Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Hii Kashifa sasa

Print Email Add to My Stories

Albinos targeted in witchcraft killings
Posted Tue Jul 22, 2008 12:33pm AEST
Updated Tue Jul 22, 2008 12:55pm AEST

An undercover investigation by the BBC has found that albinos in Tanzania are still being murdered so their body parts can be used in witchcraft.

Two albinos have been killed in northern Tanzania in the past month despite government efforts to stamp out the practice.

A 52-year-old man was killed in his backyard as he ate a meal with his wife, and just a week ago, a seven-month-old baby was snatched from his parents' arms and hacked to death with machetes.

Tanzanian President Jakaya Kikwete has ordered a census of all albinos in Tanzania to be carried out in a bid to offer protection.

But there are growing suspicions that elements within the Tanzanian police may be involved in the trade.
- BBC

Tags: religion-and-beliefs, witchcraft, human-interest , law-crime-and-justice, crime, murder-and-manslaughter, tanzania

http://www.abc.net.au/news/stories/2008/07/22/2310795.htm

This story is not going away anytime soon...sasa naona pia polisi wamo eti!
 
bila ya shaka na polisi wamo kwenye mauaji hayo.......kama wangekuwa hawamo kwa nini kwenye kesi zote hizo zilizotokea wameshindwa kuwakamata hata wauaji mara moja ?

haya sasa, na salva aje asema tusizungumzie ushirikina kwa sababu tutakuwa hatupewi misaada........
 
Looh! nimeona hii kwenye BBC news jana usiku, yaani inasikitisha sana.

Kweli sisi binadamu ni wanyama kabisa. Yaani kweli kama nchi, kama raia, kama polisi, tunashindwa kulinda maisha ya hawa ndugu zetu wanyonge kwenye jamii?

Inasikitisha mno.
 
.... Matunda ya Uhuru wa Tanzania, Hata baada ya miaka zaidi ya 40 ndani ya karne ya 21, wananchi wengi bado wana imani kama hizi.

.... Hili swala la imani mbovu kama hizi, ni matunda ya elimu mbovu kwa jamii. Haikatizi akilini mtu mwenye uelewa wa mambo aamini kuwa kiungo cha binadamu mwingine ni dawa ya utajiri au matatizo yake mengine.... inakasirisha na kutia manchungu.

.... Kutumia vyombo vya dola pekee kama njia ya kuondoa haya mauaji hakutazaa matunda ya muda mrefu. Elimu na kusambaza habari katika jamii ni moja ya kinga madhubuti ya tatizo hili.

SteveD.
 
Vick Mtetema na Karren Allen wamefanya kazi nawapa big up

Hii ni mojawapo ya familia ya Nyerere Rutahiro iliyopata masaibu haya:


'We want your legs' The last adult albino to be murdered - just a few weeks ago - was Nyerere Rutahiro.

attachment.php




Chek hii link
http://news.bbc.co.uk/2/hi/programmes/newsnight/7520690.stm
 
Aslimia fulani ya viongozi wamepita kwa hao waganga, na siajabu wanavyo viungo vya hao watu kwao.
Kuwategemea wafanya jambo la maana ni kushindwa. Hawawezi kabisa, wameshazibwa midomo.
 
kama sikosei bungeni kuna mama mmoja albino, kwanini asiwasilishe hoja binafsi bungeni?
akifanya hivyo nadhani itakuwa na nguvu zaidi, kuliko suala hilo kuwasilishwa na mtu ambae hata tatizo lolote.
(kama hajui kufanya hivyo, wabunge wengine msaidieni)
 
kama sikosei bungeni kuna mama mmoja albino, kwanini asiwasilishe hoja binafsi bungeni?
akifanya hivyo nadhani itakuwa na nguvu zaidi, kuliko suala hilo kuwasilishwa na mtu ambae hata tatizo lolote.
(kama hajui kufanya hivyo, wabunge wengine msaidieni)

Nafikiri huyu mama amelipigia kelele hili suala. Hata kwenye BBC jana alikuwa miongoni mwa watu walioongea akilaani na ubaguzi mzima dhidi ya Albino.

BBC pia walimwongelea mzee wa vijisenti na vumbi yake bungeni (of course hawakutaja jina lake_
 
When I went back with other BBC colleagues, his nephew was there to receive me.
He said he knew what I wanted and said he would find me albino blood, hair, leg and palms for $2,000.


He charged me $55 for the initial consultations and asked me to return with the rest of the money.
While I was there, a man came for a consultation - the witchdoctor said he was a police officer but he was wearing civilian clothes.
However, he was made to wait until my session was over and, I later learned, told the witchdoctor that I was involved in a sting operation.
Shortly afterwards, the threatening phone calls started.
And a gang of men went round the small town where we had stayed, searching all the guest houses. Luckily, we had already moved on to the nearest city, Mwanza.
One particularly chilling message came on my mobile phone: "What have you done now? Watch your back."
The witchdoctor had boasted of working with a powerful network across East Africa, which included police officers and armed robbers.
I knew they were involved in the murder of albinos, so I was terrified.
At first, I did regret taking on this mission - especially for the sake of my family.
Had I put their lives at risk?
But then I realised that I had done the right thing. Even if I die today, those involved will have been exposed.

Courtesy of Vick Ntetema of BBC Swahili Service
 
1.Uchawi upo.
2.Ndiyo.
3.Mimi ni mkristo lakini uchawi haupingani na imani yangu kwa vile hata Biblia inakiri kuwepo kwa uchawi.
4.Vyombo vya habari na hata dola linajifanya kwamba uchawi haupo.
5.Ndiyo,mazinga-ombwe ni uchawi na majini ni washirika katika uchawi.
 
Jamani, hivi solution ya mauaji ya albino ni nini? ina maana selikali imeshindwa? au kwasababu viongozi wenyewe ndo wanashindaga huko kwa waganga na wametandaza hirizi kwenye viono vya vitambi vyao mle ndo maana wanasuasua kulimaliza?

Hawa waganga ni kuwafuta tu ili tz tusiwe na kitu inaitwa waganga wa jadi. kwasababu hawa walianza kuwaula watu wenye vipara na viungo vyao kupelekwa kwa waganga. watu wenye vipara walikuwa na wakatu mgumu sana nakumbuka kipindi fulani. ikaja watu kuchunana ngozi na kuipeleka kwa mganga. kule mbeya kulikuwa na upigaji watu nondo halafu ile nondo wanasema inapelekwa kwa mganga wa jadi aiuze kwa wenye mabusha ati ile damu aliyompiganayo mtu nyama zitatoka sana. wamekuja kwenye kung'ofoa viungo vya siri na kuviuza, hawa waganga wa nini? we need to solve this prob as soon as possible,

kwasababu, kuna siku wakimaliza albino, wataanza watu warefu na mangongochi kama sisis, wakimaliza hao watakuja watu wafupi, pengine watakuwa watu wanene, itafika kipindi yaani hapakaliki...hahaha. sasa hawa waganga wana nini haswa hata kutuyumbisha kiasi hiki? wahusika wa dola wanashindwa nini kuwashughulikia hawa watu, hivi waganga wa kienyeji wana faida kweli hapa tz? mbona ulaya watu wanaishi tu bila hawa waganga bwana....mi naona tuwafute, sheria itungwe kukataza uganga zt. nyie mnasemaje wajemeni.
 
Mimi nawashangaa sana wale wanaowavalia njuga na kuwauwa vibibi vikongwe wakionekana kuwa ni wachawi waliokubuhu na hawafi ila wakiuliwa ndio hufikwa na mauti.
Sasa kama kuna wanaharakati hawa wanaowaua vikongwe kwa nini na wao sasa hawageuzi mpigo na kuwaamkia waganga wa kienyeji ambao ndio chimbuko la wachawi,yaani ni kuwafyeka tu,kama kwenye kijiji kuna mtu anajidai kutapeli na kutoa amri za kuwaua watu wa jamii fulani ili kutumika katika mambu ya kishirikina basi na wananchi nao ili kujihami na utabiri wa waganga hawa wa kubadilisha aina za viungo vinavyohitakika kutokana na aina ya watu wawageukie na kuwacharanga mapanga.
Hili linawezekana kabisa ikiwa linawezekana kwa vikongwe kwa nini lisiwezekane kwa watu dizaini hii ya waganga wa kienyeji.
Aidha usalama wa Taifa unaweza kuiandaa killing squad kuwashugulikia watu hawa usiku wa manane.
 
Albino mwingine kauawa, mke wake naye kajeruhiwa, na sasa watoto (wawili ni albino) wako mashakani. Stori iko BBC na KLH News..
 
Shame kwa serikali ya awamu ya nne hadi watu wametoka nje na kugundua Mwema na watu wake hola

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7518049.stm

Ngoma nzito unategemea nini kwa polisi wa Tanzania ambao kwanza wao wenyewe baadhi yao wana interest katika suala hilo,pili na mbinu zao archaic watamshika nani zaidi ya kubenea,vijana wa jambo forums,wewe na wale wenye registered office ambao hata huhitaji kuwa na ujuzi wa kipolisi kuwakamata?Wee jiulize tu mtu kama mkuu wa wilaya anakataa kutoa habari kwa waandishi kuhusu mauaji ya albino na serikali imejipangeje,hiyo ina maana gani?si ajabu angekaa nao vizuri wale waandishi akakiri wazi vita ni ngumu wangeweza hata kumpa tip walizozipata akajua pa kuanzia na yeye akajikombea ujiko kuwa amefanya kazi kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.Sasa hii film ya ntetema sijui anajisikiaje?huko aliko
 
jamanieee, mbona hii mada mmeikacha? au kuna wateja wengi humu wa waganga wa kienyeji?
 
watakaofuata ni watu waliozaliwa na ulemavu!
 
Back
Top Bottom