Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Nilishawahi ku post thread hapa yenye title, SISIEM na Mradi wa Mauji ya Albino....

Naamini Mafisadi ndio mradi wao huu kwani kwao kutafuta Utajiri kwa njia zozote haramu ni ruksa.

Hakika serikali makini haiwezi kushindwa kushindwa kukabili tatizo dogo kama hili, kwani ina dola
 
Natumaini ma MoDs wataweza kutuunganishia hizi mada za Maalbino.. maana na mimi nilianzisha mada moja hapa.
 
Buswelu.. angalia hapo chini ya signature yangu:


Mzee Mkjj, hebu naomba unielekeze kaka namna ya kuipata na kuisikiliza maana naingia KLH News then nashindwa kuendelea. Najaribu Pics and Docs haifungui!
 
Indume yene ndani ya dakika kumi zijazo nitarusha onesho hilo unalolizungumzia.. na ikiwezekana nitaweka link hapa hapa kwenye hii post. Kwa hiyo ambaye amemiss anaweza kusikiliza kupitia KLHN..

MwKJJ, natanguliza shukrani kwa jinsi ambavyo umeweza kulivalia njuga hili suala. Ni aibu kwa taifa letu kuendelea kushuhudia ujinga huu ukipanda kasi huku eti wakubwa wako busy na uchunguzi wa MwanaHalisi kuwa na nyaraka za NBC. Hivi inaingia akili kweli Mwandishi asiyejua kiswahili (Alikuwa anamhoji huyo Mganga kwa Kiingereza) kupepeleza hadi kufanya mahojiano na huyo Mganga wa kienyeji anayetoa instruction jinsi ya viungo vya Albinos vinavyotumika huku Manumba na wenzake wako kimya tu, Bu@*&%**t. Ndiyo nimesema Bu@*&%**t
 
Tatizo kubwa hatuna Waandishi wa habari zinazohitaji UCHUNGUZI. Wengi tulionao ni wa habari za kuletewa kama POLISI wetu. Tatizo la Albino halijaanza leo lakini tuko "busy" na habari za kuletewa na tunaonekana mashujaa kwelikweli tukizichapisha.
 
Baada ya kusikiliza kipindi cha BBC jana jioni kuhusu mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albinos) kilichorushwa na jana tarehe 21.7.2008 na nikamsikia "LIVE" mtangazaji jasiri mwenye akili nyingi na mpenda haki VICKY NTETEMA akiongea na mganga muuaji wa jamii hii adhim ya walemavu wa ngozi, nilidhani leo hii asubuhi nitasikia tamko la kuwa mtu huyo amekamatwa mara moja. LAKINI MHHHH!!!!!!

Tanzania ya leo si ile tuliyoizoea japo kuwa kuna kila aina ya teknolojia ambazo leo hii habari kama hii tumeweza kuipata siku chache haraka iwezekanavyo licha ya kurekodiwa siku chache zilizopita zamani huenda hii ingechukua wiki mbili au hata mwezi kwani ilikuwa ni aibu kubwa kufanya hivyo na ikionekana kuna jamaa anafanya maovu kama haya ikirushwa hewani basi jamaa huyo anakua tayari yuko mikononi mwa vyombo vya sheria.

Usalama wa taifa zamani walikuwa ni watu ambao taarifa kama hizo wao ndiyo wanakuwa wa kwanza kuzipata, lakini leo hii mhhhhhh!!!!!!.

Tatizo ni nini??? Jibu ni kuwa HAKUNA UWAJIBIKAJI katika vyombo vyote vya usalama. Mimi nilipenda sana kuwa Usalama wa Taifa lakini tangu vetting ifanyike niliambiwa nijiandae kwa safari kesho yake nikaambiwa zoezi limeahirishwa, hadi leo. Hakika kama ningekuwa huko hili ningelifanyia kazi ipasavyo lakini kwa sababu ya wanayoijua wao tumekuwa ni watu wa kupewa ahadi tu.

KWA TAARIFA HII YA JANA TUNGEPENDA POLISI WAMKAMATE HUYO MGANGA TENA KWA HARAKA IWEZEKANAVYO NA AWATAJE WATEJA WAKE NA WAGANGA WENZIE ILI ANGALAU ALBINO WAWEZE KUPUMZIKA KIDOGO.


SHAME ON TANZANIA KULIKALIA KIMYA KIASI HICHO AND SHAME ON TANZANIA KUWA NA IMANI POTOFU KIASI HICHO. NGOZI YA ALBINO INAMATATIZO HALAFU WEWE MGANGA KWA KUWA ZAMANI KULIKUWA NA MBINU CHAFU ZA KUPUNGUZA IDADI YA ALBINO KWA KUWAACHA PORINI WATOTO ALBINO MARA WAZALIWAPO, LEO HII NYIE WAGANGA MNAKUJA NA MTINDO WA KUWAMALIZA MAALBINO KWA KUDANGANYA KWAMBA NGOZI YA ALBINO INAUWEZO WA KULETA UTAJIRI, KAMA NI HIVYO BASI NYIE WACHIMBA MIGODI YA MADINI WAAJIRINI MAALBINO WACHIMBE MADINI HAYO MNAYOYATAKA KULIKO KUWAUA KAMA MMEDANGANYIKA KIASI HICHO. NI DHAMBI KUWAUA MAALBINO.


STOP KILLING ALBINOS = ACHA KUUA MAALBINO
 
Very sad news indeed. Imefikia level ya ethnic cleansing kwa hawa ndugu zetu.
 
Hwawezi kumkamata huyo mganga kwani wao ndo wanaenda kwakwe halafu wamkamate si kwa imani yao watakuwa kwenye matatizo. hii jamii tuliyonayo ni ya kuone huruma sana kwani ubinadamu umeisha tumebaki kuangalia pesa tu. ulimsikia yule jambazi shaidi wa kesi ya zombe, mpaka leo yuko mtaani na alisema hawezi kuacha ujambazi.
 
Sio mtetezi mkubwa sana wa polisi wetu lakini kwa hili I can understand jinsi ambavyo ni vigumu kupata ushahidi kwenye kesi ambazo zinahusu mambo ya uchawi. Mara nyingi polisi wanaishia kuwakamata tu na kuwaachia bila kuwapeleka mahakamani kwa kuwa wanashindwa kupata ushahidi wa kutosha.
 
Bubu,Hata mimi nimeshangaa Mwandishi anafanya kazi ambayo ni ya polisi wa upelelezi wala wenyewe hawana hata habari.Robert na Peter kivuyo kitengo chao kinasimamia vipi hivi vitengo vya chini yake kutimiza huu wajibu wa upelelezi?
Baadhi ya askari polisi kwa sasa wanaacha sana jeshi la polisi na kuingia kwenye ajira huru maana hata hatima yao ya maisha haieleweki,Ndo maana upelelezi umekuwa butu.Wengi wanaoenda kusoma vyuo vikuu wakimaliza asilimia kubwa hawarudi tena vituoni.
Tunapoteza wataalam jeshini,ndo maana wanaenda kupekua computer za kubenea alafu hapo hapo wanasema hajui matumizi ya computer,what' s that kind of foolish question?Mhariri wa gazeti hajui kutumia computer?

Kwa uzembe huu watajikuta wako nyuma ya wakati na wataliingiza jeshi hili katika mgogoro mkubwa na wananchi.
 
Ni wazembe mno and they need to be disciplined.Naomba nitoe taarifa humu humu kwamba Mkoani Arusha kuna polisi mitaa ya Naaz hotel huwa wanatabia ya kusimamisha magari ya watu wanakula hongo sijapata ona.Ni kitendo cha aibu kwa kweli polisi kupokea kama 500 kama bribe.Siamini kama wanaumaskini kiasi hichi.Hawatimizi wajibu wao sasa ni swali la kujiuliza kama Said Mwema na yeye anafanya kazi yake kweli ama huo uana kamati aliopewa una mkeep busy.
 


Usalama wa taifa zamani walikuwa ni watu ambao taarifa kama hizo wao ndiyo wanakuwa wa kwanza kuzipata, lakini leo hii mhhhhhh!!!!!!.

.


STOP KILLING ALBINOS = ACHA KUUA MAALBINO

Ndugu yangu kuna kitu umesahau. Definition ya usalama wa taifa imebadilika sana. Who cares usalama wa taifa leo. Who really cares maisha ya mtanzania leo. Can you tell me nani serikalini atashituka kama wewe ukifa au ukiwa hai. Who cares mtanzania kama profesa akiuawa, leave alone albino wa kijijini? These are the facts we are living with.
we are worthless in our country, akiuawa mzungu utaona jinsi serikali itakavyokuwa makini, uawa wewe uone. Ni sisi narafiki zako ndio tukakaosikitika na kulia. Labda serikali itasikitika kwa sababu mtu mmoja wa kunyonywa atakuwa amepungua.
 
Stop Killing Albinos = Acha Kuua Maalbino
They Are Worthless To What You Believe = Hawana Thamani Katika Uchimbaji Madini Kama Mnavyoamini
 
[Usalama wa taifa zamani walikuwa ni watu ambao taarifa kama hizo wao ndiyo wanakuwa wa kwanza kuzipata, lakini leo hii mhhhhhh!!!!!!.

Tatizo ni nini??? Jibu ni kuwa HAKUNA UWAJIBIKAJI katika vyombo vyote vya usalama. Mimi nilipenda sana kuwa Usalama wa Taifa lakini tangu vetting ifanyike niliambiwa nijiandae kwa safari kesho yake nikaambiwa zoezi limeahirishwa, hadi leo. Hakika kama ningekuwa huko hili ningelifanyia kazi ipasavyo lakini kwa sababu ya wanayoijua wao tumekuwa ni watu wa kupewa ahadi tu.


Zamani ndio kulikuwa na usalama wa taifa siku hizi hamna usalama wa taifa. zamani kumjua mtu kama yuko usalama wa taifa ni issue lakini siku hizi kuwa usalama wa taifa imekuwa dili (sifa mtaani) lazima ujitangaze ili watu wakujue, wakuogope, wakununulie bia, wakiwa na issue zao za kifisadi wakuhusishe ili wafanikiwe na wewe upate hela ya kusumbua baa. usalama wetu wa taifa ndio huu siyo kama zamani.
 
Nadhani kuna haja ya jk kuwafuta kazi maofisa wa tiss na kutangaza nafasi za kazi upya, ufanyike usaili wa wazi na haki. Kwa sasa ajira tiss hazieleweki zinaendaje hatakama kuna ushemeji hakuna ajuae.

nahawa oc-cid sijui wanaajiriwa vipi! wapiga debe tu walishawashinda. unajua bila kuwa na macid makini manumba na kamanda toss hakuna watakachofanikiwa.

Mbona CIA na FBI wanatangaza nafasi za kazi tena kwenye website zao.
 
Bubu,Hata mimi nimeshangaa Mwandishi anafanya kazi ambayo ni ya polisi wa upelelezi wala wenyewe hawana hata habari.Robert na Peter kivuyo kitengo chao kinasimamia vipi hivi vitengo vya chini yake kutimiza huu wajibu wa upelelezi?
Baadhi ya askari polisi kwa sasa wanaacha sana jeshi la polisi na kuingia kwenye ajira huru maana hata hatima yao ya maisha haieleweki,Ndo maana upelelezi umekuwa butu.Wengi wanaoenda kusoma vyuo vikuu wakimaliza asilimia kubwa hawarudi tena vituoni.
Tunapoteza wataalam jeshini,ndo maana wanaenda kupekua computer za kubenea alafu hapo hapo wanasema hajui matumizi ya computer,what' s that kind of foolish question?Mhariri wa gazeti hajui kutumia computer?

Kwa uzembe huu watajikuta wako nyuma ya wakati na wataliingiza jeshi hili katika mgogoro mkubwa na wananchi.

D Moja,
Wiki iliyopita nilikuwa naongea na polisi nusura nitokwe na machozi. Jamaa wanajitahidi kuwa commited na kazi zao lakini wanadharauliwa kama mbwa. Wanafanya kazi kubwa katika mazingira ya kuuawa lakini credit wanachukua wanasiasa ambao wengi ndio hivyo tena. Nilikuwa naangalia nyumba zao mpaka unaweza kusema nyumba zao ni kama mapango ya wavuta bangi. No body cares about them. Mimi nawaunga mkono wanapojiendeleza kielimu na kuamua kuacha kazi zao, kila binadamu anastahili maisha mazuri regardless ya kazi yake halali anayofanya, lakini polisi wetu ni kinyume wao wanakuwa kama wafungwa wa kiakili.
 
kwa wale walio UK, story ya albino itakuwa hewani muda si mfupi kwenye bbc2 newsnight.
 
Hii Kashifa sasa

Print Email Add to My Stories

Albinos targeted in witchcraft killings
Posted Tue Jul 22, 2008 12:33pm AEST
Updated Tue Jul 22, 2008 12:55pm AEST

An undercover investigation by the BBC has found that albinos in Tanzania are still being murdered so their body parts can be used in witchcraft.

Two albinos have been killed in northern Tanzania in the past month despite government efforts to stamp out the practice.

A 52-year-old man was killed in his backyard as he ate a meal with his wife, and just a week ago, a seven-month-old baby was snatched from his parents' arms and hacked to death with machetes.

Tanzanian President Jakaya Kikwete has ordered a census of all albinos in Tanzania to be carried out in a bid to offer protection.

But there are growing suspicions that elements within the Tanzanian police may be involved in the trade.
- BBC

Tags: religion-and-beliefs, witchcraft, human-interest , law-crime-and-justice, crime, murder-and-manslaughter, tanzania

http://www.abc.net.au/news/stories/2008/07/22/2310795.htm
 
Back
Top Bottom