unasema mungu atusaidie?tuanze kukomaa kwanza sisi
 
Tukio lolote la kishirikina linahusisha nguvu za giza. Tuanzie hapa.
Kukabiliana nalo mhusika anahitaji nguvu ya ziada mbali na akili na zana alizotengeneza. Nguvu hii isitoke upande wa giza kwani haitatatua tatizo. Mchawi mwenyewe akikamatwa kwelikweli anayefanya haya atasema nimeelekezwa na mkuu wa giza. Sasa mapambano haya ni dhidi ya YULE anaewapa hawa wachawi UCHAWI wa kufanya wafanyayo. Inahitajika nguvu ya Mungu kuingilia kati.

USHAURI WANGU KWA KIKOSI KAZI CHOCHOTE KInachowasaka hawa majangiri. Maharifa yote yaliotumika mpaka sasa wachache sn waliokamatwa ni waliotenda bila wahusika wakuu na wateja wa wahusika wakuu. Mnawasaka bila mafanikio wao wanajificha na kuwazubaisha kwa kutumia nguvu za giza. Kuwapata tumieni NGUVU ZA GOD ni nuru. NI hivi watafuteni wanamaombi wanaomwomba Mungu katika roho na kweli; WAAMBIENI MNAHITAJI MSAADA WA MUNGU KUPAMBANA NA TATIZO BILA KUWAFICHA. SIO LAZIMA IWE PUBLIC iwekeni kimkakati. Mtaombewa pia mtafunikwa na damu ya yesu kristo. Hapo wachawi na nguvu zao hazita fua dafu japo watakuekeeni mikwala. MSINIULIZE wanamaombi wanapatikana wapi Intelligensia yenu mkitumia mnawapata. Katika makanisa ya kiroho zipo vitengo maalumu vya MAOMBI na ni bule sio kwa pesa. Mkidaiwa pesa jueni hao sio.
Kuweni kama MAKOMANDO WA VITA. KOMANDO akiona plan A inakataa anageukia plan B na kusikiliza maoni ya wanaemwelewa ADUI.
Serekali haina dini. Lakini nyie KIKOSI KAZI katika kukabili janga hili pangeni mambo yenu maofisini baada ya hapo pita najua wengine mtazarau;
HAYA utamfuata mchawi hivi hivi kwa akili zako wakati ukinyanyuka keshakuona kwenye tunguli zake. Anakutia upofu kesi inaishia hewani. Hata hao wateja wao wakuu wanawaficha kwa hizo nguvu za giza. ILA kwa Mungu hakuna linaloshindikana.
HAO waganga wanaowatuma ndio wachawi wenyewe. Mwingine anajifanya kulaani hilo tukio la kuua albino mchana Lakini usiku wanavyofanya mambo yao WANAAGIZWA NA MAGWIJI kutekeleza nao wanatenda. PRICIPLE ZAO NDIO ZILIVYO TENA HAWARUHUSIWI KUTAJANA.

Wazo zuri ,hamna namna kwa sasa,wajaribu na hiyo.
 
Jk sio kiumbe wa kawaida kwanza hana hasira ya maendeleo, haguswi na matatizo yetu, hana hamasa ya kuonesha umahiri wake ktk uongozi, hakosoi viongozi wake hata wanapoonekana dhahir wamekosea labda kwa shinikizo kubwa n.k uongozi wake umekuwa ni dhaifu zaid kutokea tz na Mungu saidia asitokee kiongozi kama huyu. Pongezi kwako Ndg W. Mkapa

nenda bagamoyo kiwangwa ukaone maisha ya hawa wakwere, hawafai hata kuongoza familia.
 
Ah..hii nchi nishaikatia tamaa kitambo sana....basi tu hatuna sehemu ya kwenda..
- mafisadi..wanaiba mali za umma...wanateteana...polisi wako upande wa mafisadi...hadi marekani walivoshupalia wahusika wawajibishwe ndo tukaona hatua eti

- wanyama wanaibiwa..juzi kati hapa tanzania ilitingisha dunia kwa biashara ya pembe za ndovu.

-sasa ivi ndo kama ivo tena....tunaskika duniani kwa kukata viungo vya wanadamu wengine

nakadhalika..

natamani tungekua na raisi.
 
watanzania sote ni ndugu kutokana na kuguswa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi weka hapa taarifa za wauaji maana hawa tunaishi nao mitaani .fichua ili vyombo vya dola viwatie nguvuni
 
Mashambulizi dhidi ya albino: Usalama wa Taifa wako wapi?
Lula wa Ndali Mwananzela
Toleo la 396
11 Mar 2015

KAMA vile walikuwa wameenda likizo watu wenye kuhusika katika utekaji na ukataji viungo ndugu zetu albino wameibuka tena; na wameibuka kama wana kisasi. Hadi hivi sasa watoto kadhaa tayari wamekutana na jinamizi hili ambalo ni binadamu wenzetu, na cha kutisha zaidi ni kuwa dalili za watu hawa kutokomea kimoja hazipo. Wapo na wamerudi tena. Hili linahitaji tafakari ya aina yake. Nasema jambo hili linahitaji tafakari ya aina yake kwa sababu hadi sasa mwitikio wetu na hasa wa vyombo vya usalama na viongozi wa kisiasa unasikitisha na kwa kweli unapaswa kubezwa na kila mtu mwenye kutaka kukomesha vitendo hivi.

Mwitikio wa wana usalama wetu ni wa kushtuka na kufuata matukio; si mwitikio ambao unaweza kusifiwa kuwa unaonyesha weledi, mikakati, mbinu au teknolojia. Wameshindwa Jambo la kwanza ambalo ni lazima tuliweke wazi na sidhani kama linahitaji mjadala zaidi ni kuwa vyombo vyetu vya usalama vimeshindwa kukomesha matukio haya na kushindwa huko inawezakana kuna sababu zake nyingi. Inawezekana wameshindwa kwa sababu ya kukosa vitendea kazi, mbinu hafifu, utaalamu au hata weledi wa kuweza kufuatilia mambo haya.

Hili ni muhimu kufikiriwa kwa sababu kila vitendo hivi vinapotokea tumesikia kuwa ni zaidi ya mtu mmoja anahusika na watu wanaofanya vitendo hivi wamekuwa kama mizuka ya aina fulani; wanaingia na kufanya unyama na kutoweka. Kushindwa huku kunatisha. Na naomba kupendekeza kuwa kushindwa huku kunatokana pia na kutokuwa na uongozi wenye weledi na wenye maono ya kuweza kupambana na uhalifu ambao hauko katika vitabu. Ni rahisi kuwafuatilia watu wenye kufanya uhalifu wa ujambazi, wizi, au ubakaji, lakini unaweza vipi kufuatilia watu ambao wanafanya mauaji au kukata viungo katika mazingira ambayo ni vigumu kufuatilia? Lakini kushindwa huku kunafunua jambo ambalo nimekuwa nikiliandika mara nyingi – kulegalega kwa usalama.

Hakuna jambo la hatari kwa taifa lolote lile kama kuwa na vyombo ambavyo ama vimelegalega au havina uwezo wa kukabiliana na changamoto za usalama za zama hizi. Na binafsi naamini kuwa hakuna chombo ambacho kimeshindwa kazi hii, kama Idara ya Usalama wa Taifa.

Usalama umetengenezwa kushindwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ni Rashid Othman, maarufu kwa baadhi yetu kama R.O. Rashid Othman amekuwa katika kiti cha enzi cha Idara hiyo muda mfupi tu tangu Rais Kikwete aingie madarakani na pamoja wamekaa muda wote huu na kuna uwezekano hatoondoka sasa hadi ngwe hii ya pili ya Rais Kikwete itakapoisha, baadaye mwaka huu. Hata hivyo kama kuna jambo tunaweza kulisema kwa uhakika mkubwa – hasa tukiangalia matukio mbalimbali – ni kuwa hakuna chombo ambacho ni sehemu ya matatizo yetu sana kiusalama kama Idara ya Usalama wa Taifa. Na hapa sizungumzii kirahisi rahisi.

Matatizo haya ya msingi ya Idara hii yanatokana zaidi na kisheria na kimfumo kwani kati ya sheria mbovu zilizowahi kutungwa na Bunge letu ni ile iliyounda Idara hii. Wakati mwingine tunaweza kusema kuwa ilikuwa ni vizuri wakati Idara inaongozwa kutokana na sheria mbalimbali za Usalama wa Taifa kuliko ilipoundwa sheria kuifanya idara hii rasmi mwaka 1996. Sheria ile imetengeneza chombo ambacho kwa jina kinatisha lakini kivitendo kinaonekana kuwa legelege. Ni kama sanamu ya simba iliyowekwa kwenye nyasi na kutishia kila anayepita karibu; hadi pale wanapogundua kuwa si simba wanaweza kufanya lolote.

Matukio haya ya mauaji na ukataji viungo albino ni ishara kuwa kuna watu wanaamini kabisa kuwa vyombo vya usalama havina uwezo wa kuwafuatilia. Na hili ni kweli hasa unaposikia kuwa watu wanaolipwa na Watanzania wanakuja na masuluhisho ambayo ni ya kihisia kuliko kihalisia. Kwa mfano, mwitikio wa serikali yetu ni kuwalaumu waganga wa kienyeji. Wanataka watu waamini kuwa vitendo hivi dhidi ya albino vinasababishwa na waganga wa kienyeji; wanashindwa kujiuliza maswali mawili rahisi tu: Mbona waganga wa kienyeji wamekuwapo tangu enzi na enzi na havikuwapo vitendo kama hivi? Kweli wanaamini kabisa kuwa waganga wa kienyeji wakifutiwa usajili Tanzania ndio utakuwa mwisho?

Kwani nchi nyingine jirani na Watanzania wengi wanaenda kwa shughuli mbalimbali hakuna waganga wa kienyeji? Lakini hata kama tukikubaliana kuwa wapo waganga wa kienyeji wenye kufanya biashara hii tunajiuliza hivi kweli kabisa Polisi na Usalama wa Taifa miaka yote hii wameshindwa kabisa kwenda kwa kujificha (under cover) kuweza kuzama kwenye mtandao huu? Miaka yote hii kweli kabisa tumeshindwa kupeleka watu wakaweza kuufuatilia mtandao huu na kuukata kuanzia kwenye mzizi badala ya kuhangaika na majani yake? Hatari ya kushindwa ni kubwa zaidi Kinachonitisha mimi na kwa namna fulani kimshtue kila Mtanzania ni hatari ya kushindwa huku.

Ukiondoa ukweli kuwa kushindwa huku kumesababisha kuibuka tena kwa vitendo hivi naamini kunaweza kuwa na matokeo mengine yasiyotarajiwa; tunaweza kujikuta tunanyonga watu wasiohusika. Mojawapo ya mambo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara vinapotokea vitendo hivi ni mara moja kuwashuku baba wa watoto hao; na kama baba hajui kujieleza vizuri au anababaika basi mara moja ni rahisi kuonekana kuwa na hatia. Matokeo yake vyombo vya usalama vinaweza kujikuta ili kutuliza hasira za wananchi vinawashikilia wazazi (hasa baba) kwa kuwahisi kuhusika na vitendo hivi.

Kama ikatokea kweli baba hakuhusika lakini ameshindwa kujieleza vizuri au kupata utetezi mzuri wa kisheria basi tunaweza kujikuta tunawapeleka watu kunyongwa wasiohusika na hivyo kufanya janga hili kupiga mara mbili! Ni kwa sababu hiyo naamini suala hili linahitaji kukabiliwa kisayansi na kwa mbinu za kisayansi zaidi. Lakini pia linahitaji kuangaliwa kwa kuhakikisha kuwa badala ya kuwa tunaitikia matukio ni muhimu tuangalie nje ya kawaida tuliyozoea.

Je, hakuna njia bora zaidi ya kuhakikisha tunajua watoto albino katika mazingira yenye matukio haya walipo; je, hatuwezi, kwa mfano, kuhakikisha kuwa kila familia yenye albino hasa kwenye maeneo yenye matukio haya inapatiwa simu maalumu ambayo wanaweza kupiga namba sekunde moja tu (speed dial) pale watu wasiofahamika wanapobisha hodi majumbani mwao? Je, inawezekana kuhakikisha kuwa Helikopta ya Polisi au za jeshi zinakuwa tayari kuruka sehemu yoyote kwenye mikoa ya Geita, Shinyanga, Rukwa na Mwanza endapo simu inapigwa kuwa kuna mtoto kashambuliwa? Je, maofisa wa Usalama wanaweza vipi kujipanga kwenye hili?

Ni wazi kuwa hadi hivi sasa chini ya R.O wameshindwa na inaonekana Rais Kikwete bado – kama ilivyo kwenye Jeshi la Polisi – haamini kuwa kuna tatizo katika uongozi wa idara hizi. Labda mpaka tutakaposikia watoto wa vigogo wanaanza kukatwa viungo kwa imani za kishirikina; nina uhakika sidhani kama watafikia watoto hata kumi kabla dunia nzima ya Watanzania haijapinduliwa. - See more at: Raia Mwema - Mashambulizi dhidi ya albino: Usalama wa Taifa wako wapi?

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, Ablessed, Michelle, KikulachoChako, kill 3, Daudi Mchambuzi, everlenk, MziziMkavu, Ablessed, afrodenzi, Heaven on Earth, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Shark, mirisho pm, Camp 05, Ngoami, Kamakabuzi, jerrytz
 
Vyombo vya usalama vinangoja mpaka wasikie mtoto wa kiongozi kakatwa kiungo ndio waanze kuchukua hatua maana wao wapo kuwa ajili ya kuwalinda watawala baada ya wananchi ambao ndio waajiri wao na ndio hao hao wanaowalipa mishahara yao kupitia kodi zao....miongoni mwa walipa kodi hao ni hao hao walemavu wa ngozi walioshindwa kuwalinda na kuwasababishia waishi maisha ya wasi wasi.......kama idara husika imeshindwa kazi basi ifanye uungwana kwa kujiuzuru na wanaoweza kazi wachukue nafasi.....
 
Wao wamejikita zaidi kwenye usalama wa mafisadi akina fisadi Tibaijuka AKA Hela ya mboga, Chenge AKA Joka lenye Makengeza, Shaban Gurumo AKA mifuko yangu yote imejaa pesa n.k. kama wewe si fisadi basi kamwe hawatakulinda.

'Kulega kwa idara ya usalama wa taifa'
 
Bandiko zuri sana, kama ambavyo baadhi walivyochangia, usalama wa raia sio kipaumbele cha idara hii, leo tunaweza kuona kawaida kwa kuwa wanaosakwa ni ndugu zetu hawa albino, ushirikina una tabia ya kubadilisha matakwa hivyo ipo siku watahitajika watu weusi au wenye vipara, wenye makengeza, wenye matege au watu wa aina yoyote, tukifika hapo ndipo tutajua kuwa hili jambo ni very serious na kama taifa tumeandika historia chafu kabisa ya kuua binadamu wenzetu huku vyombo vya usalama vikionekana kushindwa kabisa.
 
Si kwamba usalama wa taifa wamelala, isipokuwa wanaelewa fika kuwa mauaji ya albino ni mradi wa kishirikina wa vigogo wa CCM ambao ni mabwana zao!
 
Hili tatizo ni la jamii nzima sio mtu mmoja au taasisi moja.acheni uvivu wa kufikiri
 
Kaz zao ni zipi?hata sidhani km kuna huo usalama wa taifa hapa tz

Kwa hiyo kuna usalama wa mkoa? Mnaua na kutesa watu kwenye chumba maalum huko chadema makao makuu mnakuja kusingizia wengine hapa
 
Usalama wa taifa kwa sasa ni usalama wa wanasiasa,hawajishughulushi kabisa na usalama wa wananchi na taifa hili,hata polisi pia ni jeshi la ulinzi na usalama wa wanasiasa watawala,hili tunajionea wenyewe jinsi wanavyojikomba kwa watawala na kupiga raia bila kuzingatia sheria,sijawahi kuona au kusikia jeshi la polisi likashindwa kukamata wahalifu,hata wakiwa wapi watapatikana tu,iweje kwa wauaji wa albino hawajulikani?lakini baadhi ya watu wanahisi wauaji wa albino ni haohao wanasiasa,ndiyo maana haya mauaji hutokea kila tunapokaribia uchaguzi,kwahiyo bi vigumu polisi kuwashughulikia.
Ni hadi hapo ccm watakapoondoka madarakani ndipo haki itarejea nchi hii.
 
Back
Top Bottom